Mwaka 2018 ni miaka 6 imepita wakati Tanzania tunacheza mechi za kufuzu AFCON 2019 ambapo tuliwahi kumfunga Cape Verde goli 2 bila hapa nyumbani katika dimba la Benjamin Mkapa ambapo Tanzania na Uganda ndio tulifuzu AFCON 2019.

Mwaka 2024 katika michuano ileile ya mataifa barani Afrika, Cape Verde anatinga katika hatua ya 16 bora kwa kushinda mechi zake zote 2 za mwanzo za makundi katika michuano ya mataifa barani Afrika (AFCON) huku Taifa Stars wao wakianza vibaya kwa kipigo kutoka kwa Morocco.

Hebu tujiulize kwanini wenzetu wanatuacha sisi Tanzania? Hawa Cape Verde leo wanafuzu 16 bora AFCON 2023 tena mbele ya mataifa makubwa kama Nigeria na Ghana. Tanzania inakwama wapi? Ipo haja ya kwenda kujifunza kwa Mataifa kama haya namna ambavyo yanapiga hatua. Kwa sasa Ligi ya Tanzania ni bora kuliko Ligi ya Cape Verde ila ukija katika upande wa timu ya Taifa unawaona hawa wametuacha mbali kabisa.

Michuano ya AFCON (Cup of Nations) ni mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya soka barani Afrika, na kila timu inayoshiriki ina ndoto ya kufanya vizuri na kufika mbali. Kuna mambo kadhaa yanayoweza kuchangia mafanikio ya timu katika michuano hii:

Ukiitazama Cape Verde nit imu ambayo ina wachezaji wenye uzoefu wa kimataifa ambao mara nyingi hufanya vizuri. Wachezaji waliozoea mazingira ya michuano mikubwa wanaweza kushughulikia vizuri shinikizo la mchezo wa kimataifa na hali ya uwanja wa mashindano.

Wakati mwingine kukiwa na maandalizi sahihi na makini kabla ya michuano ni muhimu. Timu zinazofanya mazoezi mazuri, kuweka mikakati imara, na kuchunguza wapinzani wao kwa makini zinaweza kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri. Ukiitazama Tanzania wamekua na mchezo mmoja pekee kwa ajili ya maandalizi ya AFCON.

Uongozi bora kutoka kwa makocha na viongozi wa timu ni muhimu kwani siku zote kocha anayewaelekeza wachezaji na kuwapa mbinu bora za mchezo anaweza kuleta mafanikio makubwa haswa kwa wachezaji wanaofanya kazi kwa pamoja na kujituma. Ushirikiano kati ya wachezaji, pamoja na kufahamu majukumu ya kila mmoja, ni muhimu.

Cape Verde ina wachezaji wenye uwezo wa ubunifu ambao wameweza kuleta utofauti kwenye uwanja. Uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka na kutumia vipaji vyao vya kumeweza kuwa na  athari kubwa kwenye matokeo ya timu.

Katika michuano ya AFCON, mambo haya yanaweza kuchangia kufanya tofauti kati ya timu inayofikia hatua za mwisho na ile inayotolewa mapema. Kila timu inayoshiriki ina nafasi yake ya kung’ara, na mchanganyiko wa mambo haya unaweza kuleta mafanikio kwa timu hizo.

SOMA ZAIDI: Tuwekeze Kwa Vijana Taifa Stars, Ndio Msingi Wa Mafanikio

 

1 Comment

  1. Pingback: Mauritania Mmejitahidi Bahati Sio Yenu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version