Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa usalama viwanjani nadhani zina kitu cha kutolea maelezo au kujifunza kutokana na uzembe kama huu ambao umekua ukijitokeza mara nyingi katika baadhi ya mechi, ikiwezekana watu wawajibike au kuwajibishwa kwa uzembe kazini. TFF na Bodi ya Ligi Kuu, Afisa Usalama wa viwanja wa TFF ambaye amepata kozi nyingi za CAF & FIFA wanaweza kuelezeaje hili.

Mpira ni sayansi wenzetu wanawekeza kwa kuwanunua wachezaji wenye uwezo mkubwa wachezaji ambao wataweza kuwapa matokeo muda wowote lakini sisi kama watanzania tumekua tukiamini katika masuala ya Imani za kishirikina michezoni na mpaka karne hii bado utakuta ipo timu inaamini katika ushirikina zaidi kuliko wachezaji wao, inasikitika.

Sipendezwi na tabia hizi ambazo tumekua tukizionesha huku tunajiandaa kwa ajili ya michuano ya AFCON tusijeendekeza na kupata aibu kubwa zaidi na kinachonisikitisha zaidi kwani walizni huwa wako wapi? ndo uingie uwanjani tena mchezo unaendelea halafu langoni kwa Golikipa, hapo ungeaminika vipi kama haukwenda kumdhuru mchezaji, tungeamini vipi hicho ulichokibeba kilikuwa ni kitu cha kawaida.

Naamini hili limeoneka Shabiki aliyevalia jezi ya Simba SC aliivua wakati akiruka toka jukwaani akienda kufukia vitu golini Kwa Golikipa wa Mashujaa FC, tunaamini vitendo hivi havikubali na kama vikiachwa vitaleta madhara zaidi. Kwaiyo tunaamini mmeviona na hatua Kali zichukuliwe.

Hii siyo tu Kwa Klabu ya Simba SC na nyingine yoyote ikitokea imefanya vitendo hivyo hatua Kali zichukuliwe Kwa kuulinda mpira wetu na vitendo kama hivi. Jamani tupunguze ULOZI zaidi tuwekeze kwenye kusajili wachezaji wazuri.

SOMA ZAIDI: Mnamchanganya Dickson Job, Tungeamua Kunyamaza Tu

1 Comment

  1. Pingback: Barua Kwenu Washirikina Wa Mpira Wa Miguu Tanzania - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version