Wakati huu ambapo kuna maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kumekuwa na upatikanaji wa habari mbalimbali kwa urahisi na uharaka sana na kumepelekea kuwa na uhuru zaidi kwa wapenzi, wafuatiliaji na wanachama kufuatilia vilabu vyao wanavyofanya kila siku.

Huu ndiyo wakati ambao watu wengi sana wanatumia mitandao ya kijamii kuiingizia pesa vilabu vyao halikadhalika kutoa maoni, nje ya kuvipatia vilabu vya mapato ila imekuwa sehemu kubwa sana kusifia na kuponda timu zao na pinzani kulingana na matokeo na muenendo wa timu husika.

Bila shaka ni faraja kwa wapenzi na wafuatiliaji ila ni faida zaidi kwa wasimamizi wa mpira wetu pamoja na vilabu husika kwani imekuwa ikisaidia sana kuipambana na kuikuza Ligi yetu nje ya uwanja na ilo kwa sasa halina ubishi kila timu ya nje inapocheza na timu zetu hususa Simba SC na Yanga SC basi inanufaika zaidi nje ya uwanja kwa kuongeza wafuasi kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii.

Lakini kuna jambo moja kwa sasa limekuwa maarufu sana nje ya uwanja, timu ikiwa inacheza kuwa na “Hype” kubwa nje ya kiwanja, kusifia wachezaji wao na kuwaponda wa upinzani na ilo siyo mbaya kwa kuwa ni sehemu ya ladha ya mpira hususa mpira huu wa Tanzania.

Nje ya ilo kuna jambo limeanza kuwa mazoea sasa watu kutumia nafasi hiyo vibaya, ni takribani msimu wa pili sasa watu wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kuponda wachezaji ingalikuwa hata robo ya mechi hazijachezwa imefikia kipindi, hadi watu wa kimpira na tunaoamini wanauwelewa mkubwa wa kisoka kuanzia mbinu na mifumo nao kuingia kwenye mkumbo huu.

Ni dhahiri kuwa hakuna mchezaji bora anayepimwa kwa mechi moja tu na ilo halina ubishi, lakini imekuaje tena ? Inafikia hatua tunaanza kuponda wachezaji ikiwa ndiyo kwanza mechi moja zimechezwa na hata vilabu vingine havijacheza mechu yoyote ile ya ufunguzi wa Ligi. Tumekubali kupima wachezaji wetu kwa mchezo mmoja au miwili tu ?

Wacha niwakumbushe kuna baadhi ya wachezaji tulifanya kitendo kama hicho lakini mwisho wa siku walikuja kutuumbua kadri muda na michezo mjngu waliyokuwa wakicheza nani asiyemkumbuka namna Clatous Chama alivyoanza msimu kwa mara ya kwanza akiwa na Simba SC, Gerson Fraga, Joyce Lomalisa, Cheikh Sidibe,,Ayoub Lakred, Kibu Denis, Frans Kazadi na wengine.

Wachezaji hao kuna baadhi ambao walianza vizuri na kwa moto sana tukaanza kuwasifia ila kadri siku zinaenda walishindwa kutoa kile walichoonyesha mwanzo mfano mzuri ni Frans Kazadi aliaanza kwa ubora sana kwenye michuano ya Mapinduzi Cup na kuibuka mfungaji bora, Cheikh Sidibe alianza kwa ubora ila tulishindwa kukumbuka kuwa mambo yanabadilika na mwisho wa siku akaanza kuwekwa benchi na kijana wa kitanzania Pascal Msindo.

Hata hivyo kuna baadhi yao pia walianza wakiwa chini sana hawakuonyesha ubora mkubwa ila kadri siku zinaenda walidhihirisha ubora wao na mfano halisi ni Clatous Chama alikuja kwa mara ya kwanza, Joyce Lomalisa, Gerson Fraga na Ayoub Lakred ni wachezaji waliyoanza wakiwa chini ila kadri siku zinaenda walionyesha ubora mkubwa sana kiwanjani.

Lakini nani anasahau kuwa kuna kupitia kipindi kigumu kwa wachezaji ? Kuna wakati alionyesha ubora mkubwa ila katikati alipitia kipindi kigumu na wengi wakaanza kuponda na kuonyesha mchezaji huyo siyo bora na kusahau kuwa kuna nyakati mbaya tu ila ubora wa mchezaji huko pale pale ikiambata na msemo maarufu kwenye Soka “Class is permanent, but form is temporary” nani amemsahau Kibu Denis? Bakari Mwamnyeto je?  Tujifunze hapo.

SOMA PIA: Kwa Maboresho Haya Wadhamini Wa Ligi Kuu Mmetisha

Leave A Reply


Exit mobile version