Tanzania (Taifa Stars) ni mojawapo ya nchi ambayo imebarikiwa kuwa na vipaji vingi sana vya soka ambavyo tumekua tukivishuhudia miaka na miaka kuanzia kizazi cha kina Said Mtupa mpaka sasa tunavyotamba na wachezaji kama kina Mbwana Samatta na Feisal Salum.

Kuitwat imu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania ambayo inafahamika kama Taifa Stars inajulikana kama kioo cha mafanikio kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (Ligi Kuu)  na wale wanaocheza ligi mbalimbali za nje ya Tanzania.

Hivi karibuni, kumekuwepo na mjadala mkubwa kuhusu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na mgogoro wa chini kwa chini kuhusu wachezaji wa Taifa Stars kwenye suala la posho. Ijapokua kuna wakati Shirikisho lilisema kuwa hakuna jambo kama hilo.

Wakati Taifa Stars wakiwa nchini Ivory Coast kwa ajili ya AFCON ameibuka tena Rais wa TFF Bwana Wallace Karia akisema kuwa wamesaidiana na Serikali kuhakikisha kuwa wanawalipa wachezaji wote posho zao na akienda mbali zaidi kwa kusema kuwa watasaidiwa na serikali kupunguza madeni ambayo tayari wako nayo lakini tujadili kwa Pamoja. Je, hatua hii inaleta ufanisi na kuongeza motisha, au ni kichocheo cha kuwayumbisha?

Posho ni sehemu muhimu ya motisha kwa wachezaji wa Taifa Stars na timu nyingine. Kuwapa wachezaji stahiki zao ni njia mojawapo ya kuonyesha heshima na kutambua mchango wao katika kupeperusha bendera ya Taifa. Hata hivyo, mjadala huu unazua maswali kuhusu jinsi TFF inavyoshughulikia suala la posho kwa wachezaji.

Ukitazama wengi ambao huwa hawapendezwi na mambo haya ya posho huuliza hivi hizi posho zinawawezesha wachezaji au huwa zinawadhoofisha? Wakosoaji wanasema kuwa TFF imekuwa ikichelewesha au kutowapatia wachezaji wao posho zao kwa wakati, jambo linaloweza kuathiri utendaji wao uwanjani. Hii inaweza kusababisha wachezaji kupoteza morali na kuwa na mawazo mengine yanayoweza kuathiri matokeo ya timu. Kwa upande mwingine, TFF inaweza kuwa na sababu zake za kuchelewesha posho hizo, kama vile changamoto za kifedha au taratibu za kiutawala.

Motisha ni moja kati ya kichocheo muhimu cha mafanikio katika michezo. Wachezaji walio na motisha wanaweza kufanya vizuri zaidi uwanjani na kuleta heshima kwa nchi yao. Posho zinaweza kuwa sehemu muhimu ya kuongeza motisha, na hivyo, ni muhimu kwa TFF kuhakikisha kuwa wachezaji wanapata posho zao kwa wakati ili kuwa na kikosi kilichojawa na hamasa na ari ya ushindi.

Kuwayumbisha wachezaji wa Taifa Stars kwenye ishu za posho ni suala linalohitaji utatuzi wa haraka na wa busara. TFF inapaswa kutambua umuhimu wa kutoa posho kwa wachezaji kwa wakati ili kuimarisha motisha yao na kuboresha utendaji wa timu. Hata hivyo, pia ni muhimu kwa TFF kufanya maboresho katika usimamizi wa fedha ili kuepuka matatizo ya kifedha yanayoweza kusababisha kuchelewesha posho. Kwa pamoja, hatua hizi zinaweza kusaidia kuimarisha soka la Tanzania na kuleta mafanikio zaidi kwa Taifa Stars.

Endelea kufuatilia zaidi kuhusu taarifa mbalimbali za AFCON kwa kugusa hapa.

 

1 Comment

  1. Pingback: Puma Na Funzo Kubwa Kwa Sandaland Kupitia AFCON - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version