Katika kila timu moja kati ya nafasi ambayo mara nyingi huwa inazingatiwa sana katika kikosi ni pamoja na nafasi ya mlinda lango au unaweza kusema golikipa kwani yeye ndio anajukumu zito la kuzuia mpira usiingie nyavuni na hapa lazima umtaje golikipa Ayub Lakred.

Wengi watakua wanajiuliza sasa Ayoub anawaingizaj matatani klabu ya Simba? Nadhani kwa sasa licha ya kurejea kwa Aishi Manula bado kocha wa magolikipa wa klabu ya Simba atakua anawaza nani aanze golini kati ya Manula,Charles Abel au Ally Salim katika mchezo wa ugenini wa dhidi ya Asec Mimosas.

Hii ni kutokana na kuwa mpaka sasa klabu ya Simba hakuna ambae anaweza kusema kwamba yeye ndio golikipa namba moja kutokana na viwango vyao na ubora wao walionao magolikipa wa timu hii yenye asili yake mitaa ya Msimbazi.

Katika michezo sita ambayo Simba imecheza baada ya mapumziko mafupi kupisha michuano ya AFCON, tayari makipa watatu kati ya wanne wameonekana katika michezo toafuti, akiwemo Ayoub alidaka mechi tatu dhidi ya JKT Tanzania, Azam FC na Tabora United.

Kwa upande Aishi Manula amesimama katika mlingoni katika mchezo kati ya Geita Gold FC na Mashujaa FC na Hussein Abel alidaka mechi moja ya Kombe la Shirikisho FA dhidi ya Tembo FC ya Tabora, uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar-es-Salaam.

Swali ni kwamba nani aanze? Kati ya Abel, Ally Salum pamoja na Manula kwani Ayoub Lakred yeye atakosekana katika mchezo dhidi ya ASEC kutokana na kuitumikia adhabu ya kadi za njano.

SOMA ZAIDI: Kama Una Tabia Hizi Hupaswi Kuitwa Shabiki Wa Yanga.

1 Comment

  1. Pingback: Vita Ya Mbinu Itakavyoamua Asec Mimosas vs Simba Sc - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version