Kundi la Wagombea wa Tuzo ya CAF “Goli Bora la Mwaka (Msimu)” Lazinduliwa, Upigaji Kura Sasa Wazi kwa Mashabiki Kupiga Kura ya Mshindi

Mashabiki wa mpira wa miguu sasa watakuwa na sauti ya mwisho kumchagua mshindi wa kategoria ya Tuzo ya CAF “Goli Bora La Msimu” kwa Tuzo za CAF za mwaka 2023, huku upigaji kura ukifunguliwa kwa siku chache zijazo.

Kikosi cha wataalamu kimeteua mabao 12 ya kushangaza kutoka katika mashindano mbalimbali ya CAF ili yapigiwe kura na umma wa wapenzi wa michezo.

Kura za umma zina uwiano wa asilimia 70 ya mchakato huo, huku zikifanya tuzo hii kuwa maalum ikilinganishwa na makundi mengine.

Asilimia nyingine 30 inaamuliwa na Wataalamu wa Kiufundi wa CAF.

Upigaji kura umeanza leo kupitia tovuti ya CAF na utafungwa tarehe 8 Disemba 2023.

Mshindi atatangazwa kwenye Gala ya Tuzo za CAF siku ya Jumatatu, tarehe 11 Disemba 2023, katika Palais des Congrès, Movenpick, Marrakech, Morocco.

Hapa ni majina ya wagombea;

  1. Alex Ngonga (DR Congo, TP Mazembe) – TP Mazembe vs AS Real
  2. Dango Ouattara (Burkina Faso, Bournemouth) – Burkina Faso vs Eswatini
  3. Jennifer Owusuaa (Ghana, Ampem Darkoa) – Ampem Darkoa vs Sporting Club Casablanca
  4. Khaled Bousseliou (Algeria, USM Alger) – AS FAR vs USM Alger
  5. Mahmoud Abdelmenem ‘Kahraba’ (Egypt, Al Ahly) – Al Ahly vs Al Hilal
  6. Mahmoud Saber (Egypt, Pyramids/Zed FC) – Egypt vs Morocco
  7. Mohamed Dhaoui (Tunisia, Al Ahly) – Tunisia vs Zambia
  8. Nadege Nguessan Koffi (Cote d’Ivoire, Sporting Club Casablanca) – Atletico FC VS Sporting Club Casablanca
  9. Patient Mwamba (DR Congo, TP Mazembe) – TP Mazembe vs AS Real
  10. Saul Coco (Equatorial Guinea, Las Palmas) – Equatorial Guinea vs Botswana
  11. Teboho Mokoena (South Africa, Mamelodi Sundowns) – Mamelodi Sundowns vs Al Ahly
  12. Refilwe Tebogo Tholekele (Botswana, Mamelodi Sundowns) – Mamelodi Sundowns vs Sporting Club Casablanca

Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

Leave A Reply


Exit mobile version