Waswahili wametembea wakakaa na kutuambia kuwa “Mkaa bure siyo sawa na mtembea bure” ila hawakuishia hapo wakatuongezea kuwa “Mpambanaji hachoki na akichoka basi wakati wa kufa umefika” ni kutoka Kaskazini mwa Afrika yenye ukanda wa pwani ya Mediterania na sehemu ya ndani ya jangwa la Sahara.
Ni nchi ambayo ina Milki nyingi za urithi ikiwemo magofu ya kale ya Kirumi katika Tipaza ya bahari. Amezaliwa miaka 60 iliyopita katika eneo la El Djazair huko Algeria ni muhumini wa kutumia zaidi 4-2-3-1 maisha yake Ya soka amekuwa akifundisha vilabu vya Kaskazini mwa Bara ili la Afrika Morocco na Nyumbani Algeria, maisha yake Ya ukocha alikuwa akiyatekeleza huko na sasa kwa Mara Ya kwanza anatoka nje Ya kanda hiyo na kutua Mashariki mwa Afrika ni Abdelhak Benchikha wa Simba SC
Ikiwa ni saa chache kwakeakishuhudia timu yake ikiipoteza mchezo wa wa pili na wa kwanza akiwa kama Kocha mkuu wa kikosi hicho kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kwenye Ligi kuu ya NBC, anaondoka nchini kuelekea kwao Algeria na kukiacha kikosi kwa Kocha msaidizi, Abdelhak Benchikha tokea amepokea kikosi cha Simba SC ameonyesha natumaini makubwa kwa kukibadilisha kwenye maeneo mengi sana kiwanjani.
Abdelhak Benchikha ameibadilisha kwa kuongeza hali ya upambanaji kwa wachezaji wa timu hiyo kwani tokea amepokea kikosi hicho wachezaji wa Simba SC waneonekana kujitoa kikosini na kukimbia eneo kubwa la uwanja jambo ambalo lilikosekana mwanzoni mwa Msimu, pia amewapa nafasi wachezaji wengi kikosini kuonyesha kile alichonacho kikosini jambo ambalo ni silaha sahihi kwa Kocha kuwa na imani na wachezaji anaowafundisha na kuwamini wanaweza kufanya kitu ndani Ya timu hiyo
Ni muhumini wa mfumo wa 4-2-3-1 akitumia zaidi viungo wengi kikosini na hususa viungo wakabaji na hiyo ameionyesha ndani Ya kikosi cha Simba SC, kukosekana kwake kwenye michezo miwili ya Ligi kuu ya NBC ni pengo kwa kiasi chake kwani amekuwa Kocha ambaye muda mwingi wa mchezo amekuwa mkali kwa wachezaji wake jambo ambalo limemfanya kuwakumbusha majukumu wachezaji wake wawapo kiwanjani na kuongeza hari Ya upambanaji. Pengo ilo kuna nafasi kubwa likaonekana ndani Ya michezo hiyo kwani makocha waliyobaki hawaonekani kuwa na sifa kama Ya Benchikha.
Upande wa kimbinu ni ngumu kubadilika kwani mfumo wa Kocha mkuu ndiyo mfumo mama unaotumika kikosini, namna Ya uchezaji na mbinu zitakazotumika nyingi hazitakuwa nje sana na namna kocha Benchikha atakavyokuwepo.
Zaidi ni kuwa moja Ya Sifa kubwa na Ya mafanikio kwa kocha yoyote yule ni uwezo wa kumudu chumba cha kubadilishia nguo “Dressing room” ilo ndiyo eneo pekee ambalo makocha wengi wanajitahidi kulimudu ikiwa ndiyo eneo mama zaidi la kutengeneza matokeo mazuri na hali ya kupambana kwa wachezaji wake na ilo linaonekana kuwepo kwa Benchikha tokea aanze kukinoa kikosi hicho.
SOMA ZAIDI: Azam na Simba Inawarahisishia Yanga Kuchukua Tena Ubingwa?
1 Comment
Pingback: Dube Unapoelekea Unakosea Ungekaa Kimya Tu - Kijiweni