Kuna wakati unaweza kujiuliza hivi mashabiki wanataka nini?Maana kila mmoja huwa na kauli zake endapo kutakua ni kipindi kuhusu jambo Fulani. Ukitazama kwasasa macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania ni michuano ya AFCON kwakua ligi kuu kwa uande wa wanaume hapa nyumbani haichezwi kupisha michuano hii.

Sababu kubwa inayowafanya mashabiki wengi kutazama michuano hii ni kuitazama timu ya taifa ya Tanzania ambayo imejaa nyota kadhaa wanaocheza ndani na je ya Tanzania huku wakiongozwa na kapteni Mbwana Ally Samatta ambaye anakipiga katika ligi kuu ya Ugiriki katika kikosi cha PAOK.

Siku zote ambazo Taifa Stars wamekua wakicheza katika mechi za kufuzu au zile za kalenda ya FIFA kumekua na wimbi kubwa la mashabiki ambao wamekua wakimbeza Samatta wakihoji anacheza chini ya kiwango, hii si sawa na inatufanya tuamini kuwa moyoni tuna mashabiki wa mpira ila sio wapenzi wa mpira kwani hawatazami athari za mtu akiwa ndani ya uwanja au pale anapokua hayupo ndani ya Uwanja.

Kuna tofauti kubwa sana ipo kati ya kucheza ndani ya nchi na kucheza nje ya nchi haswa katika ligi kubwa barani Ulaya kuanzia miundombinu ya kimichezo mpaka kucheza na wachezaji ambao wanajua njia halisi za kupeleka mpira na sio kucheza ilimradi kuwafurahisha watu tu.

Kwanza kabisa Kapteni Samatta amekua ni moja kati ya wachezaji ambao wana rekodi nzuri barani Ulaya katika ligi mbalimbali ambazo amekua akicheza kutokana na uwepo wa viungo wazuri wanaomchezesha hivyo kucheza vizuri zaidi sasa tazama aina ya viungo tulionao na angalia vibanda umiza maneno yanavyokua.

Kwa viungo wetu wa Tanzania matusi kwa captain Diego bado yatakuwa mengi sana kutoka kwa watu wasiojua football na uchezaji wa Tanzania upande wa viungo hata ungekuwa na Haaland bado tusingepata hata goli la offside kwa mechi moja pekee ya AFCON tuliyocheza mpaka sasa.

Timu inacheza nyuma sana timu inakosa kucheza kimbinu muda wote tupo nyuma tu unategemea kushida au kufunga goli gani kama mpira wanacheza kipa na mabeki.

Nawashangaa sana wanaombeza Samatta kuwa anacheza hovyo nawakumbusha tu tusiwe watu wa maneno mengi timu yetu katikati kwenye viungo wa kushambulia bado sana na sioni sababu ya Feisal kuanzia nje kama timu nzima viungo wanacheza nyuma kushambulia tunashindwa.

Nitaendelea kusimama na captain Diego wewe ndo kiongozi wetu katika aya mapambano ila kocha tunaomba tatua tatizo la viungo wetu bado tuna nafasi ya kusonga mbele

SOMA ZAIDI: Huu Ni Wakati Sahihi Wa Kuruhusu Uraia Pacha Taifa Stars 

1 Comment

  1. Pingback: Kadi Nyekundu Kwa Novatus Ni Njia Ya Kujifunza Kwetu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version