Ni wazi kuwa klabu ya Yanga imetimiza miaka 89 tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni moja kati ya klabu kongwe nchini Tanzania ambayo makazi yake ni mitaa ya Jangwani zilipo ofisi za kiutendaji za klabu hii.

Ukiachilia mbali kuwa na jengo ambalo limemebeba historia kubwa ya klabu hiyo lakini pia kuna uwanja wao unaoitwa uwanja wa Kaunda ambao umekua ukikumbwa na changamoto ya mafuriko mara kadhaa kunapokua kunatokea mafuriko na jitihada mbalimbali zikafanyika kuweka vifusi ili kuwe juu na kwa hilo wakafanikiwa.

Naweza kusema moja kati ya kilio kikubwa cha mashabiki na wanachama wat imu hii kubwa ni kuhusiana na uwepo wa uwanja wao ambao wao wanatamani ujengwe palepale Jangwani zilipo karibu na ofisi za timu hiyo na sio mara moja kusikia viongozi mbalimbali wa klabu ya yanga wakizungumza kuhusiana kujengwa kwa uwanja huu.

Wakati wa sherehe za kutimiza miaka 89 ya klabu ya Yanga kulikua na taarifa kuhusiana na kuwa mdhamini na mfadhili wa klabu ya Yanga, Gharib Said Mohammed (GSM) ameridhia kujenga uwanja katika eneo la makao makuu ya klabu hiyo Jangwani Dar es Salaam taarifa ambayo ilitolewa na Rais wa Yanga, Hersi Said na kusema kuwa uongozi wa Yanga upo tayari kumpa ushirikiano GSM katika mchakato wote wa ujenzi wa uwanja huo.

Tumeona namna ambavyo viongozi mbalimbali waliopita Yanga wakizungumza kuhusu ujenzi wa uwanja huo na kushindwa kutekeleza jukumu hili kubwa zaidi ambalo bila shaka kwa ambaye atafanikiwa kulitimiza katika uongozi wa klabu hii ataacha historia kubwa sana katika maisha ya soka ya klabu hii huku siasa za mpira zikitawala zaidi.

Kwenu viongozi wa Yanga tumeona hatua zenu mbalimbali mlizoamua kuzichukua kuhusu klabu hii lakini ni wakati sasa wa kuthibitisha kuwa ni kitu ambacho kinawezekana na kinaweza kufanywa na nyie kuwa wa kwanza kuonesha mmeamua kukifanya nacho ni kuwa na uwanja wenu rasmi mtakaoutumia katia mechi zenu.

SOMA ZAIDI : Ahsante John Bocco Umeiona Fursa Kwa Soka La Tanzania

1 Comment

  1. Pingback: Wachezaji Hatari Wa Kuchungwa Ligi Kuu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version