Nitakuwa tofauti na wengi wanavyoweza kufikiri kwenye hili na hii ni kutokana na kila mtu anavyoweza kutazama haswa kuhusiana na safari ya Jean Baleke na klabu ya Simba.

Kwanza ni kweli Simba iko katika nyakati ngumu ambazo kwa shabiki yoyote ni ngumu kuweza kuvumilia lakini pia kwa upande wa timu kiujumla namna inavyoonesha uchache wa hali ya utendaji kiwanjani, lakini je ni sawa?

Simba ina performance isioridhisha lakini yapo baadhi ya mabadiliko ambayo yakifanywa ndani ya kikosi unaona ni lazima lakini mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini fyekeo lililopita kwa Jean Baleke lilikuwa ni sahihi, SIFIKIRIII HIVYO

Ni sawa na ishu ya Cristiano wakati anaondoshwa ndani ya kikosi cha Man united kabla ya kuondoka kwake yeye ndiye mchezaji pekee aliekuwa kinara wa upachikaji mabao kikosini alimaliza msimu kwa mabao 18 msimu kabla hajaondoka, mabao mengi kuliko mchezaji mwingine ambae ungeweza kumtazama.

Ni kweli, Baleke alikuwa ni mchezaji ambae anakosa nafasi nyingi kiwanjani lakini tayari ameshakupa goli 8 kikosini ndani ya duru la kwanza la ligi hujui kipi angekupa ndani ya mzunguko wa pili??? Turudi tena kwani washambuliaji wa ndani ya ligi yetu humaliza msimu kwa jumla ya mabao mangapi??? (16/17/18) Je Baleke asingeweza kufika hapa??? Au ni kwasababu hakupi goli kwenye mechi za lazima??

Sababu ipi ya msingi inamfanya watu waone kama anapaswa kukatwa kwasababu anakosa sana nafasi??? Je vipi anaekuja??? Ni sawa kukataa pesa ulonayo mkononi kwa matarajio ya pesa ya kubashiri???

Upande wangu sifikirii kama Baleke alipaswa kukatwa, wapo wachezaji wengi ambao wanabaki ndani ya timu nyingi kwa mchango mdogo sana wanaotoa katika timu lakini bado wakapewa nafasi kuendelea kubaki na kupewa imani ya kuwa watakaa sawa.

Baleke alistahili nafasi ya kubaki ndani ya kikosi cha Simba kwani bado naamini ni mshambuliaji mzuri na alipaswa kukaa walau benchi kusubiri hao wanaokuja kuona watatoa kipi lakini sio kukatwa kabisa. Kwangu bado ni mshambuliaji mzuri aliehitajika kuongezewa kujiamini.

Endelea kusoma makala mbalimbali kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version