Kote duniani biashara ya mpira ndivyo ilivyo mchezaji ni kama mfanya biashara tu siku bidhaa yake ikiwa poa ndio nyakati ambayo hua anatafuta mteja ambaye ataifikia gharama ya bei yake.

Kinachoendelea hivi sasa kwa mchezaji Stephanie Aziz Ki ni yeye kutoongeza mkataba MPYA ndani ya Yanga SC, siyo habari nzuri sana kuzisikia kutoka klabuni hapo na mchezaji wao. Aziz ni moyo wa timu kwasasa hilo halina ubishi, mabao yake mengi yaliifanya Yanga kufikia baadhi ya malengo ya Klabu.

Boss anakuna kichwa kuhusu wino mpya wa mfanyakazi wake, ni wakati mgumu kwake kwani anafahamu namna alivyowahi kuinasa saini hiyo hakuwa kazi rahisi kuipata vita ilikuwa tena dhidi ya Mtani wao Simba SC. Leo linapokuja jambo kama hili mchezaji anapata kigugumuzi cha kuongeza mkataba wala hatupaswi kuanza kumshangaa mchezaji, tumuelewe kuwa hii ndio kazi yake, hayo ni maisha yake kaja Tanzania kutengeza kipato.

Inaarifiwa kuwa STEPHEN AZIZ KI ana ofa mbili kutoka Al Ahly na Orlando Pirates, amewapa Yanga unafuu wa offer ili aweze kusaini kwao na mahitaji yake kutoka kwa vyanzo vyangu anahitaji kiasi cha dola 500,000 ili aweze kusaini ikiwa ni sawa na BILLION 1.2 za Kitanzania.

Mpaka hivi sasa Wananchi hawana kiasi hicho na klabu kwa mujibu wa vyanzo imejipiga mpaka Dola 350,000 za Kimarekani wapo tayari kumpa ila Aziz ameshikilia zifike 500,000 ili asaini, jitihada zinaendelea ila kinachohitajika ni huo mzigo.

Mpaka hivi sasa Aziz hajasaini KARATASI yoyote ndani ya Jangwani.

Kinachobaki kwenye timu na klabuni milele ni Mwanachama na Shabiki pekee yao, wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Viongozi wa timu hua siyo watu wa kudumu kwaiyo tukiyajua hayo wala hatuingii kwenye kumshangaa mchezaji. Ikitokea wameelewana katika ya boss na mchezaji ili aendelee kusalia, basi itakuwa poa sana na kama ikitokea imeshindikana ni kumtakia kheri mchezaji popote aendako.
Maoni Yako Ni Yapi? Tuambie Kwenye Comments

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

19 Comments

    • Akiondoka anaweza asipotee yeye Cha muhimu aangalie sehemu ambayo haitauwa kipaji chake aend kwenye timu itakayokuwa na combination nzuri Kama alionayo yanga hicho ndo Cha muhimu kwake asiangaloe mkwanja

    • Kuondoka kwa azizi ki kunaumiza sana mashabik lakin ndo utalatibu wa mchezaji, chakuzingatia yeye n kwamba akitoka yanga aendelee kupambana asishuke kiwango akawa namajin kama mayele

  1. star mwingne ata rise sabab tz kwanza huwa tunatamaduni ya promoshen then performance maana yake aende sababu ndiye anaelisha familia yake ila star mpya tutamuandaa kuanzia promo mpaka ajiamin na kuperform

  2. Hapo asijalibu kabisa maana yatamtokea kama luis mwisho wa siku kipaji chake kinapotea ni bora atulie tu

  3. Admin umeongea jambo muhimu sana siku zote kinachobaki milele kwenye timu ni mashabiki hivyo kama Aziz ki akiamua kuondoka kila la kheri 🙌🙌🙌

  4. Hii ni ajira kama ajira nyengine tuu ni wajibu kwake kuchagua kiasi anachokihitaji. Na inakubidi wewe ndo uridhike na pesa ambayo unaipata sehemu ulipoajiriwa. Familia inamuangalia yeye kama anaona anapoenda matunda ni mazuri zaid kuliko alipo ni kheri aende tuu. 🔜🔜

  5. Henderson Didas on

    Pesa ni muhimu kuliko vyote apo afate mahali kuna michongo mikubwa zaid .Maan izo timu zinamuhitaji ni timu kubwa mno ina maan atazidi kukuwa na kufahamika na kupata michongo mikubwa zaidi kuliko kubaki sehemu moja

  6. Some time life ndivyo ilivyo huwezi kupambana ukiwa sehem mmoja hii nikama challenge ya maish ya soka ilitokea kwawanasoka wengi tu so yot kwa yot tunamtakia Kila la kher

  7. Hakika kinachobaki kwenye klabu mpaka kifo ni sisi mashabiki, lakin wachezaji na staff nzima yaweza kubadilika Kila msimu, mwaka Jana waliondoka most important people who was the part of the team kama mayele, pro. Nabi na benchi lake la ufundi mpaka kocha wa viungo lakin still maisha yaliendelea, hivyo akisema bhana pesa anayopata haitoshi aende tunamtakia Kila lakheri ila kama ataamua kubaki tutazidi kumpenda.

  8. Yanga imekua chimbo Kwa wachezaji wenye juhudi haya ni maisha wamuache akapambane ili na sisi TUJITAFAKARI kama alivyoondoka mayele
    Wampe na baraka zooote

  9. Pingback: Funga Kazi Ligi Kuu Iko Hivi | Vita Ya Nafasi Ya Pili Na Kiatu

  10. Mi nashauli kwamba ackimbilie kwend all ahly maan wanatabia ya kupoteza vipaji vya wa2 weusi mfano Luis miqson so ni Bora akaze 2 hapo au kam vp aende hata simba sio mbaya

Leave A Reply


Exit mobile version