Ilipoishia jana ” Pili alifikia maamuzi ya kukubali kua Muuaji aliyapanga vizuri Mauaji hayo kwa maana aliweza
kufuta picha kadhaa kwenye Mboni ya Mzee Yusuf na kuacha moja ambayo haitoshi kutoa taswira halisi kua ni nani Muuaji? “
Tuendelee sasa
SEHEMU YA TATU (03)
Asubuhi ya siku ya Tatu baada ya kifo cha Mfanyabiashara Mzee Yusuf ambaye kifo chake kilianza kumsumbua Mpelelezi Daudi Mbaga, Ndani ya kijumba kidogo chenye hadhi kubwa huko nje kidogo ya Jiji la Dar-es-salaam, alionekana Mama Mmoja Mtu mzima aliyekua amekaa kwenye sofa akiitazama picha moja.
Mama huyo alikua amevalia miwani ya macho akiwa amejitanda vizuri kwa mtandio ulioendana na Baibui yake nyeusi, mlangoni akatokea Msichana mmoja mzuri, mwembamba, mweusi kidogo aliyebana vizuri nywele zake, hakua mrefu wala mfupi. Alikua amevalia Baibui nyeusi pia kama Mama huyo, alisogea kisha akamwambia Mama huyo
“Twende Mama” alisema akiwa anajiweka vizuri, kisha alichezea simu yake na kupiga mahali
“Beka tupo tayari” alipomaliza kuongea na simu alimrudia Mama yake ambaye alikua bize kuitazama
picha hiyo, picha hiyo ilikua ikimwonesha Mzee Yusuf
“Mama, Beka anakuja kutukuchukua. Ni vyena tukawahi” alisema Msichana huyo.
“Martha, kifo cha huyu Yusuf kimeniuhuzunisha sana. Natamani polisi wamjuwe kwa haraka Mtu aliyesababisha kifo chake.”
“Ni mipango ya Mungu Mama, kila jambo lina wakati sahihi, ukifika wakati wa kumpata Muuwaji basi Muuwaji atakamatwa tu” alisema Martha.
Basi, Martha na Mama yake waliokua wakiishi Bunju walitoka nje ya nyumba hiyo na kukuta Tax ikiwa imefika, wakapanda Tax na kuanza safari yao.
Safari yao iliishia nje ya Msikiti wa Maamur Upanga ambako ibada ya Mazishi ya Mzee Yusuf ilikua ikifanyika, Daudi Mbaga aliruhusu Maiti ya Mzee Yusuf iweze kuzikwa baada ya kukamilisha taratibu za kipelelezi, majira ya saa saba Mchana Magari yaliekea Makaburi ya Kinondoni kisha mazishi ya Mzee Yusuf yalifanyika. Martha na Mama yake waliongozana na familia ya wafiwa kurudi nyumbani kwa Mzee Yusuf.
Ndugu wachache walibakia kuomboleza, Martha alimfuata Sofia na kumpoza machungu hayo ya
kufiwa, walikua wakifahamiana sababu familia zao zilikua na urafiki yaani Family Friend.
“Inauma Martha, Baba alikua muhimu sana na nguzo muhimu ya Familia hii. Kifo chake ni pengo na mzigo mzito kwetu, hatujui hata tunaanzaje bila yeye” alisema Sofia akiwa ameketi kwenye kiti,
Martha alimuonea huruma sana Sofia
“Najua inaumiza kiasi gani lakini kua jasiri kwa ajili ya Binti yako Adela”
“Asante sana Mdogo wangu Martha, kiukweli napaswa kujikaza sana” Mama yake Martha naye
alikua akizungumza na baadhi ya ndugu wa Mzee Yusuf ambao walikua katika Majonzi mazito, muda huo huo Salma aliingia akitokea Uingereza.
Aliangusha kilio ambacho kwa upande wa Sofia alikiona ni kilio cha kinafiki sana, hakujali bali aliingia ndani na kuwaacha watu wengine wakimpa pole Salma. Kabla Salma hajaondoka kuelekea Uingereza palikua na mgogoro mdogo kati yake na Mzee Yusuf, alipofika ndani Sofia alinyanyua simuna kumpigia Mpelelezi Daudi Mbaga kua Salma amerejea na wanapaswa kumhoji ili aseme mgogoro wao ulikua unahusu nini na huenda Mgogoro huo ukawa ndiyo chanzo cha Mauwaji hayo yaliyojaa Utata.
Mara moja polisi walifika hapo wakiwa wametumwa na Daudi Mbaga, walimtia nguvuni Salma hali iliyozua taharuki kwa wengi.
“Jamani kuna nini?” aliuliza Hamza ambaye ni Kaka wa Sofia, Mtoto wa kwanza wa Mzee Yusuf.
“Tumepigiwa simu kuwa kabla ya kifo cha Mzee Yusuf palikua na ugomvi baina ya Salma na Mzee Yusuf hivyo tunamchukua ili tukamhoji, atarudi” alisema mmoja wa askari hao waliotumwa kumkamata Salma.
Macho ya Salma aliyatupa Mlangoni akamwona Sofia akiwa katika pozi ambalo lilimwonesha wazi kuwa aliyepiga simu hiyo alikua ni Yeye, akamsogelea na kumwambia
“You will pay for this ( Utalipia kwa hili)” alisema kwa hasira kiasi kwamba kila aliyeko hapo
alitambua msuguano mzito uliopo baina ya Sofia na Mama yake Mdogo Salma.
Aliingizwa kwenye ndinga ya Polisi na kupelekwa moja kwa moja Ostabey, alikutana kwa mara ya kwanza na mpelelezi Daudi Mbaga
“Unaitwa Salma si ndiyo?” aliuliza Daudi wakiwa chumba cha Mahojiano
“Ndiyo”
“Inasemekana kua wewe na Mzee Yusuf Mliingia kwenye ugomvi mdogo siku chache kabla ya kifo chake, ukaondoka kuelekea Uingereza” alisema Daudi akionekana kua Mtu makini sana
“Ndiyo” alijibu Salma
“Kwanini mligombana?”
“Alihisi nina Mwanaume mwingine nje ya Nchi, hakutaka niende Uingereza. Nami sikua tayari kwa hilo”
“Ni kweli ulikua na Mwanaume huko na ulikua ukichukua mali za Mzee Yusuf taratibu?”
“Hapana, sijawahi kumsaliti Mume wangu hata mara moja”
“Kifo chake kimegubikwa na fumbo zito la Nani amemuuwa, nikisema unahusika ninaweza kua nipo
sawa?”
“Kamwe siwezi kutenda unyama kwa Mume wangu, hata kama angelikua Mtu baki nisingeliweza kukatisha Maisha yake. Mzee Yusuf alisaidia Maisha yangu nikiwa nimepoteza dira ya Maisha, akanisaidia na kubadilisha Maisha yangu, siwezi kumlipa kwa unyama hata kidogo” alisema Salma huku akidondosha chozi, hata sauti yake ilijaa kilio. Basi Mbaga akampatia kitambaa Salma afute chozi lake kisha akamwambia
“Kwasasa nenda kaomboleze lakini nitakuhitaji tena hapa” Salma akanyanyuka na kuondoka.
Haraka Salma alichukua Taxi akarejea nyumbani kwake, alikuta bado ndugu wapo wakimsubiria maana alishapiga simu kua ameachiwa huru.
Kumuachia huru SALMA ni kosa kubwa ambalo Ajenti Mbaga amelifanya unajua kwanini? USIKOSE SEHEMU YA 4
KAMA ULIPITWA:
18 Comments
Hahahah nimependa itimisho apo
Kesho tena
🔥🔥🔥🔥
Part 4 mbna fupi iv duuuuh inanoga snaaa👍👍👍
Hata mimi nimeona fupi jaman😔iwe kama part 2 kidogo ndefu
Ni moto kabisa
Hata mimi nimeona fupi jaman😔iwe kama part 2 kidogo ndefu
Fupi tam
Nzur sana
Good mwandishi una kiu na Kalamu ila wasomaji tuna kiu na Maandishi yako jitahidi uongeze kidogo paragraph ya Leo fupi sana
🔥🔥🔥can’t wait part 4😂
Salma kwenye ubora wake kama namuona 😅😅
Dah! Imekuwa na paragraph fupi Sana Leo tofaut nazingne,,kesho mapema sana
Naomba jmn part 4 iwe ndefuu kama part two
nice story
Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tatu) KOTI JEUSI – 13 - Kijiweni
Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tatu) KOTI JEUSI – 14 - Kijiweni
Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tano) KOTI JEUSI – 15 - Kijiweni