Ilipoishia “Jambo hilo lilimwacha Sofia akiwa mwenye tabasamu sana, kwa namna alivyokua na chuki za wazi kwa Salma asingeliweza kukubali Mali hizo zisimamiwe na Salma ambaye ndiye Mama yao Mdogo, kifo cha Salma kilijaza Tabasamu kwa Sofia, tabasamu lililoonekana waziwazi kabisa.  “

Tuendelee
SEHEMU YA 06 

 

( Miaka kadhaa iliyopita) 

Sauti ya Mtoto Mchanga ilisikika kutoka katika kitanda alicholala Mama mmoja aliyechoka, alikua akitabasamu huku akikitazama Kichanga kilichozaliwa masaa kadhaa yaliyopita kwenye maegesho ya magari ya hospitali hiyo, palikua na gari moja aina ya Benz iliyokua imeegeshwa, mara moja Injini yake ilizimwa.

Alishuka Bwana Mmoja tajiri sana, alikua na haraka ya kuelekea wodini kumwona Mtoto aliyezaliwa, Bwana huyu ndiye ambaye Sasa kifo chake kinawasumbua Wapelelezi. Anaitwa Yusuf Balun

Alifika wodini na kumwona Mtoto aliyezaliwa, tabasamu lilikua juu alipogundua kua Mtoto huyo 

alikua wa kike, pale pale akampa jina la Sofia, jina ambalo alilichukua kutoka kwa marehemu Mama yake.

“Kila mara nimwonapo nitakua namkumbuka Mama yangu” alisema Mzee Yusuf akiwa amembeba Mtoto Sofia aliyezaliwa masaa kadhaa yaliyopita. Kando yao alikuwepo Mtoto mwingine, huyu alikua ni Hamza.

Mtoto wa kwanza wa Bilionea Yusuf, Mapenzi ambayo aliyaona kwa mara ya kwanza kutoka kwa Baba yake kwenda kwa Mdogo wake yalimfanya akasirike na kuondoka kabisa pale wodini. Kadili alivyozidi kukua ndivyo alivyozidi kua na chuki na Mdogo wake Sofia, alionesha chuki za Wazi wazi hadi ikawa shida kwa Mzee Yusuf.

Siku moja alimchukua Hamza na kumpeleka kwa daktari wa Saikolojia, kwani mwanzo waliamini huwenda ni wivu wa kawaida ambao Mtoto wa kwanza hua nao pale anapozaliwa Mtoto mwingine, lakini Dokta huyo alipomwona tu Hamza aligundua ana tatizo kubwa zaidi ya wivu hivyo akamshauri 

Mzee Yusuf amtenganishe Hamza na Sofia kwa muda mrefu, pia aongeze mapenzi kwa Hamza

Baada ya kumaliza walitoka kwa Daktari, nje walikutana na Mtoto mmoja mdogo mwenye makamo ya chini zaidi ya Hamza na Sofia, Binti huyu ndiye sasa anajulikana kama Martha, Hamza alitokea kumpenda Mtoto huyo akamwambia Baba yake wamchukue

Mzee Yusuf alicheka kidogo akamwambia Hamza

“Huyu ni Mtoto wa watu, hatuwezi kumchukua kama Bidhaa mwanangu” alisema, mara muda huo huo alifika Baba yake Martha, alipomwona Mzee Yusuf alimtambua kwani ni mfanyabiashra Mkubwa sana Tanzania.

Kuanzia hapo Mzee Yusuf na Baba yake Martha walianza kufahamiana, wakawa marafiki wazuri 

sababu Hamza alimpenda sana Martha hata ule wivu kwa mdogo wake uliondoka wenyewe. 

Miaka mitatu ya kufahamiana walitengeneza undugu, baadaye Baba yake Martha alikufa kwa ajali ya gari akiwa anatoka kazini kwa Mzee Yusuf, kuanzia siku hiyo Martha alilelewa na MzeeYusufu hadi alipokua na Umri mkubwa.

( Turudi Maisha ya sasa )

Hamza alitambulishwa kwenye kampuni kama Mkurugenzi mpya baada ya kifo cha Mzee Yusuf, 

alimtoa Dada yake kwenye kitengo cha kusimamia wafanyakazi wote wa Kampuni, nafasi ya Salma ikajazwa na Sofia. Maisha mapya ndani ya kampuni yalianza ili kukuza kampuni iliyoachwa na Baba yao, sehemu ndogo ya Mali walipewa ndugu wa Salma kama mirathi.

Siku moja Sofia na Hamza waliomba kuonana na Mpelelezi Daudi, ilikua ni miezi mitatu baada ya 

wapelelezi kushindwa kumpata Muuwaji, wakakutana Johari Rotana. Katika mazungumzo yao, Sofia na Hamza walimuomba Mpelelezi Daudi aifunge kesi ya kifo cha Baba yao kwani waliamini wapo salama na pasingetokea Mauwaji mengine.

Uamuzi huo ulikuja baada ya mashauriano kati ya Mtu na Dada yake na wakakubaliana kuifunga kesi hiyo iliyoonekana kukosa Mashiko kwani kwa zaidi ya miezi mitatu hapakua na dalili yoyote ya kumjua Muuwaji, licha ya uamuzi huo kutoka kwa ndugu hao hata Mpelelezi Daudi na jopo lake waliona kesi hiyo inawaelemea kwa namna ilivyokua inaenda.

Kesi iliondoa ufanisi wa Daudi kama mpelelezi, muda ulienda bila kupatikana kwa Muuwaji 

kuliashiria kuwa wapelelezi wameshindwa kumnasa Muuwaji, kila taarifa iliwachanganya na 

kuwapoteza kabisa. Moyoni Daudi hakuacha kuhisi kuwa Muuwaji anatoka kwenye familia ya Mzee Yusuf, yaani hapa alihisi atakua mmoja kati ya Martha na Sofia lakini kadili alivyowachunguza hapakua na dalili yoyote kua Sofia au Martha wana viashiria vya Uharifu kwani hata simu zao walikua wakizungumza mambo ya kawaida tu.

Japo alikubali kuifunga kesi lakini moyoni alijua ipo siku kesi hiyo itapata tena uhai na itarudi kwa kasi. 

“Nawatakia Maisha ya Amani, utulivu. Kwa chochote kitakachojili nitawajuza na nyie pia msisite kunieleza, hisia zangu bado zinaniambia kua Muuwaji atarudi tena” alisema Mpelelezi Daudi kisha akapiga unywaji

“Tutaonesha ushirikiano kwa lolote tutakujuza, kama ulivyosema kufunga kesi haina maana tutaacha kuwasiliana” alisema Hamza, nyuso za ndugu hawa wawili zilionekana kua na nuru kubwa sana ya furaha, nuru iliyoonesha kuanza Maisha mapya na kukubali uhalisia kua Mzee Yusuf amefariki, japo Muuwaji hakupatikana lakini walitabasamu.

Saa sita Usiku, fax moja iliingia kwenye jumba la Mpelelezi Daudi. Fax hiyo ilitoka Makao makuu ya polisi, alipoifungua aliona palikua na uhamisho wake kutoka Dar-es-salaam kuelekea Uvinza Kigoma. 

Alijulishwa kua huko ataenda kupeleleza kuhusu Uingiaji na utokaji wa Watu katika Mji huo kuelekea nje ya Nchi bila kufuata utaratibu.

Kazi ya upolisi ni kazi ambayo imejikita zaidi katika amri, Daudi alikubali kuhama Dar huku moyoni akiwa na maumivu makali ya kushindwa kesi ya kumnasa Muuwaji wa Mzee Yusuf, aliamini uhamisho huo umekuja baada ya kushindwa kwake kwa kesi, alijawa na hasira sana akachukua Pombe kali na kuigida.

Asubuhi, aliwahi makao makuu, alipewa kila kitu kuhusu kazi mpya ya Mkoani Kigoma katika Mji wa 

Uvinza. Aliondoka ofisini kwa Mkuu wake akiwa anajisonya na kujitukana, taarifa ya kuhama kwake ilitangazwa na vyombo vya habari ambavyo vingi vilihoji kuhusu kesi ya Mzee Yusuf na Marehemu Salma.

Jeshi la polisi likaingia kwenye dosari ya kushindwa kwa kesi hiyo, Mkuu aliyemhamisha Mpelelezi Daudi ambaye ni IGP Saimoni Kuga aliamua kuihamisha kesi hiyo kutoka kwa Polisi wapelelezi hadi ofisi ya Majasusi wabobevu. Alifanya hivyo ili kukwepa aibu ya kushindwa kwa kesi ya Mauwaji ya Mzee Yusuf na Mke wake Salma, vifo vilivyoitingisha Tanzania lakini viliishia kuchunguzwa na kutolewa ufafanuzi wa kawaida tu.

Sasa Jalada la kesi limefika mikononi mwa Malcom maarufu kama Agent X ambaye ametoka 

mafunzoni Nchini Misri chini ya kitengo kidogo cha Majasusi kutoka Katika kitengo cha Kijasusi cha Nchini Israel kinachoitwa Mossad. Alipelekwa masomoni baada ya kuingizwa kwemye mfumo wa Majasusi ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuisaidia Tanzania kupambana na Rais na Deusi ambao walidhamiria kuisambaratisha kariakoo kwa Bomu

xxx

Kurudi kwa Muuwaji 

Alfajiri moja iliyojaa Baridi kali sana, haikua kawaida Jiji la Dar-es-salaam kukabiliwa na hali hii tena katikati ya Mwaka. Japo palikua na Baridi lakini ilionekana kua hali nzuri kwao, wapo waliovalia makoti kuelekea kwenye mihangaiko yao. Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ulikua ukipokea ugeni

Ndege Mpya aina ya Boeng ilikua ikishusha abiria wachache waliofanya safari kutoka Misri, miongoni mwao alikua ni Jasusi Malcom. Kutokana na kazi nzito aliyoifanya, Serikali ya Tanzania chini ya Rais Mpya David Chota ilifanya maamuzi ya kuibadilisha sura ya Malcom ambaye alikua maarufu sana baada ya ule Mkasa mzito wa kuikomboa Tanzania juu ya Shambulio la Bomu na Ugaidi uliotaka kufanywa na Watu kutoka Urusi wakiongozwa na Deusi na Rais wa Tanzania kwa wakati huo.

Malcom alishuka akiwa na mwonekano mwingine kabisa, hata jina lake lilibadilishwa akawa anaitwa Agent Marcus. Serikali ilifanya hivi ili kumlinda na Maadui ambao waliamini wangerejea tena Tanzania baada ya jaribio la kwanza kufeli.

Malcom ambaye sasa tunamtaja kama Agent Marcus alipanda Tax kama abiria wa kawaida huku 

akiliangalia eneo ambalo ndege ilidondoka Usiku ule wa kutisha

Alifika makao makuu ya idara ya Ujasusi Tanzania, akampatia pesa yule dereva wa Tax 

“Asante, karibu Tanzania” alisema yule dereva akiamini Marcus si Raia wa Tanzania hasa 

alijitambulisha kua ni Raia wa Kenya, Marcus alirejea akiwa mwenye ujuzi wa kufanya upelelezi wa kesi kuliko kawaida.

Alioneshwa Ofisi yake. Lakini kabla hajaondoka hapo aliambiwa kuna Ujumbe kutoka kwa IGP 

Saimon Kuga, faili la kesi ya Bilionea Mzee Yusuf ikawekwa mbele ya Macho ya Jasusi huyu 

aliyebadilisha sura na utambulisho wa jina.

“Kazi yako hii kutoka kwa IGP Saimon Kuga. Nakutakia Mafanikio Agent Marcus” alisema Askari wa kitengo aliyekua akimwonesha Marcus ofisi alimpatia funguo ya gari na nyumba

“Ramani ya unapoishi imeshatumwa kwenye simu yako” alisema Askari huyo, akapiga saluti kisha akaondoka. Marcus akalitia faili hilo kwenye begi lake dogo kisha alielekea maegesho ya magari, akakutana na Kulger nyeusi, akatabasamu kwa maana anazijua gari hizo namna zilivyo nyepesi

Alipotekenya mara moja alianza safari ya kuifuata ramani ili afike anapotakiwa kuishi, Mfumo wa Majasusi ulibadilishwa sana baada ya usaliti uliofanywa na Majasusi ambao waliungana na Rais kufanya Ugaidi, sasa palikua na siri nzito sana na ilikua ngumu kuwajua Majasusi.

Marcus alifika mbele ya nyumba moja iliyopo Tabata Kinyerezi, alifurahishwa na namna nyumba hiyo ilivyoandaliwa, chumba chake cha kazi kilikua kimeshaandaliwa vyema, vifaa vyote vilikua humo, aliketi kwenye kiti akijizungusha.

***

Chuo kikuu cha Dar-es-salaam maarufu kama UDSM ilikutwa mchoro mmoja uliowaacha wengi 

kwenye Mataa, Mchoro ulikutwa kwenye meza moja wakati Wanachuo wapya wakiwa wanafanya Usafi humo. Aliyeuona mchoro huo alikua na Msichana mmoja, aliwaita baadhi ya wanachuo wapya watatu ambao alikua nao karibu. 

Wote walipoutazama mchoro huo waliogopa sana, wakamshauri Msichana huyo anayeitwa Riyama aupeleke Mchoro ofisini kwa Mkuu wa chuo. Naye alifanya hivyo, Mkuu wa Chuo aliukagua mchoro huo ambao naye ulimuogopesha sana. Haraka Mkuu huyo alipiga simu polisi, mara moja Polisi walifika hapo ili kuuangalia Mchoro huo uliowatisha Wanachuo hata Mkuu wa chuo.

Polisi nao walistaajabu sana kuhusu mchoro huo ulioelezea Mauwaji, Polisi wakauliza mchoro huo umekutwa wapi, Riyama akawaambia.

Polisi mara moja wakaelekea darasani, wakaliona eneo hilo ambalo alikua akikaa Mwanachuo 

mmoja wa kiume anayeitwa Michael Jomo, mara moja waliomba taarifa za Kijana huyo aliyekua 

akisomea masuala ya Sanaa katika Chuo hicho, Mkuu wa chuo akawapa na kuwathibitishia kua 

Michael alikua mchoraji mzuri sana ambaye Chuo hicho kilikua kilimtegemea kwenye Uchoraji, 

aliweza kumchora Mtu na kumtoa kama alivyo kama vile alikua amepigwa picha.

Picha hiyo ikafikishwa polisi, ikasambazwa kwa Polisi walio Dar-es-salaam, cha ajabu picha hiyo ilifanana vile vile na kifo cha Mzee Yusuf, namna alivyokua amekufa akiwa amelalia meza, kisu mgongoni na vyote vilivyomo eneo la tukio. Picha hiyo ikazua mjadala mkubwa, mara moja 

Mwanachuo Michael akaanza kusakwa na Mamlaka huku akihusishwa sasa moja kwa moja na kifo cha Mzee yusuf, kesi ya upelelezi ikaibuka upya.

Picha hiyo ikamfikia Mpelelezi Marcus, jasusi ambaye ndiye amekabidhiwa kesi hiyo. Hapo sasa 

akalivalia njuga jambo hilo, kwanza akataka kuisoma ripoti iliyoachwa na Mpelelezi Daudi Mbaga aliyehamishiwa Uvinza Kigoma.

Akaisoma kwa makini sana pia akazitazama picha za eneo la tukio, hata yeye akasadiki hivyo kua Mchoraji alilichora eneo la tukio, lakini swali la Msingi kumjia alijiuliza Kijana huyo alikua Nani hasa hadi akafika eneo la tukio na kuchora picha ya Mauwaji.

Polisi walifanikiwa kufika nyumbani kwao Kijana Michael Jomo, alikua akiishi Ukonga Banana, alikua akiishi na Mama yake Mzee na paka wao ambaye baada ya mahojiano mafupi na Mama yake Michael aliwaambia jina la Paka huyo kua anaitwa Michael Junior, jambo hilo liliwafanya polisi waone kua Kijana hakua wa kawaida.

Kwa maelezo ya Mama yake Michael aliwaambia Polisi kua Kijana wake alikua akiishi kwa hofu sana kwa zaidi ya Miezi miwili, siku moja aliwahi kumwambia Mama yake kua kuna ndoto anaiota anaogopa sana, Michael alimweleza Mama yake kua anamwota Mwanamke Mmoja akifanya Mauwaji ya Kutisha.

Akili za Polisi zilisisimka baada ya kusikia hivyo

“Yuko wapi Michael?” Mama yake Michael alinywea baada ya kuulizwa swali hilo, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akawaonesha mlango wa chumba kimoja chenye herufi kubwa Mlango iliyoandikwa ‘J’ ikiwa ni kifupi cha jina JOMO

Polisi wakaenda hadi mlangoni na kugonga, walijibiwa na Ukimya. Wakajaribu kufungua lakini 

waligundua mlango ulifungwa kwa ndani, Polisi wakafikia makubaliano ya kuuvunja Mlango ili wampate Michael, wakati huo Jasusi Malcom ambaye anatambulika kama Marcus alikua kwenye gari akienda hapo nyumbani kwa Michael.

Walipouvunja mlango walistaajabu sana, macho yaliwatoka kwa Mshangao. Japo walikua Maaskari polisi lakini washika vichwa vyao na wengine walishika viuno vyao, waliona jambo la ajabu lenye kutisha na kusisimua sana.

Ni Jambo Gani? Usikose Sehemu Ya 07

Jiunge WhatsApp Channel Ya KIJIWENI Ili Kuwa Wa Kwanza Kupata Updates Za RIWAYA Hii Kwa Kubonyeza Hapa 

SOMA Uchambuzi Na Makala Mbalimbali Kwa Kubonyeza Hapa

 

 

 

 

18 Comments

    • 😂😂😂me nkaanza kuwaza wameripua kariakoo nmepotezana na mtu angu🤧🥱 ikapita miaka kadhaa nkaja onana nae anyway namii nkaanza kujitungia stor apo😂😂💔

Leave A Reply


Exit mobile version