UTANGULIZI
Ulikua ni Usiku mwingi, mvua kubwa ilikua ikinyesha ikisindikizwa na radi za hapa na pale,ndani ya kasri moja la kitajiri palionekana kua kimya sana huku upepo mkali ulikua ukipeperusha pazia za dirishani.
Kwenye kasri hili la kitajiri ndani ya chumba kimoja palikua na Binti mmoja wa Miaka 13 aliyeitwa Adela na alikua akijisomea Usiku huo, alikua amevalia pensi, tisheti na miwani yenye kumsaidia kuona vizuri.
Upepo ulimfanya aache kusoma ili akafunge mapazia ya chumbani kwake, akanyanyuka kisha
akasogea dirishani na kufunga na baada ya hapo akarudi ili aendelee na kujisomea, bahati mbaya akajigonga kwenye meza ndogo ambayo ilikua na glasi yenye Maji, glasi ikadondoka chini na kuvunjika
“Ooooh Mungu wangu, ni nini tena Jamani?” Alijisemea kisha akaokota vipande vya glasi,
akaufungua mlango ili akaviweke jikoni, taa zilikua zinawaka na kuzima kutokana na hali ya hewa ilivyokua mbaya Usiku huo, ilimpa wasiwasi akajitahidi kufanya haraka ili awahi kurejea chumbani.
Alipofika karibu na ngazi ya kushuka chini akahisi kama kuna Mtu ametoka kwenye moja ya chumba akiwa amevalia koti kubwa jeusi na kiatu kikubwa, hakufanikiwa kujua ni nani lakini kutokana na hali ya kuzima na kuwaka kwa taa alihisi labda ni wenge lake. Akajikuta anashindwa kushuka chini na kuweka vipande vya glasi chini kisha akakimbilia chumbani kwake.
Akafunga mlango huku hofu ikiwa inazidi kumshika kila alivyomkumbuka yule Mtu ambaye hakufanikiwa kuiona vizuri sura yake isipokua koti Jeusi na kiatu kikubwa.
Adela hakuhitaji tena kuendelea kusoma, akapanda kitandani kisha akajifunika shuka Gubi-gubi.
SEHEMU YA KWANZA (01)
Jiji la Dar-es-salaam lilikua tulivu Usiku huo, purukushani zilishakauka baada ya kufika saa 7 za usiku. Ndani ya jumba la kifahari la tajiri mmoja anayemiliki makampuni ya utengenezaji wa waini ya zabibu anayeitwa Mzee Yusuf palionekana kua na Mtu aliyekua akitembea kwenye korido, mwendo wake ulikua wa taratibu huku akionekana kua na shida kidogo ya kutembea.
Wakati anafika korido moja ya nyumba hiyo ya ghorofa alisikia mlango ukibamizwa kwa nguvu.
“Aaaaaaahh” aligugumia kwa kushtuka sana, akashusha pumzi zake kisha akashikilia gauni lake refu lililoonekana kumpa shida ya kutembea vizuri, Mtu huyo alikua ni Bibi ambaye ni Kijakazi wa muda mrefu wa Mzee Yusuf, alimchukulia Bibi huyo kama Mama yake Mzazi.
Bado umeme ulikua unasumbua kutokana na mvua iliyokua ikinyesha, Bibi huyo mwenye uzito
mkubwa alijiuliza “Adela alienda wapi?” alisimama akijipa maswali yasiyo na majibu, aliamua kusogea mbele. Upande wa kulia kwake palikua na chumba cha Mzee Yusuf ambaye alikua akiishi na Mke wake aliyeitwa Salma, Mwanamke huyo kwa kipindi hicho alikua amesafiri kuelekea Uingereza kusimamia moja ya biashara zao huko.
Mzee Yusuf baada ya kufiwa na Mke wake wa kwanza ndiyo alimuoa Mwanamke huyo wa miaka 39 tu, cha ajabu chumba cha Mzee Yusuf kilikua wazi Usiku huo, jambo lililompa maswali Mengi Bibi huyo aliyeitwa Bi Choro. Alisimama kwa kitambo kidogo hadi alipoamua kubadilisha maamuzi yake,
Sasa alikielekea chumba cha Mzee Yusuf kujua kwanini kipo wazi.
Taa zilikua zinawaka na kuzima, japo hiyo ilimpa hofu Bibi huyo lakini alihitaji kujua kwanini chumba cha bosi wake kipo wazi usiku wa manane na hapakuonekana dalili ya kuingia wala kutoka Mtu yeyote ndani ya chumba hicho. Akiwa ameshakaribia mlango alianza kuona michirizi ya damu mbichi ikichuruzika sakafuni kutoka ndani ya chumba cha Mzee Yusuf, hakusubiri kuona ni kitu gani kilichosababisha hali hiyo, Bi Choro alipiga kelele za kuomba Msaada.
Kelele hizo ziliwashtua baadhi ya watu waliokua wakiishi ndani ya Jumba hilo, mmoja wao alikua ni Binti wa Mzee Yusuf aliyemwamini sana aliyeitwa Sofia, mwingine ni Kijana wa kiume wa Mzee Yusuf aliyeitwa Hamza. Wote walikutana mahala hapo, waliishuhudia damu ikichuruzika, waliifuata damu hiyo hadi chumbani kwa Mzee Yusuf, walimkuta Mzee huyo akiwa ameegemea Meza akimwaga damu mdomoni na mgongoni, kisu kilikua juu ya Mgongo wake.
Haraka zilipigwa simu kuelekea Polisi na Hospitali, mara moja wote walikusanyika hapo, wa kwanza kufika alikuwa ni Daktari Bingwa wa Mzee Yusuf. Daktari Huyo alikua wa kwanza kuthibitisha kuwa Mzee huyo alifariki dakika chache zilizopita kwani bado mwili wake ulikua wa moto, vilio vilitanda.
Sofia alilia kwa kusaga meno, Bi Choro alilia kama Mtoto Mdogo, Hamza pekee ndiye aliyekua na nguvu ya kuzungumza na daktari sababu alikuwa Mtoto wa kwanza wa kiume wa Mzee huyo, ndiye Kaka wa Sofia kwanye hiyo familia yenye Watoto wawili pekee ambao ni Sofia na Hamza.
Daktari alimshauri Hamza kutokuugusa mwili huo sababu hilo ni tukio la Mauaji.
Tayari wapelelezi walikua hapo wakiongozwa na Agent Daudi Mbaga aliyekua kiongozi wa wapelelezi hao, pia gari ya wagonjwa ilikua tayari imefika hapo ikiwa na Madaktari ambao nao walipewa taarifa kuwa Mtu waliyemfuata hapo alikua tayari ameshakufa.
Familia ya kitajiri ilizizima kwa Majonzi Usiku huo, wapelelezi waliwataka Wanafamilia kukusanywa sehemu moja, wakagawana kazi za kufanya hapo, Agent Daudi akabakia ndani ya chumba hicho ili kutafuta shahidi za kimazingira wakati timu iliyobakia ikiwa inawahoji wanafamilia.
Dakika moja ya kutazama eneo hilo la tukio, Daudi aligundua kua kwenye meza ambayo Mzee Yusuf alikua ameilalia palikua na glasi mbili zenye vinywaji, peni moja pia chupa moja ya Waini ikiwa imevunjika kwa chini, vyote vikampa picha ya haraka kua aliyemuuwa Mzee huyo alianza kuzungumza naye Kwanza kisha pakatokea vurugu ndiyo maana chupa ya waini ilianguka kutokea juu ya Meza.
Mkononi Mzee huyo alikua ameshikilia Bastola nyeusi ndogo, hapa Daudi akashindwa kufasili kwa haraka haraka ni kwanini alikua na Bastola ambayo haikuonekana kutumika. Pia ilionekana kwenye kabati la kuhifadhia makabrasha palikua pamepekuliwa sana, hii ikamfanya Daudi ahitimishe uchunguzi wa awali kua muuwaji alihitaji kitu fulani kutoka kwa Mzee huyo, lakini swali aliloondoka nalo ndani ya Chumba hicho lilikua
“Nani amemuua Mzee huyo tajiri?” Usikose KOTI JEUSI Sehemu Ya Pili Sasa
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Pili) KOTI JEUSI – 02
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tatu) KOTI JEUSI – 03
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Nne) KOTI JEUSI – 04
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tano) KOTI JEUSI -05
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Sita) KOTI JEUSI -06
KOTI JEUSI (Sehemu Ya Saba) KOTI JEUSI – 07
KOTI JEUSI (Sehemu Ya Nane) KOTI JEUSI -08
KOTI JEUSI (Sehemu Ya Tisa) KOTI JEUSI -09
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi) KOTI JEUSI -10
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Moja) KOTI JEUSI -11
KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Mbili) KOTI JEUSI -12
43 Comments
Sehemuu ya pili iendelee Hadith nzur sanaa🔥🔥💪
Patamu hapo
Nzuri sana
Nzuli sana
Nzurii
Angalau mfanye utaratibu wa kuziuza Ili ziwe downloadable
Nice story… but kuna vitu jadhaa vya kiuandishi vinahitaji marekebisho all in all it’s a nice story Admin
Nzuri sana
Nice. Iendelee sehemu inayofuata tafadhali
Nzuri sana
Nzuri sana
Nzuri sana
Story nzuri nimeipenda
Na Mimi nina story yangu inaitwa kifo ni haki yangu ..tuwasiliane ili nikupatie uiweke hapa pia watu wasome
0711986518
nimependa
It seems to be a nice story, we are in this together 🧡
Mwanzo mzuri… Nmeipenda, nikuombe admin kuwa unatuma Kila Siku kwa maana sehemu Moja Moja Kila Siku ili utamu usipoe
Hakuna Noma Familia
Sehem ya pili ienderee good story
Daaaahhhhh……..nzuri sana
Good story I love it
Story safi nimeipenda sema mwandishi kuna vitu inabidi arekebishe ili story ikae bomba zaidi
🔥🔥🔥
Vp sehem ya pili inaendelea lini au mpaka tusahau admin
Leo Jioni Mkuu
Dah mwanzo tu inasikitisha
I like it. Always I like to read but what to read about was a problem. Now for this I think gonna be a best story, let’s move it admin………..put on ep 2
nimewahi kwanza comment section then nirud kusoma
Ukiwa kijiweni unapata Moja moto Moja Baridi swafi kabsa
Hakika Mzee Yusuf kuna kitu alikifanya Hadi kupata huo utajir siyo bire , sehemu ya pili iendeleee ni nzuri sana
Stori Nzuri Sana Ngoja Tuone Muuaji Ni Nani?
Good story I like it
Nzuri
Iko gud
Sana
Adhithi tamu san hii
Sehem ya pili chap🥱🥱
Nice story
Iendelee katika sehemu nyingine
Nzuri Sana pia ina mafunzo 👪
Pingback: KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Pili) KOTI JEUSI - 02 - Kijiweni
Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tatu) KOTI JEUSI – 14 - Kijiweni
Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tano) KOTI JEUSI – 15 - Kijiweni
Riwaya mpya ningeomba itoke mida km hii, maana wengine kushika cmu usiku ni issue….
Na hii iliyoisha ni bonge moja la PSYCHOLOGICAL THRILLER story, natumai mpya itaizidi hii iliyokwisha.