Ilipoishia “Akamzaa Adela, akafanya siri kubwa sana mbele ya Baba yake kuhusu Baba wa Mtoto huyo, akamwambia Baba yake kuwa Baba yake Adela yupo nje ya Nchi, uwongo huo haukua na Mashiko kwa Bilionea Yusuf ambaye alikua na siri ya kumwua Baba wa Adela.

Mzee Yusufu akamtendea mazuri Salma huku akiwa na siri ya kumuulia Mume wake, akamtendea mazuri zaidi Adela kwa kumpa Utajiri mwingi kisiri kama fidia ya kumfanya awe Yatima “

Endelea

Sehemu ya 13

“Baba unafikiria nini Kumwoa Msichana anayelingaa umri na Mimi, unataka nimwite Mama yule”? Siku moja Sofia alimuuliza Baba yake wakiwa ofisini, Blionea Yusuf hakujibu chochote.

“Halafu ukanitoa kwenye nafasi yangu ukamweka yeye, amekupumbaza na Nini Baba?” aliuliza Sofia kwa Jazba, mara hii Bilionea Yusuf hakumkalia Kimya

“Haya ni maamuzi yangu Sofia, ulitaka nikae bila Mke hadi lini? Yule anastahili kua Mke kwangu na kwa heshima mtamwita Mama” alijibu akifoka

“Labda Hamza, lakini Mimi siwezi kumwita Mama yule Muuwaji” alisema Sofia kisha akaondoka zake, Japo Bilionea Yusuf alikua akijua kuwa Sofia na Salma hawafahamiani lakini aliziona chuki za waziwazi. 

Aliziona wazi hasira za Sofia, alijua namna Sofia alivyokua akimtazama Salma kama Muuwaji japo alichagua kukaa kimya bila kusema popote, kwa nama ambavyo mambo yalikua yakifukuta taratibu ndipo alipo mwamishia Salma Nchini Ungereza kusimamia Biashara.

****

Machozi yaliwabubujika waliokua wakiusikia mkasa huo Hamza alikosa nguvu akaketi kwenye kiti

“Ulijuaje kama Baba yako ndiye aliyemuuwa Julius?” akauliza Mpelelezi Marcus

“Nilikuta tepu rekodi yenye maongezi yake ya siri akizungumza na Muuwaji na kumpa kazi ya 

Kumuua Julius, Baba naye alishtuka kuwa nimeshajua kwani mahali alipoiweka Tepu rekodi sipo alipoikuta tena, Mtu pekee niliyeingia ofisini kwake kwa muda huo nilikua Mimi” alisema Sofia huku chozi likimbubujika.

Saa 2:15 Usiku, siku ya tatu baada ya Mzee Ysuf kutambua kua Sofia amegundua siri hiyo, alimwita Binti yake Mahali pa siri na kumwambia

“Najua moyo wako umebeba siri nzito yenye maumivu ndani yako, umejua kuwa Mimi ndiye 

niliyemuua Baba wa Mtoto wako. Sikutaka Uzae Mtoto nje ya ndoa, niliamini utakaposikia kuhusu kile kifo ungeitoa hiyo Mimba, haikua hivyo. Kama unahitaji kulipa kisasi nipo tayari Sofia” ndiyo kauli pekee aliyoisema Mzee Yusuf kisha alimwacha hapo Sofia akiwa anavuja mchozi.

“Nilimuuwa Baba yangu sababu yeye ndiye chanzo cha Binti yangu kukosa mapenzi ya Baba yake” alisema Sofia, wote waliomsikia waliguswa sana na tukio hilo, rasmi akajithibitisha kua ndiye Muuwaji aliyekua akisakwa muda wote.

“Unamfahamu Sakina yule Msichana anayetumikia adhabu ya Mauwaji?” akauliza Mpelelezi Marcus

“Hapana, hata Mimi nilishangaa kwanini yeye aseme mbele ya Mahakama kuwa ndiye aliyemuuwa Baba yangu”

“Ulimuuwa Salma”

“Hapana, baada ya kugundua siri ya kifo cha Julius nilimsamehe Salma kwa dhati ya moyo wangu lakini sikutaka aendelee kuwa miongoni mwa Familia yetu ndiyo maana nilimtegenezea kesi, na mimi ndiye niliye sababisha Baba na Salma wagombane, nilitaka Baba amwache Salma sababu hakustahili kusimama nafasi ya Mama yangu, lakini cha ajabu aliuawa na Mtu nisiyemfahamu” alisema Sofia, 

Marcus akamwuliza swali lingine

“Ulimuuwaje Baba yako?”

“Nilimchoma kisu mgongoni. Taarifa ya kwamba Baba yangu aliuawa kwa sumu ilinishangaza pia, nilichukua nyaraka za siri ambazo Baba yangu alikua akijiandaa kumpa utajiri Salma” Maelezo ya Sofia yalionesha wazi kua hakumuuwa Baba yake bali Baba yake aliuawa kwanza kwa sumu na Mtu anayemfahamu ambaye alipata naye kinywaji muda mfupi kabla ya kifo chake.Akaruhusu Sofia apelekwe kwanza Rumande, papo hapo akapokea simu na kutaarifiwa kua Adela amekutwa akiwa hai kwenye jokofu la kuhifadhia Maiti, Sofia akakiri kupanga njama na yule Daktari za kumuuwa Binti yake ili asitoboe siri ya kifo cha Babu yake, akaeleza kua Daktari hakumuuwa Adela na ndiyo sababu ya yeye kurudi tena Hospitali akiwa na kisu ili ammalize Binti yake, Sofia aliyasema yote akiwa analia.

Mipango yote ya Mauwaji aliyojaribu alifeli, kama alivyoshindwa kummaliza Baba yake ndivyo 

alishindwa kummaliza Binti yake, akapelekwa Mahabusu.

Marcus akaagiza wale vijana watatu marafiki wa Michael Jomo waletwe mara moja, vijana hao 

pekee ndiyo wenye kumtambua Muuwaji wa Mzee Yusuf, walikua wamechoka mbaya kwa mateso waliyopewa

“Niwarudishe kwenye siafu au mtasema ni Nani yule Msichana?” vijana hao wakatazamana, hakuna jibu lililotoka, Marcus akawauliza tena

“Mtasema ni Nani yule Msichana au mteseke kwanza?”

“Mimi nitasema” alisema mmoja wao mwenye woga ambaye ndiye aliyekua akizungumza kua 

atasema ukweli, Marcus akamsogelea akiwa amepiga magoti sakafuni

“Nani yule Binti?” Akauliza

Kijana mmoja amekubali kusema kwa hakika ni Nani yule Msichana ambaye wapelelezi wanaamini kuwa ndiye Muuwaji aliyemuuwa Mzee Yusuf

Miezi mingi iliyopita

Vijana wawili walikua wakiwasiliana kwa Njia ya Telegram, Kijana Mmoja alikua akiitwa Denis na mwingine alikua akiitwa Michael. Ulikua ni Usiku wa saa tano, katika mawasiliano yao wakakubaliana kukutana Mikocheni kwenye kiwanja kimoja wafurahi.Saa moja baadaye walikutana Mikocheni, wakaingia kwenye klabu moja ya Usiku ili wafurahi. 

Wakaagiza Vinywaji na kuanza kunywa huku wakicheza na kula

Saa 7:15 Usiku walikua tayari wamelewa, wakajivuta hadi nje ili kupata Usafiri. Walipofika nje 

wakamwona Msichana mmoja akiwa anawapungia mkono kama vile alikua akiwaita, Msichana huyo alikua mweusi mwenye kuvunga nywele kwa nyuma

“Mambo?” aliwasalimia kwa Bashasha, wakaongea kidogo kisha akawaambia atawapa lifti Usiku huo, wakakubali sababu ya pombe zao, wakaingia kwenye Brevis.

Akampeleka kwanza Denis kwao kisha akampeleka Michael kwao, alipomshusha Michael akamwuliza

“Unaitwa Nani?” Michael akacheka kisha akajibu

“Naitwa Michael Jomo” 

“Kadi yangu ya mawasiliano hii hapa, kwa chochote usisite kunitafuta” akasema Huyo Msichana 

ambaye alijitambulisha kwa akina Michael kama Miss Laya.Mawasiliano kati ya Michael na Miss Laya yakazidi kunoga kwasababu Miss Laya alipenda sana sanaa ya Uchoraji ya Michael Jomo, urafiki wao ukaimarika hatimaye wakawa wapenzi. 

Msichana huyo alikua na nyumba moja ya kifahari maeneo ya Ununio, alikua akiishi peke yake.

Siku moja akawaalika Michael na rafiki zake kwenye hilo jumba la Kifahari, wakafanya sherehe fupi kisha Michael na Miss Laya wakaingia chumbani. Wale marafiki zake Michael wakapata muda wa kulizungukia jumba hilo la Kifahari ambalo Miss Laya alikua akiishi peke yake.

Walipofika nyuma ya nyumba hiyo waliukuta mwili wa Mtu aliyekufa ukiwa unaning’inia, ukiwa unavuja damu Mbichi, hapo wakaingiwa na woga wakakimbia bila kuaga.

Miss Laya aligundua hilo kupitia kwa Michael Jomo Mpenzi wake kuwa waliona Maiti nyuma ya nyumba hiyo, Miss Laya akamwita Michael mahala pa siri akamwambia

“Mimi siyo Muuwaji, Mimi ni Jasusi naifanya kazi kwa ajili ya Taifa langu. Kazi niliyopewa na 

Mamlaka ni kuhakikisha nafyeka wote ambao wamepanga kuigeuka Serikali” alisema Miss Laya na kutoa kitambulisho kilichoonesha ni kweli Msichana huyo alikua ni Jasusi.

“Kama umeligundua hili, waeleze marafiki zako kuwa endapo watafungua vinywa vyao nitawamaliza. Kuna kazi nataka uifanye” Maneno haya yalianza kumtia hofu Michael Jomo akiwa anahema na kutetemeka

“Nataka uyachore kila Mauwaji ninayoyafanya, utaambatana na Mimi kila Mahali. Baada ya 

kukamilisha nitakupa utajiri mkubwa sana” alisema Miss Laya akiwa anafunga nywele zake, Michael alikubali japo alikua mwoga sana, akawaeleza rafiki zake yote na kuwataka kukaa kimya kwani wangeingiza mkwanja mrefu

Marafiki hawa wakaanza kushirikiana na Miss Laya kutunza siri za Mauwaji, hivyo picha walizopiga na Miss Laya zilihakikisha haionekani sura ya Msichana huyo akidai kua ni Agent wa Siri sana wa Serikali, wote wakamwamini sana Miss Laya, akawabadilishia Maisha yao wakawa wanatumia pesa nyingi hapo chuoni.

 

Baada ya kuyasikiliza maelezo ya Denis, haraka Jasusi Marcus akaagiza Mtu atafute taarifa za Jasusi anayeitwa Miss Laya, na kama kweli ni Jasusi basi atakua anafanya kazi za siri hivyo kifo cha Bilionea Yusuf kinaweza kutokana na Idara ya Kijasusi kwa maslahi ya Taifa.

Akawa bize anaitazama simu yake ili ikiita aipokee haraka, baada ya dakika tano simu iliita na sasa aliichukua haraka na kuipokea, akaiweka sikioni

“Ni kweli kuna Jasusi anaitwa Miss Laya, anaishi Ununio” alisema mtoa taarifa, Marcus akameza mate kwa tabasamu la kuanza kufikia mwisho wa kesi, kama atapatikana huyo Miss Laya basi itakua rahisi kutatua kitendawili kizito cha Nani Muuwaji na anauwa kwasababu gani, akaagiza gari liandaliwe ili amfwatilie Miss Laya.

Taarifa zote za Mwanamke huyo alipatiwa na Mtoa taarifa hivyo ikawa rahisi kujua anapoishi, 

akaingia kwenye gari akiwa na Polisi Mmoja kisha wakaanza safari kutoka Kituo cha Polisi Ostabey kuelekea Ununio Hapo hapo Jijini Dar-es-salaam kupitia Bagamoyo Road.

Mara zote inatambulika kuwa Majasusi wamewekewa zuio la kupelelezwa kwani wanakua wanafanya mambo mengi yanayokiuka sheria za Nchi lakini kwa Maslahi ya Taifa hivyo Marcus akaomba ruhusa akiwa ndani ya gari kutoka kwa Mkuu wake wa kazi ili akampeleleze Miss Laya ili ijulikane kuwa ndiye Muuwaji na anauwa kwasababu gani, kama ni agizo la Serikali basi kesi hiyo ifungwe mara moja kwani ni agizo lenye Mamlaka makubwa na kibali kutoka ngazi za juu ya Serikali.

Saa moja na robo iliwatosha Marcus na polisi aliyeongozana naye kufika mbele ya geti la nyumba ya Miss Laya, alishapewa kibali cha kumpeleleza Jasusi huyo, akagonga alam kisha akasubiria Mlango ufunguliwe, alipoitazama vizuri nyumba hiyo alipata taswira ya jumba la kifahari ambalo Denis alilielezea kua ndipo anapoishi Miss Laya ambaye ameficha sana sura yake kwenye zile picha.

Alipoona kimya alitaka kugonga tena lakini akasikia Makubasi yakija hapo getini, mara moja geti lilifunguliwa na Mwanamke ambaye sifa zake haziendani na Muuwaji ambaye Marcus alikua akimtafuta, Mwanamke huyo alikua Mkubwa wa miaka zaidi ya 30, mweupe, mnene kidogo aliyefuga rasta.

Kwa tabasamu akawakaribisha ndani akionekana kumfahamu Marcus, wakaingia wote hadi ndani lakini bado taswira ya Nyumba hiyo ilifanana sana na ile aliyoielezea Denis kua ndimo anamoishi Muuwaji

“Marcus, karibu” alisema

“Umenijuaje?”

“Nakujua hilo lisikupe presha, nimeambiwa unakuja kuzungumza na Mimi” alisema, ikampa ahueni Marcus kua Mkuu wake wa kazi alimpigia simu huyo Mwanamke kuwa Marcus anaenda kuzungumza 

naye

“Miss Laya si ndiyo?”

“Yeah!! Kuna chochote?” aliuliza Miss Laya kisha aliketi kitako akiwa ana tabasamu.

“Unafahamu chochote kuhusu kifo cha Bilionea Yusuf? Ni wewe ndiye uliyetekeleza Mauwaji yale?” Marcus akazama moja kwa moja kwenye mada iliyomleta tena akimkazia macho Miss Laya ili kuona kama kuna kitu atakificha.

“Hapana sijui chochote kuhusu kifo chake, sihusiki kwa namna yoyote ile Marcus” Kisha Marcus akatoa picha na kumwonesha Miss Laya

“Unamfahamu huyu Msichana?” Miss Laya akacheka kidogo kisha akamjibu Marcus huku 

akimrudishia picha

“Ntamfahamu vipi Mtu nisiyemwona sura yake hapo?” Marcus hakugundua chochote kwenye 

macho ya Miss Laya, kama kuna kitu anakijua Miss Laya basi amekificha Kijasusi kweli kweli maana hata macho yake hayakubabaika, labda kwasababu alikua Jasusi.

Mara simu ya Miss Laya ikawa inaita, mara ya kwanza akaikata sauti, ya pili akaikata sauti, ya Tatu akaomba kuipokea tena akatoka nje kabisa. Marcus akawa anamwona Miss Laya akizungumza na simu tena kwa Mkazo sana huku akitoa na ishara za vidole.

Marcus akautumia Mwanya huo kuanza kupiga picha mazingira ya nyumba hiyo kwa ndani, hadi 

Miss Laya anarejea alikua ameshamaliza

“Oooh Marcus kuna la zaidi? Nimepata simu ya dharura” alisema 

“Nafikiri hakuna, nitakurudia kama kutakua na jambo la zaidi” alisema Marcus kisha walinyanyuka na kuondoka Hapo, wakarudi kituo cha Polisi kwa wale vijana. Akawaonesha ile picha ya ndani ya nyumba ya Miss Laya Wote kwa pamoja walikubali kuwa ndiyo penyewe, Marcus akawaambia

“Muda siyo mrefu nitamnasa Muuwaji, mtakua huru lakini msirudie kuficha mambo mazito kama haya” akawapa tumaini na kuwaacha hapo Mahabusu wakiwa wanafuraha wakijua muda siyo mrefu watarudi Uraiani. Nini kitaendelea? Miss Laya ndio muuaji mkuu?  Usikose sehemu ya 14

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kwanza) KOTI JEUSI – 01

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Pili) KOTI JEUSI – 02

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tatu) KOTI JEUSI – 03 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Nne) KOTI JEUSI – 04 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tano) KOTI JEUSI -05

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Sita) KOTI JEUSI -06 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Saba) KOTI JEUSI – 07

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Nane) KOTI JEUSI -08 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Tisa) KOTI JEUSI -09 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi) KOTI JEUSI -10 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Moja) KOTI JEUSI -11

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Mbili) KOTI JEUSI -12

14 Comments

    • Bintii kimmy on

      Mwandishi apewe maua yake 🥳🤗UTUNZI anaujua habahatishii🔥🔥Ana kitu atafika mbalii😄😄🤗

  1. Me naamini muuaji wa billioner yusuph ni martha kwa sababu huyo billioner yusuph aliimua mzee George ambae ni baba yake na martha huku mtoto akishuhudia kile alicho tendewa baba yake

Leave A Reply


Exit mobile version