IlipoishiaMuda siyo mrefu nitamnasa Muuwaji, mtakua huru lakini msirudie kuficha mambo mazito kama haya” akawapa tumaini na kuwaacha hapo Mahabusu wakiwa wanafuraha wakijua muda siyo mrefu watarudi Uraiani.

Endelea:
SEHEMU YA 15


Giza nene likiwa limeifunga anga ya Jiji la Dar-es-salaam, Mtu mmoja alikua akishuka kwenye gari moja nyeusi aina ya Toyota Crown, Mtu huyo alikua ni Miss Laya. Mbele yake palikua na jengo la Hospitali ambapo Adela alikua akipatiwa matibabu baada ya kukutwa Mochwari kwenye jokofu la kuhifadhia Maiti.

Kwa ajili ya Usalama wa Adela, Marcus aliagiza ulinzi wa Polisi kuzunguka wodi hiyo ili atakapokaa sawa aeleze alichokiona Usiku ule, kukawa na hisia kua huwenda aliwaona wauwaji wote, lakini walichohitaji zaidi wapelelezi ni kujua Mtu wa kwanza kuingia kwenye kile chumba cha Bilionea Yusuf ni Nani.

Miss Laya alishuka kisha akaishika korido akiwa na taarifa ya wapi anaelekea, alielekea moja kwa moja kwenye chumba alicholazwa Adela, namna alivyovaa alionekana kuwa ni Daktari wa Hospitali hiyo, wale polisi wakamruhusu kuzama ndani.

Humo alimkuta Hamza akiwa amejiegesha kwenye sofa, Adela akiwa anasaidiwa kupumua na 

Mashine, hakuna aliyekua na fahamu hapo ndani, Hamza alikua Usingizini , Adela alikua hajitambui. Kitu cha kwanza kufanya Miss Laya ni kutazama Mashine inayomsadia kupumua, haikujulikana ana lengo lipi hapo huku tayari akiwa anafahamika kua ni Jasusi wa siri wa Serikali.

Mashine ilionesha kiwango cha Oksijeni ambacho Adela alikua akikipata, akamsogelea kisha  akamwambia

“Mungu alikulinda sana Adela, imefika wakati ambao ameshindwa kufanya hivyo” akachomoa ile mashine, Adela akaanza kuhema kwa shida kisha haraka Miss Laya akachomoka ndani ya wodi hiyo bila wale Polisi kushtuka kuwa Mtu huyo hakua Daktari na alikuja hapo kwa lengo baya dhidi ya Adela.

Adela akawa anahema kwa shida huku akiwa ametoa macho, akawa anajaribu kutaka kupiga kelele kuomba msaada lakini alikua anashindwa, akawa anapoteza nguvu huku chozi likimbubujika akimtazama Hamza akiwa amejilaza. Adela akawa anajaribu kutaka kusukuma enga iliyotumika kuwekea dripu, akawa anajaribu kujisukuma lakini anashindwa. 

Hali yake ikawa mbaya zaidi, akakosa hewa huku akiitumia kidogo aliyonayo kuvuta nguvu kisha akaisukuma enga ikamwangukia Hamza ambaye alishtuka na kumwona Adela akipupa pale kitandani, haraka akairudisha ile Mashine ya kupumulia, akaita Madaktari mara moja

Polisi ndiyo wakafahamu kuwa aliyeingia pale hakua Daktari bali ni Mtu mbaya, wakazunguka kumsaka Hospitali nzima lakini hawakumwona, tayari Miss Laya akawa ametoka nje ya Hospitali, akiwa kwenye gari akapiga simu mahali

“Tayari, hakikisha unaihama hii Nchi haraka sana. Majasusi wamenifikia hiyo ni ishara kua kuna taarifa zako zinazoweza kuvuja” alisema Miss Laya, ikasikika sauti ya kike kwenye simu ikisema

“Sitoondoka hadi Nimuuwe Mama yangu, yeye ni Mtu wa mwisho. Endelea kunificha” Miss Laya akaikata simu kwa hasira huku akigonga Usukani. Akakanyaga mafuta akiamini ameshamuuwa Mtoto Adela, Usiku ule Madaktari wakamwamisha Adela na kumpeleka wodi nyingine kuhofia Muuwaji angeliweza kurudi tena kumdhuru.

Saa 6:10 Usiku, mpango wa Marcus ulikua ni kurudi kwenye ile nyumba ya Miss Laya. Alipofika hapo Usiku huo aliona gari moja aina ya Range Rover nyeusi ikitoka hapo, akajificha kwenye maua yaliyo nje ya Nyumba hiyo, kisha Akamwona Miss Laya akilifunga geti hilo.

“Nani anatoka hapa?” alijiuliza Marcus akiwa amebana vizuri mahala hapo, Miss Laya wakati 

analifunga akahisi jambo, akatoka nje na kuangaza huku na kule kuona kama kuna Mtu amekuja 

hapo. Hisia zake zikamwelekeza kwenye Maua, mahala hapo ndipo alipojificha Marcus, kwa namna yoyote kama atafika hapo basi atamwona Marcus na kugundua kuwa anapelelezwa kwa siri.

Akasogea taratibu akiwa amevalia pensi nyeusi na tisheti jeupe, akaziweka vizuri rasta zake, mara simu yake ilianza kuita, ikamtoa kwenye njia kabisa, akaipokea na kusahau alichopaswa kukifanya kisha akafunga geti na kurudi ndani.

Marcus akapumua kwa pumzi kuu ya kushusha, akaelekea kuchungulia kwenye geti akamwona Miss Laya akiufunga mlango wa kuingilia ndani ya jumba hilo, kuna kitu kimoja tu kilichomleta Marcus, alihitaji kupeleleza uwepo wa eneo la nyuma ya nyumba hiyo mahali ambapo Denis alisema aliiyona Maiti

Aliamini hapo angepata shahidi fulani za kimazingira kuelekea Ushindi wa kesi ya kumsaka Muuwaji

 

Miss Laya alifunga Milango yote huku akizungumza na Mtu kwa njia ya simu lakini hisia zake 

zilimwambia kitu japo alionekana kuongea na simu ila hisia zote alizielekeza nje ya Jumba lake la Kifahari. Marcus akautumia ukuta uliozungushiwa vyuma vidogo vinavyokata, alishajiandaa kwa hilo mikononi alivalia Glavu ngumu zenye kumkinga. Kisha akatua ndani ya jumba hilo, akatulizana kwa makini kwa zaidi ya dakika moja kuona kama Miss Laya ameshtuka.

Alipoona hali ni shwari akanyata taratibu hadi nyuma ya jumba hilo, akamulika tochi. Ni kweli palikua na dalili zote kua ni eneo la kutesea Watu, palikua na vifusi vidogo vya udongo vilivyofanana na Makaburi hivi, Marcus akajua sasa kua Muuwaji ni huyo Miss Laya. 

Hakutaka kupoteza Muda akapanga kumvamia ili amnase Usiku huo, kwanza akatuma Meseji kwa Polisi anayemwanini sana akamtaka aende hapo nyumbani kwa Miss Laya.

Hata Marcus alijua kuwa si rahisi kumnasa Mwanamke huyo sababu ni Jasusi wa kuaminika hivyo ni lazima atakua na ujuzi mkubwa sana wa mapigano ya aina yote. 

Marcus akasogea hadi kwenye mlango wa kioo ambao hutumika kuingia ndani ya Mjengo huo wa kifahari, alipofika alishangaa kuukuta uko wazi hivyo akajua sasa hata Miss Laya yupo mawindoni akimwinda Mtu aliyeingia ndani ya nyumba yake.

Kabla hajapiga hatua yoyote aliwekewa Bastola kichwani, nyuma yake alisimama Miss Laya, akamwita Marcus kwa jina lake halisia, hapo Marcus akajua kua Miss Laya aliamua kujidhihirisha kua yeye ndiye Muuwaji, akakumbuka kuwa hata Sakina aliye magereza alimwita kwa jina lake halisi hivyo huwenda Miss Laya ndiye aliyempandikiza Sakina na kujifanya ndiye Muuwaji. Maswali mengi yalizunguka kichwa cha Jasusi Marcus

“Dondosha Bastola yako” alisema Miss Laya kwa sauti ya kukaza isiyo na Mchezo, Marcus akaweka Bastola bila kufanya mchezo wowote ule kisha akaambiwa ageuke

“Isukume kwangu hiyo Bastola” akasema tena Miss Laya, Marcus akaisukuma Bastola kwa Jasusi huyo, kisha Miss Laya akainyanyua na kuisweka kiunoni

“Unataka nini Marcus?” akauliza Miss Laya kwa sauti ile ile yenye mkazo sana

“Nataka kumjua Muuwaji anayeisumbua idara ya Upelelezi” alijibu Marcus mikono yake ikiwa juu kama alivyoambiwa na Miss Laya

“Unafikiria baada ya kumjua Muuwaji itakuaje, utaendelea kuishi?” alihoji Miss Laya

“Kitu muhimu kwangu ni Kumjua Muuwaji, nitaendelea kuishi au nitakufa hilo sitojali lakini nataka kujua Muuwaji ni Nani?” alisema Marcus kwa Kujiamini sana akiamini pia kua Polisi anayemtumaini atafika hapo na kumsaidia endapo itatokea akahitaji kumwua.

Miss Laya akashusha Bastola yake kisha akamwambia Marcus

“Kama leo itakua ndiyo siku yako ya mwisho kuishi basi yote uliyoifanyia Serikali yatazikwa pamoja na jina lako, pengine hata wasijue uko wapi, vipi kama nitakuzika hapa kwangu Marcus?” maelezo haya yakampa taswira Marcus kua Miss Laya ndiye Muuwaji. 

“Ina maana wewe ndiye Muuwaji unayewatesa Watu?” 

Miss Laya akacheka kidogo kisha ukaonekana Mwanga wa taa ya gari getini, akili ya Marcus ikamwambia kuwa Polisi wake amefika lakini kicheko cha Miss Laya kilimpa hofu ikabidi atulie kwanza huku akipiga mahesabu baada ya Miss Laya kuonesha Dalili zote kuwa ndiye Muuwaji.

Miss Laya alionekana kujiamini, akairejesha Bastola nyingine kiunoni kisha akasogea getini 

akimwacha Marcus akiwa huru kitu ambacho hata Marcus alikishangaa, ikabidi asubirie kuona ni Nani amefika hapo. Range moja ya kitajiri sana iliingia hapo, Marcus akajua huyo si Polisi wake kwani asingeliweza kuja na gari ya kitajiri namna ile.

Akashuka Msichana mmoja ambaye sura yake Marcus alishawahi kuiyona zaidi ya mara moja, 

akapiganisha kumbukumbu zake alimwona wapi, akakumbuka kua alimwona kwenye nyumba ya Mzee Yusuf, alimwona mara kadhaa akiwa na Sofia. 

Akalikumbuka jina la Msichana huyo kuwa ni Martha, pia akakumbuka kuwa ndiye ambaye Mpelelezi Daudi Mbaga aliwahi kusema kuwa Muuwaji anapatikana kwenye picha ile ya familia ambayo Mzee Yusuf aliipiga akiwa na Martha, Hamza na Sofia.

Muuwaji namba mbili alishapatikana, sasa alichohitaji ni kumfahamu Mtu aliyemuuwa Mzee Yusufu kwa kutumia sumu. Martha na Miss Laya walisogea karibu na Marcus aliyekua akipiganisha akili yake.

Kisha Martha aliyevalia sweta Jeusi na suruali ya Jinzi ya Bluu akamnyooshea Bastola Marcus tena bila utani kabisa.

“Kumbe ni wewe?” aliuliza Marcus, sasa Martha alijidhihirisha kuwa ndiye aliyemuuwa Mzee Yusuf, alimeza mate kisha akamwuliza Marcus

“Umewahi kumpoteza Mtu uliyempenda, namaanisha uliyempenda kwa moyo wako wote?” 

aliongea kwa hisia iliyojaa kilio cha ndani kwa ndani, ilionesha moyo wa Martha ulikua na maumivu makali sana, akauvua mzura aliouvaa kisha akamwambia Marcus

“They have Killed my Father, they have killed Me since then, so it’s Imposible for them to live ( 

Wameniulia Baba yangu walishaniuwa tangu nikiwa mdogo kwahiyo haiwezekani wao wakaendelea kuishi)” Miss Laya alikua akitazama mkononi naye akiwa ameshikilia Bastola aliyoielekeza chini.Bastola ya Martha ilikua ikilenga paji la Uso la Jasusi Marcus.

“Nani amemuuwa Baba yako?” alihoji Marcus

Miaka kadhaa iliyopita

“Una hakika itaonekana alikufa kwa ajali?” ilikua ni sauti ya Mama yake Martha baada ya Bilionea Yusuf kurudi kuutelekeza mwili wa Baba yake Martha baada ya kumuua.

“Ndiyo ila uwe makini na huyu Mtoto ameona kila kitu sawa?” 

“Sawa nina hofu sana Yusuf, sijui itakuaje jamani” alisema Mama Martha akiwa mwenye wasiwasi.

“Nitahakikisha nakulinda kwa njia zote, nitabeba majukumu ya kumsomesha Martha na kila kitu 

kinachomhusu” Alisema Bilionea Yusuf,wakati huo Martha alikua akisikia kila kitu. Hata baada ya kukutwa mwili wa Bwana George ukiwa umepondeka ndani ya gari taarifa kubwa iliyosambaa ni kua alikufa kwenye ajali ya gari.

Tokea siku hiyo Martha alijenga kisasi juu ya kifo cha Baba yake. Aliamini anapaswa kulipa kwa kile kilichomfika Baba yake, akaivaa chuki ya siri aliyoificha ndani ya moyo wake, hakuna aliyejua kuwa Martha alibeba kisasi kizito ndani yake.

Miaka ilisonga akiwa anaendelea kusoma kwa ufadhili wa Bilionea Yusuf ambaye alibadilisha Maisha yao kabisa, Bilionea huyo alimpatia Martha utajiri mkubwa sana huku akimwambia kuwa ni analipa fadhila za Baba yake ambaye alikua mtiifu kwake akiamini Martha alikua mdogo kwa wakati ulehivyo hakuelewa chochote.

Martha aliushikilia utajiri huo ambao ndiyo uliofanikisha mipango ya Kisasi chake, kwanza alitafuta Mtu ambaye angeliweza kumfundisha kufanya mauwaji yenye kutumia akili ili asikamatwe, ndipo akiwa chuo alikutana na Miss Laya akiwa hapo kama Mwalimu aliyepandikizwa kukichunguza chuo kuhusu rushwa za ngono.

Akafahamiana na Martha wakajenga ukaribu ambao mwisho waliishia kusagana kwani Miss Laya alimweleza Martha kua yeye si Mwalimu tu bali ni Jasusi wa Kuaminika hivyo angeliweza

kumfundisha vingi kama angekubali kushiriki mapenzi ya Jinsia moja, japo Martha alikubali kwa shida zake lakini alijiahidi kua ipo siku atamwua Miss Laya kwa Unyama huo wa Mapenzi ya Jinsia moja.

Alifundishwa kila kitu na Miss Laya, hapo ndipo alipofanikisha kumuuwa Bilionea Yusuf, taarifa zote za kuchanganya ziliwekwa kitaalam kwa mafundisho ya Jasusi Miss Laya, ndio maana ikawa ngumu kwa Wapelelezi kumjua Muuwaji, aliitumia nyumba ya Miss Laya kutesa, kuzika na kupanga mipango mingi ya Mauwaji ya kutisha.

Aliuwa wote aliowaona wanalenga kumgeuka, ili kupata furaha zaidi ndipo alipomtafuta mchoraji ambaye ni Michael Jomo.

ilikuaje Usiku Mauwaji ya kwanza ya Mzee Yusuf?

Usiku ule wakati gari ya Mzee Yusuf inaingia getini, Martha alipita kwa kutumia ukuta mvua kubwa ikiwa inanyesha, Bilionea huyo alipoingia chumbani kwake akiwa mwenye wasiwasi baada ya kupokea simu nyingi asizozifahamu, alijipumzisha kwa masaa kisha alipoamka alikuta mafaili na kuanza kuyapitia kabla hajatulia ndipo Martha alipomnyooshea Bastola na Mzee Yusuf alipomwona Martha alikumbuka tukio la Miaka mingi iliyopita akajua kuwa Martha amekuja kulipa kisasi ndiyo maana alimpa kwanza kinywaji na kuzungumza naye bila kuita mlinzi hadi alipouawa kwa sumu. Umemjua Sasa Muuwaji Wa Bilionea Yusufu? 

Martha akashusha Bastola, kisha akamwambia Marcus 

“Nimeua wote waliotenda unyama dhidi yangu na kwa Baba yangu, bado Watu wawili tu” akasema

“Watu gani hao?” akahoji Marcus, mara moja Martha akanyoosha Bastola na kumpiga risasi ya 

shingo Miss Laya ambaye hakua amejiandaa, kitendo cha risasi kulia kilimfanya Polisi wa Marcus aliye nje naye afyetue risasi kumlenga Martha ambaye alichumpa pembemi kisha akaukwea ukuta na kutimka, Haraka Marcus akamwahi Miss Laya ambaye alikua akitapatapa pale chini, yule polisi akamfukuzia Martha aliyetimkia gizani

Marcus akataka kupiga simu ya dharura kuita watu wa Huduma ya kwanza lakini Miss Akamzuia kisha akamwambia Marcus

“Nastahili kufa nimeiasi Nchi yangu kufanikisha Mauwaji, nenda nyumbani kwao Martha haraka 

sana” alisema Miss Laya kisha alifariki papo hapo, Marcus akapiga simu kituoni kisha akachukua gari hiyo hiyo ya Martha huku akiomba usaidizi wa Polisi kujua mahali anapoishi Martha.

Akatumiwa anuani ya Binti huyo, akakanyaga Mafuta kuelekea nyumbani anakoishi Martha, alipofika alikuta geti likiwa wazi. Kwa mujibu wa anuani ilionesha ni hapo, akachomoa Bastola kisha akasogea taratibu, milango ilikua wazi huku taa zikiwa zinawaka, akamtafuta Martha nyumba nzima lakini hakumwona bali maiti ya Mama yake Martha ikiwa na jeraha la risasi kichwani

Usiku huo huo, Marcus akampigia simu Daudi Mbaga na kumweleza kuwa ameshamjua Muuwaji lakini hajulikani alipo, kisha akafanya safari kuelekea gerezani ambako Sakina alikua amefungwa. Mara moja Sakina akaletwa hapo kisha Marcus akamwuliza

“Una hakika wewe ni Muuwaji?” Aliuliza kwa mtego, Sakina akatabasamu kwa kujibaraguza na 

kusema

“Nilishalithibitisha hilo mbele ya Mahakama Marcus” akapigwa kofi na Marcus kisha akamwambia

“Unamahusiano gani kati yako na Miss Laya na Martha?” Sakina aliona wazi namna jazba ilivyoipamba sura ya Marcus akajua hapo mchezo umeungua

“Siwajui hao” akasema, Marcus kwakua ni Jasusi akaomba kuondoka na mfungwa huyo ili akaseme anachokijua, Marcus akakabidhiwa Sakina Usiku huo akaondoka naye akiwa amemfunga pingu, Sakina alijitahidi kumwelekeza Marcus lakini hakusikilizwa

Akafikishwa Ostabey Usiku huo huo, akaingizwa chumba cha Mateso, Marcus akaamuru Sakina ateswe sana. Japo alikubali mapema sana kuwa atasema lakini Marcus alihitaji ateswe kwanza ili akili imkae sawa sawa.

Hadi Alfajiri inaingia Sakina alikua akiteswa akiwa analalamika na kupiga yowe za Maumivu, kisha Marcus akaomba aletewe Sakina kwenye chumba cha Mahojiano, akaletwa akiwa ametapakaa damu mwili mzima huku akiwa amechoka sana kutokana na kipigo alichopewa

“Wewe ni Nani?” ndiyo swali aliloulizwa, kama Muuwaji ni Martha basi huyu Sakina ni Nani?

“Mimi ni Kopi ya Muuwaji, niliahidiwa kuwa nitapewa pesa nyingi sana ili niufiche ukweli, sikutenda Mauwaji yoyote yale bali nilipandikizwa kwenye tukio kule chuoni” alisema akiwa anatema damu 

“Nani alikupandikiza” 

“Miss Laya”

“Nani alimuuwa yule Mwanachuo?”

“Ni Miss Laya” Maelezo haya yakamfanya Marcus amtambue Miss Laya na Martha kama washirika wa Matukio yote ya Mauwaji, sasa akaagiza vituo vyote vya Polisi Nchi nzima vitaarifiwe juu ya Kutafutwa kwa Martha.

 Picha ya Martha ikasambazwa kila kona, Kila mtu alishangaa kusikia eti kifo cha Bilioena Yusuf kilitokana na Binti aliyemlea kama Binti yake, akampa utajiri na kuhakikisha familia yao inaishi maisha bora baada ya kifo cha Bwana George.

MSAKO

Mchana wa siku ya tatu tangu kutoweka kwa Martha, huku harakati za kumtafuta zikiwa 

zinaendelea. Moja ya Mashamba ya zao la Chikichi huko Kigoma alionekana Mwanamke aliyekua akikatiza hapo akiwa amejifunika sana sura yake kwa kutumia Mtandio.

Mkulima Mmoja alimwona Mtu huyo ambaye kwa sifa zake alionekana kuwa Mwanamke, Mwanamke huyo alikua na Begi kubwa jeusi alilolishikilia mkononi, aliweka kambi shambani hapo huku akionekana kuzungumza sana na simu. 

Siku ya pili, yule Mkulima aliendelea kumwona yule Mwanamke shambani kwake, akionekana kuwasha moto na kuchoma vyakula kisha anakula, kwa hofu yule Mkulima akaenda kutoa taarifa Polisi.Kwa maelezo ya yule Mkulima, Polisi waliona ana sifa zote za Ugaidi, hivyo Magari matatu ya polisi yakachomoka yakiwa na askari wa kutosha wenye Bunduki na silaha nyingine, Yule Mwanamke alipowaoana alianza kukimbia kukatiza shamba jirani, polisi wakamtaka asimame lakini hakutaka kusimama bali alizidi kusonga kwa kasi ndipo Polisi walipoanzisha mashambulizi ambayo yalijibiwa kwa haraka na Mwanamke huyo aliyeonekana kuzielewa zaidi mbinu za Vita.

Aliwashanbulia kwa kutumia Bastola na kufanikisha kuuwa Askari tisa, kisha Polisi wakazidi kuongezeka huku tukio hilo likitajwa kama Ugaidi, miongoni mwa walioongezeka hapo alikua ni Mpelelezi Daudi Mbaga.

Kwa zaidi ya Masaa mawili mashambulizi yaliendelea hadi Mwanamke huyo alipoonekana kua kimya bila kujibu Mashambulizi ya Risasi, alikua amejificha nyuma ya Mchikichi Mkubwa, Polisi wakamzunguka.

Wakamshambulia kwa mbele na kufanikisha kumwangusha, wakamsogelea na kugundua alikua ameshafariki, wakamfunua kitambaa, Polisi wakamtambua Mwanamke huyo kua ni Martha anayetafutwa sana kwa Mauwaji aliyoyafanya huko Dar. 

Mpelelezi Daudi Mbaga akalipokea begi la Martha na kulikagua, akakuta nguo na baadhi ya picha za wote aliowaua, hapo hapo Daudi Mbaga akapiga simu Kwa Marcus na kumweleza kua wamefanikiwa kumuuwa Martha wakimdhania kuwa Gaidi.

Kifo cha Martha kiliitikisa Tanzania, kilivitikisa vyombo vyote vya Ulinzi, akawekwa katika Historia ya Tanzania kua ndiye Mwanamke aliyefanya Mauwaji yenye utata zaidi kuwahi kutokea Tanzania. 

Sakina na Sofia wakafikishwa Mahakamani na kuhukumiwa vifungo vya Miaka 10 kila mmoja kwa kujaribu kufanya Mauwaji. 

Wiki tatu mbele, afya ya Adela iliimarika akarudishwa nyumbani. Miezi ilienda, kila kitu kilikaa sawa kabisa, siku moja aliikumbuka ile kadi aliyopewa na Babu yake, aliitoa kwenye begi lake la nguo mahali alipoificha sana kisha jioni alimweleza Mjomba wake Hamza.

Wakapigia hiyo Namba iliyoandikwa kwenye kadi hiyo, ikapokelewa na Mwanamke mmoja ambaye kwa namna alivyoongea alionekana kuwa ni mwenye kusubiria simu hiyo kwa muda mrefu sana. Adela akajitambulisha, huyo Mwanamke akamjibu kuwa anamfahamu na alitarajia angepokea simu hiyo.

Mwanamke huyo alikua akiishi Uingereza, akawaambia kuwa yeye ni Mtu wa siri wa Marehemu 

Bilionea Yusuf hivyo Adela na Hamza wafanye safari kuelekea Uingereza katika Jiji la London.

Walisafiri kuelekea huko, wakakutana na Mwanamke huyo Mtu mzima ambaye alimpatia Adela 

funguo ya kufungulia kwenye Maboksi ya Posta, akawaambia

“Alinipatia hiyo funguo muda mrefu sana, alinitaka nisubirie nipigiwe simu na nyinyi kupitia kadi sababu alijua atakufa.” Akawatajia Posta ambayo wataweza kufungua kwa kutumia funguo hiyo, wakapanda treni kuelekea Jijini Manchester ambako Bilionea huyo alikua akimiliki Biashara nyingi huko, walipofika Posta Hamza akampa nafasi Adela afungue hapo kwani ndiye mlengwa.

Waliona nyaraka Mbalimbali, walipozisoma wote walishangaa, Mzee Yusuf alimpa Adela utajiri 

mkubwa sana ambao aliuficha kwa muda mrefu, palikua na kadi za Mabenki tofauti tofauti na cheki zenye pesa, pia walikuta Barua fupi iliyosomeka

“Adela Mjukuu wangu, katika Maisha yangu sikuwahi kujua na kuuthamini upendo, hali hiyo ndiyo iliyopelekea maafa katika familia yangu hata kifo changu, nilifanya mengi kwa jeuri ya pesa yangu. Nisamehe sababu nimesababisha wewe kua Yatima kwa kumuua Baba yako, kwa kulitambua hilo nakuachia Mali nyingi japo najua haziwezi kufuta uchungu ulio nao, Nisamehe Mimi, Mwambie Mama anisamehe pia” Barua hiyo iliibua Machozi, Hamza akamwuliza Adela

“Utalipa kisasi kama alivyofanya Martha?” Adela akakataa kwa kutikisa kichwa kisha akamkumbatia Mjomba wake.

—‐—-‐–MWISHO——–‐
Ahsanteni Wote Mliosoma Riwaya Hii Toka Sehemu Ya 1 Mpaka Hii Ya 15 Na Msiondoke Kwani Inakuja Mpya Inayoitwa FUNGATE 

 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kwanza) KOTI JEUSI – 01

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Pili) KOTI JEUSI – 02

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tatu) KOTI JEUSI – 03 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Nne) KOTI JEUSI – 04 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tano) KOTI JEUSI -05

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Sita) KOTI JEUSI -06 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Saba) KOTI JEUSI – 07

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Nane) KOTI JEUSI -08 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Tisa) KOTI JEUSI -09 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi) KOTI JEUSI -10 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Moja) KOTI JEUSI -11

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Mbili) KOTI JEUSI -12

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Tatu) KOTI JEUSI -13

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Nne) KOTI JEUSI -14

 

25 Comments

  1. Asante yaan leo mpaka nilinuna simulizi kuchelewa but all in all hii ni kali kuliko mnajua na mnajua tena🔥🔥🔥❣❣❣❣

  2. duh bonge moj la story yaan,ni zaid ya mkasa maan c kwa familia hyo🤔🤔🤔…….admin tuletee nyingine🙈🙈😁

    • 🙏🏾Kwakwelii huu usanii wa utunzi!! SALUTII kwenu mlofanikisha 2meinjoy na kujifunza meng sana😉n ya kusisimua mnoo ok

  3. Pingback: Tuijadili KOTI JEUSI Hapa Wana KIJIWENI - Kijiweni

  4. Story fupi inaeleweka, ipo detailed, mwandishi hazunguuki, akikupa kisa Cha nyuma ya pazia kinaeleweka, yaan imenyoooka hakuna Kona aisee.
    Kazi nzuri kijiweni👏👏👏

  5. Nzuri sana hongera sana mwandishi,Mungu azidi kukupa maalifa mengi zaidi uzidi kutufundisha na kutuburudishaa

Leave A Reply


Exit mobile version