Ilipoishia“Muda siyo mrefu nitamnasa Muuwaji, mtakua huru lakini msirudie kuficha mambo mazito kama haya” akawapa tumaini na kuwaacha hapo Mahabusu wakiwa wanafuraha wakijua muda siyo mrefu watarudi Uraiani. Nini kitaendelea? Miss Laya ndio muuaji mkuu?  

Tuendelee 

SEHEMU YA 14 

Giza nene likiwa limeifunga anga ya Jiji la Dar-es-salaam, Mtu mmoja alikua akishuka kwenye gari moja nyeusi aina ya Toyota Crown, Mtu huyo alikua ni Miss Laya. Mbele yake palikua na jengo la Hospitali ambapo Adela alikua akipatiwa matibabu baada ya kukutwa Mochwari kwenye jokofu la kuhifadhia Maiti.

Kwa ajili ya Usalama wa Adela, Marcus aliagiza ulinzi wa Polisi kuzunguka wodi hiyo ili atakapokaa sawa aeleze alichokiona Usiku ule, kukawa na hisia kua huwenda aliwaona wauwaji wote, lakini walichohitaji zaidi wapelelezi ni kujua Mtu wa kwanza kuingia kwenye kile chumba cha Bilionea Yusuf ni Nani.

Miss Laya alishuka kisha akaishika korido akiwa na taarifa ya wapi anaelekea, alielekea moja kwa moja kwenye chumba alicholazwa Adela, namna alivyovaa alionekana kuwa ni Daktari wa Hospitali hiyo, wale polisi wakamruhusu kuzama ndani.

Humo alimkuta Hamza akiwa amejiegesha kwenye sofa, Adela akiwa anasaidiwa kupumua na 

Mashine, hakuna aliyekua na fahamu hapo ndani, Hamza alikua Usingizini , Adela alikua hajitambui. Kitu cha kwanza kufanya Miss Laya ni kutazama Mashine inayomsadia kupumua, haikujulikana ana lengo lipi hapo huku tayari akiwa anafahamika kua ni Jasusi wa siri wa Serikali.

Mashine ilionesha kiwango cha Oksijeni ambacho Adela alikua akikipata, akamsogelea kisha 

akamwambia

“Mungu alikulinda sana Adela, imefika wakati ambao ameshindwa kufanya hivyo” akachomoa ile mashine, Adela akaanza kuhema kwa shida kisha haraka Miss Laya akachomoka ndani ya wodi hiyo bila wale Polisi kushtuka kuwa Mtu huyo hakua Daktari na alikuja hapo kwa lengo baya dhidi ya Adela.

Adela akawa anahema kwa shida huku akiwa ametoa macho, akawa anajaribu kutaka kupiga kelele kuomba msaada lakini alikua anashindwa, akawa anapoteza nguvu huku chozi likimbubujika akimtazama Hamza akiwa amejilaza. Adela akawa anajaribu kutaka kusukuma enga iliyotumika kuwekea dripu, akawa anajaribu kujisukuma lakini anashindwa. 

Hali yake ikawa mbaya zaidi, akakosa hewa huku akiitumia kidogo aliyonayo kuvuta nguvu kisha akaisukuma enga ikamwangukia Hamza ambaye alishtuka na kumwona Adela akipupa pale kitandani, haraka akairudisha ile Mashine ya kupumulia, akaita Madaktari mara moja

Polisi ndiyo wakafahamu kuwa aliyeingia pale hakua Daktari bali ni Mtu mbaya, wakazunguka kumsaka Hospitali nzima lakini hawakumwona, tayari Miss Laya akawa ametoka nje ya Hospitali, akiwa kwenye gari akapiga simu mahali

“Tayari, hakikisha unaihama hii Nchi haraka sana. Majasusi wamenifikia hiyo ni ishara kua kuna 

taarifa zako zinazoweza kuvuja” alisema Miss Laya, ikasikika sauti ya kike kwenye simu ikisema

“Sitoondoka hadi Nimuuwe Mama yangu, yeye ni Mtu wa mwisho. Endelea kunificha” Miss Laya akaikata simu kwa hasira huku akigonga Usukani. Akakanyaga mafuta akiamini ameshamuuwa Mtoto Adela, Usiku ule Madaktari wakamwamisha Adela na kumpeleka wodi nyingine kuhofia Muuwaji angeliweza kurudi tena kumdhuru.

Saa 6:10 Usiku, mpango wa Marcus ulikua ni kurudi kwenye ile nyumba ya Miss Laya. Alipofika hapo Usiku huo aliona gari moja aina ya Range Rover nyeusi ikitoka hapo, akajificha kwenye maua yaliyo nje ya Nyumba hiyo, kisha Akamwona Miss Laya akilifunga geti hilo.

“Nani anatoka hapa?” alijiuliza Marcus akiwa amebana vizuri mahala hapo, Miss Laya wakati 

analifunga akahisi jambo, akatoka nje na kuangaza huku na kule kuona kama kuna Mtu amekuja 

hapo. Hisia zake zikamwelekeza kwenye Maua, mahala hapo ndipo alipojificha Marcus, kwa namna yoyote kama atafika hapo basi atamwona Marcus na kugundua kuwa anapelelezwa kwa siri.

Akasogea taratibu akiwa amevalia pensi nyeusi na tisheti jeupe, akaziweka vizuri rasta zake, mara simu yake ilianza kuita, ikamtoa kwenye njia kabisa, akaipokea na kusahau alichopaswa kukifanya kisha akafunga geti na kurudi ndani.

Marcus akapumua kwa pumzi kuu ya kushusha, akaelekea kuchungulia kwenye geti akamwona Miss Laya akiufunga mlango wa kuingilia ndani ya jumba hilo, kuna kitu kimoja tu kilichomleta Marcus, alihitaji kupeleleza uwepo wa eneo la nyuma ya nyumba hiyo mahali ambapo Denis alisema aliiyona Maiti

Aliamini hapo angepata shahidi fulani za kimazingira kuelekea Ushindi wa kesi ya kumsaka Muuwaji

Miss Laya alifunga Milango yote huku akizungumza na Mtu kwa njia ya simu lakini hisia zake 

zilimwambia kitu japo alionekana kuongea na simu ila hisia zote alizielekeza nje ya Jumba lake la Kifahari. Marcus akautumia ukuta uliozungushiwa vyuma vidogo vinavyokata, alishajiandaa kwa hilo mikononi alivalia Glavu ngumu zenye kumkinga. Kisha akatua ndani ya jumba hilo, akatulizana kwa makini kwa zaidi ya dakika moja kuona kama Miss Laya ameshtuka.

Alipoona hali ni shwari akanyata taratibu hadi nyuma ya jumba hilo, akamulika tochi. Ni kweli palikua na dalili zote kua ni eneo la kutesea Watu, palikua na vifusi vidogo vya udongo vilivyofanana na Makaburi hivi, Marcus akajua sasa kua Muuwaji ni huyo Miss Laya. 

Hakutaka kupoteza Muda akapanga kumvamia ili amnase Usiku huo, kwanza akatuma Meseji kwa Polisi anayemwanini sana akamtaka aende hapo nyumbani kwa Miss Laya.

Hata Marcus alijua kuwa si rahisi kumnasa Mwanamke huyo sababu ni Jasusi wa kuaminika hivyo ni lazima atakua na ujuzi mkubwa sana wa mapigano ya aina yote. 

Marcus akasogea hadi kwenye mlango wa kioo ambao hutumika kuingia ndani ya Mjengo huo wa kifahari, alipofika alishangaa kuukuta uko wazi hivyo akajua sasa hata Miss Laya yupo mawindoni akimwinda Mtu aliyeingia ndani ya nyumba yake.

Kabla hajapiga hatua yoyote aliwekewa Bastola kichwani, nyuma yake alisimama Miss Laya, akamwita Marcus kwa jina lake halisia, hapo Marcus akajua kua Miss Laya aliamua kujidhihirisha kua yeye ndiye Muuwaji, akakumbuka kuwa hata Sakina aliye magereza alimwita kwa jina lake halisi hivyo huwenda Miss Laya ndiye aliyempandikiza Sakina na kujifanya ndiye Muuwaji. Maswali mengi yalizunguka kichwa cha Jasusi Marcus

“Dondosha Bastola yako” alisema Miss Laya kwa sauti ya kukaza isiyo na Mchezo, Marcus akaweka Bastola bila kufanya mchezo wowote ule kisha akaambiwa ageuke

“Isukume kwangu hiyo Bastola” akasema tena Miss Laya, Marcus akaisukuma Bastola kwa Jasusi huyo, kisha Miss Laya akainyanyua na kuisweka kiunoni

“Unataka nini Marcus?” akauliza Miss Laya kwa sauti ile ile yenye mkazo sana

“Nataka kumjua Muuwaji anayeisumbua idara ya Upelelezi” alijibu Marcus mikono yake ikiwa juu kama alivyoambiwa na Miss Laya

“Unafikiria baada ya kumjua Muuwaji itakuaje, utaendelea kuishi?” alihoji Miss Laya

“Kitu muhimu kwangu ni Kumjua Muuwaji, nitaendelea kuishi au nitakufa hilo sitojali lakini nataka kujua Muuwaji ni Nani?” alisema Marcus kwa Kujiamini sana akiamini pia kua Polisi anayemtumaini atafika hapo na kumsaidia endapo itatokea akahitaji kumwua.

Miss Laya akashusha Bastola yake kisha akamwambia Marcus

“Kama leo itakua ndiyo siku yako ya mwisho kuishi basi yote uliyoifanyia Serikali yatazikwa pamoja na jina lako, pengine hata wasijue uko wapi, vipi kama nitakuzika hapa kwangu Marcus?” maelezo haya yakampa taswira Marcus kua Miss Laya ndiye Muuwaji. 

“Ina maana wewe ndiye Muuwaji unayewatesa Watu?” 

Miss Laya akacheka kidogo kisha ukaonekana Mwanga wa taa ya gari getini, akili ya Marcus ikamwambia kuwa Polisi wake amefika lakini kicheko cha Miss Laya kilimpa hofu ikabidi atulie kwanza huku akipiga mahesabu baada ya Miss Laya kuonesha Dalili zote kuwa ndiye Muuwaji.

Miss Laya alionekana kujiamini, akairejesha Bastola nyingine kiunoni kisha akasogea getini akimwacha Marcus akiwa huru kitu ambacho hata Marcus alikishangaa, ikabidi asubirie kuona ni Nani amefika hapo. Range moja ya kitajiri sana iliingia hapo, Marcus akajua huyo si Polisi wake kwani asingeliweza kuja na gari ya kitajiri namna ile.

Akashuka Msichana mmoja ambaye sura yake Marcus alishawahi kuiyona zaidi ya mara moja, akapiganisha kumbukumbu zake alimwona wapi, akakumbuka kua alimwona kwenye nyumba ya Mzee Yusuf, alimwona mara kadhaa akiwa na Sofia.  Msichana huyo ni nani? Na kwanini anamtumia Miss Laya?  Usikose Sehemu Ya 15  Zikifika Comments 200 Naiachia Asubuhi Mapema Tu

 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kwanza) KOTI JEUSI – 01

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Pili) KOTI JEUSI – 02

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tatu) KOTI JEUSI – 03 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Nne) KOTI JEUSI – 04 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Tano) KOTI JEUSI -05

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Sita) KOTI JEUSI -06 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Saba) KOTI JEUSI – 07

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Nane) KOTI JEUSI -08 

KOTI JEUSI (Sehemu Ya Tisa) KOTI JEUSI -09 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi) KOTI JEUSI -10 

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Moja) KOTI JEUSI -11

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Mbili) KOTI JEUSI -12

KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kumi Na Tatu) KOTI JEUSI -13

27 Comments

  1. Martha anataka kumuua mamaake????🥺🥺🥺🤒.. anhaaa kisa alimuua babaakee bhn na Mr george😅😅🥲… yaaniii watafarikiiiii hiii ni kila paradox cjui double killer mulemule

  2. Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tano) KOTI JEUSI – 15 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version