Kocha wa Manchester United Erik ten Hag ameiambia Manchester City kwamba Mashetani Wekundu wanaweza kuwashinda tena.

Ten Hag alisema kuwa Man United tayari wameonyesha kuwa wanaweza kukishinda kikosi cha Pep Guardiola, lakini akasisitiza kila kitu kinapaswa kuwa sawa ili hilo lifanyike.

Pande zote mbili zimetinga fainali ya Kombe la FA msimu huu na zitamenyana kwenye Uwanja wa Wembley mnamo Juni 6.

City inayonolewa na Pep Guardiola inafukuzia mataji matatu msimu huu na wakati Real Madrid wakisimama kwenye Ligi ya Mabingwa, Arsenal wakimenyana nao ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, Man United, timu pekee ya Uingereza iliyowahi kushinda mara tatu, inasimama katika njia Kombe la FA.

Manchester United waliwashinda Brighton kwa mikwaju ya penalti uwanjani Wembley na kukata tiketi ya fainali, huku Man City wakiandikisha ushindi wa 3-0 dhidi ya Sheffield United Jumamosi.

Mholanzi huyo aliiambia talkSPORT, “Tunataka kushinda fainali, yote ni kuhusu hilo.

“Tayari tumeonyesha msimu huu kwamba tunaweza kuwashinda.

“Pia tulipata kipigo kikali, lakini tulionyesha katika mchezo wetu wa nyumbani kuwa tunaweza kuwashinda, lakini kila kitu kinapaswa kuwa sawa.”

Leave A Reply


Exit mobile version