Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa mashindano ya kombe la dunia ka upande wa klabu (FIFA CLUB WORLD CUP) ambayo ni tarehe 12 hadi  22 ya disemba 2023 michuano itakayofanyika nchini Saudi Arabia.

Mashindano hayo yatakayofanyika nchini Saudi Arabia yatahusisha timu kutoka mabara yote Duniani ambazo ni Al Ittihad (Saudi Arabia), Auckland City (Australia), Léon [Mexico] , Urawa Red Diamonds (Japan) ,Fluminense (Brazil), Al Ahly (Egypt) na Manchester City (England).

Saudi Arabia linakua taifa la sita kuandaa michuano hii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 na kufanya Saudi Arabia kuendelea kuwa kivutio  katika masuala mbalimbali ya kimichezo nchini humo.

Toka kuanzishwa kwake mwaka 200 hii ni orodha ya washindi wa kombe hili kubwa zaidi kwa upande wa klabu :

Mwaka 2000 michuano hii iliandaliwa nchini Brazil na bingwa alitoka katika nchi hiyo ambapo alikua ni Sport Club Corinthias Paulista. Japan ilishika hatamu katika kuandaa michuano hii ambapo waliandaa mfululizo na mabingwa ni katika mabano ,2005(Sao Paulo), 2006 ( Internacional) , 2007 ( AC MILAN) , 2008 ( Manchester United) .

Mwaka 2009 na 2010 michuano hii ilifanyika UAE ambapo 2009 bingwa alikua Barcelona kisha mwaka 2010 bingwa akawa Inter Millan. Mwaka uliofuata Japan akaandaa tena michuano ambapo 2011 (Barcelona) na 2012 akawa Corinthias.

Morocco aliandaa mwaka 2013 bingwa akawa Bayern Munchen  na 2014 bingwa akawa Real Madrid  na baada ya hapo msimu wa 2015 bingwa alikua Barcelona na msimu wa 2016 bingwa alikua Real Madrid michuano ambayo iliandaliwa na nchi ya Japan. Mabingwa walikua hivi 2017(Real Madrid) 2018( Real Madrid) 2019( Liverpool) 2021( Bayern Munchen) 2022 ( Chelsea).

Kwa mwaka huu vilabu hivi ndio vinashiriki Al Ittihad , Auckland City , Léon  , Urawa Red Diamonds ,Fluminense , Al Ahly na Manchester City unadhani bingwa atakua nani mwaka huu?

Endelea kusoma taarifa zetu na makala mbalimbali za michezo kwa kugusa hapa.

 

 

 

 

 

2 Comments

  1. Pingback: Washindi Wa Tuzo Za CAF Mwaka 2023 - Kijiweni

  2. Pingback: Mechi Kali Za Kutazama Leo - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version