Kocha msaidizi wa Chelsea, Anthony Barry amechukua uamuzi wa kuungana na Thomas Tuchel katika klabu ya Bayern Munich.

Tuchel kwa sasa ndiye kocha mpya wa Bayern Munich kufuatia kutimuliwa kwa Julian Nagelsmann.

Kocha huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain alifanya kazi na Barry wakati akiwa Chelsea na tayari ametangaza hadharani nia yake ya kumleta Ujerumani.

Kwa mujibu wa Sky Germany, Barry anataka kufanya kazi chini ya Tuchel kwa mara nyingine licha ya Chelsea kutotaka kumruhusu kuondoka Stamford Bridge.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa Chelsea na Bayern Munich sasa wako kwenye ‘mazungumzo ya juu’ kuhusu dili la kumnunua Barry.

Leave A Reply


Exit mobile version