KOCHA MASHUJAA AKIRI MAMBO NI MAGUMU , MBINU ZIMEJULIKANA

Kocha Mkuu wa kikosi cha Mashujaa kutoka Kigoma Abdallah Mohammed almaarufu kama Baresi amekiri kuwa kwa sasa kikosi chao kinapitia wakati mgumu na wana hali mbaya sana.

Baresi amezungumza hayo baada ya kupokea kichapo cha tano mfululizo kwa kuchapwa na KMC mabao 3:2 mchezo uliokuwa wa kuvutia uliochezwa katika uwanja wa Uhuru.

Kocha huyo anasema kuwa kwa hivi sasa tayari wapinzani wao washajua mbinu na njia zake hivyo kuyatumia madhaifu hayo kuwafunga.

Tulianza vizuri tumeonyesha ushindani wa kutosha sasa tunapitia mambo magumu ambayo ni muda wa kurekebisha kabla ya kurudi tulikotoka tunarudi tumekaribiswa sasa ni wakati wa kupambana”

Klabu ya Mashujaa haijaonja ushindi tangu ilipoifunga Ihefu kwenye mechi ya ligi kuu bara iliyopigwa Septemba 16 jambo ambalo limewafanya mpaka sasa kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi kuu bara.

Leave A Reply


Exit mobile version