KLABU ya Crystal Palace imemtaja kocha atakayesimamia mchezo wao wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal wikendi hii kufuatia kutimuliwa kwa Patrick Vieira siku ya Ijumaa.

Kulingana na talkSPORT, nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Paddy McCarthy atakuwa msimamizi wa safari yao ya Uwanja wa Emirates siku ya Jumapili.

Klabu hiyo ilitangaza kuwa McCarthy, ambaye ndiye kocha wa sasa wa Vijana wa U-21, ataungana na kocha msaidizi wa U21 Darren Powell watakapowatembelea viongozi wa ligi.

Kocha wa makipa, Dean Kiely, ambaye hakuwa miongoni mwa wakufunzi wa Vieira waliofukuzwa kazi pamoja na Mfaransa huyo, pia atafunga safari.

McCarthy aliongoza mazoezi ya kikosi cha kwanza siku ya Ijumaa asubuhi lakini Palace haijatoa habari zaidi kuhusu nani anaweza kumrithi Vieira kwa misingi ya kudumu baada ya mapumziko ya kimataifa.

Leave A Reply


Exit mobile version