Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuondoka kwao kwenye Ligi ya Mabingwa kumewapa “kazi kubwa” kuokoa msimu wao wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Hata hivyo, Klopp ameeleza kuwa mechi tatu ndani ya wiki moja dhidi ya Manchester City, Chelsea na Arsenal zitatengeneza au kuvunja matumaini yao.

Bao la dakika za lala salama la Karim Benzema katika kipindi cha pili lilitosha kwa Real Madrid kupata ushindi wa 1-0 wa hatua ya 16, mkondo wa pili Uwanja wa Santiago Bernabeu na ushindi wa jumla wa 6-2.

Kuondolewa kwa Liverpool kunamaanisha watamaliza msimu bila taji.

Kwa sasa Wekundu hao wako katika nafasi ya sita kwenye Ligi ya Premia na wanakabiliwa na vita ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Wako pointi sita nyuma ya Tottenham Hotspur walio nafasi ya nne na mbili nyuma ya Newcastle ambao wana mchezo mkononi.

“Tunataka kuwa katika Ligi ya Mabingwa kila mwaka na ni kazi kubwa kwetu [kumaliza nafasi ya nne] na tunajua hilo,” Klopp alisema.

“Baada ya mapumziko ya kimataifa, tuna wiki sahihi mbele yetu – City, Chelsea na Arsenal.

“Hiyo labda itafafanua kile tunachopata kutoka kwa msimu.”

Leave A Reply


Exit mobile version