Ni takribani wiki moja sasa imebakia kabla michuano ya AFCON haijaanza kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali nchini Ivory Coast ambapo itaanza kuchezwa Januari 13 mpaka Februari 11 mwaka 2024.
Ni moja kati ya michuano inayosubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na uwepo wa wachezaji wengi waliovuma kutoka bara la Ulaya bila kusahau wale maarufu wanaocheza ligi ya ndani. Zaidi ya wachezaji 80 kutoka katika vilabu vinavyoshiriki ligi mbalimbali barani Afrika walau kuna mchezaji kaitwa katika timu ya Taifa na hii leo tutazame klabu ambazo zimetoa wachezaji wengi zaidi kwa ajili ya AFCON 2023.
Tukianza na klabu kutoka Afrika Kusini ambayo ni Mamelodi Sundowns wao katika michuano hii wametoa wachezaj 11 kwa ajili ya timu ya taifa ya Afrika Kusini kwa ajili ya michuano hii ya AFCON na kuwa moja kati ya klabu iliyotoa wachezaji wengi zaidi.
Katika orodha anayefuatia ni klabu ya karne kutoka Misri ambayo ni Al Ahly wao wametoa wachezaji 10 ambao watawakilisha nchi zao na miongoni mwa wachezaji hao yupo Percy Tau atakayechezea Afrika Kusini bila kusahau Aliou Dieng wa Mali Pamoja na wengine watakaochezea Misri.
Kutoka hukohuko Misri anayefuatia ni Pyramids ambaye katika orodha anashika nafasi ya 3 akiwa ametoa wachezaji 9 kwa ajili ya Afcon na moja ya mchezaji maarufu ni Fiston Mayele anayeenda kuitumikia nchi ya demokrasia ya Congo.
Simba na Yanga wao kila mmoja ametoa wacheza pia katika michuano ya msmu huu ambapo wekundu wa msimbaziwametoa wachezaji 7 huku Yanga wakitoa wachezaji 6 bila kusahau Orlando ambao nao wametoa wachezaji 6 wakifuatiwa na Mazembe aliyetoa 4 msimu huu.
Endelea kusoma zaidi kuhusu AFCON kwa kugusa hapa.