Ilipoishia “Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni mrefu kwa Wanandoa hawa kuungana pamoja, Alexander hakuamini kabisa kwamba mwanamke aliekuwa akiishi nae kumbe alikuwa anagrade za juu kwenye ufahamu wa hisia zake kwanini Sasa alienda kwa Maina muda huo Hadi amsababishie Minnie matatizo?

Endelea 

SEHEMU YA ISHIRINI 

Ni Asubuhi kunapambazuka Alexander alikuwa wa kwanza kuamka aliingia bafuni kuoga Minnie ndio anaamka anashangaa kumuona Alexander tayari kashabadili mavazi kakaa kitandani akimsubili aamke.

“” Alee hata kuniamsha hamna jamaniii mbona Hivyo..!?”

Alexander ikabidi amtizame vizuri huku akimshika kidevu kwa kumuinua baadae alimkisi kwenye paji la uso.
“” Nategemea siku ya Leo tuwe tumepiga hatua katika maisha yetu, naona familia yetu inaenda kuongezeka kwa matokeo ya usiku mmoja tu.”

Minnie akachukia akainuka haraka haraka akiwahi bafuni kuoga, baada ya kumaliza alivaa nguo zake za ubandit make hakuwa na nguo nyingine za kubadilisha.

“” Vipi… Mbona wanikodolea mimacho?” Minnie akamhoji Alexander huku akifungua nywele zake zilizokuwa zimefugwa na Alexander misri ya kamba za katani.

Alexander hakutaka kumuona mrembo wake anazidi kuhangaika tayari ashampenda, aliinuka na kumsaidia kufumua kisha alimsaidia kubana misri ya mkia wa farasi kama alivyodai awali.

Wakati wanazidi kuandaana Ghafla sauti ya Bunduki ililindima ikawapelekea wote washituke walibaki kutazamana kwanza.

Muda huo huo Mlango ukabishwa alikuwa ni Abdul.
“” Miniii!! Miniii!! wahi haraka nje tumevamiwa chukua hii hapa Bastola itakusaidia.”” Akifanya kumrushia.

Alexander yeye hakuelewa kipi kinaendelea ilibidi amtizame Minnie ambae anataka kumuacha mule ndani alimshika mkono Kisha akamvuta karibu yake.
“” Tafadhari usiende baki na Mimi ndani! Please Minnie nakuomba tenaa, huko unaweza dhurika.””

“” Alexander jamaniii!! Ngoja tukaone kinachoendelea nje, Mimi nitakuwa salama tuongozane pia, au ubaki tu.”

“” Miniii fanya haraka Baba’ngu Mimi anauwawa huko!” Abdul akamrudia Minnie baada ya kuona anakawia.

“” Nakuja Abdul, Alexander Naomba ubaki hii misheni ipo sereous.”

Huku kwa Kamanda Mzobe akawa amesikia taarifa ya Nyumba ya waziri wa kilimo imezungukwa na wanajeshi pamoja na Maaskari,, hapo hapo ndio akakumbuka Binti yake yupo kule akajua kabisa hizo ni njama za White House! Alichukua jeshi lake nayeye kuwahi pale haraka kwa usalama wa bintie.

Minnie ndio akafanikiwa kutoka nje anashangaa kuona wanajeshi wamezunguka jengo Hilo huku sauti za mtutu wa Bunduki zikipishana yaani wale wanyanganyi wa waziri wa mifugo nao walikuwa wakishambulia kuwarushia wanajeshi mabomu ya machozi.

Alexander nae alishidwa kukaa ndani aliangalia kwenye hicho chumba kulikuwa na koti kubwa akawa amevaa akienda kumsaidia Minnie.

Taharuki iliyoendelea pale ilikuwa kubwa sana mji mzima uliingia hatiani, White House ilibidi atoke pamoja na walinzi wake akiwa na hofu kubwa kuhusu kijana wake Alex alijua kabisa ndio yupo kwenye Mission hiyo, lakini muda si mrefu Bibi akamletea taarifa hata Alexander nae alikuwa kule na ndiko alipolala! Alihisi kuchanganyikiwa yaani vijana wake wawili wapo kule lakini pia kunae Binti yake Minnie make ni mtoto wa aliewahi kuwa mkewe yaani Mama Alex nae ni miongoni mwao hakuwa na budi kuwahi.
Aliwasha gari haraka kuelekea eneo la tukio.

Huku Kamanda Mzobe nae akawa amefika akiwa kavalia kiraia zaidi make angevalia kijeshi Sheria ingemlazimu kushambulia waasi akaona bora kuungana upande wa Minnie Ili amtoloshe.

Alifika mpaka kwenye jengo alikuta mashambulizi ni makubwa sana yaani kumechangamka, muda huo huo akapokea simu kutoka Mbeya kuwa Nickison yupo kwenye kikosi Cha kukamata waalifu alikuwa ni Kamishina wa jeshi la Mbeya akimjulisha baada ya kupata taarifa kwasasa ni Mwanajeshi aliomba sapoti ya kuwasaidia vijana wake!
“” Sheet Nini hiki kinanikuta yaani kijana wangu ndio kaja kunikamata? Na vipi Binti yangu atakuwa kwenye wakati gani sahii?”

White House nae akafika akiongea na Kamishina azuie mashambulizi lakini Upande wa majambazi walikuwa wamejipanga hawakuwapa muda kuwashambulia.

Kamanda Mzobe alishidwa kuvumilia alijipenyeza akiwa anakimbilia upande aliohisi Minnie yupo kule aliita kwa nguvu.. “” Minniiiiiiiii….!!”

Minnie ndio akashituka akajua sauti Ile ni ya Baba’ke ilibidi ashushe siraha yake kwanza haamini Baba’ke kama angetoboa kukwepa risasi zilizokuwa zinamiminika mfululizo.

Huku kwa Nickson akawa amesikia sauti ya Baba’ke alijikuta akishidwa kushambulia akiwaamuru waache lakini sauti yake haikuwa kitu muda huo zaidi ya mlio wa risasi ukipishana.

Muda huo huo White House nae akapaza sauti baada ya kumuona Alex kamuweka Target Baba’ke Minnie, alipaza sauti.. “” Alex acha usifanye hivyo..”

Huku Kamanda Mzobe alibahatika kujificha kwenye Moja ya nguzo huku akinyosha Bastola kumuelekea White House mara tu baada ya kusikia sauti, hasira ya kisasi ikawaka moyoni mwake akaona ni wakati wa kumalizana nae iwe kama ajari tu.

Huku kwa White House aliendelea kumzuia Alex asishambulie make alijua huko alikoelekeza Bastola yupo Minnie na huenda Alexander akawa pembeni yake pia.

Muda huo Alex ndio akaona Kuna mtu pembeni kanyosha Bastola kuelekea uelekeo wa Baba’ke akaona kama atashangaa Baba’ke atapoteza maisha ikabidi amuwahi target akikikoki bastola vizuri, huku kwa Kamanda Mzobe alichelewa kumfyatua risasi baada ya kusikia sauti ya Minnie ikimuita hii ilimfanya achelewe kuweka target hapo hapo sauti ya risasi ikasikika imetua kifuani na risasi hii ilitoka Moja kwa Moja kwa Alex.

Minnie ndio akapiga kelele akiita Baba hapo hapo Alex akasikia sauti ya Minnie huku akiwa kashikilia Ile Bastola akitetemeka, Nickison nae alikuwa busy upande wa pili kushambulia ndipo anashangaa watu wameacha kushambulia wamesogea sehemu moja hata wale majambazi waliacha kushambulia na hii ni baada ya kumuona Baba’ke Minnie yupo chini, ndipo akasogea anashangaa kumuona ni Dada’ke Minnie akiwa kamkumbatia Baba’ke na kifuani nguo ililowa kwa damu huku Minnie aliizuia kwa kiganja chake.

White House ndio akapata kusogea karibu hutaamini alipiga magoti akilia Kisha alimshika mkono Kamanda Mzobe akiongea.
“” Mimi sikumuua Mkeo ilikuwa ni ngumu wewe kunielewa,,, kwa kuweka kisasi ndiomaana leo tunaishia pabaya!”

Nickison akabaki kushangaa baada ya kumuona Baba’ke yupo chini alilia zaidi huku akizidi kulalamika.
“”” Nilijua haya yote yatatokea angalia Sasa kwaajili ya kisasi ulimuweka Target kumuua Kamanda Denishoo lakini mwanae nae ni Kamanda isingekuwa ngumu kuruhusu Baba’ke awekwe Target, kwanini lakini Baba inakuwa hivi,, eti Minnie si nilikuzuia habari ya kisasi… kwanini Sasa hukunielewa..?””

Minnie ndio akawa amesikia akajua moja kwa aliehusika ni Alex akachukua Bastola yake akimuwekea target, Hapo hapo Alexander akawahi mbele ya Alex akitangiza.
“” Tafadhari Minnie usifanye hivyo kama utamuua Kaka’ngu utafaidika Nini? Acha kisasi Cha namna hiyo,, hivi kweli hujabadilika tu na wakati nimekuomba sanaa?”

Minnie akachoka anawezaje kumnyoshea Bastola mwanaume wake wakati usiku wa jana tu walikuwa kwenye penzi zito kingine Kuna upendo ulikuwa umezaliwa ndani yake! Alifunga macho na kuanza kulia akimtizama Baba’ke ambae yupo chini ikabidi akae kwanza, Ile kakaa tu Nickison akashika Bastola akaamua amalizie game isingekuwa rahisi kumuona Baba’ke anatapatapa chini na wakati muuaji yupo kuwatizama, alimsihi Minnie atafute namna ya kumuwahisha Baba yao hospitalini kwanza.

Hapo hapo sauti nzito ya White House ikasikika.
“” Nickison mwanangu usifanye hivyo! Huyo ni ndugu yako tafadhari usimnyoshee Bastola! Kama unataka kumuua yeye basi Niue Mimi Ili ulipize kisasi Cha wazazi kwa wazazi achana na kisasi na ndugu yako yeye hajakosea alikuwa kikazi.””

Muda huo huo Familia ya White House ikawasili yote ikiongozwa na Bibi! Huku Kamanda Mzobe akawa kachukuliwa na jeshi kuwahishwa hospitalini Minnie yeye Bado hajielewi tu muda huo Alexander alikuwa sambamba kamkumbatia pale chini, ndipo Bibi nae alisikika akizungumza;-

“” Minnie mjukuu wangu! Naomba unisamehe pia Mimi na Mwanangu tuliamua kuficha Siri hii tulijua kama tutasema ukweli huenda tungempoteza Alex, Mama’ko wewe… ndie Mama’ke Alex na pia alikuwa ni mke wa Denishoo na walibahatika kupata mtoto Mmoja ambae ndio Alex ilikuwa ni ngumu kuweka wazi Siri hii lakini hata Baba’ko nae alipata ugumu kuwaeleza Moja kwa Moja kuwa Mama’ko aliwahi kuwa mke wa white house, Najua mngejisikia vibaya kwa hilo Naomba mnisamehe mimi pamoja na White House najua ni ngumu kumuita Baba ila muite kwa niaba ya Kuwa mkwe angalau kupitia Alexander muite Baba.”

Nickson muda huo alihisi kuchoka alienda kuegama kunako Moja ya nguzo akisikiliza ilifikia wakati alishidwa hata kuelewa ni kipi kinazungumzwa zaidi ya kuona midomo ikicheza cheza,, taratibu nguvu zilianza kumuisha huku akishuka taratibu kuelekea chini.

Alex nae alishidwa kabisa kuamini alijikuta anasogea karibu alipo Minnie akimtizama kwa makini ni kweli wao ni watoto wa Mama mmoja? Alikumbuka siku Ile ya sherehe atoke kuomba Dua kwenye Kaburi la Mama’ke akutane na Minnie inamaana alikuwa pia akienda kufanya Dua? ikabidi amuulize.
“” Ile siku kwenye bustani ulienda kufanya Nini? Inamaana hata wewe ulikuwa ukifahamu Mimi ni ndugu yako?”

“” Sikufahamu ila nilitaka kuchunguza tu! Baada ya kuona majina ya Mamangu yapo pale. Hata hivyo niliwauliza familia lakini sikupata majibu,, Alexander analifahamu hilo nilimuuliza japo alijua naigiza. “”

Upande wa Alexander aliona mambo yamekuwa magumu kama Minnie ni tumbo Moja na Kaka’ke anawezaje kuwa nae tenaa katika mahusiano tayari ni ndugu yake yule kingine alihisi maumivu yaliyopenya ndani ya moyo wake ilibidi ainuke lakini Alex akamshika mkono akimrudisha karibu akimtizama.
“”” Najua mdogo wangu unampenda sana Minnie kwasasa! Usijali mambo yatakuwa sawa tu.””

Huku kwa Nickson akawa ametua chini kwa kuzungu-zungu, Minnie akawahi kwenda kumsaidia tayari alikuwa hoi mwili wote umelegea.

+++++++++

Baada ya Nusu saa waziri wa kilimo alikamatwa kuelekea kituoni tayari kwa kuhojiwa kwanini alikuwa akikaa na kundi la wahaarifu nyumbani kwake?

Huku kwa Minnie alikuwa yupo hospitali akisubili majibu kwa wagonjwa wake, huku akiwa sambamba na familia ya White House japo bado anamaswali mengi kama White house hakumuua Mama’ke basi ni nani alimuua?

Baadae Daktari alikuja kutoa majibu .. Nickison anaendelea vizuri ilikuwa ni mshituko tu ulipelekea hari yake kuwa vile, lakini upande wa Baba alikuwa bado yupo ICU akipambania uhai wake.

Kwa Alex alikuwa ni mtu mnyonge sana mara baada ya kugundua risasi yake ilitua kifuani kwa Baba’ke Minnie hakupata Amani kabisa mwisho kabisa aliomba ruhusa aingie kumuona Baba’ke na hii ni baada ya kuona madaktari wakitoka chumbani akawa ameruhusiwa. Alifika akamtizama hali aliyonayo Kisha alimshika mkono huku akilia sana akiwa bado kaushika mkono .
“” Baba Naomba unisamehe sikujua kama Mimi leo hii kazi yangu Kuna siku mikono yangu itaumiza maisha ya watu wengine, angalia hali yako kwasasa upo hapa kwaajili ya mikono yangu, nawezaje kuishi kwa furaha ukiwa katika hali hii vipi kuhusu Nickison na Minnie watanitazama vipi Mimi? Nisamehe Baba najuta Mimi.”

Kilio Cha Alex ni kama kilienda kumuamsha Kamanda Mzobe, taratibu alifungua macho akimtizama Alex Kisha alitamani kumshika mkono lakini alishidwa akawa ameongeza nae kwa Shida kabisa.
“” Ikiwa upo katika kazi hutakiwi kujilaumu ulivyofanya ni sahihi hata Mimi ningefanya Vile vile kumuangamiza adui, muda ule nilikuwa kama adui ndio maana ukanishambulia! Umefanya Haki na umeitendea vizuri kazi yako! Hata nikipumnzika Naomba uwe na Amani lakini watizame ndugu zako hawana familia nyingine zaidi yako, Niahidi utafanya hivyo.”

Kamanda Mzobe akamaliza kuongea Kisha akaanza kukohoa huku Alex akimuahidi kufanya vile! Muda huo huo Nickson na Minnie wakaruhusiwa kuingia ndipo wanashangaa kumuona Baba angalau anapepesa macho, alionesha ishara Alex asogee kisha aliwashika mkono ni kama anawaunganisha.
“” Naomba mkae kwa amani! Msiendeleze kisasi! Kisasi hiki Naomba kiishie hapa hata mkimjua aliehusika na kifo Cha Mama yenu! Msameheni Ili muishi kwa furaha kisasi pekee Mungu ndio mlipaji.””

Huku Mahakamani White House alipata ushahidi ambao alikuwa akiutafuta miaka ishirini ya kifo Cha mkewe, siku zote alikuwa akituma watu mbalimbali kufatilia ushahidi ndipo leo ushahidi ukafika mahakamani ilikuwa ni flash iliyonasa matukio yote kipindi kile taharuki inatokea, ushahidi ukawa umekwa mbele ya mahakama hutaamini mtu aliemshoot risasi alikuwa ni Baba’ke Abduly, wakati mzozo unaendelea yeye alionekana kushuka kwenye gari ndipo alijipenyeza katikati ya watu ndipo aliachia risasi ikawa imetua kifuani kwa Miricka Deusdely na hapo umauti ulipomkuta.

Huku Hospital baada ya Kamanda Mzobe kuwaunganisha wanandugu hawa watatu hapo hapo alipoteza maisha.

+++++++

Yapata mwezi kuisha mwili wa Kamanda Mzobe ulistiriwa White House ukiwekwa sambamba kabisa karibu na mwili wa Mama’ke Miniii.

Msiba ulikuwa mkubwa sana kwani watu wote hawakuamini hata hivyo Kila kitu kilikuwa wazi aliehusika na kifo Cha Miricka Deusdely alikuwa ni waziri wa kilimo! Hata alipohojiwa alikili yeye ndio alipanga njama mapema ya kumteka Minii kule porini Nia ilikuwa ni kuwatumia katika kazi zake za unyampala na ndipo waliingia mkenge wakizani wamepata mtu wa kuwasaidia kulipa kisasi kumbe aliwatumia tu na hata kumuua Miricka Deusdely ilikuwa ni kuwagombanisha wao na White House na hii ni kwakuwa alikuwa na kisasi na kisasi chake kilikuwa baina yake na White House yote ni maswala ya kibiashara ndio yalipelekea kuwa na uasama ikabidi na yeye kisasi chake akielekeze kupitia familia ya Kamanda Mzobe make walionesha kuwa na kisasi na kama angefanikiwa kumuweka ndani White House basi biashara zake zingesimama na yeye akitumia nafasi hiyo kukuza biashara zake.

++++++++++

Mambo yote yalipita ilikuwa ni muda wa kutengeneza maisha tenaa upya japo kwa Alexander hakuwa na amani kabisa ilikuwa ni ngumu kukubali maamuzi kuwa yeye kwasasa hawezi kuwa na Minnie, siku hiyo alikuwa akizunguka zunguka uwani mara simu yake iliita alikuwa ni Maina kampigia simu.
“” Hallow Bwana Alexander! Vipi kwasasa haunihitaji tu? Nishajua Minnie ni ndugu yako si bora urudi kwangu tufunge Ndoa unajua kipindi kile nilidanganya na mimba lakini Sina mimba! Panga siku basi tuonane.”

“” Aaa Maina sitaki habari hiyo tenaa! Kwasasa hakili yangu haipo kwenye Ndoa tena natakiwa nifanye mambo yangu tu. Sitaki usumbufu.”

Huku kwa Minnie aliamua kumtafuta Abdul alijua kabisa yupo katika wakati mgumu, kitu ambacho hakuamini yaani Baba’ke Abdul alivyomuoneshea upendo kumbe alikuwa akiwazunguka, hakuwa na namna zaidi ya kuachilia waanze upya aliamua Leo kumpigia simu angalau ajue hali yake anajua kabisa kwasasa atakuwa kwenye wakati mbaya, alipokea wakazungumza;-
“” Ee Abdul upo wapi lakini.. nataka nikuone basii.”

“” Minnie nahisi umechelewa tayari nipo Airport hapa naelekea USA nataka nikaanze maisha upya Kuna miradi mingi ya kusimamia ilianzishwa na Baba! Ila wakati mwingine nitarudi kwaajili yako nataka nikuombe radhi mbele yako naimani utanisamehe.”

Minnie akachoka akaona na yeye ni kama Dunia imemzunguka inamaana hana pakuegamia tena watu wake wa karibu wameondoka, aliamua kumfuata Kaka’ke ambae nae muda huo alikuwa anaongea na simu ikabidi amsikilize kwa kuibia.

“” Asia! Hivi karibuni nitarudi huenda nikawa na furaha nikiwa kando yako lakini vipi Dada’ngu nikimuacha ataishije hapa, Minnie hana furaha kabisa nahisi amepoteza pakubwa naona Ndoa aliyoifunga aliipa kibari lakini Alexander tayari ni Kaka’ke, na kuhusu Abduly yule kwasasa hayupo tena Tanzania,, amemuacha ameondoka na huyu ndie nilitegemea ampatie furaha lakini ndio hivyo tenaa!”
Alikuwa ni Kamanda mwenzake wa kike na hawa walikuwa wapo kwenye mahusiano na Nickson. Alimuacha kambini.

Minnie akawa amesikia vizuri maneno yale ilibidi aondoke mdogo mdogo hata kumuuliza tu alishidwa, ila aligundua Kaka’ke siku si nyingi atarudi kambini.

Aliamua siku hiyo atoke angalau akabadilishe mazingira huenda akawa sawa lakini muda huo huo Alexander alikuwa akimfatilia tu alivyoona katoka akajua huenda kaenda kujiua akafanya kumfatilia nyuma nyuma.

Safari ya Minnie ilienda kuishia ufukweni alikaa huku akitizama mawimbi huku upepo mwanana ukivuma pande za Dunia, Alexander akaamua kumsogelea na kukaa karibu yake huenda akawa mfariji muda huo.

Lakini wakati huo huo Alex pamoja na Brighton pamoja na Mama Miriii walikuwa wakiwafatilia pia, walijua kabisa kwasasa wanapitia wakati mgumu kama unavyojua mazoea Yana tabu ndio hali anayokutana nayo Minnie na sio yeye tu hata Alexander nae anaumia vile vile.

Minnie alishituka baada ya kuguswa begani alimtizama aliemgusa ndio alimuona ni Alexander hapo hapo alisimama na kumkumbatia huku akilia.
“” Alexander nimeshidwa kumove on! Tayari nishakupenda na kingine nahisi kama hali ya tofauti katika mwili wangu. Sijui itakuwa sahihi..?”

Alexander akamkumbatia kwa big hugs( kumbatio kubwa ) huku machozi yakidondoka.
“” Hata Mimi nimeshidwa kumove on,, Nawezaje kuyakimbia Mapenzi yangu,,, je nani alaumiwe ni sisi kupendana au ni wazazi wetu? Au tulaumu kisasi ndio kimetukutanisha au tushukuru kisasi ndio kimetuunganisha..?”

Huku kwa Alex , Brighton pamoja na Miricka walibaki kuwatizama tu mpaka na wao nyoyo zao zikajawa simanzi walijikuta wakiugumia moyoni wakilia, Mama Miricka alishidwa kuyahimidi maumivu yake alijikuta akiwakimbilia na kwenda kuwakumbatia huku Alex, Brighton nao wakaenda kuungana nao. Hapo hapo Hali ya Minnie ikabadilika kutokana na Hali ya hewa ilimchanganya alihisi kichefu chefu alijitoa kwenye kumbatio na kwenda kutapika pembeni.

Muda huo huo anatapika White House pamoja na Bibi nao walifika inamaana walikuwa wakiwafatilia, hawakuamini kitu walichokiona inamaana tayari Minnie ni mjamzito na ujauzito wake ni wa hivi karibuni, labda niwakumbushe ni Ile siku wakutane na Alexander kwao Abduly ndipo ujauzito ukipatikana usiku huo.

Alexander ikabidi akamsaidie mkewe make alipata shida kweli alihisi mwili wake kulegea ikabidi ambebe na kwenda kumpakia kwenye gari huku akitoa koti lake akimfunika asipigwe na baridi Kisha alimpigia Daktari wa nyumbani afike mara Moja.

Ikabidi wote waongozane nyumbani Kila mtu alifika nyumbani akiwa na mawazo wakisubili majibu ya Daktari, Daktari alitoka akiwa na majibu Minnie ni mjamzito wa wiki nne. Wanafamilia wote wakabaki kwenye sitofahamu je ni njia gani watumie kuwatenganisha ndugu hawa wasiwe kwenye mahusiano na kingine Minnie ni mjamzito..

UNAHISI NI BUSARA IPI ILITAKIWA KUCHUKULIWA HAPA…? 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

 

12 Comments

  1. Mwendelezooooo admin 🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌mbon kmya au tuanze kuchanga pesa😋😋😋😂😂😂😂

Leave A Reply


Exit mobile version