Ilipoishia ” Baada ya kugeuka Minnie; Alexander akashituka ikabidi alale kwanza ikiwa ni karibu yake Ili afanye kumtizama kwa kumchungulia. Akawa anazisogeza nywele zake zilizomwagika usoni Kisha alifanya kuegama begani kwake, Minnie akataka kujinasua ndio anakumbuka muda si mrefu usingizi ulikuwa mzito kwahiyo anafaa kuendelea kuigiza.
“” Minnie kipi umekifanya Leo? Unajua siamini Ani,, nilitrack simu yako nikaona upo chumbani umefungiwa kwani ulitokaje Minnie, inakuwaje unakuwa spy wa white house? Si uniambie mission yako hapa ni Nini? Uliniomba nifatilie kuhusu yule mwanamke na leo nilipata majibu,,, ila sizani kama naweza kukwambia tena… Unajua umenichanganya?

ENDELEA 
SEHEMU YA KUMI NA TANO 

 

Minnie muda huo kajikausha tu kama hajui kinachoendelea alivumilia ukaribu wote wa Alexander mpaka alipoamua kumuachia na kulala pembeni yake.

Huku chumbani kwa Alex usiku ulikuwa ni mkubwa kwake Kila mara kumbukumbu ya Minnie ilikuwa ikijirudia kichwani ni kama Kuna ukweli furani kichwani mwake anajiuliza huyo Minnie garden alifata Nini? Lakini alizidi kukumbuka sura yake sio ngeni akazidi kuwazua zaidi ndipo kumbukumbu zinamjia ni kama aliwahi kumuona karibu na Nickson.

Mama Mirii ndio akashituka usingizini anashangaa kumuona mmewe anazunguka chumbani ni kama Kuna jambo lamtatiza.
“” Baba Miriii Kuna shida, mbona usiku wote hujalala?”

“”” Aaa Kuna mambo tu yananichanganya hapa ya kazini kwangu.”

Mama Mirii ikabidi asimame akimsogelea Mmewe akamshika mkono akimkalisha kitandani.
“” Tulale Baba Miriii Ani upo nyumbani bado unaendelea kufikilia maswala ya kazini kwako, hebu relax basii.”

Alex ikabidi amkumbatie mkewe huku akitafuta usingizi japo ulikuja kwa shida sana.

Asubuhi kunapambazuka Minnie ndio anaamka akiwa bado ana usingizi make alichelewa kulala siku hiyo anatizama saa kupitia simu yake muda ulikuwa umeenda tayari ilikuwa ni saa tatu kasoro, aliamka upesi upesi huku akiwahi bafuni kuoga Kisha alijiandaa haraka haraka akitoka, anafika sebuleni anakutana na Alex ni kama alikuwa akimtafuta.

“” Aaa Shem, mzima lakini…?” Minnie akajiwahi kumsalimia.

“” Ooh mzima tu, vipi kichwa kimepoa?”

“” Kichwaa…?”

“” Yaah! Alexander kanambia waumwa.”

“” Yaani huyu Alexander Mimi siumwi bhana!”

“” Hahahaa! Mna utani nyie, Aya twende nikusogeze kazini kwako make pia naelekea huko.”

Ikabidi Minnie waongozane na Alex pamoja kazini wakiwa kwenye gari Alex alitoa simu yake na kumuonesha Minnie ilikuwa ni picha.
“” Wamfahamu huyu..?”

Minnie ndio akaona picha akashangaa kwani alikuwa ni Kaka’ke Nickson, alifanya kuitizama picha kwa hofu huku akimtizama Alex anaesubili majibu.

“” Ni nani yako…!!?”

“” Simfahamu.”

“” Ahaa! Nilijua utasema vile, lakini nishakufahamu vizuri, wewe hapo ni Kaka’ke na Nickison na siku ya mwisho tulionana na wewe ukienda kuwinda ndege porini, kinachonishangaza ni wewe umefikaje hapa na tena ukaolewa na mdogo wangu imekaaje anii..?”

Minnie akahisi tumbo la kuhara lakini alijikaza.
“” Vizuri umenifahamu, hata wewe ulinitia mashaka siku Ile ya sherehe nikuone garden uso kwa uso sura yako haikuwa ngeni nilianza kufatilia wapi nilikuona ndipo nikamtumia picha Nickison akashangaa nimekufahamu vipi, yaani hata wewe sikuelewi hapa umefata Nini? ”

Alex ikabidi acheke kwanza huku akisogeza gari na kupaki nje ya ofsi make alifika.
“” Yaani wewe unaniuliza hapa nimefata Nini? Mimi hapa ni kwetu, Sasa mwenzangu Mbeya to Zanzibar halafu white house umefata Nini yaani connection umeitoa wapi wewe?”

“” Mimi mwenyewe hapa hata sielewi kikubwa nimeolewa tu, kingine hata Sijui nimeolewaje hapa.””

“” Una furahisha ujue..!? Sitaki kupata majibu kwako ila nitafatilia kwa makini jambo hili. Lakini vipi kuhusu Ndoa yako na mmeo?”

“” Mimi Sina Mme bhana! Ndoa gani ya kupangiwa..?””

“” Kwahiyo huna furaha nayo?”

“” Hivo hivo tu.”

Muda huo Alexander alikuwa anatoka nje akiongea na simu. Alex akawahi kumuona akamuonesha Minnie.
“” Unamuona mmeo! Yaani Mnafaa kuwa pamoja.”

“” Anafaa kuwa na Maina, ndio maana na leo yupo nae.”

Minnie akaongea huku akifungua Mlango akishuka japo Alex hakumuelewa vizuri. Ikabidi na yeye ashuke wakipiga hatua kwa pamoja wakiingia ofsini wakafanya kumpita Alexander aliekuwa busy na simu.

Alex ikabidi aingie ofsini kwa Alexander huku Minnie ikabidi aingie ofsini kwake anafika anashangaa kumuona Maina kakaa kwenye kiti chake akifanya kuzunguka huku akimtizama kwa Dharau, Minnie akabaki kumtizama kwanza hakutaka maneno mengi alifanya kuweka mkoba wake Kisha akamsalimia.
“” Maina habari yako..!?”

Maina hakumjibu akawa kasimama huku mkono mmoja akiwa kabebelea splay alizidi kumsogelea, Minnie ikabidi kujihami akisogea nyuma lakini alichelewa Maina akawa kampulizia Ile splay usoni Minnie akaanza kulalamika macho yake yakiuma.

Maina akabaki kucheka huku akizidi kumsogelea.
“” Kitu kidogo tu Nimefanya, kama utaendelea kukaa karibu na Alexander Kuna siku nitakumwagia tindikali usoni.”

“” Maina kwanini lakini unanifanyia hivi, Mimi sipo na Alexander wako…?””

Huku kwa Alexander ndio anamaliza kuongea na simu, alitoka nje akija ofsini kwa Minnie amseme vizuri kwanini kachelewa kazini?”

Alex muda huo huo na yeye alikuja kumuaga Minnie aende zake hata hivyo alikuwa yupo na mishe mishe zake wakawa wamekutana.

“” Ooh kaka umemleta mchelewaji wangu kazini! Shida ya kufanya na watu kazi wasiojua maana ya kazi.”

Alexander akaongea huku akishika kitasa na kufungua, Alex nae akazama ndani ndio wanashangaa kumuona Minnie akipikicha macho huku akilalamika sana. Wote wakamuwahi kwa pamoja wakimtoa mikono machoni.

“” Minnie Nini shida… Fungua macho, kipi kimekupata?” Wakauliza kwa pamoja maneno Yale Yale yenye kuduwaishwa.

Alex ikabidi amtizame Maina akimsogelea.
“” Ni wewe umefanya hivi? Kwanini Sasa umefanya hivi Maina, yote ni kwasababu ya wivu tu?”

Alexander nae akashikwa hasira baada ya kumtizama, akamfuata…
“” Maina Nini lakini my unafanya? Unanifanya nichoshwe na tabia zako! Sahii ndio umekuwa na Kila Hira, jana nilikuoneshea ushahidi wa kumkamatisha Minnie lakini uliufuta tenaa, halafu kwanini uliwapigia Police waje nyumbani! Ulitaka familia yangu idhalilike? Kwanini lakini?”

Alex akawa anawasikilizia tu anashidwa kuelewa Alexander yupo anamtetea Minnie au anamkalipia tena.
“” Alexander kelele zenu zinachosha hebu mtizame kwanza Minnie hari yake kwasasa! Tumpeleke hospitalini.”

Alexander akawa kageuka kumtizama Minnie huku akizidi kumkata jicho Maina, Maina yeye baada ya kuona mambo yamekuwa mazito alichukua mkoba wake akatoka nje akichukua usafiri kuelekea nyumbani kwao.

Huku wakafanikiwa kumfikisha hospitali Minnie! Daktari wa macho akazidi kumpima vizuri.

Nje Alexander na Alex walibakia kuzunguka wakisubili majibu kutoka kwa Daktari.

“” Yote umesababisha wewe kwanini lakini unamganda Maina muda wote muweke mbali uishi maisha yenye furaha na mkeo, ona Sasa kamsababishia matatizo mtu aliekuwa akiona vizuri, na vipi asipoona?””

“” Hapana haiwezi kuwa hivyo, mbona unamchukulia hivyo, Minnie atakuwa mzima tu.”

Daktari akawa ametoka Ile kumuona tu wote wakamuwahi.
“” Minnie yupo salama, si anaona hakuna shida yoyote itamtokea si sawa?”
Alexander akawahi kuuliza.

“” Naona ni sumu imeingia kwenye mboni yake ya macho, hapa tumempatia dawa lakini tumemfunga kitambaa atakaa nacho Ili dawa ifanye kazi kwa siku mbili na siku ya tatu mtamrudisha hapa, kama tutamfungua akawa vizuri basi atakuwa kapona na ikiwa bado kunashida basi itabidi afanyiwe upasuaji.”

“” Upasuaji….!!!!!!!!!!!!!?” Wakarudia kwa kuuliza semi Moja.

“” Ndio, Ili macho yake yawe na mwangaza.”

Walihisi kuchoka kwa majibu ya Daktari, waliingia chumbani huku wakimtizama Minnie ambae Bado kalala kitandani na kweli alifungwa kitambaa usoni.

Alexander alikosa hata ujasiri wa kumsogelea zaidi ya kujishikiza mlangoni, Alex akawa amesogea Hadi kitandani alimshika mkono kwanza huku akimtizama kwa kumuonea huruma sana.
“” Minnie utakuwa salama! Hakuna jambo baya litakupata.”

Alexander akafanya kusogea huku akimpapasa Minnie kwenye paji la uso, alishidwa kuzungumza kitu zaidi ya machozi tu! Kila akifikilia Minnie bandit hatakuwa akimuona tenaa alizidi kuumia zaidi, Alex akawa ameligundua hilo alimshika mkono huku akimtizama usoni.
“‘ Atakuwa sawa, ngoja nikafatilie utaratibu unaoendelea turudi nyumbani.”

“” Kaka, Baba je unafikili nitamwambia Nini Mimi?”

“” Usijali mambo yatakaa sawa tu.”

Alex ikabidi aondoke akazungumze na Daktari huku Alexander akabakia kakaa na Minnie angalau alipata muda wa kuzungumza nae.
“” Minnie Naomba unisamehe kwa hiki kilichotokea naahidi nitakufanya uwe sawa kama ulivyokuwa hapo mwanzo.”

Minnie hakutaka kuzungumza zaidi ya mdomo wake kutetemeka yaani haamini ni kweli haoni, uoga wa kiza kutanda machoni ndio ulizidi kumnyima amani inamaana hizi siku atakuwa akiongozwa njia na vipi akiwa White House ni nani ataefaa kumuongoza inamaana mmewake ndio atapatiwa hilo jukumu alijiona ni mtupu kabisa wakati huo kama atakuwa karibu na Mmewe, sauti ya kwikwi ya kilio ndio ilitawala alimuita Alexander.
“” Alexander namtaka Baba hii hari sitaweza kuivumilia nikiwa mwenyewe! Nipe simu nimpigie kwanza aje anichukue.”

Alexander akahisi kuchoka yaani Minnie alitaka akae kwa Baba’ke kweli, na vipi yeye angemueleza kitu gani akamuelewa? Ikabidi aongee nae kwa utaratibu.
“” Minnie kukupeleka nyumbani utanisamehe! Baba’ko yupo busy na kazi na pale nyumbani hakuna mtu wa kukuangalia sitopenda ukakae mwenyewe lazima twende House white waangalizi wapo wengi.”

“” Mpigie simu Baba kwanza niongee nae.””

“” Usijali nitaongea nae!

Muda huo Alex akafika akiwa kaambatana na Daktari.

“” Mgonjwa wetu anaendelea vizuri kwasasa mnaruhusiwa kwenda nyumbani kupumzika baada ya siku tatu mtamleta mgonjwa tumfanyie checkup.” Daktari akatoa ruhusa na maelekezo pia.

Alexander akawahi kumshika mkono Minnie akimpatia sapoti ya kutembea.
“” Utakuwa sawa tu!”

“” Sawa wapi..? kila kitu kwasasa kimesimama nitaweza vipi kuangalia kitu kilichombele yangu?”

Alexander akafanya kutabasamu angalau akafarijika akiamini hizi siku chache Minnie hataweza kufanya ubandit tenaa.

Waliingia kwenye gari Moja kwa Moja kuelekea nyumbani, Wanafika hivi wanakuta familia nzima imewasubili inamaana wamepata taarifa, Bibi ilibidi amuwahi Minnie akimpapasa usoni .
” Imekuwaje Mjukuu wangu jamaniii, yaani huyu Maina huyu Kuna siku atakuua kimasihara tu.”

Brighton nae akasogea kumtizama Minnie Kisha akamfuata Alexander kwa hasira akafanya kumuwasha kofi kwanza mpaka likampeleka ukutani akafanya kushika shavu haamini kweli alipigwa Kofi na Brighton.

“” Kila siku nakwambia kuhusu Maina achana nae lakini huelewi, muone ulivyomsababishia mtoto wa watu upofu sahii haoni tena na asipopona kabisa nitakuadhibu kwa hiki, ngoja nianze na Maina kwanza.”

Muda huo Mirii akafika kutoka shule nae akamuona Minnie alivyowekewa bandage alibaki kumtizama tu Kisha akamsogelea na kumshika mkono.
“” Ma’mdogo macho yako yanauma? Inamaana haunioni tenaa, au unataka tucheze mchezo wa kutafuta a..?”

Mama Mirii ikabidi amshike mtoto wake mkono akimtoa pale.
“” Mama kaumia, atakuwa sawa tu.”

Muda huo Mrs Brighton alikuwa akitoka chumbani kwake akitembea taratibu alionesha ni mnyonge sana ni kama anaumwa, Brighton ikabidi amfuate.
“” Mbona umekuja huku tena Mamaa? unaendeleaje lakini?”

“” Minnie kafanya nini tena… Huyu Maina jamaniii..!?”
Mrs Brighton akalalamika akitikisa kichwa kwa huruma kweli.

“” Usijali nitalishughulikia hilo.”

Mama Miricka ikabidi ampeleke Minnie chumbani kwanza akapumnzike hata hivyo mvutano katika wanafamilia ulizidi kuwa mkubwa. Wanafamilia baadhi nao wakaondoka wakaendelee na majukumu yao.

Huku kwa Kamanda Mzobe alikuwa kapokea taarifa za Minnie aliahidi kufika mara baada ya kutoka kazini.

Minnie muda huo alikuwa kalala akilia tu anafikilia namna ya kukamilisha mission yake inazidi kuwa ngumu, Mama Miricka alikuwa akimtizama tu alijua kabisa moyo wake unaumia hata hivyo alikuwa akilia moyoni, machozi ilikuwa ni ngumu kuyaona Ila sauti yake ya kwikwi ndio ilionesha kilio chake.

Mama Miricka alifanya kumkumbatia tu huku akizungumza nae.
“” Utakuwa sawa! Naomba ujikaze hata hivyo majibu ya Daktari yanaridhisha.”

Muda huo Alexander akawa kafika kabebelea chakula kwenye sahani alifanya kusimama mlangoni akiwatizama jinsi wanavyoliwazana mtu na Dada’ke hata yeye lilimuumiza kwa namna fulani alitaka kuondoka lakini Mama Miricka akawa amemuona alimpatia ishara asogee kisha yeye alisimama akiwaachia nafasi.

Alexander akasogea karibu kabisa na kitanda Kisha akavuta stuli akiweka chakula.

“” Ni wewe Alexander..!? Vipi Umempigia simu Baba aje ?”

Alexander akashusha pumnzi kwanza anafikilia inamaana Minnie aliweza kumtambua mapema namna ile?
“” Atafika muda si mfupi japo alisema yupo busy na kazi lakini kaghailisha kazi zake.”

“” Nahisi njaa kwanza.” Minnie akaongea baada ya kuahisi harufu ya chakula.

“” Usijali nimekuletea.”

Minnie akafanya kukaa kwanza ni kama alitazama chakula kisha alizungumza.
“” Alexander,,, nipo tayari kuhudumiwa na wewe kwa chochote kile ila usivuke mipaka yako najua Mimi na wewe hatujaridhiana kuwa Wanandoa Naomba mipaka yako uzingatie. Naomba uniahidi tu nitaweza kuona Tena, kuhusu Maina Naomba achana nae usimfanye kitu chochote make yeye ni kipofu wa Mapenzi.””

Muda huo huo Mzee Mzobe akafika akiwa kaambatana na Abdul walikuwa wakipiga hatua kuelekea chumba Cha Minnie wakiwa wameambatana na Alex japo Mzee Mzobe alikuwa mwenye jaziba kweli.

“” Uzembe uzembe tu, Binti yangu nimewakabidhi akiwa mzima sahii mmemletea shida nyingine hawezi tena kuona! Eti Bwana Alex hata wewe ulishidwa kumuangalia?”

“” Aaa Baba.. ilikuwa ni ngumu kufahamu kama Maina angemdhuru! Nisamehe kwa hilo.”

Mlango ukabishwa Alexander ikabidi asitishe kumlisha kwanza aliinuka na kwenda kufungua Mlango ndio anakutana na ugeni.
“” Aaa.. Baba Shikamoo!! Karibuni ndani.”

Mzee Mzobe hakutaka kusikia salamu zaidi ya kuingia akimuwahi Minnie.

“” Aaa Baba..!? Minnie Alimsikia Baba’ke alifanya kumkumbatia huku akizidi kulia.

Alexander aliamua kuondoka na kwenda kusimama nje akisikilizia tu mazungumzo yao.

“” Mainah…!” Abdul alimuita huku akimshika mkono.”

“” Abdul,, nitakuwa sawa halafu sikukushukuru siku Ile.. Nashukuru sana bila wewe siku hiyo ningekamatika vizuri kwa ushahidi wa Alexander unajua ulijitosheleza sijui ningekuwa wapi leo.”

Abdul akacheka kwanza anakumbuka siku yenyewe aliingia kama Askari pale na ndie aliefuta ushahidi kwenye simu ya Alexander ilioonesha Minnie kaingia kwenye chumba Cha White House.

Muda huo Mr Gelu akafika akimhitaji Mzee Mzobe anahitajika akaonane na White House.

“” Minnie nakuja mara Moja.” Mzee Mzobe akamuaga Minnie akimuacha Abdul ndani.

Abdul baada ya kuachwa alitazama vizuri mazingira yapo sawa akapata muda mzuri wakuongea na Minnie kwanza kabisa aliishika mikono yake na kuibusu huku akifanya kumkagua vizuri usoni, ni kabinti fulani hivi amazing kanavutia hata kwa kukatazama tu sijui huyu Bwana Alexander anafeli wapi tu.
“” Minnie.. kipenzi chako Niko hapa hebu tabasamu basi sitapenda unune hivyo unajua Nini… Nimekumisi tu angalau hata nimepata chance ya kuingia hapa.”

Taratibu Minnie akaachia tabasamu akafanya kumkoa kichwani kwanza.
“” Wewe mjinga kweli yaani kuumia kwangu ndio unafurahi kisa nimekuwa kete.”

“” Aaa sio hivyo, afu unajua Nini niliwaza nikwepeshe kichwa ukoe chakula kwakuwa nakupenda nisingetaka uumie mara mbili unajua msosi wa moto huu, halafu Kuna malupulupu mengi hapa mezani acha nijisevie.””

Muda huo Alexander akawa anarudi chumbani Ile anatua macho anashangaa Minnie yupo kwenye tabasamu wakifurahia chakula na kaka alieingia kama mgeni na Mzee Mzobe akafanya kuwatizama kwanza wakizidi kuongea.

“” Yaani Minnie unajua nashidwa kuishi mwenyewe kule, uliniacha na kumbukumbu zako! Natamani kumbukumbu hizo ziwe kweli tukikaa pamoja.”

Tobaa Alexander ndio akasikia maneno Yale yakamuumiza yaani mke wake alipaswa kuambiwa maneno Yale na mwanaume mwingine akataka kwenda lakini akasita baada ya kusikia Minnie akilitaja jina la kaka huyo.

“” Unajua Nini Abdul bora uendelee kukaa hapa sahii najisikia vizuri, angalau moyo wangu umekuwa na amani.”

Alexander ikabidi aingie make ustahimilivu ulimshinda alifika akakaa kitandani huku akichukua kipande Cha embe akimlisha Minnie.
“” Abdul,,, huyu ni mkewangu Mimi inatosha sasa! Naweza kufanya chochote kikubwa mkewangu akawa salama, Naomba niachie kazi yangu tafadhari.”

Nini Kitaendelea?  Usikose SEHEMU YA KUMI NA SITA YA KISASI CHANGU

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

6 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version