IlipoishiaMinnie ikabidi atoke nje akapata muda wa kuongea na Kaka’ke lakini Kaka’ke alimweleza kuhusu Alex mpaka akashangaa kumbuka Nick hakuifahamu kuhusu Minnie kuolewa lakini siku hiyo akamueleza kila kitu jinsi ilivyokuwa mpaka akaolewa White House, Nick akahisi kuchoka lakini alizungumza.

   “” Ni sawa yote yametokea lakini Mimi sitaki kuona hii habari ya kulipa kisasi ikiendelea katikati yenu, tuseme yalitokea yamepita kwasasa wewe kaa na familia yako!! Kwenye kulipa kisasi siwaungi mkono kabisa, visasi vimejaa vitu vingi ukishangaa unaweza kuondosha maisha ya mtu.”

“” Aaa kaka mbona unakuwa na kigugumizi kuhusu hili ? Kwani wewe huumii Mama kuuwawa? Ni sawa, kama haupendi wewe lakini kisasi lazima kikamilike ikiwezekana tena Cha damu.”

Muda huo anamaliza kuzungumza akasikia makofi yakipigwa kuelekea alipo hakuwa mwingine zaidi ya Alexander 

ENDELEA 

SEHEMU YA KUMI NA NNE

Minnie baada ya kusikia sauti ya Alexander alifanya kuikata simu huku akiwa anatetemeka kwa hofu, alifanya kuficha Ile simu kwanza Kisha akamgeukia.
“” Ooh bwana Alexander upo hapa?”

“” Eee nipo hapa kusikiliza madhambi yako.””

“” Utakuwa haupo sawa wewe.”

Minnie akafanya kumpita Alexander akabaki kumtizama tu huku akimfuata nyuma.
“” Vipi twaweza kuondoka! Naona kazi tumelipua.””

Muda huo Minnie alikuwa akikusanya vitu vyake yupo busy kweli.
“” Tuondoke tu, kwanza kichwa changu hakipo sawa Leo.”

Ikabidi Alexander atangulie kwenye gari Minnie nae akafatia.

“” Ni kawaida kutokuwa sawa, ” Kesho tutakuwa na mgeni Maina ataanza kazi hapa.”
Alexander akaongea baada ya kumuona Minnie kakaa.

“” Sawa, naona utakuwa una furaha kuwa karibu na mwanamke wako! Naimani hutakuwa ukifatilia mazungumzo yangu ya faragha, Maina atakuweka busy na Mimi nitakuwa sawa.””

Alexander hakutaka kumjibu safari yake ilienda Moja kwa Moja kwenye restaurant kubwa iliyokuwa karibu na kisiwani hapo.

“” Mbona huku tenaa..!? ” Minnie akauliza baada ya kuona gari imepaki pembezoni na hotel.

“” Ni kwakuwa hukula mchana.”

“” Sina njaa.”

Alexander akafanya kumshika mkono huku wakiingia na kutafuta sehemu nzuri itakayofaa wote wawili.

Mhudumu alifika kuwasikiliza,!! Alexander akawa ameagiza nyama za kuchoma iliyotiwa rost pamoja na kinywaji, Minnie akabaki kumtizama akifikili yeye angeagiza Nini labda? Alexander akawa ametambua hilo akafanya kumuagizia kama yeye alivyoagiza.

Chakula kikawa kimeletwa na mhudumu Minnie akawa busy kukaa lakini Alexander alikuwa akimtizama jinsi anavyokula akatambua kabisa alikuwa na njaa, alifanya kukohoa kwanza akiongea.
“” Ooh! Kumbe njaa ilikushika na haukusema, okay malizia twende.”

Ni upande wa pili kwa white house akiwa na Mr Gelu Katika ofsi Yao kubwa iliyojihusisha na uuzaji wa dhahabu walikuwa wakikagua dhahabu mbalimbali zilizoletwa na wateja huku vijana baadhi walikuwa wakichoma dhahabu hizo, mazungumzo baina ya watu hawa yaliendelea.

“” Nishajua kabisa yule Binti katumwa nyumbani kwangu kunichunguza mimi! Lakini Mimi sikumuua yule mwanamke, ni sitofahamu tu ilitokea.”

“” Sasa tunafanyaje, naona Mzee Mzobe kafungua faili mahakamani anataka kufatilia kifo Cha mkewe.” Mr Gelu akaongea.

“” Sitaruhusu mtu mwingine aingilie familia yangu, kwa vyovyote vile nipo radhi kumdhibiti.”

“” Sasa kwanamna ipi tenaa…!!?”

White House akacheka kwanza huku akijitizama Moja ya madirisha ya nyumba Ile iliokuwa na vioo.
“” Hapa sitasimana kama White House bali nitasimama kama Denishoo.”

“” Oohuuuu!!! ( Mr Gelu akashusha pumnzi kwanza) sitataka umwage damu tenaa.”

“” Sawa wewe ondoa hofu tu.””

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°

Yapata mwezi mzima kupita Minnie alipata wakati mzuri wakufanya upelelezi wake hata alipokuwa kazini alifanya kazi zake mapema baada yakukamilisha alienda kuonana na Baba’ke kwani Alexander alikuwa busy sana na Maina wawapo kazini walizidisha kuonesha Mapenzi yao yaliovuka mipaka hata kwa wafanyakazi wote waliyajua.

Ilikuwa ni Majira ya Jioni Minnie alifanikiwa kuingia katika chumba Cha White house leo, na hii ni baada ya kusikia kasafiri mara Moja!

Baada ya kuingia katika kile chumba alianza kukichunguza kwanza ndipo anakuta picha ya Mama’ke mzazi yaani imebandikwa ukutani, alisogea na kuanza kuipapasa kwanza huku akizidi kuikagua.
“” Huyu si Mama lakini..!? Hapa kafata Nini tenaa hivi ni kweli White House alimuua Mama?”

Wakati anazidi kushangaa picha Ile alisikia michakacho ni kama mtu anaingia ilibidi abane nyuma ya kabati aangalie mtu alieingia pale alikuwa ni Alex, alifika akasimama na kuanza kuangalia mazingira ya chumba yalivyokaa baadae alisogea kwenye Moja ya meza iliokuwa na Droo akafanya kuvuta Kisha alitoa Album yenye picha akianza kuikagua ndipo anakutana na Moja ya picha iliyofanana na Ile alokuwa akiitizama Minnie aliichukua na kuanza kuitazama vizuri, Minnie akawa anamtizama tu.
“” Mbona picha ya Mamangu tenaa kaishika..?”

Alex akazidi kuitizama kwa makini lakini Kuna simanzi furani ilimshika alijikuta akilia huku akizungumza maneno.
“” Mama kwanini lakini uliondoka mapema namna hiyo ni nani aliesababisha kifo chako ilihali Mimi mwanao Bado nilikuhitaji, kwa kifo chako ulichofanyiwa lazima niwaweke ndani watu hawa.”

Minnie ndio akaduwaa yaani Mama’ke yeye aliitwa Mama.. na Alex? Kiaje Ani alikuwa Mama kwake na huyo Alex nae anakisasi Cha kulipiza juu ya kifo Cha Mama’ke..? akahisi kuchanganyikiwa.

Alex baada ya kumaliza kulia pale alifanya kufuta machozi huku akichukua picha Ile akiiweka ndani ya kitabu kilichokuwa mezani na kutoka nacho.

Baada ya kufika mlangoni aliutizama Mlango mara mbili mbili kama ulikuwa umeegeshwa au ulifungwa na kufuri ni kama haelewi tenaa, alitizama mezani ndio akaona funguo ya kitasa alichoamua ni yeye kufunga na funguo Kisha ufunguo ule alienda kuukabidhi kwa Bibi.

Huku Minnie ndio akawahi Mlango akijaribu kuvuta lakini wapi akajua tayari kafungiwa.
“” Ooh unafanya Nini Minnie ukiwa umefungiwa? Sasa natokakaje kwenye mdomo wa mamba mimi!?”

Minnie akahisi kuchanganyikiwa akiongea na nafsi yake.
Ndipo anapata ufahamu kuwa anae simu angeweza kuitumia muda huo akapata msaada, swali linakuja yaani yeye alienda chumbani kwa White House akafungiwa labda alifata Nini mle? Akahisi kuchoka akaamua kukaa kwanza huenda akituliza akili yake atapata majibu lakini bado mambo yalikuwa magumu vilevile.

Huku kwa White alikuwa kafika sehemu aliyokusudia afika alikutana na Mwanasheria wake mmoja anamkumbuka vizuri wakati wa nyuma alisimamia kesi yake iliyosemekana alimuua mkewe lakini aliweza kushinda kwasasa alimhitaji tenaa.

“” Habari yako Bwana Kamau nimekutembelea tenaa, habari ya siku lakini?”

“” Ni nzuri,, aaa karibu tukae kwanza, Ooo Kado tuletee kahawa kwanza.
Alimuita kijana wake aitwae Kado.”

Kahawa ikawa imeletwa pale wakaendelea kunywa huku stori zikiendelea.

“” Aaa unajua nimekuja hapa kuhusu kesi ya miaka ishirini kupita naona inaenda kujirudia, Kamanda Mzobe kafungua kesi ya mauaji ya mkewake kwanza na hapa kafungua kisiri Siri lakini Kuna mtu wangu pale kanitonyaa,, kinachotakiwa kesi hii iangukie kwake make ninao ushahidi hapa.”

Bwana Kamau ikabidi apokee ushahidi kwanza ilikuwa ni flash alifanya kuichomeka kwenye laptop yake.
“” Ooh hapa sawa, inaonesha risasi yake ndio ilishoot kuelekea aliko Mkewe,, vipi una ushahidi mwingine zaidi ya huu?”

White House akatoa Bastola na kuiweka mezani, bwana Kamau akashangaa sana akifanya kusimamisha Crip aliyokuwa akiitizama kwanza alifanya kuzoom mkono wa Kamanda Mzobe uliokuwa na bastola akawa amegundua kitu.
“” Hii si ndio Bastola yenyewe iliyotumika kwenye mauaji?”

White House akafanya kucheka huku akichukua tishu aliyokuwa kaikunja vizuri na kuitia kwenye Moja ya mfuko wake wa suruali akiiweka mezani akizungumza.
“” Hii ndio risasi iliyotumika siku hiyo hapa lazima afugwe kifo.””

Upande mwingine tenaaa alionekana Mzee Mzobe akiwa faragha na Mwanasheria wake akizungumza.

“” Mr Denishoo ndio anahusika kwenye mauaji ya mkewangu! Ile risasi Mimi sikuielekeza kwa Mkewangu, ilienda kutua mlangoni Kisha ikanirudia, lakini nikiwa pale nimeduwaa sijielewi nilishuhudia Denishoo akiwa kashikilia mkononi bastola huku nguo zake zikiwa na madoa ya damu, inamaanisha alimuua pia ndio damu ikamrukia?”

“” Aaa! Hapa kazi ipo kama mara ya kwanza Mr Denishoo wakati mnakutana uso kwa uso hakuwa na Bastola ila baada ya tukio akawa na bastola, unahisi wakati ule mnaonana alikuwa nayo tayari?”
Mwanasheria nae akazidi kuumiza kichwa.

“” Hapa ndio fumbo, kama hakuwa nayo huenda Kuna mtu alimrushia akafanya Hilo tukio. Mzee Mzobe akazidi kuwazua pia.

“” Inawezekana lakini ni nani huyo alikuwa karibu yenu siku hiyo?”

“” Wakati tunazidi kuzozana walinzi wa getini walifika, lakini hapohapo kulikuwa kunae vijana wake walikuwepo ni hawa watoto wa Kaka’ke walikuja kuzuia lakini hakuna aliyewasikia.”
Mzee Mzobe akaongea.

“‘ Hapa naona kazi Bado tunayo inatakiwa tuishie hapa tutafute Camera nahisi Kuna ushahidi ulihifadhiwa kwa white house, ukipatikana hapa tutashinda.”

Upande mwingine tenaa alikuwepo Maina na Alexander wakiwa kwenye hoteli Moja wakiendelea kufurahi pamoja lakini ugomvi uliinuka alikuwa ni Maina akitaka kujua hatima yake.

“” No Alexander nimechoka Mapenzi Gani haya ya Kila siku starehe, uliniwekea njiti nisizae Sasa naenda kutoa,, nimechoka kuishi na wewe kama mwizi, siku hizi huzungumzi kuhusu swala la Ndoa muda wote unasema mpaka umkamatishe Minnie afukuzwe kwa kuzalilishwa nyumbani, kwani Minnie mpori-pori anaweza kuja kukuchunguza Nini wewe? au anaugomvi na familia yenu, Na kama mnae ugomvi unatokea wapi kwa Binti asiekuwa na kitu chochote yule Hadi awahusishe?

“” Aaa Maina achana na maswala ya kifamilia bhana! Kama utataka kuzaa bila ridhaa yangu huyo mtoto sitamtambua, Baba’ngu Mimi ataniadhibu kwa tambia mbaya ya kuzaa Nje, nimekwambia swala la Minnie niachie Mimi ni muda tu.”

“” Kuzaa nje…!!!? Unaona utaabika? Vipi kuhusu kunitumia muda wote na wazazi wangu Ulienda kujitambulisha wewe mwenyewe kuwa muda si mrefu twaoana huoni wanivua nguo? okay kauvunje uchumba nyumbani angalau wazazi wangu wasitegemee kitu chochote kuhusu Mimi na wewe?”

“” Maina please! Kuwa na subira mambo yatakaa sawa! Muda si mrefu Minnie atafahamika kwa ubandit wake! Hebu nipatie simu yangu kwanza nione.”

Maina akafanya kumpatia simu Kisha Alexander akaingia mtandaoni akiitruck Simu ya Minnie, kumbe bhana alimtega makusudi ni yeye ndie alimtengenezea mazingira Yale baada ya kusikia Baba’ke anaondoka aliomba funguo za chumbani kule akaenda kufungua Mlango na kuuacha wazi alijua Minnie lazima afanye uspy wake! Kisha funguo aliiacha mezani hata alipoingia Alex aliingia aliona funguo imezani Ile kutoka akawa amefunga.

“”” Ooh waoooo afadhari umenifurahisha! Basi pigia familia yote iende chumbani kwa White House wamfumanie vizuri naamini hapo lazima wamfukuze kama kibaka na ndipo tunaenda kuoana kiwepesi kabisaa, Yaani nakuwa Mrs Alexander Denishoo wallah na furaha mie…””

Maina hakusita kumkumbatia Alexander akihisi tayari ushindi upo mikononi mwake.
“” Ooh Sweetheart I’m sorry kwa Kila kitu, najua nimeongea ujinga mbele yako ni vile sikufikilia mapema swala hili.”

“” Basi Naomba nikuache mara moja! Nitakurudia hivi karibuni.””

“” Aaa twende wote..!”

“” Maina samahani! Nakuomba niachie Mimi kama tutaongozana watasema hii triki tumeicheza wote! Kwasasa kuwa na Imani Baby… enjoy!”

Alexander ikabidi atupie mkoti wake huku akifungua Mlango aondoke lakini Maina akamuwahi na kumkumbatia tenaa.
“” Baby I’m sorry! Nakutakia safari njema! Upendo wangu ni zaidi ya unifikiliavyo.”

Alexander akatabasamu tu Kisha akamgeukia Maina akimbusu kwenye paji la uso akiondoka.

Huku kwa Minnie alikuwa kasakula Kila sehemu akitaka ushahidi akawa kapata faili furani lilikuwa ni faili lenye maandishi mengi kuhusu kesi ya Mama’ke mzazi ambae muda huo alitambulisha kama MIRICKA MZOBE Minnie akazidi kusoma lakini anashangaa shutuma zote zilizotolewa hakuzielewa kwanza aliona ujumbe wa Baba’ke yaani alishitumu White house alikuwa yupo kimahisiano na Mama’ke lakini alivyozidi kusoma akaona huyo White House alimfanya Mama’ke kama mke hapo ndio akachoka akaona ni kama alifanya ujinga kufatilia kesi ya watu waliokubaliana kuwa pamoja yaani wapenzi halafu wakauana ikabidi afunike lile faili tenaa.

Huku nje chumba Minnie akasikia sauti ya Bibi akiwa anakuja katika chumba kile akiongea na simu.
“” Sawa ngoja niangalie.”

Minnie ndio akasikia sauti ya funguo ikifungua Mlango akafanya kurudishia faili sehemu yake haraka haraka Kisha akarudi tenaa kubana nyuma ya kabati akiyazuia mapigo yake yamoyo yasimsaliti lakini ndio akaona hio ndio njia nzuri ya kutoka.

Bibi alifika na kuanza kukagua mafaili pale huku akizungumza na simu.
“” Atakuwa Alex alikuja kwenye hiki chumba ndio maana kipo hivi sasa hili faili litakuwa wapi tenaa?” Akafanya kupika simu tena kwa mtu aliekuwa akizungumza nae.

“” Aaa Mwanangu mimi Mama yako nimezeeka umesema la blue ee..?”

Minnie ndio akagundua faili linalotafutwa ndio alikuwa nalo muda wote akiliangalia sehemu lilipo akaona lipo karibu kama mtu atachukua akapiga jicho pembeni kumuona inakuwa rahisi, alichofanya alitizama ukutani ndio akaona Kunae socket kama atazima taa itamfanya yeye aweze kuescape, alifanya kubonyeza switch akawa kazima muda huo Bibi akabaki kutoa macho.
“” Nini hiki tenaa, au umeme umekata.?”

Muda huo Minnie tayari katoka mputa mputa Hadi chumbani kwake alifanya kufunga Mlango haraka akiangalia mazingira ya chumba asije akarudia makosa tena Ile siku viatu vyake vilikutwa na tope iweje leo ajulikane alitoka alichofanya ni kujitupia kitandani na kulala gubi.

Huku Bibi ndio akafanikiwa kusogea kunako switch akafanya kuwasha Ile kuwasha ndio akaona faili ikabidi atabasamu tu.
“” Huu uzee huu, inamaana kumbe sikuona wakati li peupe namna hii?”

Akafanya kulichukua Kisha alienda kumpatia mtu aliyeagizwa alipelekwa kwa white house.

Huku Alexander ndio anaingia White house alipaki gari yake pembeni Kisha alizama ndani akianza kuita watu wote kwa jaziba…
” Bibi,,,.. Alex…., Bright, shemuuu, Aunt… Ba mdogo,,, ma mdogo..”
wote ikabidi wasogee sebuleni kusikiliza wito wao.

“” Naombeni mnifuate wote, Bibi njoo na funguo ya White House naona wote hamuishi kumsifiwa Minnie kwa tabia nzuri nawaambia yule ni spy hamuelewi njoeni muone sasa.”

Wakabaki wakitizamana kwa pamoja hawaelewi ikabidi waoongoze njia Hadi kunako chumba Cha White House. Alexander baada ya kufika aliomba funguo kwa Bibi akawa kafungua aliwasha taa huku akizungumza.
“” Aya jitokekeze mapema leo Kila mtu atajua tabia yako!”

Ukimya ukatanda Alexander akazidi kuchukizwa ikabidi asogee karibu na kabati nyuma anaangalia hamna mtu.

Muda huo huo Mlango ukagongwa Askari wakawa wameingia na hii ilikuwa ni plan ya Maina kwamba Leo Minnie lazima alale ndani..!!”

Huku kwa Minnie akiwa chumbani alikuwa akiwasiliana na Baba’ke kuwa aliingia chumba Cha White House kutafuta ushahidi lakini anamashaka ni kama anaweza sanukiwa, Mzee Mzobe alimwambia afatilie Kila kitu alichofanya mwishoe Alimwambia Kuna Askari watafika pale Mzee Mzobe akasema aachie kazi hiyo ataimaliza kistaarabu tu.

Huku kunako chumba Cha White House wakazidi kumshangaa Alexander ikabidi Bibi asogee karibu.
“” Wewe unashida gani kwanza? Minnie huku awe kafata nini kwanza? Mimi ndio nilikuwepo huku chumbani Nimefanya kazi zangu mbona hakuna Minni..?”

Alex nae akaingilia.
“” Mimi pia nilikuja huku chumbani kuchukua vitabu vya kusoma hakuwa na mtu hapa, iweje Minnie aje huku na kaja kufanya Nini?”

Muda huo wakasikia sauti ya Afande mmoja katika watatu akizungumza.
“” Kunaendelea Nini katika familia ya White House? ”

Alexander hakutaka kuchelewa alitoa simu na kumpatia yule Afande atazame Ile video ya Minnie inayoonesha yupo ndani.

Alichojichanganya Alexander alimpatia simu Afande bila kwenda kwenye video yenyewe zaidi ya kutoa password tu, Afande alikagua vizuri video iliyomo ndipo akapunguza sauti akisikilizia ndio akaona ni ya Minnie kweli alifanya kuifuta yote mpaka kwenye trash akawa ameongeza na sauti akizidi kukagua,, Askari mmoja pia akasogea nayeye akachukua simu akague vizuri.

“” Ooh Mbona video nyingi sana Sasa ni ipi?”

Alexander ikabidi ashike simu anakagua hivi haipo .
“” Mh mbona ilikuwepo? Au Maina kaifuta?”

Bibi ikabidi amsogelee Alexander.
“” Mjukuu wangu unakuwaje lakini mbona humuamini mkeo, angalia sahii watu umewaachisha usingizi bure kwani Minnie hayupo chumbani..!!?”

“” Aaa sijaangalia…!!”

“” Ifike hatua ukue hio nyumba ndogo itakuchanganya mara mbili yake.”
Bright akaongea huku akimkata jicho Alexander kwa upande wake anamwamini sana Minnie anahisi Alexander ni vile kajiwekeza kwa Maina tu.

Ba mdogo ikabidi awatake radhi maafande Kisha aliwaomba waondoke.

“” Wakati mwingine mshitaki akifanya hivi itabidi yeye ndio awe mshitakiwa ataenda kituoni kutoa maelezo kwa kina kwa kosa na kumshuku mtu lazima atapewa Adhabu.
Afande huyu akaongea akiwa sereous kabisa na ndie Afande aliefuta ushahidi.”

Alexander ikabidi aambatane na Kaka’ke Hadi chumbani kwa Minnie waligonga Mlango lakini Minnie alikuwa akiwasikilizia tu ndipo message ikaingia kwenye simu yake.
“” Kila kitu kimekaa sawa, kuwa makini.”

Huku Alexander ndio akafungua Mlango anatizama kitandani ni Minnie kalala, Alex nae ikabidi asogee baada ya kuona usalama upo.

Alexander ikabidi akae kitandani kwanza akimuasha Minnie kwa kumtikisa.
“” Minii! Minnie..!! Umelala…?”

Minnie ndio akajigeuza huku akizidi kulalamika na usingizi.
“” Mhuu,, Nini bwana Alee.”

Alex akaona Aage hata hivyo kashuhudia Minnie yupo ndani.
“” Dogo usiku mwema, muamini bhana mkeo.”

Akawa ameondoka, Alexander ilibidi siku hiyo alale kitandani yaani haamini ni kitu gani kimefanyika pale mpaka Minnie akatoka chumbani, alitumia muda mwingi kumtizama Minnie akiwa kalala. Minnie muda huo anahisi kabisa anatizamwa na Alexander akawa anawaza ageuke au afanye Nini kuficha sura yake.

Alexander ikabidi akae kwanza kitandani hapo hapo Minnie akamgeuzia mgongo akiangalia pembeni Kisha akatabasamu tu akiongea moyoni.
“” Umegonga mwamba Alee, kuwa makini Alexander Minnie hayupo hivyo.”

Baada ya kugeuka Minnie; Alexander akashituka ikabidi alale kwanza ikiwa ni karibu yake Ili afanye kumtizama kwa kumchungulia. Akawa anazisogeza nywele zake zilizomwagika usoni Kisha alifanya kuegama begani kwake, Minnie akataka kujinasua ndio anakumbuka muda si mrefu usingizi ulikuwa mzito kwahiyo anafaa kuendelea kuigiza.
“” Minnie kipi umekifanya Leo? Unajua siamini Ani,, nilitrack simu yako nikaona upo chumbani umefungiwa kwani ulitokaje Minnie, inakuwaje unakuwa spy wa white house? Si uniambie mission yako hapa ni Nini? Uliniomba nifatilie kuhusu yule mwanamke na leo nilipata majibu,,, ila sizani kama naweza kukwambia tena… Unajua umenichanganya?

Nini Kitaendelea?  Usikose SEHEMU YA KUMI NA TANO YA KISASI CHANGU

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

 

5 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version