Ilipoishia ”

Bright akachombeza baada ya kumuona.

   “” Basi wewe ndio Mfalme wangu. Karibu kwenye himaya yangu.”

Minnie akazidi kuonesha furaha kwa shemeji yake, Bright akawa kamchukua huku wakipiga hatua.

   “” Leo twende ukamuone Dadako najua hujawahi muona hata mkapiga stori nae. Nifuate.”

Muda huo Alexander kwa mbali ndio anamuona Minnie akiwa na Bright ikabidi amtizame kwanza Dada’ke aliempatia kazi ndipo anamuona yupo busy na Rafiki zake wakipiga picha akabaki kulalama kimya kimya.

   “” Hamna kazi niliyoifanya hapa, Mimi pekee ndio nafaa kuwa karibu nae! Na hapo hatochelewa kuwatoroka.” 

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA TATU 

Minnie alishangaa mkono wake unashikwa aliutazama mkono akaona unae saa akajua moja kwa moja ni Alexander alifanya kufunga macho akilalamika..

  “” Hajawahi kuniacha nipumue kabisa, sijui anataka Nini tenaa?”

Bright akawa amemuona Alexander akawahi kumsogelea.

   “” Ooh bwana Alexander muache Minnie nimtambulishe kwanza kwa Dada’ke, ee unamumisi sanaa…!?”

Alexander ikabidi ajichekeleshe kwanza huku akinong’ona na Kaka’ke.

   “” Hakikisha unamrejesha kwangu.”

Minnie akawa amesikia akapaniki kwanza kwa maneno Yale anafikilia inamaana yeye alikuwa ni ujumbe wa riport fulani itasambazwa Kisha irejee kwa mhusika?” Hakuwa budi kuendelea kusikiliza Utambulisho.

“” Minnie huyu hapa ni mkewangu Mimi , muite Mama Anisha.”

“” Ooh Nashukuru, Sasa huyu si Dada ..? Dada nafurahi kukuona.”” Akifanya kumpatia mkono wa kumkalibisha nae hakusita kumpatia mkono wake pia.

   “” Ngoja Mimi niwaache kwanza. Minnie twende kwa mmeo.”

Bright ndio anatizama hivi anashangaa kumuona Alexander yupo na Maina akahisi kuchoka, ikabidi amuache Minnie pale.

Huku kwa Alex nae hakuisha kumtizama Alexander alipo ndipo anamuona yupo karibu na Maina kitendo hiki kilimuuzi sana ikabidi aongee na mkewake.

   “” Mama Mirii sitaki unifiche, hivi Alexander na Maina siku zote wapo karibu namna hii?”

Mama Mirii hakusita kumuelezea yote Hadi uchafu waliofanya chumbani kwa mkewe, alionesha kabisa kutokupendezewa na tabia za Maina.

Alex alihisi kuchoka alimtizama Minnie kwanza alionesha hana shida yoyote alikuwa busy na mke wa Kaka’ke yaani Bright.

   “” Mbona Minnie anaonekana kutokujali swala hili? Huu ukaribu yeye haumuathiri?”

   “” Ndo Minnie alivyo, nahisi amechagua furaha yake mwenyewe na sio furaha ya kupewa na Alexander.”

    “” Sawa, ngoja nifanye kitu kwenye mahusiano Yao yaimalike.”

Kwa Minnie simu yake iliita ikabidi asogee pembeni kuongea alikuwa ni Nickson kampigia simu.

   “” Oooh waoo! Nambie kaka’ngu mzuri na bora nimekupata Kuna kitu kinanitatiza hapa nahisi Kuna kitu hakipo sawa hapa.””

   “” Aaa Nini tena wewe kama ni maswala ya kisasi usinishilikishe.”

   “” So hivyo,, hebu washa data nakutumia kitu .”

Minnie ikabidi akate haraka akamtumia picha ya Alex Kisha akamnyokea.

   “” Mhuu Kaka umeona huyu wamfahamu wewe?”

   “” Mbona ni Alex huyu, sahii yupo rikizo kwani vipi?”

   “” Heee Alex….!? Yaani huyu ndie alikuwa kundi Moja na Amri? 

    “” Wewe mbona unashangaa hivyo! Nashidwa kukuelewa ujue, Kuna tatizo?””

   “” Aaa kaka subili kwanza, baadae nakupigia.”

Ikabidi akae huku akiegama ukutani kwa hofu, Ndio kumbukumbu ikamjia, siku Ile alivyotoka nyumbani kuelekea msituni alikutana na Amri akiwa na wenzake wanne! Wakati huo Amri akawa akimchimba biti kuwa anaenda kuwinda, lakini huyu Alex ndio alikuwa kainama akifunga Buti siku hiyo,. Sasa Leo White House kafata Nini teenaa?

Muda huo huo Alishangaa anaguswa begani alikuwa ni Alex mwenyewe, Minnie akahisi kuzima kwanza akishuka chini! Alex akawahi kumshika na kumkumbatia karibu kabisa huku akimtizama usoni kwa muda baadae alimuachia.

   ”” Shem upo sawa lakini?””

   “” Eee nipo sawa.”  Huku akiondoka.

Alex ikabidi amfuate akajua kabisa ana maumivu kwenye Ndoa yake.

   “” Shem haupo sawa najua, yote ni kwaajili ya Maina usihofu hawezi kumchukua mmeo.”

Minnie hata hakujibu alihisi ni kama akili yake kwasasa haifanyi kazi yupo kama kimvuli.

Alexander nae alipo akapata ujumbe kutoka kwa Alex.

   “” Vipi hautomjali mkeo ila huyo hawala..?”

Baada ya kuona Ile Message ikabidi asogee karibu na Minnie anae hisi kufa kufa masaa yote. 

   “” Minnie vipi unaumwa…!?”

   “” Aaa nipo sawa.”

Alex ikabidi amfuate Maina Kisha alimvuta pembeni azungumze nae.

   “” Maina mzima lakini? Leo sitataka stori nyingi naomba kaa mbali na Alexander kwasasa anae mke.”

Maina hakumjibu zaidi ya kumtizama Alex anavyoondoka.

 

Huku Sherehe ilizidi kuendelea lakini Drama za hapa na pale nazo ziliendelea kimya kimya mwisho kabisa, mshereheshaji aliomba mziki upunguzwe alikuwa ni white house anaingia.

 

Ukumbi wote ulibaki kimya wakati house white anaingia. Minnie yeye akawa anamtizama vizuri white house akimfananisha na Alex make tayari ashajua ni Baba’ke. 

Wakati anaendelea kushangaa Kuna vinywaji vilikuwa vinapitishwa na watumishi, Minnie ikabidi achukue na kunywa, wakati Minnie kanywa huku upande wa pili kwa Sandra alicheka huku akigonga chears na Maina.

   “” Dill Done” wakaongea kwa pamoja wakivuta funda moja katika Glass iliyokuwa na Whynne laini wakinywa.

Huku White House aliendelea kutoa Utambulisho mwisho kabisa alimuita Alex pamoja na Alexander waambatane na wakezao kufungua uwanja angalau kwa mziki laini.

Alex alienda kumchukua mkewe na kumleta Moja kwa Moja uwanjani huku Alexander akiwa na wasiwasi anajiuliza huyo bandit kweli angeweza kucheza bila shaka angemzuru kwa mateke tumboni, hakuwa na namna alimfuata hivyo hivyo huku akijipa ushindi kama atashidwa basi angeaibika mwenyewe na sio yeye.

Mziki wa taratibu wa Westlife ukaachiwa, anakwambia Queen of my hart! Upande wa Alex akamshika vizuri mkewe kiunoni huku mikono ya mwanadada huyu akiikusanyia begani na kumtizama kwa Mahaba kabisa huku macho yake malegevu yalijaa amsha amsha yakizungumza.. “” angalau nafasi Moja tu kwa Leo nafaa kuitumia na Mmewangu vizuri “

Huku kwa Alexander Bado ametulia tu mpaka mziki unaanza anafikilia angeanzia wapi kumshika mwanamke huyu, watu wote wakawa wamewatolea macho wanazidi kufikilia kwanini wamesimama kwa sekunde… Huku kwa Maina alikuwa akienjoy sana akawa kamfata Sandra akiongea nae.

   “” Nilikwambia mpori-pori hawezi kitu, ona anavyomuaibisha mpenzi wangu jamaniii.””

Minnie muda huo kile kinywaji kilikuwa kikizidi kupambana na ubongo wake, mwisho kabisa alimtizama Alexander akatabasamu Kisha akamwambia.

   “” Unaweza vumilia fujo zangu kweli katika uchezaji?”

   “” Olewako unitoe nyongo nitakuua, hapa sio mazoezini kumbuka!” 

Alex akajiwahi kwa onyo.

Minnie akafanya kucheka Kisha alielekea aliko Dj akaomba maiki azungumze kwanza huku mziki ukikatishwa.

   “” Hellow Mabibi na Mabwana! Siku ya Leo ninae furaha sana  wakati huu nimuachie shemeji yangu afungue uwanja baadae nitakuja kumalizia Mimi na Mmewangu.”

Watu wakapiga vigelegele ni vile walimuamini sana! Lakini kwa Alexander akahisi mauza uza ! Yaani ni bora wangecheza wakiwa na kampani hata kuaibika ingekuwa siyo sana, Sasa hii wawe wawili jukwaani si watu wote wanawatizama? Akaona hana ujanja kukwepa zari hili.

Shoo ya Alex na Mmewe ikawa imeisha! Minnie ndio akaomba wimbo wake, goma likalindima masikioni likiwa linaamsha amsha utazani Shakira alivamia jukwaa, Alexander Bado ameduwaa anashangaa akivutwa na Minnie Tena kwa Mahaba mazito kabisa Kisha alianza kumzungusha katika jukwaa Hilo! Alexander akawa amesalenda yaani ni hakuamini,, sio yeye tu watu wote hawakuamini kuona Minnie akichezea namna Ile.

Alexander alihisi kuenjoy sana anakumbuka mambo kama haya aliyafanya akiwa marekani masomoni ndio ilikuwa zao, nakwambia ukiambiwa upele umempata mkunaji ndo huku sasa.

Minnie hakuwa haba Ukiangalia wale waliomtia kilevi ni kama walimpa hatua za kucheza vizuri mbele ya watu, Wakati Bado wanaendelea mziki ukabadilishwa ghafla na huu ulikuwa ni ziro distance na nyimbo hizi huchezwa taratibu hasa upate mtu anaeweza kuutumia mwili wako vizuri kucheza, Alexander hakuacha kumtizama mrembo huyu ambae amekuwa akimuita Bandit kumbe anae vitu adimu namna Ile,mikono yake aliielekeza kiunoni akikamatia vizuri kiuno hiki kilichoonekana kulainika sana sio wewe unakuwa na kiuno kigumu kama boroti yenye kutu.

Minnie akawa ametulia tu akizidi kumtizama Alexander baadae alimuuliza.

   “” Wewe hapo unaona kama Mimi siku zote nakuwa mkosefu lakini Mimi sifanyi vile makusudi, najitahidi kutafuta Haki ya Mamangu, Vipi ulifatilia kuhusu Ile picha?”

Alexander akajishituka inamaana Bado anamfanyia u spy hata jukwaani akafanya kujaribu kujitoa kwa Minnie lakini Minnie ndio akazidi kumkumbatia.

   “” Vipi Bwana Alexander! Sitaki kuingilia maisha yako ilanisaidie kazi yangu tu, kingine sio kwamba Mimi nimekuja kuvunja mahusiano yako na Maina! Hata Mimi hii Ndoa siitambui kama unaweza wewe muoe mwanamke unampenda, kingine mwambie Sandra na Maina Mimi sitaki drama zao! Sitapenda nione wanaendelea kunifatilia, Leo walinipatia juice yenye kilevi niliigundua tu, nikaona ninywe funda moja Ili nikate aibu ya kucheza na wewe! Basi wafikishie salamu zangu.””

Alexander akaona Minnie kavuka mipaka alijiondoa na kumtega mguu aanguke lakini Minnie aligundua Hilo akawahi kumtega yeye akawa anashuka chini, akafanya kumzuia kwa mkono wake akimuokoa , alitabasamu tu huku akizungumza.

   “” Hutaki kubadilika usiwe Buibui, Acha kutega mtego unaokufunga mwenyewe.””

Makofi ya shagwe yalisikika Alexander ilibidi ajitahidi kushuka na mkewe kamshika mkono Ile wametoka tu akamuachia huku akimtizama kwa hasira, lakini Minnie hakushidwa kumpatia tabasamu hii ikazidi kumkasirisha zaidi.

Muda huo Maina na Sandra wakafika huku wakimtizama Minnie kwa hasira, Minnie yeye akabaki kucheka tu.

   “” Wifi umelewa eee! Unakunywaje Pombe white house?” 

Sandra akaanzisha kelele, Maina naye akazidi kupaza sauti watu wakazidi kusogea pale.

   “” Amekunywa pombe, amekunywa pombe, ndio maneno yaliyoendelea lakini Alexander akawa amefika pale akamshika mkono.

   “” Hajanywa pombe ila Kuna mtu alikuwa akigawa kinywaji alimpatia bila kufahamu! Haina shida yupo vizuri.”

Heee! Macho yakamtoka Maina na Sandra kwamba huyo Alexander alimtetea Minnie?

   “” Vipi upo sawa lakini…!? Alexander alimuuliza baada ya kumpatia maji kwenye chupa anawe uso.”

Minnie hakuelewa yaani Alexander kashidwa kumpazia sauti muda ule na wapo wenyewe tu! Kwani huo wema alianza lini kijana huyu? Alimpatia na kitambaa akaushe maji katika uso wake Kisha alimwambia waongozane.

Wamefika tu Alex akawa kamfuata.

   “” Unajua sijaamini eti, yaani shemeji yangu huyu huyu ndie anacheza vile! Halafu sura yako inashabiana na ya Mamangu.””

   “” Aaah shemu umeanza utani wako.”

   “” Aaa hebu subili kidogo.”

 Alex akamsogelea karibu Kisha alimtengenezea nywele zake Kuna kibanio kilikaa vibaya.

   “” Unajua Nini Minnie! Ni kama tuliwahi onana ila kesho nitakupa majibu naona hakili yangu hainidanganyi kuhusu wewe.”

Muda huo Alexander akawa amefika akashangaa kumuona Alex yupo karibu na Minnie kwambali Kuna kawivu kalimshika.

   “” Aahaa,,, Kaka upo hapa!?”

Wote wakashituka wakimtizama Alexander, Minnie yeye ashahisi kihoro akatoka kimya kimya lakini Alexander akamshika mkono.

“” Waweza nisubili..?”

Alex ikabidi awaache bila shaka sehemu aliyocheza alitaka kumpatia wivu Alexander taratibu akili yake angeihamishika kwa mkewe.

Minnie akabaki amesimama akimsubili Alexander azungumze, akawa kamsogelea karibu huku akimshika mkono wakizidi kusogea mbele.

   “” Ushaanzisha katabia kengine tena kabovu, umeona ubandit haitoshi Sasa wataka kujirahisisha kwa wanaume wa watu.”

   “” Tangu lini wewe umeanza kuwa na wivu na Mimi! Kwamba unaumia? Kingine nikwambie Alex ni Shemeji yangu.”

Minnie akafanya kuuchomoa mkono wake akiondoka pale na kwenda kukaa kwa Bibi.

Huku kwa Maina ilibidi amfuate Alexander na kuzungumza nae.

   “” Hivi unafikilia Nini wakati huu, naona upo karibu na Minnie tu Vipi kuhusu Mimi na wewe hatma yetu itakuwaje?”

 

   “” Aaa Maina! Mimi Alex kanizuia.””

Maina akahisi kuchoka akamshika mkono kwanza akimsusasusa.

   “” A you sereous Alexander! Yaani unasema Alex kakuzuia unakubali, hauwazi hata kuhusu upendo wetu?”

“” Maina Naomba unielewe tu. Nipe muda kuhusu swala hili basi.”

Muda huo Mlinzi alifika akamuita Alexander alihitajika kwa white house.

“‘ Mhuu! Baba nimefika.” Aliongea baada ya kufika.

“” Sawa keti hapa kwanza.”

Alexander akaketi huku akimtizama Maina.

“” Upo tayari kumuoa Maina! Sema mapema tutangaze siku ya Ndoa yenu leo.””

“” Mhu lakini Baba Mimi nimeoa” Aliongea huku akimtizama Minnie anavyozidi kucheka na Bibi yake.

“” Nataka majibu usipindishe kwanza, nataka niondoke hapa, usinipotezee muda.”

“” Nipe muda kwanza Baba, natakiwa kumpatia Minnie taraka kwanza Kisha ndio nimuoe Maina.”

“” Lini unampatia hio taraka..!!?”

“” Aaa niongee nae kwanza.””

“” Sawa ni Hilo tu waweza rudi.””

Ile ametoka tu Maina akamshika.

  “” Vipi kasemaje Baba.”

   “” Kasema mambo yameingiliana kwanza kuhusu swala letu atanipa majibu siku ya kesho.””

   “” Aaa naona ni kama naenda kukupoteza muda si mrefu lakini Alexander nakupenda sana! Na Sina mwanaume ninaemtegemea katika maisha yangu zaidi yako wewe.””

Alexander ikabidi amkumbatie tu huku akimuegemeza kifuani kwake.

   “” Sawa najua hilo kesho nitaingia kazini, nitafanya namna uwe karibu yangu hata Mimi natamani kuwa karibu na wewe muda wote.””

   “” Ayaa, ngoja niende nyumbani ,,, kweli sipo sawa hapa.”

   “” Naomba unisubili kwanza nitakusindikiza.”

Muda huo hata sherehe ilikuwa imemalizika ilikuwa ni wakati wa kupumzika hata hivyo muda ulikuwa umeenda, Minnie ilibidi apate maji kwanza huku akivalia suruali yake moja aliiteua kama ya kulalia akivalia na vest. 

Alilala kitandani kwani Alexander yeye alichagua kulala kwenye sofa. Masaa yalizidi kusonga mida ya saa Sita Alexander ndio anaingia ndani akivizia kwa woga woga! Alifungua Mlango taratibu make Minnie aliuegesha ndio anamuona Minnie kapitiwa usingizi hakutaka kumsumbua zaidi ya kuingia bafuni kupiga maji Kisha alikuja kulala pembeni na Minnie japo kwa tahadhari hakutaka kumgusa akizingatia uwepo wake.

Mida ya saa nane Minnie ndio anagutuka usingizini na hii ni baada ya kugundua pindi analala Alexander hakuwepo, alifanya kuwasha taa ndio anashangaa kumuona Alexander yupo pembeni yake nae alishituka kwa ule mwanga wakawa wanatazamana kwa muda baadae Minnie hakutaka kuzungumza alichukua mto na kwenda kulala kwenye sofa lakini Alexander akamstopisha.

   “” Hapana njoo ulale kitandani! Mimi mwanaume kwa hili lazima nijali.””

Minnie hakutaka kumsikiliza zaidi akajilaza kwenye sofa huku akichukua simu yake nakuanza kupitia Message za Nick alilipomuuliza kuhusu Alex.

   “” Sijui kesho anakuja na majibu gani, vipi kama atanikumbuka?”

Alexander muda huo alibaki kumtizama tu akiwa kakaa kwenye kitanda.

   “” Huyu mbishi mbishi mtu unafanya kabisa kwa Mapenzi yote lakini anavyokuchukulia ni tofauti, ndo maana huwa sipendi kujipa umuhimu kwa watu wasioona umuhimu wangu.”

Minnie huku aliwasha data ndio anaona Message ya Abdul kamtumia kama robo saa Whatsup.

   “” Vipi sherehe ilikuwaje,, wasije wamemnyanyasa wife wangu huko.”

Ikabidi atabasamu baada ya kusoma Ile message akiijibu.

   “” Kila kitu kipo sawa! Sema nimepamisi huko.”

Abdul nae alikuwa hewani baada ya kuona ujumbe wa Minnie ikabidi akae Kwanza kitandani achati nae vizuri.

   “” Ooh kipenzi Changu! mgumu kusema Direct kuwa umenimisi… Sasa maana yako Nini kusema umepamis huku?”

Minnie akatabasamu tu lakini muda simu yake ikaita ilikuwa ni video call, Abdul kampigia.

   “” Jamaniii Nini tena unafanya Abdul?”

Minnie akalalamika huku akimtizama Alexander akaona yupo busy ikabidi achukue Earphones zilizokuwa mezani akachomeka na kupokea.

Abdul muda huo alibaki kumtizama kwa sekunde Minnie Kisha alizungumza.

“” Sitavumilia tenaa kukuona unaendelea kukaa huko wiki kesho nakuja kukuchukua, mbona unateseka hivyo wewe ni wakulala kwenye sofa kweli! Kwani hakuna kitanda?”

Minnie ikabidi atupe macho kwanza akimtizama Alexander Kisha akazugumza.

   “” Hapana ni sawa tu! “

Alexander muda huo alikuwa kajikausha kumbe anafatilia vizuri mazungumzo Yale, kwani aluchowaza kwa Minnie yeye muda wote huwa anawaza ni anamspy tu.

   “” Abdul Mimi nataka kulala kesho basi.”

Minnie akajisahau kwa kutaja jina la Abdul, Alexander akawa amelidaka vizuri akajua huenda ni mwanaume wake na Minnie ndio maana kampigia usiku namna Ile  lakini alikuwa sawa kwani Minnie alikuwa yupo kwenye mahusiano ya Siri na Abdul, akaanza kumkolomea..

   “” Hey Mrs Abdul! Kwanini Sasa uliolewa na Mimi wakati unae Mme?”

Minnie ndio akashituka akaona bora kukaa kimya kama ataanza kujibizana nae ingewachukua muda.

Asubuhi ya siku hiyo Alexander na Minnie siku hiyo waliingia ALEMI MECHANIC GROUP kwa mara ya kwanza kabisa! Baada ya kufika huku walielekezwa utaratibu wote wa kazi wakawa wameanza kazi rasmi wakishirikiana na wafanyakazi wengine japo wao walikuwa kama mabosi.

Kwa Minnie ilikuwa ni kazi ngumu maana hakuzoea na yeye alipatiwa mafaili ya kuratibu mauzo yote yaliyofanyika, mpaka muda wa saa nane hata chai kunywa ilikuwa ngumu muda huo Alexander akawa ameingia kwenye ofsi yake.

“” Aaa Minnie mbona mzembe mzembe sana! Kujaza hizo documents umeshidwa au unamuwaza Abdul.”

“” Yaah namuwaza kama wewe unavyomuwaza Maina, siku Ile ulinambia nimekunyanganya furaha yako lakini hata wewe umefanya Vile vile.”

Alexander akawa kasogea karibu yake akijaribu kutizama jinsi anavyoingiza taarifa kwanza akifanya kuipotezea kauli ya Minnie.

   “” Mhuu sawa kumbe na wewe umewahi kupenda?”

   “” Sipo kama wewe huo upendo wa kunifanya kichaa sikufikia stage hiyo.””

   “” Ahaaa! Okay vizuri..! Basi kwangu utakuwa kichaa siku Moja kwa huo ubandit wako.”

Minnie ikabidi amalizie taarifa zake nae akamkaushia, baada ya kumaliza ndio anaona mezani kunae vitafunio tu inamaana chai pekee ndio alikunywa.

   “” Mchana hauli, sijaona mhudumu wa chakula akiingia huku.”

   “” Nimeshiba, kazi yako naona nimeimaliza.””

  “”  Vizuri. Ngoja niipitie hapa.””

Minnie ikabidi atoke nje akapata muda wa kuongea na Kaka’ke lakini Kaka’ke alimweleza kuhusu Alex mpaka akashangaa kumbuka Nick hakuifahamu kuhusu Minnie kuolewa lakini siku hiyo akamueleza kila kitu jinsi ilivyokuwa mpaka akaolewa White House, Nick akahisi kuchoka lakini alizungumza.

   “” Ni sawa yote yametokea lakini Mimi sitaki kuona hii habari ya kulipa kisasi ikiendelea katikati yenu, tuseme yalitokea yamepita kwasasa wewe kaa na familia yako!! Kwenye kulipa kisasi siwaungi mkono kabisa, visasi vimejaa vitu vingi ukishangaa unaweza kuondosha maisha ya mtu.”

“” Aaa kaka mbona unakuwa na kigugumizi kuhusu hili ? Kwani wewe huumii Mama kuuwawa? Ni sawa, kama haupendi wewe lakini kisasi lazima kikamilike ikiwezekana tena Cha damu.”

Muda huo anamaliza kuzungumza akasikia makofi yakipigwa kuelekea alipo hakuwa mwingine zaidi ya Alexander.

 Je Alimsikia…………? Nini Kitaendelea?  Usikose SEHEMU YA KUMI NA NNE YA KISASI CHANGU

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

 

6 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version