Ilipoishia “Minnie ndio akatulia Kuna kitu alikipata hii ikamfahamisha kama picha hii ipo nyumbani kwa white house huenda akifatilia ndio atapata ushahidi kamili wa kumfunga white house, swali linakuja atapataje huo ushahidi wakati amekataa kurudi kwa white house na kamuahidi Alexander hatoongozana nae tena?”

Huku sebuleni kwa Mzee Mzobe nae alikuwa Bado anamawazo sana alichukua picha ya Mama’ke Minnie akizidi kuitizama kwa makini Kisha aliongea peke yake.

“” Nick na Minnie hawapaswi kufahamu kuwa Mama Yao aliwahi kuwa mke wa Mr Denishoo, wanachotakiwa kufahamu wao ni alikuwa akifanya kazi kwa Mr Denishoo basiii.”

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA MOJA 

Baadae Minnie na Alexander waliongozana kushuka mpaka sebuleni Wanafika wanamkuta Mzee Mzobe yupo mezani na makaratasi wakagundua ni maswala ya kazini kwake, Alexander ikabidi amsogelee ni alihitaji kuongea nae.

“” Baba samahani kwa kile kilichotokea kwa Mkewangu huenda ni kutokuelewana tu! Ila Naomba niondoke na mkewangu wangu! Kama nimemkosea Naomba msamaha mbele yake,,, natakiwa kumchukua mkewangu Baba.””

Minnie yeye katoa macho ni anashangaa ni lini yeye alikuwa mke wa Alexander Tena kwenye matamshi ya mkewangu, alihisi anamuigizia Baba’ke ikabidi akaze.

“” Baba Mimi sitaongozana nae nitabaki na wewe Leo kesho nitarejea mwenyewe.””

Alexander akashangaa mbona kamugeuka, kumbe walipobaki chumbani Minnie ilibidi azungumze vizuri na Alexander alimpa masharti kama atamrejesha White House itabidi akamuuliza White House Ile picha aliyoiona chumbani ni yanani tenaa aulize kwa akili na sio kusema niliona kwa Minnie, Alexander akawa ameafiki na wakakubaliana atafanya hivyo lakini kafika pale kamugeuka.

“” Minnie,,,, mbona unakuwa hivyo teena si umekubali twende wote halafu unakataa teenaa…!!?”’

“” Ooh! Lazima nikatae make kule kwenu hamnaga hata ruhusa ya kuona familia yangu, kesho Nitakuja.”

Baba ikabidi aingilie alijua kabisa Binti yake kamkumbuka.

   “” Alexander muache kesho nitamkumbusha afike kwenu mapema, angalau kwa Leo apumnzike tu hata Mimi nimemkumbuka sana.””

“” Sawa. ” Akamgeukia Minnie Kisha alimtizama sana na kuzungumza. 

“” Kama utaniangusha nami nitavunja ahadi.”

“‘ Nimekuelewa bhana wewe nenda.”

Alexander akawa ameondoka kinyonge huku ndani Minnie hakuchelewa kuanzisha maada make ndio muda aliokuwa akiungoja.

   “” Kule chumbani Alexander aliona picha ya Mama na akasema ipo white house Mimi naona huyu Alexander ndie atatupatia ushahidi wa maovu ya White House, kwanini alimuua Mama..?”

Mzee Mzobe akatulia kwanza anafikilia kama Minnie ataanza ufukunyunyu atagundua mapema kuwa Mama’ke yeye alikuwa mke wa White House, ikabidi apangue.

“” Sawa ni njia nzuri lakini kutafuta ushahidi kwa kumtumia Alexander unamwamini vipi na vipi kama ataenda kukugeuka unafikili itakuwaje!!?”

    “” Ooh… Alexander anigeuke, Sizani lakini kama namwamini hivi.”

   “” Usimwamini sana, ushahidi kafatilie wewe halafu umemshilikisha mapema sana ujue.”

    “” Aaah Baba ushaanza na wewe, kujua kwake ndio kutatua mapema upelelezi wetu, kingine nataka niende kambini.”

    “” Aaa kambini tenaa..!? Wale majambazi wanaweza kukuzuia tenaa halafu sahii wewe ni mke wa mtu inatakiwa kujisimamia.”

    “” Nitaenda tu Baba, hivi wafikili Mimi napumua pale. Ani mpaka unatamani kutoka nje! Tafadhari Baba Naomba niruhusu tu.”

    “” Sawa, utaenda.”

Minnie alifurahi kweli ikabidi atoe vyombo haraka Kisha alianza kuosha hakuchelewa kumaliza kujiandaa Kisha alichukua pikipiki ya Baba’ke akikata njia.

Alifika mpaka kwenye jengo kubwa na hapo ndio Kambi ilipokuwepo, Aliingia akiendesha pikipiki kwa Fujo Sema walimzoea sana hawakuisha kumpigia kelele na kusogea kumkalibisha.

Kwa ujumla jengo hili lilikuwa likimilikiwa na kiongozi wa serikali akiwa ni waziri wa kilimo na ndie alikuwa na kikosi hicho Cha majambazi kwenda ukagundue pale huwa Kuna biashara haramu zinafanyika sio rahisi.

Minnie baada ya kuingia aliingia Moja kwa Moja Kuna Holl la vijana wakifanya mazoezi pale, hakuchelewa kuwavamia kwa kuwaenjoy akiomba wajaribu kupigana, utani wa hapa na pale uliendelea huku furaha ya Minnie ndio ilizidi kuonekana akiwa na wenzake, baadae walisitushwa na sauti ikimuita Minnie.

Minnie baada ya kusikia sauti Ile ilibidi aifuate make aliitambua vizuri akawahi kumkumbatia.

   “” Baba nimerejea tenaa unajua Nilikumisi kweli, yaani huku kuolewa unakosa hata kufurahi na wenzako.”

Wenzake ikabidi wamcheke tu ni kweli aliwamisi sana baadae aliongozana na kiongozi huyo akizidi kumfuata nyuma nyuma akiruka ruka kama kumbi kumbi.

   “” Boss Kendo. Sasa Mimi nitarejea hapa lini..!?”

Bosi kendo akabaki kucheka tu huku akizidi kuzungumza.

   “” Wewe tayari ni mke wa mtu, halafu umetokaje white house wewe ni mke wa mtu ujue.””

   “” Nishachoka tayari.””

   “” Ni kwakuwa hujampenda huyo mwanaume, lakini Ndoa ni tamu endapo nyoyo zenu zitamechi sawa, kingine ipe muda Ndoa yako.”

Minnie ni kama hamuelewi kabisa kuhusu swala la Ndoa lipo kushoto, alimfikilia Alexander vile wapo busy na Maina akaona wanafaa wawe hivyo hivyo wanaendana na sio kwa upande wake huenda anahisi Kuna mtu hapo nyuma ni kama alifaa kuwa nae.

“” Sasa Boss Kendo,,, kesho inatakiwa nirudi pale white house tenaa, Kuna kazi nataka nikaimalizie.”

“” Umejipanga kikamilifu, halafu Kaka’ko anasemaje kwanza…?”

Muda huo tayari waliingia ndani na kuketi kwenye meza kulikuwa na chakula kiliandaliwa pale, Minnie hakuchelewa kupakua hata hivyo maisha ya pale aliyazoea.

     “” Mimi nataka kumwambia Nick kila kitu kinachoendelea huku ikiwezekana afunge safari aje kutuona, Nimemumisi kweli kaka,, Sema baba anakataa kumwambia.”

   “” Wewe unaona ni sahihi kumwambia..!?”

Boss Kendo aliongea huku akizidi kula pepcon zilizokuwa mezani.

   “” Aaa huyu nae Sasa maswali mengi kasoro anijibu direct anapindisha, swali kwa swali Mimi Sina jibu bhana.”

Wakati Minnie anazidi kuwazua , Boss Kendo alimuacha pale akiendelea na kazi zake, kwaujumla ni mtu mwenye harakati nyingi sana kama ungetaka kuongea nae kwa uharaka nahisi ungegaili kwa Ile mizunguko atakayokupigisha ndani Hadi upate majibu yako ni sio Leo inahitaji uvumilivu, Minnie akaona asimtanie mpaka apate majibu aliamka nae akimfuata Kila Kona lakini alishangaa anavutwa chemba kwenye chumba kimoja huku akizibwa macho.

“” Aaa Abdul… Bilashaka ni wewe.” 

Minnie aliongea akiwa na uhakika na maneno yake. 

“” Ooh! Umenipata kumbe, Nambie mbona unamfuata Baba unataka kumwambia Nini, make wewe kasumbufu.”

Minnie akamtizama,, akaona kampotezea muda tayari, isitoshe niwatu wenye ukaribu sana wawapo pamoja, kama ataanza kumsikiliza itachukua muda ni bora ajihami mapema.

“” Na shida nae, sitaki uanze Maada zako za nyuma yaliyotokea ni yamepita.”

“” Minnie,,, kwanini Sasa ulinifanyia hivyo!! Ukaolewa na Alexander kweli..!?”

“” Aahaa! Ushaanza maneno yako, Mimi ndo nishakuwa mke wa mtu,  kwani hujapata tu mtu wa kumuoa..! Halafu unauliza kama hujui kuwa Mimi pale ni mission tu.”

“” Sio rahisi kihivyo make Mimi hapa, nilikupenda wewe na nitazidi kukupenda siku zote swala la kupata mwanamke nalitoa wapi wakati nishakupata wewe,,, ayaa Niambie Alexander hakusumbui chumbani?”

Minnie akatulia kwanza huku akimtizama Abdul, bilashaka position ya watu hawa ilionesha ni walikuwa na mahusiano ya chini chini pindi Minnie akiishi pale alianzisha mahusiano na mtoto wa Boss wao yaani Mr Kendo.

“” Minnie macho yako yanaonesha tayari umefanya hivyo si ndio, kumbuka upo pale kwa Dili tu. Au umempenda Alexander…?””

Minnie akafikilia kwanza akajiuliza hata kama ingekuwa vile sio rahisi kumwambia.

  “” Aaa Abdul jamaniii sio hivyo nina mipaka yangu pia.””

Abdul hakuchelewa kumkumbatia Kisha alimpatia busu la kwenye midomo yake, Minnie alibaki katulia tu baadae alisimama aondoke.

“” Na Leo utaniacha wakati huu teenaa…? Siku Ile ulikimbia na sikukuona tena na ukaenda kuwa mke wa Alexander, vipi na leo utaniacha teena?”

Minnie akabaki katulia vilevile make Abdul alimkumbatia na kumshika kiunoni,,, Mihemko aliyokuwa nayo Minnie ilikuwa ni ngumu kuikabili kwenye mwili wake alibaki katulia tu, Abdul alifanya kumgeuzia upande wake na kufanya kumtizama Kisha alimkumbatia huku moyo wake na mwili wake ulikili ni alimkumbuka kweli Minnie; Minnie nae hakusita kumkumbatia hata yeye ni ngumu kuzizuia hisia zake make alihama kwenye jumba Hilo na kwenda kuishi kwa White House kama miezi mitatu akisubili Ndoa yake, na muda huo Minnie hakupewa ruhusa ya kuonana na mmewake mtarajiwa mpaka siku ya Ndoa ilipotimia na hata walipooana hakuna kitu kilichoendelea baina yao kama Wanandoa, kwahiyo hakuwa na budi kujiachia kwa Abdul make joto la mwili wake lilichukuwa centigrade za nyuzi kadhaa ni ngumu kuzihimili kwa haraka haraka bila tiba.

Huku kwa Mzee Mzobe alizidi kumsubilia Minnie lakini hakutokea akajua kabisa tayari amenogewa na kukaa kule hapo angemsubili mpaka Asubuhi yake.

Masaa yalizidi kusogea Minnie ndio anakuja kusituka anashangaa kuona yupo kwenye kumbato la Abdul, hakusita kuonesha tabasamu lake kwanza Kila alipomtizama Abdul.

Kumbukumbu zake zikamrejea ndipo anakumbuka alimuahidi Baba’ke kurejea mapema haraka alifumbua macho kwa nguvu usingizi umtoke.

   “” Ashiii!!! Nini Sasa Nimefanya inamaana baba atakuwa akinisubili.”

Akawahi kuishika simu yake haraka ndipo anakuta missed call mbili za Baba’ke akajua tayari alimtafuta, akaangalia muda akaona ni saa sita usiku inamaana hawezi tena kutoka na hii ni kutokana na Sheria za hapo kutoka ni mwisho saa sita kamili na hapa ilikuwa ni kama robo saa imepita, aliamua kumuamsha Abdul haraka aone atamsaidia Nini.

Abdul ndio anaamka huku akijinyosha alifanya kumkumbatia Tena Minnie ambae hakuchelewa kumsukuma.

   “” Unaona nipo hatarini bado unanikumbatia teenaa… Aya nafanyaje? Baba ananisubili nyumbani na nilimuahidi nitarejea mapema.'”

“” Kwani saa ngapi hapo…!!?”

Minnie akahisi kumkoa kwani aliongea kwa sauti ya usingizi akaona bora ambust akili zake kwanza. Aliingia bafuni na kuja na maji kwenye kikopo Cha kuogea akamumwagia usoni.

“” Ayaa angalia saa uniambie ni saa ngapi..!?”

“” Lakini Minnie maji yabaridi haya..!?”

Ikabidi Minnie arudishe kopo bafuni akaja kumkalia pembeni yake make muda huo Abdul ndio alikuwa akitizama saa.

“” Hamna namna tenaa, kesho Asubuhi nitakupeleka nyumbani kwa Mzee Mzobe, ninayo majibu ya maswali yake.””

Minnie ikabidi anune tu baadae aliona ujumbe uliingia kwenye simu yake, alifungua hivi anashangaa ni Alee alimtumia ujumbe inamaana huyu ni Alexander ila yeye aliamua kumsave Ale vile hataki kuitwa na ndio alimsave vile, akafanya kusoma ule ujumbe.

   “” Hellow Bandit girl, kesho usiniangushe hakikisha unajiandaa mapema sawa.. uwe na Usiku mwemaa mke wangu kipenzi.”

Minnie baada ya kusoma alihisi kukasirika kwa kuitwa bandit halafu mwishoni aliitwa mke kipenzi akajua ni uhadaaji wa khari ya juu alimfanyia, alichoamua hakumjibu ila nafasi yake ikaapiza ni hiyo kesho atajutia kwa maneno yake Wala swala la kwenda Asubuhi angeligaili mapema mno.

“” Abdul nitafutie chumba Cha kulala, Baba’ko akiniona nipo hapa ataniadhibu sana.””

Abdul akafanya kucheka tu huku akimkumbatia kifuani kwake, angewezaje kumtenganisha mrembo huyu usiku wote uwe wake wakati anajua kabisa ni ngumu wao kupata siku kama hiyo wakaenjoy pamoja.

   “” Minnie Mama, Asubuhi tunaamka mapema, Baba hawezi jua naomba ondoa shaka ukiwa na Mimi.””

“” Unaongea kama Mwana wa Mfalme!! Ila maneno yako ni matamu lakini machungu nikiyapokea yote.””

 “” Lakini Minnie… vipi kama utaacha kisasi chako kwa White House Mimi nikakuoa tu, wewe hufikili kuwa na familia?”

  “” Ushaanza, Mamangu hakutaka apumnzike mapema kabla ya siku zake, aliefanya hivi nae atapumnzika vilevile bila ridhaa yake.”

“” Mhuu basi bhanaa! Basi tulale.”

Asubuhi kulipokucha Minnie alikuwa wa kwanza kuamka tena alidamka Asubuhi na kuingia kwenye mazoezi kwa mtu angemuona pale isingekuwa rahisi kugundua kuwa usiku wa jana walikuwa na mtoto wa Boss teena wanae mahusiano?

Minnie aliendelea kupiga mazoezi akiwa na wenzake, mwisho kabisa Abdul ndio anafika akiwa bado macho yake yana usingizi, akasogea mpaka kwa Minnie akimsalimia.

“” Ooh Minnie bondia habari ya Asubuhi..!?”

Akabaki kumtizama tu Kisha akaminya midomo yake.

“” Bwana Abdul naomba unisindikize nyumbani! Hata hivyo nimewasalimia sana, Bosi Baba yupo wapi?”

“” Mara hii umuone, kaingia kazini mbona.”

“” Basi twende wewe.”

“” Kajiandae Sasa, au unaenda na hizo nguo zako za mazoezi.”

“” Ikiwezekana.”

Abdul ikabidi amuache kwani Minnie kwenye mdomo hashikiki. 

Minnie ikabidi amfuate huku akizidi kuongea nae.

“” Umelala tu mpaka sahii, nilitegemea uniamshe ungeniamsha kweli?”

 “” Aaa si ushaamka…!? Hebu jiandae basi upesi nikuwahishe.”

Baadae Minnie alikwisha jiandaa tayari, Abdul aliwasha pikipiki akimpeleka Hadi nyumbani kwa Mzee Mzobe.

Walifika wakamkuta Mzee Mzobe ndio anafunga geti atoke akashitushwa na ugeni wa haraka pale.

“” Ooh! Abdul bora hata umemrejesha mapema make niliwaza kuhusu yeye.””

“” Aaa Baba Shikamoo! Jana ilikuwa ni ngumu yeye kurudi make tulimumkumbuka sana na hapa kaondoka kwa basi tu ila tunamhitaji bado.

Abdul akaongea huku akitupia macho kwa Minnie.

Minnie yeye akawa kapitiliza ndani asingeweza kuvumilia maneno ya Abdul aliyoyajaza mafumbo yenye ukweli ndani yake.

“” Wewe Minnie husalimii, Kuna siku utakula bakola wewe! Ayaa njoo haraka hapa.”

Minnie ndio akakumbuka ni kweli hakusalimia alirudi na kupiga magoti kwa Baba’ke huku akiomba msamaha anaujua utata wa Baba’ke.

“” Baba samahani Ani nimechanganyikiwa huku simu hazikati kwa white house wananisisitiza kweli!”

“” Ayaa kajiandae mapema. Abdul ngoja nifike kazini mara Moja.”

“” Sawa Baba.”

Abdul ikabidi azame ndani Moja kwa Moja Hadi chumbani kwa Minnie make aliijua vizuri nyumba hii, ni Moja kati ya nyumba za Baba’ke inamaana kina Minnie walipewa kuishi bure.

   “” Vipi Sasa umejiandaa kwenda Ukweni kwako..!?” 

Kabla Minnie hajajibu  Simu ya Abdul ikaita alikuwa ni Baba’ke kampigia, ilibidi atoke chumbani na kwenda kuipokea pembeni.

   “” Wewe mbona haupo kazini Leo? Fanya haraka Kuna kazi inakufikia hapo ifanye haraka Kisha nitumie.”

“” Sawa Baba.”

Ikabidi arudi kwa Minnie kapoa.

   “” Mimi naondoka nahitajika kazini, Baba kanipigia simu niende kazini,, halafu naomba uzingatie maelekezo yangu, hata kama ni mission.. Kaa mbali na Alexander usiruhusu akuguse ovyo ovyo.”

“” Mhuu sawa!”

Abdul akaamua kumuaga kwa busu Kisha aliondoka, Minnie akabaki kutafakari ni aende au asiende, akaona ngoja alale huenda akiamka atakuwa na majibu.

Usingizi ulimchukua huku kwa Alexander alipiga simu mfululizo asipokelewe, hasira aliyokuwa nayo ilikuwa ni ngumu kuimudu ilibidi atoke chumbani kwake angalau amfuate Minnie.

Ile anafika sebuleni alikutana na Bibi akawa kamsimamisha.

    “” Mjukuu vipi, wapi tenaa Asubuhi hii?  kumbuka Sandra na Alex wapo njiani na jioni tutafanya sherehe inatakiwa wewe uambatane na mkeo.” 

“” Bibi, Minnie ndo hapokei simu zangu hapa Nampigia Simu hapokei na tulikubaliana atafika ona Sasa huyu mkamwana mnaemtaka alivyo na Dharau, acha nimfuate tu si ana kiburi…?””

“” Sawa wahi kumrejesha.”

Alexander aliwahi kwenye gari haraka Ile anaingia tu anashangaa Maina tayari yupo kwenye gari alifanya kumuongelesha.

“” Alexander popote utapoenda nitakufuata, hivi kweli unaenda kumrejesha Minnie na vipi kuhusu Mimi? Kwanini siku ya leo isiwe Ndoa na watu wote washuhudie?”

Alexander akashusha pumnzi kwanza haelewi atafanya Nini wakati huo huku Maina na kule Minnie ni wapi aegamie? Akaona sio shida mambo yataeleweka mbele ya safari ikabidi achochee gari hadi nyumbani kwao Minnie.

Alifika nje ya geti akapaki gari kisha alishuka kwa hasira akielekea getini, Maina nae akafatia nyuma Alexander akawahi kumrudisha.

   “” Tafadhari nisubili hapo, hautaruhusiwa kuingia kwenye nyumba za watu bila ridhaa ya wenye nazo.”

“” Lakini Alexander…. Maina akajaribu kumshika lakini geti likarudishiwa akabakia nje.”

Alexander akaingia Hadi chumbani kwa Minnie make alikuwa tayari ni mwenyeji kwenye chumba hicho, alifungua Mlango anashangaa kumuona Minnie akiupiga usingizi, alitamani kumuwasha kofi kwa hasira alizokuwa nazo ilibidi ajizuie na kukaa make akileta ubabe wake ni ngumu kumuondoa Minnie kwao! Alichukua muda mwingi kumtizama na mwisho kabisa ilibidi amshike kwenye paji la uso akimuita. “” Minnie…!!”

Minnie kwa mbali ndio anaota njozi ni kama kachelewa kwenda kwa Alexander alishituka akiiita “” Alexander”” Ile kutua macho anaonana uso kwa uso na Alexander akawa haamini kwanza akafanya kumshika usoni ndio anashangaa ni yeye kweli?

Alexander alipo ni kama alipandikizwa hasira yote yaliyoendelea pale ni aliona Minnie alizidi kumhadaa, alifanya kusimama huku akiondoka akimuachia maagizo.

   “” Nimekufuata wewe Naomba tuongozane white house.””

“” White house…? Kuzimu…?” Mimi siondoki.”

Minnie akazidi kumkela Alexander na alifanya yote nikwasababu ya Ile message ya kumuita Bandit.

Alexander ikabidi asimame kwanza ni alimkela kweli muda huo, lakini Ghafla Maina akatia timu sijui aliongea Nini na walinzi wakamruhusu aingie, Alexander ndio akawahi kumuona ikabidi amuite.

“” Maina umeingia tenaa …..?”

Minnie ndio akasikia jina la Maina ikabidi atoke alivyovaa Sasa kweli alikuwa kinyumbani kwao alivaa prova lenye pensi yake nyeusi Kisha alivaa na raba nyeupe, Maina akawahi kumuona akimshangaa anajiuliza inamaana Minnie ndio huvaa hivi mbona ni kigensta vile na sio alivyomchukulia mshamba mshamba? Alexander ikabidi ageuke kumtizama Minnie hakuamini na muda huo alikuwa akinyosha mikono yake juu.

Maina akamtizama Alexander jinsi anavyomtizama Minnie akajua muda si mrefu atakimbiwa, ikabidi amshike mkono kwanza akizungumza nae.

   “” Muache akae kwao unaona kabisa anaefuraha kuwa hapa, twende tukamilishe Ndoa yetu leo.”

Minnie ndo kwanza akawapita akisogea mezani nakuanza kumenya nanasi, wakazidi kumtizama jinsi ambavyo hana muda nao, Alexander ikabidi amsogelee karibu akisimama nyuma yake akimuongelea sikioni.

“” Please Minnie acha maigizo basi, Nyumbani wanakusubili wewe, kumbuka ahadi yetu Mimi na wewe niliahidi kutoivunja,, angalau kwa hili niamini turudi wote basii.” 

Nini Kitaendelea?  Usikose SEHEMU YA KUMI NA MBILI YA KISASI CHANGU

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

 

12 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version