IlipoishiaTobaa!!! Alexander akahisi joto kuongezeka na kujiona mjinga inamaana alishidwa kweli kujiongeza kumzuia Minnie asiondoke wakati ndoa yake ilipitishwa na White House kwa matakwa yake na yeye akaikubali na vipi Leo…!? “” Na kingine alijisahau kuwa Sheria za White House ni kama moto wa tanuru ukichochewa hata kwa mvua hautazima  iweje kwakwe Bwana mdogo mdogo Alexander ambae ndio kaingia kwenye hii Ndoa hata wiki hajamaliza eti mwanamke anarudi kwao kwa kuendekeza penzi lake la kwanza ni yupo sahihi  kweli..?”

Endelea 

SEHEMU YA KUMI

 

Alexander hakuwa budi kuongozana na Mlinzi kuelekea kwa Baba’ke, alibisha Mlango akawa ameruhusiwa kuingia.

   “” Aaa Baba nimefika.””

White House muda huo alikuwa yupo busy na komputa ni kama hakumuona kijana wake, baadae alizungumza huku akiendelea kutyping.

   “” Unampenda Maina..!? Basi kesho jiandae kwa Ndoa nyingine, Alex pia kesho anarejea.”

   “” Aaa Baba Ndoa tena…!? Si nimeoa majuzi tu.”

“” Nimesema jiandae na Ndoa, basiiiiii.”

Alexander akabaki kaduwaa tu akimfikilia huyu Baba’ke alikuwa na maana gani kumwambia ajiandae kwa Ndoa hapo kesho, ilibidi ashuke taratibu chini akiwa na mawazo sana Ile anafika chini alimuona Bibi akinyunyuzia maua ikabidi amsogelee akiwa ni mnyonge sana.

   “” Ooh mjukuu wangu umenifuata? Bilashaka unawasiwasi sana na kauli ya Baba’ko, Si unampenda,, basi muoe.””

   “” Lakini Bibi ni haraka sana isitoshe nimeoa Juzi tu, sahii nimuoe Maina ni haraka mno, halafu Kaka akifika unafikili nitamwambia Nini, Juzi tu nimeoa akasema atakuja kumuona shemeji yake halafu akute Tena nafunga Ndoa na mtu mwingine si aibu hii.””

“”” Eeehee!! Umebadilika sana Alexander yaani Mimi sahii natambulika kama mtu mwingine, inamaana hata Maina jina linakuwa gumu kuliita..!?”

Wote wakashituka inamaana Maina alikuwa akiwasikiliza, Bibi akaamua kuwaacha pale wawili wayamalize.

“” Alexander kwanini unanifanyia hivi usitake kuniambia umempenda Bandit girl.””

“” MAINAA…! Hebu acha Dharau basi unahisi moyo wangu ni package ya Kila kitu unahifadhi…? Siwezi Penda mwanamke wa sampuli hiyo.””

“” Ila Nini Sasa, mbona unakuwa na kigugumizi Cha kunioa wakati Baba kakubali, kwanini hutaki..?”

“” Basi niache nikae mwenyewe kwanza.”

“” Alexander… Nini lakini….!!?”

Alexander ikabidi amuache pale akienda chumbani kwake. Maina nae akafatia nyuma nyuma akiirusha miguu yake ni kama alilazimika kutembea.

Huku kwa Minnie alikuwa tayari kafika kwa Baba’ke kama robo saa hivi ilipita, muda huo alikuwa jikoni akipika chakula baadae aliivisha na kupeleka mezani, ambapo alikuwepo Mzee Mzobe pamoja na Kamanda SU ni miongoni mwa Kamanda wenzake.

   “”” Ooh Minii umekuwa tayari naona Leo umemkumbuka Baba’ko.

Kamanda SU aliongea huku akimtizama Minnie usoni. “”

   “” Aaa Baba nimekua ndio! Bilashaka matazimio yako ni vile ulivyonipokea nilivyoingia hapa.”

Mzee Mzobe ikabidi acheke tu huku akivuta taswira ilivyokuwa mpaka anakutana na Kamanda SU, Alianza kukumbuka miaka mitano kupita ilikuwa ni hivi ……………………

              ++++++

Ni Siku Ile alivyotaka  kumtafuta Miniii msituni, alizunguka msitu karibia wote ndipo aliona Kuna hema msituni ni kama watu waliweka Kambi pale ndipo alifanikiwa kufika kwenye Kambi hiyo kumuulizia Minnie kwa bahati nzuri alimkuta Minnie yupo pale inamaana siku Ile alivoenda kwenye Ile kambi baada ya kunusa ule unga ndio alizima pale pale kumbe ilikuwa ni madawa ya kulevya, baadae wale majambazi walipita katika eneo hilo ndio kumuona Minnie akiwa amelala wakawa wamemchukua na kumpeleka kwenye Kambi Yao walipohamia na kumpeleka kama mateka.

Mzee Mzobe anazidi kukumbuka baada ya kufika pale alimuomba Minnie kwa wale majambazi arudi nae lakini haikuwa vile wale majambazi walimkatalia wakawa wamewachukua mateka Minnie na Baba’ke! Ndipo Waliendelea kukaa kwenye Kambi hiyo kama watumwa hawakuweza kuruhisiwa kutoka pale zaidi ya kushinda ndani baada ya kuona wanaweza kuwatoroka.

Ni miezi mitatu ilipita wakiendelea kuishi pale, mwisho Kuna kiongozi mkubwa alikuja katika ngome Ile akawa amepewa habari ya Minnie na Baba’ke akawa ameonana nao ndipo akaomba aondoke nao wakamtumikie, Usiku huo huo Minnie pamoja na Baba’ke wakasafilishwa ikiwa ni safari ya mbali anakumbuka walipanda ndege lakini fahamu zake alikuwa haelewi ni wapi walielekea na hii ni flaudi walifanyiwa kwani waliweza kuchomwa sindano iliowafanya akili zao kutokuwa sawa.

Na baada ya siku mbili walijikuta wakiishi kwenye mjengo mkubwa na hii ilikuwa ni visiwani Zanzibar, waliishi kwenye himaya ya majambazi vilevile takribani ni miaka miwili kupita walianza kuzoea mazingira ya pale huku Minnie alianza kufundushwa kazi za kijambazi aliweza kupambana na vikosi mbalimbali baada ya kuchukuliwa na kwenda kupola vitu vya vya watu na hapa ndipo Minnie alivyozidi kuwa bandit, Wakati Minnie alivyokuwa akifanya vile Mzee Mzobe yeye alikuwa kaungana na mumiliki wa kile kikosi wakifanya kazi kwa pamoja wakishirikiana kwa pamoja hata hivyo Mzee Mzobe hakuwa zuzu kiasi hicho alitaka kupata nguvu kubwa kupitia kikosi kilekile cha majambazi Ili aweze kulipiza kisasi.

Minnie alizidi kuiva kwenye mapambano akawa ni mtu mwenye ujuzi mkubwa. Mzee Mzobe baada ya kuona mwanae yupo fit aliamua kuongea na mkuu wa kikosi kile Cha majambazi akawa amemueleza vizuri kuhusu kisasi alichowahiwa kufanyiwa katika familia yake aliomba nguvu ya kulipiza kisasi katika familia ya Kamanda mmoja aliyeweza kuiangamiza familia yake.

Mzee Mzobe akazidi kuvuta kumbukumbu akizidi kutukumbusha ilikuwaje yeye akataka kulipiza kisasi au moyo wake unawiwa kulipa kisasi muda wote?

Ni siku Moja akiwa Bado yupo jeshini aliweza kutaharukiana na mwanajeshi mwenzake aitwae Kamanda Denishoo, Kamanda huyu alikuwa akitoka na Mkewe kisirisiri yaani Wana mahusiano na aliekuwa Mama’ke mzazi na Minnie pamoja na Nick, ugomvi huu ulizidi kuongezeka Kila kuchwapo Kamanda Denishoo alizidi kupalilia penzi lake na Mama Minnie na kujikuta akibeba ujauzito wa Kamanda Denishoo mpaka alijifungua mtoto wa kiume.

Kamanda Denishoo alionekana kuwa wadhifa mkubwa serikalini na hata katika maisha ya kawaida alikuwa akimiliki miradi mbalimbali iliyomfanya jina lake lizidi kukua. Kwa Mzee Mzobe ilikuwa ni ngumu kumkabili Kamanda huyu kutokana na nafasi yake ilikuwa ni ndogo kukabiliana nae. Kamanda Denishoo alifanikiwa kumuoa mke wa Mzobe wanakwambia pesa ni sabuni ya roho na hiki ndio kilifanya Mke wa Mzobe amkimbie na kwenda kutua mikononi kwa Denishoo ale Maisha vizuri, wanakwambia ukipata nafasi itumie lakini usisahau nafasi hiyo chimbuko lilianzia wapi.

Anazidi kukumbuka ilikuwa ni siku Moja Mzee Mzobe alishidwa kabisa kuvumilia siku hiyo aliamua kuvamia kwa Kamanda Denishoo kumfuata Mkewe, aliingia pale akiwa na siraha walinzi walizidi kumzuia lakini haikusaidia mwisho kabisa Kamanda Denishoo aliwazuia walinzi huku akitoka kifua wazi kwa kujiamini akiwa kavaa pensi, alimsogelea Mzee Mzobe japo kwa wakati huo aliitwa Mr Mzobe alianza kuzungumza nae.

   “” Aaa Kamanda Mzobe huu ugomvi wetu endapo utafanya kitu chochote kikamwaga damu naimani ugomvi huu hautakuja kuisha kamwe, hebu tuongee vizuri tulimalize hili,, Mimi nimempenda mkeo na yeye kanipenda inatakiwa ukubali matokeo tu.”

Kwa Mzee Mzobe ilikuwa ni ngumu kukubali hapo hapo alimnyoshea bastola angalau amuue lakini ilikuwa tofauti walinzi walifika kumzuia huku ugomvi ukawa umechukua nafasi kubwa mlio wa risasi ulisikika ukirindima pasina mpangilio na mwisho kabisaa sauti ya risasi ilisikika wote wakatua macho kwa mshangao hawaelewi muda huo huo Mke wa Mzobe alishuka chini ikiwa risasi imetua kifuani mwake, hakuna alieamini kwa kile kilichotokea ikabidi wote wamuwahi lakini kwa bahati Mbaya risasi Ile ilitua kwenye moyo na hapo hapo Mama Minnie alipoteza maisha. 

Mzee Mzobe akazidi kutukumbusha kuhusu chanzo Cha mkewe kupoteza maisha, japo kifo chake hakikueleweka vizuri ni nani alishoot risasi make wote walikuwa na bastola mkononi na muda huo Mr Mzobe alikuwa kamnyoshea Kamanda Denishoo amfyatue, ilikuwaje akafyatua risasi kumlenga Kamanda Denishoo lakini risasi ikatua kwa Mrs Mzobe? Hapo mpaka Sasa haikujulikana lakini Mr Mzobe aliamini Kamanda Denishoo aliamua kumuua mkewe akitumia kauli bora tukose wote.

Baada ya Mzee Mzobe kumaliza kumhadithia kiongozi wa majambazi ndio taratibu zikaendelea kumfatilia Kamanda Denishoo, huku target kubwa ikawa ni Mzee Mzobe kutafuta namna ya kurudi jeshini hata hivyo umri wake uliruhusu kulitumika jeshi takribani miaka kumi, alianza kufatilia taratibu zote ndipo akafanikiwa kurudi jeshini huku akizidi kumfatilia Kamanda Denishoo.

Kwa bahati nzuri walipata taarifa zote na nzuri zaidi Kamanda Denishoo kwa Ile taharuki aliweza kuhama Mbeya na Sasa alikuwa akiishi Zanzibar na kingine zaidi Kamanda Denishoo alikuwa ni mtu mashuhuri sana jina lake lilikuwa ni kubwa na lilibadilika kwani Kamanda Denishoo wasasa aliitwa “” White House “”

Mzee Mzobe kumbukumbu zake ziliishia hapo baada ya kusikia Mlango unabishwa ikabidi ainuke na kwenda kufungua, anashangaa mlangoni anamuona ni Alexander kasimama, alimuamkia Mzee Mzobe Kisha alizama ndani akimuita Minnie.

Kamanda SU alibaki kutizama tu asielewe kipi kinaendelea pale.

   “” Aaa Kuna utofauti wa Minnie na Mmewe make kama kaja kwa Shari?”

   “”” Aaa Sijajua, Si unamjua Binti yangu alivyo lakini labda wamekwaluzana acha tuwaache.””

“” Aaa Sawa” hata hivyo nahitaji kuondoka kwanza hapa nimekimbia kidogo ofsini.”

Mzee Mzobe ikabidi amtoe nje akimsindikiza huku stori chache zikiendelea.

Huku ndani Minnie ndio anatoka chumbani ni baada ya kusikia sauti ya Alexander.

   “” Mhuu wewe…!? Hapa..? Umefata Nini kwetu?”

Alexander akabaki akimtizama huyu mwanamke anaejiamini mbele yake kwa kumuuliza maswali kama hakumtambua vizuri kwasasa yeye ni Mmewe kiasi kwamba angeenda sehemu yoyote bila ridhaa yake angemzuia au kumfuata. Akafanya kumsogelea Kisha alimshika mkono.

   “” Minnie tafadhari nimekufuafa nikurejeshe white house.”

“” White House..? Jela..? Ile ni nyumba kweli jila linamulika lakini ndani yake haipo vile! Nyumba Haina Uhuru muda wote imejaa Sheria, angalia hapa kwa Mzobe unafanya unachotaka,, nikiamua sahii tu nafanya ninachotaka.”

Alexander akabaki kumshangaa Minnie make muda huo alimpita na kusogea sebuleni, aliangalia kwenye Moja ya drool Kisha alivuta na kuchukua bastola halafu akamtizama Alexander akimwambia amfuate.

Hakuwa na namna zaidi ya kupiga hatua akimfuata mwisho kabisaa Minnie aliingia kwenye chumba kimoja kilichokuwa na Giza totolo zaidi ya mwanga mdogo wa simu ndio ulimulika chumba kile na haikuwa rahisi kuona picha ya chumba hicho. Lakini Minnie alikielewa vizuri kabisa.. Alexander yeye akawa na hofu akitetemeka.

     “” Mhuu vipi Bwana Alexander..! nikufyatue make umekuwa ukiniita Bandit…. Hapa vipi Sasa au niendelee…!!?”

Minnie aliongea akizidi kumfuata Kisha alimuwekea  mtutu wabastola kifuani akifanya kumshika kidevu akimuinua juu.

“”” Vipi nifyatue ama, naona umejileta kwenye himaya yangu,, eti Mwana wa Mfalme White House… Hapa unasemaje..?”

Alexander muda huo mwili umetota jasho anapumulia juu juu huku hasira zikiwaka juu yake anajiuliza huyu Binti ndie wa kumuendesha kweli vile?

   “” Aaa Mini.. Minnie tafadhari usifanye hivyo, Mimi nimekufuata twende nyumbani, kama wewe hautoenda Mimi nitamuoa Maina.”

   “” Ahaa! Kama Mimi sitoenda utamuoa Maina, okay habari njema hii, kwani Kuna ubaya wewe ukimuoa mwanamke umpendae yaani mwanamke wa ndoto zako, isitoshe Maina ni Mapenzi yako ya kwanza. Iweje Sasa wataka kumrudisha bandit girl white house,,, Mimi na wewe tulimaliza habari yetu pale nilipotoka nje ya geti la White House biashara yetu iliisha mbona…!!?”

Huku kwa Mzee Mzobe ndio anarudi ndani baada ya kukumbuka alipishana na Alexander kaingia ndani ikabidi awahi kuingia ndani huku akiita “” Minnie, Miniiiiii…!! Lakini ukimya ulitanda.

   “” Huyu Minnie asije kamfanya mbaya mtoto wa White House nikashidwa kutimiza ndoto zangu.”

Chumbani Minnie alizidi kumsumbua Alexander alihakisha siku hiyo angekoma kwa kumfuata pale.

   “” Minnie tafadhari toa basi siraha yako kifuani,,, inaua hiyo.”

“” Ni sawa nafahamu lakini ndio hii hii ilimwaga damu, tena kwenye mikono ya Uzao wako, Kingine….. Mwana wa Mfalme naona kwenu mmetengeneza ufalme wenu kabisa kwamba mna Mfalme lakini Malkia yupo wapi..? Vipi na wewe prince unajua Malkia alielala kule nyuma alikuwa ndio kila kitu kwangu, vipi wewe Malkia wako atakuwa kalala wapi?”

Aisee Alexander ndo kabisaa hamuelewi kwani hakuwa anajua chochote kuhusu maisha ya Minnie, zaidi alimfahamu ni mwanamke alietafutiwa na Baba’ke na alifaa kumuoa, kuhusu back ground ya huyu mkewe hakuifahamu hata kidogo inakuwaje Leo akutane na maneno yake mazito kwani ni rahisi kumuelewa?.

Mlango uligongwa Minnie akajua kabisa ni Baba’ke yupo pale ikabidi aongee.

   “” Baba Kuna kazi namuelekeza Alexander nakuja sahii tu.”

   “” Wewe fungua Mlango, usifanye kitu kibaya kwenye mikono yako, halafu kumbuka hiyo ni Mali ya serikali ukifanya kitu chochote Baba’ko nitakuwa hatiani.””

 

   “” Baba jamaniii, tangu lini umeacha kuniamini Mimi mwanao…!? Kuwa na Amani kaendelee na kazi zako, au uende kazini tu.”

Mzee Mzobe akahisi kucheka kweli mwanae alimuamlisha aende kazini muda huo na alifaa kumsikiliza kweli? 

Huku kwa Minnie alitoa bastola kifuani kwa Alexander Kisha alipiga sehemu na kumfanya Alexander ashituke, na hapo hapo taa ikawaka kwenye chumba kile, Alexander ndio anashangaa mbona ni chumba kikubwa na kilijaa picha ya Minnie akiwa na familia yake yaani, alionekana ni Mama’ke mzazi, Baba , Nick na Minnie wakipiga picha ya pamoja halafu viwe kwenye chumba Cha Minnie ni rahisi kuchanganyikiwa.

Alexander alibaki kustaajabu huku akipata ujasiri wa kusimama akielekeza macho kwenye Moja ya picha ya Mwanamama mmoja akiwa kavishwa vazi zuri na la thamani, Alexander akawa amesogea na kushika Ile picha.

Upande wa pili kipindi Alexander anasogea kushika Ile picha , White House nae alikuwa akiitizama picha Ile Ile Kisha alifanya kuipapasa akionesha kuumia sana kwa kuitizama picha hiii aliishia kuzungumza nayo.

   “” Pumnzika salama huko uliko, Dua yangu siku zote nitakuwa nikikukumbuka daima.”

Baada ya kumaliza kuongea maneno Yale aliirudisha picha Ile mezani akifanya kuifunika isionekane lakini kumbe aliifunika nusu yake baada ya kusikia kishindo Cha miguu ni kama Kuna mtu alikuja katika chumba hicho.

Muda huo huo Mr Gelu akafika akitoa maelekezo.

“” Alexander yupo kwa Mr Mzobe, Nahisi kaenda kumrejesha Minnie.”

“” Sawa. Hebu ingia kwanza tukae.””

Mr Gelu akaingia lakini muonekano wa White House ulimchanganya sana, akawa katazama mezani ndipo akaona Kuna picha ilifunikwa kitambaa lakini ilikuwa ikionekana kwa mbali ikabidi amuulize.

“” Leo umekuwa hivi kwasababu ya huyu mwanamke, kwanini umeshidwa kumsahau…!?””

“” Nahisi nilimpenda sana, aliondoka nikiwa Bado namhitaji lakini ndio hivyo tenaa, tayari hayupo. Lakini nashangaa kwanini Alexander anashidwa kukaa karibu na mkewake.

Mr Gelu akazidi kumtizama Kuna kitu aligundua huenda White House alitamani sana kumuona kijana wake anakuwa na Minnie akaamua kupotezea Maada ile.

   “” Boss leo nilienda kuangaza mradi wetu wa madini naona unaendelea vizuri nilikuja kukupatia taarifa hii mapema kama itawezekana basi tuongeze vijana tenaa.””

   “” Sawa nitakujulisha, Kesho itabidi uandae mazingira ya kumpokea kijana wangu , lakini pia Sandra nae kanitumia ujumbe baada ya kusikia Kaka’ke anakuja nae atafika pia.””

“” Sawa, nitatekeleza pia.”

Huku kwa Alexander alifanikiwa kuishika Ile picha huku akitetemeka kwa woga kabisa, Minnie yeye alikaa kitandani kwanza huku akimtizama tu.

Baadae Alexander akatoa Ile picha ukutani akirudi nayo mpaka kitandani kwa Minnie akafanya kukaa.

   “” Mi mi Minnie… ..!! Wewe unamfahamu huyu..!?”

Minnie akabaki kukaza sura asimjibu baadae alisimama na kumpatia mgongo alijiuliza swali la Alexander alifaa kulijibu hapana au ndio? Ikabidi amgeukie akimtizama.

   “” Wewe pia unamfahamu huyu…!!?”

   “” Kama niliwahi ona picha yake nyumbani, kwani uliichukua…!!?”

Minnie ndio akatulia Kuna kitu alikipata hii ikamfahamisha kama picha hii ipo nyumbani kwa white house huenda akifatilia ndio atapata ushahidi kamili wa kumfunga white house, swali linakuja atapataje huo ushahidi wakati amekataa kurudi kwa white house na kamuahidi Alexander hatoongozana nae tena?”

Huku sebuleni kwa Mzee Mzobe nae alikuwa Bado anamawazo sana alichukua picha ya Mama’ke Minnie akizidi kuitizama kwa makini Kisha aliongea peke yake.

   “” Nick na Minnie hawapaswi kufahamu kuwa Mama Yao aliwahi kuwa mke wa Mr Denishoo, wanachotakiwa kufahamu wao ni alikuwa akifanya kazi kwa Mr Denishoo basiii.”

Nini Kitaendelea?  Vipi kuhusu kaka yake Minnie atalipaje Kisasi? Na vipi Minnie ambaye tayari kamkumbuka mama yake Kisasi chake kitakuaje? Usikose SEHEMU YA KUMI NA MOJA YA KISASI CHANGU

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

 

6 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version