Ilipoishia Asubuhi Alexander ndio alikuwa wakwanza kuamka kwani baridi la chini lilimuelemea alihisi ni kama yupo ndani ya freezer, aliamka anashangaa kwa pembeni yake juu ya sofa alilala Minnie, alitizama vizuri shuka alizokuwa Nazo chini zilikuwa kitandani inamaana Minnie alimpatia? akaona ni sawa tu ilibidi achukue zile shuka na kuzikunja tayari kwa kufuliwa Kisha alitoa shuka kabatini akatandika vizuri kitanda badae akaingia kuoga.

Wakati anaendelea kuoga aliona ndoo imefunikwa ikabidi afungue anashangaa kukuta nguo za Minnie zikiwa zimeloweka, alinyanyua nguo Moja juu aikague vizuri si ndo anaona ni zile za ubandit, hapo akahisi kuchoka huku akipiga taswira ya kukuta viatu vya Minii vinae tope inamaana ni kweli alitoka na kipi alienda kukitafuta Nje..!!? 

Endelea 
SEHEMU YA TISA

Muda huo huo akaoga haraka na kubadilisha nguo Kisha akakinga maji kwenye ndoo akitoka nayo mpaka alipolala Minnie alifanya kumumwagia kichwani, Minnie akaamka kwa pupa akipiga kelele lakini Alexander ndio akazidi kumumwagia, Minnie alibaki kujikunja kwenye kochi huku akifunika uso wake kwa vitanga vya mikono yake akitia huruma sana.

Alexander hakuchoka kumsumbua alimshika na kumvuta akawa ameanguka mpaka chini, Akijitahidi kuinuka lakini kwa bahati mbaya aliteleza na kwenda kuiangukia Ile ndoo usoni, alilalamika kwa kuugumia maumivu huku akishika mkono wake kwenye paji la uso na kutoka na damu, aliitizama Ile mikono ilivyokuwa imetapakaa damu kitu kilichofuata ni kulia tu haamini ni kweli alimkosea namna hio Hadi aadhibiwe adhabu Kali namna Ile.?

Alexander alimsogelea karibu Kisha akapiga Makoti akimtizama usoni hutaamini aliaachia kicheko huku akiendelea kuzungumza.

    “” Naona ulitaka uone mkono wa pili wa Alexander huwa umebeba nini, Bado hatujamaliza nambie kule nje ulifata Nini?”

Minnie muda huo alikuwa akitetemeka tu, aliona ni bora kuomba msamaha.

   “” Alexander Naomba unisamehe, kule nje Mimi nilienda kuzunguka tu! Hakuna nilichofuata.”

    “” Mhuuu unani spy Mimi…!? Minnie Mimi ni mpole lakini na roho chafu! Kazi ulioianzisha naona tamati ndio nitafika Mimi, kingine sitaki nione umetoka humu ndani na olewako utoe taarifa ya kile kilichotokea humu.””

Alexander alifanya kuondoka huku akiipiga ndoo kwa hasira akimsukumiza kichwani. Alitoka mpaka nje angalau akapunge upepo.

Minnie ndani ndipo alijikongoja aliinuka taratibu huku mwili wake ukitetemeka kwa baridi alifanya kusogea karibu kunako kioo Kisha alitazama sura yake kwenye kioo, alifanya kufuta machozi kwanza Kisha aligeuka na kutizama maji yalivyojaa kwenye chumba hakuwa na namna nyingine alichukua Moja ya nguo yake kisha alianza kudeki maji yote huku akilifuta sofa lililolowa chepe chepe angalau kuzuia machi yasiendelee kuchurizika, akawa kamaliza Kisha alichukua mashuka na kuingia nayo bafuni alifanya kuyafua na kuyaanika bafuni kwa kuyarundika, baada ya kumaliza aliamua pia kujimwangia mwili Kisha alichukua mashine ya kukaushia nywele zake alianza kuzikausha taratibu baada ya kuona zimekauka alizipaka mafuta mazuri Kisha alivaa suruali ya jinsi akitupia na tsheti nyeusi akawa amekaa kwenye kioo akitizama mchubuko katika paji lake la uso ulionekana kuwa kama nundu.

Huku kwa Alexander alikuwa kakaa bustanini akizidi kufikilia kwa kitendo alichokifanya chumbani anaona ni kama hasira zake zilizidi kiwango. Wakati amekaa pale Bright alifika akiwa kavalia nguo zake za kazi, akamsemesha.

   “” Hey! mbona Asubuhi Asubuhi upo hapa na hiki kibaridi hiki unakuwa kama hujaoa…?”

   “” Aaa Kaka, Niache bhana Asubuhi Asubuhi ushaanza maneno, nimeamua tu.”

   “” Mhuu kuamua gani huko, bilashaka wewe na mwenzako hampo sawa.?”

Alexander ikabidi ainuke kwanza ni kama alizidi kumchanganya tu, muda huo huo Simu yake iliita alikuwa ni Maina.

   “” Hello Baby, Nimekumisi kweli! Unajua jana mwenzio uliniacha nyang’anyang’a , Nimechoka kweli anii.”

Alexander kabla hajajibu alimtizama kwanza Bright ajue ni kama anaondoka au ataendelea kumkela hapo.

   “” Samahani nitakutafuta baadae.” Alexander ikabidi akate simu huku akimsogelea Bright.

   “” Kaka mbona umesimama tu.”

   “‘ nakuitazama wewe unavyohandle mahusiano mawili, Daah! Sijui unawa- menage vipi tu, lakini Minnie hana shida yule na ni mrembo kuliko hata huyo Maina.”

Bright alimaliza kuongea huku akimuacha pale. Alexander ikabidi apandishe juu kwanza Ile anafika juu anamuona Bibi yake ni kama anaelekea kwenye chumba chake ikabidi amuwahi.

“” Bibi,. Asubuhi hii ushaamka!! Njoo basi Kuna kitu nilitaka nikufundishe.””

“” Aaa mjukuu na wewe Asubuhi hii ushaamka, sisi kipindi hicho tungekuwa tumelala mpaka Sasa, kumbuka hii ndio wiki yenu ya mwisho mmalize fungate, Aya nenda kwa mwenzako haraka.””

“” Aaa,,, Bibi lakini njoo kwanza huku.”

Bibi ikabidi amfuate wakawa wameshuka mpaka chini walielekea kwenye chumba kikubwa kilionekana kuwa na vitu vingi vya mazoezi.

“” Aaa Bibi nilitaka Leo ufanye zoezi Moja, ni muda mrefu sana haufanyi mazoezi ndio maana nilikuwa nikikusubili utokeze tu nikudake tufanye mazoezi.”

“” Mazoezi Gani na wewe huoni huu uzee wangu Mimi Siwezi.”

Alexander alimtizama Bibi Kisha akaenda kusimama nyuma yake.

    “” Aaa usije kusema wataka nikubebe, make wewe unapenda sana kudekezwa.”

    “” Sio hivyo Bibi, nilitaka nikufanyie massage ya shingo yako, Aya kakamaza shingo kwanza, twende kushoto, kulia, geuka, nitazame vizuri.. ooh hapo sawa Hebu endelea kufanya mwenyewe kwanza.”

Alexander ikabidi akae kwenye Moja ya viti vilivyopatikana katika chumba hicho.

   “” Sasa mbona wewe hufanyi mazoezi unanitazama tu..!!?””

    “” Ooh Bibi nafanya bhana.”

Ikabidi Alexander alazimike kufanya mazoezi Ili aende nae Bibi sambamba. Baadae walimaliza mazoezi Bibi akatoka hapo akiwa kachoka kweli alitembea huku akilalamika njia nzima.

   “” Angalia Sasa,… Mgongo unauma.,, Sasa haya ndo mazoezi gani ya kuanza kuumwa tenaa…!?”” 

Alexander yeye alifanya kucheka tu huku akimsindikiza Bibi katika chumba chake.

Huku kwa Minnie baada ya kuchoka kutizama jeraha lake ilibidi ajilaze kitandani huku akiendelea kuchati na Baba’ke kwa kitendo kile kilimuuma sana mpaka akaamua kumwambia Baba’ke, Baba nae alimweleza mambo mengi na mwisho kabisa alimwambia hivi karibuni Nick alimpigia simu, ikabidi amtumie namba wazungumze nae.

Minnie Baada ya kuipata namba aliisev kwanza aone kama ipo Whatsup, kitu aluchowaza ni yeye kuongea na Kaka’ke kwa njia ya Whatsup.

Alifanya kumpigia simu Kaka’ke Whatsup akashangaa inaita ndio akakumbuka kama atapokea simu ni dhahili angeona ngeu kwenye paji lake la uso alichoamua alichukua tango lilokuwa mezani alifanya kulikata  akachukua kipande na kuweka kwenye ngeu.

“” Hapa sawa hakuna shida nitaongea nae vizuri.”

Muda huo kwa Nick akaona namba ngeni imempigia akafanya kuipuuza na kupasi nguo yake, Eliud akawa amefika akaiona Ile simu ikabidi amshitue.

   “” Oyaa simu yako inaita sana, pokea huenda Dili.”

   “” Sijui nani anasumbua Asubuhi Asubuhi, hebu pokea.”

Eliud ikabidi apokee Ile anatizama camera alihisi kutetemeka kwanza asiamini ikabidi asogee kwa Nick.

   “” Si si… Minnie huyu…!?”

Tobaa!! Nick alihisi kutupa Pasi, Eliud akawahi kuishika akizima swetch Kisha wakakusanyana kuangalia Camera wote.

Huku kwa Minnie alikuwa katoa macho akimtizama Kaka’ke muda wote haamini kabisa baadae alimuita.

   “” Kaka Nick,, ni wewe kweli inamaana sahii mwanajeshi..!!?”

Nick yeye Bado kaduwaa tu ni anamshangaa, Eliud ikabidi amkoe kwanza, Alexander ndio akachukua simu nakusogea kwenye kitanda chake akakaa ndipo akafunguka kuzungumza.

“” Minnie ni wewe kweli, Nimekumisi mdogo wangu, Ulienda wapi siku hiyo? Kwanini Sasa hikuniaga?””

Eliud ikabidi amnyang’anye simu make ni kama anauliza maswali ambayo majibu yangekuwa marefu sana kabla wasalimiane kwanza ashaanza maswali. Ikabidi yeye ndio azungumze.

   “” Minnie za siku jamaniii,, upo salama lakini tulikumisi sana, Baba yupo wapi..!!?”

Nick akaona ni kama anambania kuzungumza nae ikabidi achukue simu na kutoka nje huku akiwa anaruka ruka kama kashikwa wazimu.

   “” Minnie Mdogo wangu hivi ni mzima lakini!!? Nilifikilia kuhusu nyie, Juzi niliongea na Baba anasema mzima, halafu mbona kachumbali usoni?””

Minnie ndio akacheka hivi kweli alikuwa kachumbali? 

   “” Hapana Kaka, ni namna ya kuweka uso wangu uzidi kuvutia! “”

   “” Sawa Cha urembo wangu, Baba yupo wapi..!!?””

Kabla Minnie hajajibu Mlango ukabishwa akajua tayari Cha ukorofi kaja na jipya, ikabidi aangalie camera ya simu yake kwanza.

“” Kaka sevu namba yangu hiyo, tutaongea baadae ila nimefurahi sana kukuona! Ingia kazini namimi najiandaa sahii niingie kazini nikitoka tuwasiliane.”” 

Minnie akawa amekata simu lakini Kila mtu alionekana kulizika furaha pekee ndio ilijaa kwenye nyoyo zao.

Ikabidi ainuke na kwenda kufungua Mlango make alifunga kwa funguo, anafungua hivi ndio anamuona ni Alexander kabebelea sahani yenye kifungua kinywa alimfungulia na kubaki kumtizama tu huku akimfuata nyuma Kisha akampita na kwenda kukaa kitandani.

Alexander alibaki kutazama mazingira ya chumbani akawa kama haelewi hivi, make tayari maji yalikaushwa akamtizama Minnie tayari alikuwa kaweka Kipande Cha tango kwenye paji la uso akilala kitandani Chali tenaa muda huo alikuwa akichati mtandaoni akicheka kwa furaha, Alizidi kumtizama akaamua kukaa kwanza aachane na huyo mwendawazimu angalau apate kifungua kinywa Ile kukaa tu alipiga kelele… “”” Ayaaaaah..!!! Majiiii…!!?”

Minnie ndio akashituka akafanya kuinuka ndio anamuona suruali ililowa nyuma chepelee mbona alihisi kucheka na sio taratibu ila ni kwa nguvu. Alexander ikabidi ageuke ndio anamuona Minnie yupo Cheka Cheka akapaniki na kuchukua nguo Kisha aliingia bafuni kubadilisha Kisha akawa ametoka nje na kuwaita watumishi watoe lile sofa nje walianike.

Muda huo Minnie anamtizama tu vile anavyojizungusha ni kama anatafuta sehemu ya kukaa mwisho kabisa aliamua kuvuta meza akiisogeza kitandani huenda kitanda pekee ndio kilifaa kuwa kiti Cha kukalia.

    “” Mhuu kwahiyo unacheka Nini….!!?”

Minnie akafanya kutoa kipande Cha tango, Alexander ndio akapata kumtizama kumbe aliumia na sio alifanya massage ya uso wake. Ikabidi atulie tu amtizame kipi atazungumza lakini Minnie alichukua chai kwenye chupa na kumimina Kisha alianza kunywa, Alexander akamtizama tenaa huenda alihisi Minnie angezila kula lakini wapi, baada Minnie aliamua kujibu swali lake alimuuliza.

    ” Bilashaka wewe na Buibui ni mtu na pacha wake yaani mtengo unaoutengeneza wewe ndio unaokunasa.”

Alexander ikabidi amtizame kwanza ni alimaanisha Nini katika maneno yake.

  “” Mhuu bilashaka ni mwanafalsafa humu ndani, lakini kuwa makini na Hilo fumbo make muda si mrefu utalifumbua.””

Minnie hakutaka kujibu swali lile zaidi ya kuendelea kunywa chai ni kama hamsikilizi tenaa.

Muda huo Alexander akapokea simu ni Maina alimpigia tenaa ikabidi apokee huku akimtizama Minnie kwanza Kisha aliendelea kuzungumza baada ya kusikiliza maongezi upande wa pili.

   “” Haikuwa hivyo ila Bibi alinipatia kazi ya kufanya, si unamjua kabisa ukikataa hapo hapo presha yake inapanda. Hata hivyo niliwaza kukutafuta muda si mrefu.”

“” Sawa, basi ingia online nakupigia mara moja.”

“” Sawa…”

Maina akawa amepiga simu Ile kupokea tu alianza kuangaza mazingira ya mle ndani ndipo anabahatika kumuona Minnie akivuta chupa ya chai, ugomvi ukawa umeanzia hapo.

“” Alexander kwanini lakini umekuwa ukiniongopea hauishi chumba kimoja na Minnie na huyo pembeni yako nani?””

Alexander ikabidi amtizame kwanza Minnie ambae anaonesha kutokujali kabisa swala Hilo.

   “” Okay Baby, Minnie kaja mara moja huku chumbani kwangu na sio tunashea chumba.””

Minnie akabaki kumtizama tu Kisha akatabasamu tu, aliuona kabisa uongo wa Alexander peupe.

“” Si hamshei sawa nitaona.””

Muda huo huku nje kulisikika kelele ya mama Mirii na Bibi wakizungumza kwa sauti.

“” Bibi mzuie huyoo asiingie.” Alikuwa ni Mama Miricka.

“”” Wewe Maina unafanya nini hapa hiruhusiwi kuingia huko.” Bibi akazidi kuzuia hutaamini ni Maina alikuwa kafika pale na muda anaongea na Alexander alikuwa getini.

Huku chumbani Mlango ukafunguliwa kwa nguvu, Maina ndo anatoa macho ni mbele mbele yao tena wamekaa kitandani wakinywa chai kwa pamoja, alifika akasukuma kikombe Cha chai kwa bahati mbaya kikamumwagikia Minnie mkononi akawa kaungua japo kwa muda huo hakuna alieona.

   ”” Alexander Nini hiki unafanya sahii tu umesahau Mapenzi yangu yote niliyojitoa kwako nikikuoneshea unadiliki kunisaliti na mwanamke mwingine? ” ziko wapi ahadi zetu tulizoahidiana Leo ndio unazipoteza namna hii kweli…!!? Na vipi kuhusu hisia zangu… Upendo wangu Mimi kwako si kitu tenaa? Kwanini Sasa ulisema unanipenda..!?” 

Maina akazidi kulalamika, lakini Bibi na Mama Miricka wakafika na kuingia chumbani.

“” Maina nakuomba tafadhari usimvunjie mji mjukuu wangu, nakuomba urudi kwenu haraka.

Bibi aliongea kwa msisitizo.

“” Siwezi kurudi Bibi, tenaa kuanzia Leo nitakaa hapa, na nitakuwa natumia hiki hikichumba si kasema hakai na mtu humu?.”

Mama Miricka ikabidi amfuate na yeye azungumze nae.

“” Wifi jamaniii kuwa muelewa basi Alexander kashaoa na huyu ni mke wake hivi vituko unavyovifanya vinamuumiza mwenzio.””

Maina alikuwa hasikiki muda huo alisogea kwenye kabati akapakua nguo zote za Minnie akishusha chini akizidi kugomba.

“” Lazima uondoke humu ndani hauwezi ukawa chanzo Cha kuninyima furaha, kwani huko nje hukuona wanaume wengine hata awe Alexander tu?.””

Minnie kwa kitendo kile Cha kuona nguo zake zinazidi kutupwa ovyo hapo ustahimilivu ulimshinda aliinuka huku akishika mkono wake na kuungalia kwanza kwa maumivu aliyoyasikia make ulikuwa unauma na kuvuta. Alijikaza na kuanza kuokota Moja ya nguo Kisha akaweka kwenye begi akifanya kuzikunja vizuri, ilibidi wote wabaki kumtizama Minnie huenda hawakumuelewa vizuri akili yake na leo ndio watamuelewa make naona tayari washamvuruga.

Alichofanya baada ya kumaliza kukunja alichukua begi lake akivuruta na kuondoka kimya kimya huku wakizidi kumuita asiondoke lakini ndio alizamilia hivyo, kwanini apate mateso kwenye nyumba Ile kisa ni kisasi tu wakati anaweza fanya mambo yake kwa utulivu mkubwa akiwa nje Ili akili yake ipate kufafanua vizuri kazi ya kufanya.

Alizidi kusogea akiliacha jumba la White House huku akisogea getini, Ile anafika karibu Mlinzi mmoja akapokea simu na kusogea pembeni azungumze Kisha alirudi na majibu ya Minnie asitoke nje ya geti.

   “” Kaka fungua basi Mlango, Nachelewa tafadhari.”

   “” Samahani madam, Bosi kasema geti lisifunguliwe na hauruhusiwi kutoka humu.”

Minnie ikabidi aanze kuleta vurugu lakini muda huo Familia ya White House walisogea karibu kushuhudia tamasha lililokuwa likiendelea pale, Minnie alikuwa hashikiki mwisho kabisa alimsogelea Mlinzi mmoja aliekuwa kachomeka bastola kiunoni aliinyakua na kuwanyoshea wasimsogelee lasi hivyo atajifyatua.

Huku kwa Alexander alishidwa kujizuia yote ya yote kutokea yule kwasasa alikuwa ni mwanamke wake tu, Kuna kitu Mungu huwa anaunganisha hasa mnapokuwa mnaapa viapo vya kuwa mwili mmoja Mungu nae huwabariki Ili muishi pamoja kama alivyowaunganisha. Ilibidi asogee kumzuia.

    “” Minnie tafadhari usifanye hivyo! Usiondoke kwenye jengo hili tafadhari. Basi Leo nisikilize kama mmeo tu.”

Wote wakabaki kushangaa inamaana alimhitaji asiondoke kweli? Maina kauli Ile ikamvunja moyo kwakuwa kazamilia kuwa na Alexander ikabidi asogee huenda uwepo wake ungemkumbusha anafaa kuwa na yeye endapo Minnie angeondoka.

Minnie ndio akapata hasira akaona wasinichezee make hawa ndio wameleta kizaazaa ndani ikabidi amnyoshee bastola Alexander Ili Maina amkinge vizuri.

    “” Tenaa kama wewe ndo nitakufa kabisa unisahau si umekuwa ukiniita Bandit unanichukia?, Labda nikwambie huenda ikawa kweli.. unaona hapa nilipofikia ndio ubandit wenyewe unaanzia hapa, halafu nakuomba fata maisha yako kingine… Kuanzia leo Mimi na wewe ndoa basi tena, Ndoa gani humwamini mkeo. !?.””

Alifanya kuvua Ile cheni ya Ndoa yenye Utambulisho wa White House kisha akavua na Ile Pete akafanya kumrushia baadae ndio akatoka nje ya geti Kisha Ile bastola akamrushia Mlinzi akitoka nje ya geti kabisa.

Wakati huo tukio lote linaendelea White House alikuwa akilishuhudia vizuri kwenye laptop yake, baada ya Minnie kuondoka tu alifanya kufunika laptop huku akipiga makofi na kusimama Kisha aliongea “” The game is over.” Muda huo Mr Gelu alikuwa akimtizama tu make na yeye alikuwa ni chawa wa white house.

   “” Kwahiyo tumrudishe..!?”

   “” Hapana mwache aende, huenda hii situation ya Minnie kuondoka itamfanya kijana wangu akae sawa, waache wakae na huyo mwanamke nawapa muda tu lazima atamrejesha Minnie ,, ila acha sisi game letu liendelee vizuri kwa Mzee Mzobe.”

Ilibidi wakae kikao kati ya Mr White House pamoja na Mr Gelu wajadili kitu kinachofuata baada ya hapo.

Huku upande wa pili walibaki wameduwaa tu huku wasiamini kama Minnie ndio aliondoka hivyo, kwa Bibi ndio alikuwa akiumia zaidi kwani alianza kumkubali Minnie kuwa ndie mkwe katika nyumba hiyo. Hakuwa na namna zaidi ya kusambaa kurudi ndani wakawa wamebakia wawili tu ni Maina na Alexander.

Alexander alibaki kuitizama Ile cheni pamoja na Pete ikawa inamkumbusha matukio mengi ya Minnie lakini akaona ni bora kupotezea hata hivyo mwanamke huyo kwake alimfanya aongee maneno mengi kwa siku nzima hakuisha kumkela hata kwa tabia zake zisizo eleweka kabisa.

Maina ikabidi amsogelee Kisha alimshika mkono huku akimkokota Hadi ndani, baada ya kufika chumbani alikuwa bado hajielewi mpaka akawa wakukalishwa kitandani.

   “” Kunywa maji angalau akili yako itulie,, mwache aende tuanze maisha yetu mapya.””

Maina aliongea huku akimnywesha maji.

Muda huo huo Mlinzi akafika akigonga Mlango.

   “” Samahani Bwana Alexander! Baba’ko anakuhitaji huko juu upandishe.””

Tobaa!!! Alexander akahisi joto kuongezeka na kujiona mjinga inamaana alishidwa kweli kujiongeza kumzuia Minnie asiondoke wakati ndoa yake ilipitishwa na White House kwa matakwa yake na yeye akaikubali na vipi Leo…!? “” Na kingine alijisahau kuwa Sheria za White House ni kama moto wa tanuru ukichochewa hata kwa mvua hautazima  iweje kwakwe Bwana mdogo mdogo Alexander ambae ndio kaingia kwenye hii Ndoa hata wiki hajamaliza eti mwanamke anarudi kwao kwa kuendekeza penzi lake la kwanza ni yupo sahihi  kweli..?”

Nini Kitaendelea?  Vipi kuhusu kaka yake Minnie atalipaje Kisasi? Na vipi Minnie ambaye tayari kamkumbuka mama yake Kisasi chake kitakuaje? Usikose SEHEMU YA SABA

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

12 Comments

  1. Well done… lakini kuna vitu unamiss kama(Nini Kitaendelea? Vipi kuhusu kaka yake Minnie atalipaje Kisasi? Na vipi Minnie ambaye tayari kamkumbuka mama yake Kisasi chake kitakuaje? Usikose SEHEMU YA SABA

Leave A Reply


Exit mobile version