IlipoishiaAlexander akaamua kumuacha Kisha alisogea kwenye stendi ya viatu akanyanyua kiatu kimoja akimtizama Minii.

   “” Na Leo tenaa umeenda kinyume na mimi,,, Okay jiandae tushuke chini,, Usiku utakuwa ni mzuri kwetu kujadili Maada hii.”

Endelea 

SEHEMU YA NANE 

Huku upande wa Nick walifanikiwa kupanda mlimani walifika mpaka eneo la juu kabisa walianza kuangaza mazingira mwisho kabisa Amri alimuomba amfuate.

“” Eneo hili hili ndio hupendelea kukaa, tufanye kushuka.”

Nick ikabidi afuate maelekezo ya Amri walifika kwenye kichaka kimoja kilichoonekana kama hema ikabidi watafute upenyo waingie, Ile wamefika walishangaa kuona chupa za bia pamoja na punje za sigara zimeachwa mle kwa kuangalia tu Yale mazingira yalioneshwa ni kama siku kadhaa watu walioishi pale Wana muda hawapo.

   “Nahisi walihama Kambi, kesho itabidi tuchukue kikosi tuzungukie msitu huu, huenda majambazi wengi wamekuwa wakiishi humu, kama tutawapata itakuwa rahisi kugundua Minnie yupo wapi?”

Amri aliongea lakini kwa Nick mawazo yake yalikuwa tofauti kabisa kitu alichofikilia ni kujua Minii anaishije muda huo.

         °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°

Huku kwa Minii alikuwa tayari kajiandaa Vizuri akishuka chini kama maelekezo ya Alexander yalivyo muelekeza, Ile anazidi kushuka Mama Mirii alimuita ni kama alikuwa akimsubili.

   “” Ooh Minnie waooo! You’re so beautiful… Nilikuwa nikikusubili tushuke wote, Alexander aliniachia maelekezo nikufuate.””

   “” Sawa Nashukuru sana! Hivi Binti yako anaitwa Mirii…!!?” Aliuiza Minii

   “” Yaaah ni Mirii, japo wanafupisha tu yeye anaitwa Miricka.” Akajibu Mama Mirii

   “” Sawa, siku Ile walikuwa wakiitana Mirii na Baba’ke mdogo nikafikilia ni Mimi, halafu shemeji yangu na yeye yupo chini unajua sijawahi muona.” Aliongezea Mirii

   “” Yeye hayupo na sisi..””

Minnie akatulia kwanza akimtizama Mama Miricka ni kama hakumuelewa vizuri ikabidi amuulize tena.

   “” Unamaanisha Nini kuwa yeye hayupo..!?” Alidakia Minii

Kabla Mama Mirii hajajibu Kuna mtumishi alifika pale.

   “” Madam! Mnasubiliwa chini.”

Ikabidi stori Yao iishie hapo, walizidi kusonga mbele kwa lile jumba ilikuwa ni kama Dakika nane au kumi kufika.

 

Miniii muda wote hakuisha kuangaza Kona zote akikagua jumba lile kwa makini, kwa mbali sauti ya mziki ilisikika Minii akawa ametulia kwanza akiamini huenda wanakoelekea kutakuwa Kuna sherehe.

   “” Hivi Bibi anakuwa kwenye chumba chake…!?” Aliuliza Minii

Mama Miricka ikabidi acheke tu, ilionesha Minii kutokuelewa ratiba za ” white house”.

    “” Leo weekend watu wa House white hufanya sherehe siku ya jumamosi na Jumapili ndio maana Leo ulitakiwa ufike wakakutambue pia.”” 

Minii ikabidi atulie tu akili yake inaona ni kama itauliza maswali mengi huenda mama Miricka angemuona wa tofauti.

Hatimae wakafika mpaka kunako party wanafamilia wa white house walikuwa wakijiachia kucheza mziki wa taratibu huku wengine wakiendelea kupata vinywaji, Minii baada ya kufika pale aliduwaa kwanza kwani alikua anashangaa ni wapi ataenda kukaa, kwa mbali kidogo ndio akamuona Alexander akiwa kapendeza kabisa na muda huo alivalia suruali nyeusi huku akitupia shati nyeupe ya mikono mirefu na neckties nyekundu ilimfanya apendeze zaidi, Miniii alitumia muda mwingi kumtizama lakini akili yake inawaza msala wa Asubuhi kiatu chake kuonekana kinatope labda atamueleza Nini wakati huo?

Alexander akawa amemuona akaamua kumfuata na kusema   “Naona huna Amani kwa makosa uliyoyafanya, okay… Ongozana nami.”

Minnie akafanya kumfuata nyuma nyuma Hadi kwenye meza aliyoenda kukaa, ilikuwa ni meza ya watu wakubwa bila shaka Minii ndio alihitajika kwenye meza hii kwa Utambulisho.

Alexander alipofika alienda kukaa karibu na Bibi yake akifanya kumuinamia.

   “” Bibi mjukuu wako huyu hapa.”

   “” Sasa mbona hujampatia kiti, unataka Mimi nisimame. Mjukuu wangu hebu njoo hapa.” akauliza Bibi 

Minii ikabidi asogee japo ni kwa uoga sana kumbuka muda wote haachi kumtizama Alexander akihisi kamchomesha. Alexander nae hakuacha kumuangazia macho tayari ashamshuku kabisa akafanya kumuachia kiti Kisha akasimama nyuma yake.

“”” Aaa Bibi, Shikamoo..!!’ Minnie akajibaraguza akisalimia huku mikono yake ikiweka sawa gauni yake shingoni ni kama anahisi Alexander akimuangalia muda wote.

“” Ooh! Marhaba mjukuu wangu, ila umependeza sana na unaendana na Alexander kweli, hakika umechagua Mume sahihi.”

Minnie ikabidi amtizame Alexander kwani muda huo tayari alishakaa mbele yake, walibaki kutazamana kwanza huku Kila mtu akimjaji kivyake.

Muda kidogo mtumishi alileta vinywaji pale akafanya kuwamiminia, lakini Minnie alibaki kashikilia Glass kwa muda huku akiwatizama wanaokunywa katika meza Ile, alimtizama Bibi ambae alikunywa juice ikabidi amsogelee karibu akimnong’oneza.

   “” Bibi Mimi nataka kinywaji kama chako.”

Alexander akawa amesikia akamkazia macho kwanza .

  “” Haina kileo wewe kunywa tu.”

Miniii akabaki kumtizama Bibi huenda huyu ndie angekuwa na majibu ya mwisho.

   “” Hapana hii ni whynne kunywa tu.”

Alexander ikabidi aondoke na kwenda kukaa sehemu nyingine iliyokuwa na vinywaji vingi, Minii akawa akimwangaza tu aliona kabisa kwenye Ile meza watu walionekana kulewa kuashilia vinywaji walivyokuwa wakitumia vina kilevi, lakini akaamua kuachana nae akijali mambo yake wakati huo akijiweka busy na Bibi.

Muda kidogo Kuna wageni waliingia pale alikuwa ni Dada mmoja akiwa kaambatana na kaka mmoja wakiwa wameshikana mikono, Dada huyu alionekana kupendeza sana kwani mavazi yake aliyovaa yalionekana ni yenye gharama kubwa sana, Baada ya kufika walifanya kuachana pale huku kijana yule alienda kukaa na vijana wenzake.

Bibi baada ya kumuona Dada yule alionesha kutokupenda ujio wake ikabidi amtizame Minnie akiongea nae.

 Bibi akasema  “Macho yako yamtizame mumeo, Kaa nae karibu.”

 Minnie akajibu  “” Aaa Bibi Mimi mtu anaetumia kileo wapi na wapi, akae tu huko.”

Muda huo huo Dada aliengia alifika sehemu waliyokaa akafanya kumkumbatia Bibi huku akiongea nae.

   “” Waoo Bibi, Nilikumisi sana,,, Alexander wapi..?”

“” Alikuwa hapo na wenzake sijui kaenda wapi..!!?” Bibi akajibu

Dada yule alimtizama kwanza Minii ni kama sura yake sio ngeni kwake, alimsemesha..

   “” Mrs Alexander how are you..!!?”

Miniii alimtizama tu hakumuelewa vizuri make ni kama aliongea kwa Shari alimjibu… “” Fine.” Kisha Dada yule aliondoka…

“” Mainah…!!! Bibi alimuita kwa utambulisho wa majina yake, Maina akawa amegeuka.

“” Alexander kwasasa ni Mume wa mtu hupaswi kuandamana nae muda wote.”

“” Lakini ananipenda Mimi.”

Minii akabaki kucheka ndio akakumbuka kumbe mwanamke aliemtambulisha kwa sentensi ndefu majuzi kati… kumbe alikuwa Maina inamaana ni girlfriend wake, alihisi kuenjoy tu.

Maina akawa ameondoka na kwenda kumtafuta Alexander, Bibi ikabidi amfurumshe Minii akamtafute Mmewe. Minnie ikabidi aende shingo upande lakini kulazimishwa kwake na Bibi ni kama alimpiga teke chura aliona muda atakaotumia kumtafuta Alexander ndio muda sahihi wa kutafuta ushahidi wa  White House.

Alipandisha juu akizidi kumuangaza ndipo akawaona wapo chemba wakiwa wamekumbatiana tena wanakiss, Minii akawatizama tu akaona ni kama washezi wa tabia  inamaana walikosa hata haya wakatafuta faragha wakajisitiri, hutaamini Minii aliwaacha pale pale akipandisha mpaka juu! Wakati anashuka Kuna vyumba aliviona akamua aanze kupiga msako.

Katika kutembea kwake aligota kwenye chumba kimoja kilichokuwa ni kama maktaba kwani kilijaa vitabu vingi aliamua kuingia mle na kuanza kukagua mafaili kwa awamu, alijaribu kupiga picha baadhi ya documents ilioashilia kuwa na ushahidi fulani na mwisho kabisa aliona Kuna flash ilichomekwa kwenye computa akafanya kuichomoa na kutoka upesi.

Huku kwa Alexander walikuwa Bado wapo faragha, wakiendelea kuweka ukaribu wa miili yao mwisho kabisa walishidwa kujizuia na kuamua kupandisha Hadi kwenye chumba Cha Alexander Ili kutuliza mihemko ya miili yao.

Kwa Minnie muda huo anatoka katika chumba hicho huku akiwa na flash pamoja na simu yake aliamua kupita katika chumba chake Ili ampatie taarifa njema Baba’ke, alifika na kujaribu kufungua Mlango lakini ulikuwa mgumu na mwisho kabisa akajua kuna mtu ndani ndie alifunga.

Wakati anaendelea kugonga mlango Mama Miricka alifika na kumtoa pale, aliielewa kabisa kinachoendelea pale.

   “” Minnie, Bibi anakuita ni muda mrefu imekuwa.”

Minnie kama machale yalimcheza kwa situation aliyoiona kwa Alexander na Maina akawaza kabisa huenda wapo chumbani wakiburudika pamoja lakini akaamua kufuata maelekezo ya Mama Miricka.

Baada ya kufika Bibi alimuita pembeni Mama Miricka wazungumze.

   “” Minnie nae kashuhudia wapo pamoja? Kwanini lakini mjukuu wangu anakuwa hivi,, huenda hata miili yao na mke wake haifahamiani. Nakupatia kazi fatilia kuhusu shemeji yako ujue kama Ndoa yao wanaitimiza ukipata majibu Niambie na kama haipo hivyo itabidi huyu Maina tumuweke mbali na Alexander naona akiendelea kuwa karibu Alexander hatajua thamani ya Ndoa yake.”

Minnie yeye muda wote alikuwa na shauku ya kumpigia Baba’ke amwambie kitu alichokiona maktaba ilibidi amtumie zile documents alizotuma Kisha alikaa kwa makini akisubilia majibu.

Bibi akawa akimtizama muda wote hamuelewi ni kama anawasiwasi sana akafikilia ni situation aliyoiona kule huenda imemkosesha raha.

Muda huo Alexander na Maina wakawa wanashuka taratibu wakiwa wameongozana sambamba Minii aliwatizama tu Kisha akapindisha sura yake pembeni kitu ambacho hataki kukisikia ni kero za watu hawa, Mama Miricka ilibidi amfuate Alexander Kisha alimshika mkono akimtoa pembeni.

“” Sio vizuri kabisa kwa kile unachomfanyia mwenzako, Minnie kwasasa ni mkeo, Maina kwako ni X girlfriend jifunze kumove basi.”” 

“” Shemu, huyo mwanamke unaesema ni mkewangu ni sawa lakini moyo wangu Mimi haupo kwake kabisa hata mara Moja sijawi waza kuhusu yeye, kama atakaa kama Utambulisho wa Mrs Alexander sawa lakini sio kwa lidhaa ya moyo wangu, sijui nikwambieje tu unielewe,, yaani hata Ile chembe ya hisia nahisi sinayo kwake.””

Mama Miricka alihisi kuchoka alimtizama kwanza Minnie muda huo alikuwa busy akiangalia watu wanavyocheza, Ghafla Kuna mtu alifika pembeni yake na kumpatia mkono wacheze, Mama Miricka alimtizama vizuri akajua ni Brighton mtoto wa Mdogo wake na white house.

   “” Unaona lakini kule, Bright kamchukua mkeo tayari kwa kucheza nae Halafu wewe unaweka ubusy na Maina Kuna siku utajuta.”” Mama Miricka alifanya kumuonesha lakini Alexander Wala hakujali zaidi ya kupiga hatua akimuacha eneo lile ikabidi na yeye amfuate tu.

Huku Minnie alikuwa akiendelea kucheza na Bright angalau alipata hata muda wa kuburudika, Bright alikuwa akiendelea kumpigisha stori Minnie akawa anacheka tu.

   “” Naona ulikuwa mpweke sana, kwani huyo mumeo Alexander hakutaka kucheza na wewe..!?”

   “” Aaa,,, Kwani nae huwa anacheza? Mimi nikajua hawezi kucheza.”

   “”” Anacheza! Utamuona muda si mrefu akiwa na Bi mkubwa wake.”

   “” Ooh Bi mkubwa,,, Naona nimekuja kuwaingilia ni kweli anampenda sana mpaka hawezi zuia hisia zake akimuona.””

 

Huku kwa Alexander ukaribu huo ulimfanya awe na maswali mengi, kitu anachofikilia ni Minnie alikuwa akifanya ubandit gani pale, Maina nae alimtambua kabisa anamtizama ikabidi amfuate Kisha alimshika mkono akifanya kumuegamia.

   “” Baby I want to dance with you! Please…!! Come on baby.””

Alexander akamtizama jinsi alivyomshika akaona ni nafasi nzuri ya kucheza na Maina kama atasogea karibu yake huenda angesitisha ukaribu unaoendelea.

Minnie alitambua kabisa uwepo wa Alexander na Maina pembeni yao lakini hakutaka kujihusisha kuwatizama zaidi kuendelea kupiga stori na Bright.

Huku kwa Bibi na Mama Miricka walikuwa wakimtizama Alexander anavyojiachia kucheza na Maina hawakupendezewa kabisa na tabia Yao, inamaana Alexander alishidwa kuwa na mipaka kwa mwanamke huyu ilihali anae mwanamke tena hata mwezi mmoja haujaisha kweli alionesha kiburi chake mapema mno.

 

Ndani ya nyumba alionekana White House akiwa juu kabisa ya Ghorofa yake akiwa na Bwana mmoja mtu wa karibu kabisa na miradi yake aitwae Mr Gelu, alikuwa akitizama matukio yanayoendelea chini kupitia laptop yake alifanya kutazama kwa makini baadae alisitopisha na kuzungumza.

   “” Kama Alexander asipofata nyayo zangu ni bora atolewe white house.”

 

White House akazidi kukagua vizuri tukio lile baadae, alibadilisha camera yake iliyokuwa ikinasa kwenye sherehe akirudisha kuangaza vyumba vyote vya Pale ndani ndipo anashangaa kumuona ni Minnie akiingia maktaba, alizidi kumumulika vizuri mpaka anachukua Ile flash na kutoka, akaamua kwanza kusogeza Mvinyo nakuendelea kunywa.

   “” Ooh Vizuri, Sema anajitahidi sana kujificha anasahau jicho langu muda wote linaangaza kila mwanafamilia wa White House, kwahiyo Mzee Mzobe alituigizia? Hakujua Mimi akili yangu iliwaza kuliko yeye..!?”

   “” Tayari kashanasa kwenye mtego wetu! Itakuwa anafatilia kesi ya mauaji ya mkewake lakini kifo Cha Mama Minii ilikuwa ni bahati mbaya.

Mr Gelu aliongea huku akizidi kurudia kukagua Ile video kuhakiki.

“”” Hahaaaa!!! Inatakiwa Mzee Mzobe atoweke kama alivyopotea mkewe, kama tutazidi kumlea-lea huyu atatufikisha pabaya siku Moja.””

Mzee Mzobe akaongea huku mguu wake akiweka juu ya meza akiendelea kuzungumza.

 “” Basi mtizame kwa ukaribu Miniii, na kama itawezekana wiki kesho waanze kwenda kwenye kampuni yao, najua atapata muda wa kujiachia sana nasi tutamkamata mapema.””

“” Sawa, itabidi iwe hivyo. Nitashughulikia.””

Huku masaa yalikuwa yameenda watu walianza kuingia kwenye vyumba vyao, Minnie akawahi kuingia ndani baada ya kuona Alexander yupo busy na mwanamke wake, aliingia ndani alichokuta kilimstaajabisha kwani kitanda chote kilikuwa kimevurugika, aliishia kuitizama Kisha akasogea karibu kunako kabati alichukua shuka na kulala kwenye sofa akimsubili Mwenye kitanda chake aje alale hivo hivo.

Alexander ndio akaingia chumbani anashangaa kumuona Minnie kajikunyata akawa anamfikilia inamaana kwa huu muda tayari usingizi ulimchukua au ni hataki kuulizwa kuhusu Maada ya Asubuhi iliyoishia njiani? Akamsogelea karibu huku sauti yake ikiwa imejaa ulevi.

   “” Mi ..nnie ma my wife..!”

Minnie akawa amesikia vizuri ikabidi ajikaushe kwani muda huo yeye alikuwa ni wife kwa Alexander na wakati muda huo huo alikuwa na Maina angeweza vipi kumsikiliza mwanaume huyu mbele yake teena muda huo alimfanya kuwa mke ni lini labda alimpokea kwenye moyo wake na kumdhibitisha ni mkewe?

Alexander akafanya kumfunua shuka katika uso wake ndio akamuona Minnie kasinzia lakini alifanya kumshika mkono akimuinua.

   “”” Sijasahau bilashaka, amka uniambie Leo Asubuhi kule bustani ulifata Nini…!!?”

Ooh Minnie akaona kumekucha inamaana hakusahau Maada hii richa kunya pombe nyingi ni alikumbuka..? Kwa zile kelele za Alexander ilibidi ainuke na kukaa, Alexander nae akafanya kukaa pembeni yake akimshika begani huku akimtizama usoni.

   “” Kwanini lakini unanifanya nishidwe kufikilia mambo yangu nibaki kukutizama wewe, yaani nijue muda wote umeamka na umeenda wapi, kwanini unanipatia adhabu namna hii? Eti Minnie wewe ni Spy…!!?”

Minnie ikabidi ainuke kwa hasira kwanza, miarufu ya pombe ilijaa kwenye kifua chake akahisi ni kama atatapika muda si mrefu lakini Alexander aliwahi kumshika mkono akimtizama usoni kwa ulevi ni kama anashauku ya kusikia kitu fulani.

   “” Uliongea Nini na Bright Leo..!!?”

“” Maina ndie mwanamke uliempenda, kwanini sasa hukumuoa?”

Minnie nae akaongeza swali hakika pwagu na pwaguzi walikutana.

“” Kwasababu yako Leo hii nimetegwa na mwanamke ninae mpenda, Bright uliimuuliza kitu chochote kuhusu Mimi make huchelewi…?”

Minnie akaona ni kama anataka kumganda sana ikabidi asimame aliwaza kuhamia kitandani lakini akaona ni watu walienjoy pale na tena walichafua mashuka yao kwa furaha zao wenyewe iweje akatandike? Ikabidi amgeukie Alexander.

“” Wewe na huyo Maina Kuna mambo mnafanya kama hakili zenu hazijakamilika, hata kutandika mashuka mlishidwa..!!? Basi njoo uondoe shuka zenu Mimi nataka kulala.”

Huku kwa Alexander alikuwa akimsikia kwa mbali kwani tayari usingizi ulimuelemea muda huo alijikuta kasinzia,  Minnie akamtizama akaona asimchezee alimvuta kutoka kwenye sofa akawa kalala chini Kisha alichukua shuka zilizokuwa kitandani na kumrushia.

   “” Baridi ikukupiga utajifunika.”

Minnie alimuongelesha ni kama alihisi kusikilizwa, Kisha na yeye aliamua kulala kwenye sofa mpaka kunapambazuka.

Asubuhi Alexander ndio alikuwa wakwanza kuamka kwani baridi la chini lilimuelemea alihisi ni kama yupo ndani ya freezer, aliamka anashangaa kwa pembeni yake juu ya sofa alilala Minnie, alitizama vizuri shuka alizokuwa Nazo chini zilikuwa kitandani inamaana Minnie alimpatia? akaona ni sawa tu ilibidi achukue zile shuka na kuzikunja tayari kwa kufuliwa Kisha alitoa shuka kabatini akatandika vizuri kitanda badae akaingia kuoga.

Wakati anaendelea kuoga aliona ndoo imefunikwa ikabidi afungue anashangaa kukuta nguo za Minnie zikiwa zimeloweka, alinyanyua nguo Moja juu aikague vizuri si ndo anaona ni zile za ubandit, hapo akahisi kuchoka huku akipiga taswira ya kukuta viatu vya Minii vinae tope inamaana ni kweli alitoka na kipi alienda kukitafuta Nje..!!?

Nini Kitaendelea? Usiku watajadili mada gani? Vipi kuhusu kaka yake Minnie atalipaje Kisasi? Na vipi Minnie ambaye tayari kamkumbuka mama yake Kisasi chake kitakuaje? Usikose SEHEMU YA SABA

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

 

14 Comments

  1. stori ni tamu sema tu mfumo wa uandishi umefanya stori iwe ngumu kuielewa, Kuna matukio mengi yamerukwa kwenye hii stori

  2. Tinner Rober on

    Wapenzi wa kusoma simulizi hii unatakiwa utulize akili kwanza sio unasoma kwa kushuka kama maji yanayoporomoka mlimani😀🤗

Leave A Reply


Exit mobile version