IlipoishiaMinii alijisikia vibaya niaje aliminya Pease alilokuwa akilila kwa kucha zake utazani panya ndio aligusa pale kwa kulidonoa Kisha akalitupa.

“” Miniii,,,, unajua gharama iliyotumika kununua Hilo tunda? Au unatumia tu kwakuwa pesa si yako…!? Jifunze kukitunza kitu usicho kigharamia.”

Ghafla Kuna Sauti ilisikika nje ikiita,

   “” Mirickaaa…. Miriiii,,,… Mirickaaa!! Upo wapi jamani.”

Alexander alimtizama Mirii Kisha akamtizama Minii aliekuwa akimtizama kwa hasira ni kama alitaka kummeza, baadae aliamua kuachana nae akimtizama Miriii.

   “” Mama kakufuata, twende ukamuone.”

Endelea 

SEHEMU YA SABA

Miniii ndio akakumbuka kumbe alikuwa akijihisi ni yeye anazungumziwa pale kumbe ni Miricka inamaana waoo walimuita Mirii, alijiona mjinga kweli lakini hakutaka aibu Ile imnyime raha na akiangalia hapo haoni mtu wa kumpatia furaha zaidi ya kutumia kauli Ile “Raha jipe mwenyewe “

Muda huo Mama Mirii alifika na kuingia katika chumba kile alifanya kuwahi kumkumbatia mwanae kwanza akifanya kubinya midomo iliyokuwa na ice cream.

   “” Nilijua tu utakuwa huku kwa Ba’mdogo wako! Hivi umemsalimia ma’mdogo kweli..!!?”

Mirii ndio akamtizama ma’mdogo mwenyewe anaezungumziwa yupo busy kucheza game la “Relic Adventure run.” Tena muda huo anahisi Raha mpaka anapiga kelele.

Alexander hakupendezwa na tabia yake inamaana hakuwa na nidhamu hata mbele ya wageni wake alimuita kwa nguvu..

   “” Miniiiiii…. !!!!”

Minii alishituka mpaka simu ikaanguka chini, Mama Miricka alifika na kukaa karibu naye akifanya kuokota Ile simu na kumpatia.

   “Kuwa makini mdogo wangu, Alexander huwa hawapazii watu sauti namna hii, usimfanye azidi hapa.” Mama Miricka alisema 

  Alexander akadakia ” Achana nae ndivyo anataka kupelekwa, mwanamke Gani wewe usiejali ndugu zangu, hukuona kama na mgeni hapa umpokee.. sheet kabisa…!!” 

   “” Aaa Shem inatosha bhana,, muache huenda hakuniona alikuwa busy na simu.” Mama Mirick aliongezea 

Alexander aliishia kumkazia jicho Kisha alimruhusu Mama Mirii amchukue mtoto wake Kisha abaki na mkewe.

Mama Mirick:   “Tafadhari Shem, usifanye kitu chochote kibaya kwa mdogo wangu.”

 Alexander:  “Usijali Shem Kila kitu kipo sawa.”” 

Mama Miricka aliondoka pamoja na Binti yake huku akiwa hana amani kabisa anamjua vizuri Alexander kwa ukorofi ni hatari.

Miniii huku alibaki na wasiwasi kitu alichofikilia kichwani mwake angalau angesimama kama mwanamke wakati huo na sio bandit kama alivyozoea kumuita. Alimtizama Alexander ambae bado kasimama kwa hasira huku kamgeuzia mgongo na muda huo alikuwa akigonga gonga meza, Minii alisimama taratibu Kisha akaenda kusimama nyuma yake alifanya kumuita kwa utaratibu na utulivu.

   “” Alexander Naomba unisamehe kwa kile kilichotokea Leo, huenda ulimi wangu kwako ulikuwa mchungu sana! Najutia kwakukosa ustahimilivu lakini hata wewe ulinikosea.” Aliongea Minii

Alexander ikabidi amgeukie anajiuliza ni mwanamke gani hawezi kufikilia makosa yake mpaka amhusishe tena na yeye alimkosea labda ni kitu gani alimkosea?

Minii akawa amepoa huku akishusha macho chini kwa unyenyekevu kabisa akizidi kuchezea mikono yake kwa kuibinya binya, sijui hata ilikosea Nini muda huo.

Alexander akazidi kumsogelea mpaka akaenda kugota kwenye kitanda bado tu kamuandama, mpaka Miniii akakosa balance na kuanguka Moja kwa Moja kitandani, Alexander akajaribu kumzuia lakini akawa ameshidwa zaidi ya yeye kushuka nae mpaka kitandani, ukaribu baina yao ulichukua nafasi Alexander alifanya kumtizama kwa sekunde nyingi,, aliona kabisa Minii ni mrembo sana ila kwenye tabia yake ya kikatili ilimfanya ashikwe hasira, lakini akakumbuka Binti huyu huyu alihitaji msamaha kwake ikabidi amuulize.

   “” Kwanini unakuwa hivi..!!? Nambie Kuna kitu unataka kupitia Mimi,, Minii hivi hii kichwa yako Kuna kitu inawaza?” Alexander aliuliza 

  “” Ni kuhusu Mama’ngu.”’ Minii Aijibu

  “” Mamaa…!!?”” Alexander alipayuka kwa nguvu

Miniii akashituka kumbe alimtaja Mama’ke wakati huo ikabidi amsukume Alexander nakuinuka.

Alexander akawa hamuelewi lakini aliamua kuachana nae akisogea kwenye dressing table akitizama uso wake alihisi Kuna hali fulani anajisikia.

   “” Jioni ya leo utapaswa ushuke chini! Bibi yangu anataka kukuona wewe.” Alisema Alexander

Miniii akabaki kumtizama tu huku akiendelea kukusanya vyombo vizuri Kisha alifuta meza.

    “” Unanielewa lakini…!? Au umeng’ata buyu?” Alexander aliuliza tena 

    “” Nimekuelewa.” Minnii akajibu

    “” Ok, vizuri.. Usivae nguo zako za ubandit.” Alexander akaongezea

Alexander akaongea huku akitoka nje! Minii nae siku hiyo hakutaka kushinda ndani kwani hakupewa limit ya kukaa ndani muda wote! Alitoka nje akiwa na nguo zake za ubandit kama alivyosema asivae yeye akavaa.

Alitoka kwenye chumba chake huku akizidi kukagua jumba lile kubwa kwa Kila Mlango Nia ni kutafuta nyumba ambae anaishi “” white house ” alitumia speed Kali kuhakikisha kwa muda huo mchache angetembea robo tatu ya jengo Hilo, mwisho kabisa alitokea sehemu yenye makaburi hii ikamchanganya sana inamaana ndani ya jumba hilo Kuna miili ilipumnzishwa pia? Akazidi kusogea pale lakini alisikia sauti ikimsimamisha.

   “” Nani wewee…!!?” 

Ikabidi ageuke anashangaa ni mwanaume alievalia mavazi ya ulinzi inamaana yule alikuwa ni Mlinzi. Miniii ikabidi ajibalaguze kwanza akishika moyo wake.

   “” Miii Mimi, Nilikuwa natembea tu.” Minnie alijibu kwa uoga

Mlinzi ikabidi amsogelee karibu akamtazama mkononi anaona anae Pete ya Ndoa na shingoni Kuna cheni kaivaa, na mara nyingi cheni hii huzawadiwa wakwe wa White House, ikabidi amshangae kwanza lakini alimuuliza.

   “” Wewe mke wa Alexander, huku unafanyaje..!?” Aliuliza tena mlinzi

Minii akashituka kwani alimfahamu vipi Mlinzi huyu kuwa yeye mke wa Alexander? Mlinzi alimuomba amfuate Kisha walisogea karibu na mti mkubwa uliokuwa una bench wakafanya kukaa, huku Mlinzi akiendelea kumuuliza.

    “” Kwanini unatoka nje, Ni mmeo kakuruhusu? Mimi najua ni vigumu wakamwana kutoka nje wakiwa kwenye mavazi haya? Au hawakukwambia kuhusu mavazi ambayo white house huvaliwa..!?”

Minii ndio akakumbuka muda si mrefu Alexander kamuonya kuvaa kama Bandit halafu hakumchukulia maanani amevaa? Kweli alijihisi yeye kichwa kibovu muda wote atagombezwa na mwanaume huyu asipojirekebisha.

   “” Aaa Mimi nilivaa, nilikuwa nafanya mazoezi.”

   “” Basi Rudi ndani na hakikisha mtu yeyote hakuoni, na kingine kama utatoka kwa kujiibia hakikisha hiyo cheni ya shingoni na hio Pete hakuna mtu anaeiona, hapo utakuwa free.””

Minii ilibidi amsikilize vizuri Mlinzi huyo huku akimshukuru sana, ilibidi atafute namna ya kuingia ndani kimya kimya akawa ameingia huku akili yake ikiwa imechoshwa na maneno ya Mlinzi, aliitizama Ile cheni shingoni akafanya kuivua kwa hasira.

“” Nishasema, hii nyumba ni kuzimu kabisa, Kila unachofanya lazima usanukie,,, Ilimaanisha Nini kuvaa hii cheni na hii Pete ya Ndoa kwa mtu usie na hisia nae? haya na hio kampuni tunaenda lini kuusimamia Mimi nipate muda wa kuzunguka, ukisema uulize hapa utaambiwa fungate, fungate ipi Sasa hii kwa huyu Alee, aaahaa.. Sorry ni Alexander.”

Muda huo Mlango ukabishwa Minii akatazama mavazi aliyovaa akajua tayari kimenuka tena, alichukua cheni ya Ndoa aliyokuwa kaiweka mezani Kisha alikimbilia bafuni kuoga bila kupenda.

Huku mlangoni alikuwa ni Alexander akibisha hodi, baada ya kuona ukimya umetanda ikabidi asukime Mlango akiingia. Lakini baada ya kuingia aliona kama Kuna tope ndani ikabidi asogee katika stendi ya viatu vya Minii akaona vile viatu vinamatope, alifanya kufunga macho na kufungua kwanza Kisha alikaa akimsubili Minii atoke bafuni.

Minii huku bafuni haachi kuomba Dua yoyote yakumfanya asishitukiwe, baada ya kumaliza kuoga ndio anakumbuka aliingia bafuni pasina nguo za kubadilisha, na hizi zingine kama angezivaa angeshitukiwa mapema alitoka akaangalia juu ya kamba kunae taulo na pensi kubwa ya Alexander akawaza avae pensi, kifuani taulo atoke na vipi kama ataulizwa kavaa nguo yake angesemaje?

   “” Miniii, wahi bhana wakati wa kushuka chini umefika,, tunasubiliwa huko..!!?” Alexander aliongea kwa sauti

   “” Aaa na–  nakuja…!”” Minnii akajibu

   “” Mhuu sauti yako inaonesha tayari ushaharibu. Mbona kigugumizi..?”

Minii hakumjibu zaidi yakujikaza alifanya kuloweka zile nguo alizokuwa kavaa kama ninja Kisha akafunikia na kifuniko cha ndoo, alifungua Mlango taratibu akimchungulia Alexander aliona ni kama yupo busy na simu, kumbe alimuigizia tu Ile anatoka tu sauti ya Alexander hakuchekewa kuisikia toka masikioni kwake.

   “” Ahaaa!! Naona Sasa umelizia kuwa Mrs Alexander white house. Kitu changu Mimi kwasasa ni kitu chako wewe, si sawa..!?” Alexander aliongea huku akizidi kumfuata, Minii alihisi kutetemeka anahisi leo angefanyiwa ukatili mkubwa na kijana huyu.

   “” Alexander, Nisamehe nilijua haupo kama ningeingia kuoga ningetoka na taulo tu kubadilisha, Sasa umefika nimeogopa kutoka hivyo hivyo na taulo.””

“” Kwelii…. Au Kuna ukweli nyuma ya maneno yako.”’

“” Aaa hapana,, Ni sahihi ninachozungumza.””

Alexander akaamua kumuacha Kisha alisogea kwenye stendi ya viatu akanyanyua kiatu kimoja akimtizama Minii.

   “” Na Leo tenaa umeenda kinyume na mimi,,, Okay jiandae tushuke chini,, Usiku utakuwa ni mzuri kwetu kujadili Maada hii.””

Nini Kitaendelea? Usiku watajadili mada gani? Vipi kuhusu kaka yake Minnie atalipaje Kisasi? Na vipi Minnie ambaye tayari kamkumbuka mama yake Kisasi chake kitakuaje? Usikose SEHEMU YA SABA

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU

 

10 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version