IlipoishiaAlienda kufungua Mlango anashangaa kumuona Alexander uso wake unatiririka jasho.

“” Wewe pisha bhana mlangoni, halafu funga mlango na akikugongea mtu mlamgo! Mwambie ndo naamka, ngoja nioge kwanza.””

“” Akhaaa!! Sijui ndo nini huyu nae…!!? Eti kaamka sahii anaoga mbona simuelewi. Sijui kakimbizwa hukoo..!!?” 

Endelea 

SEHEMU YA SITA 

Ikabidi afunge Mlango na komeo Kisha alirudi na kukaa kwenye sofa.

Muda huo Alexander ndio anatoka bafuni akiwa kavaa tayari alisogea na kukaa kwenye sofa huku akimtizama Minnie.

   “” Umekula lakini..!!?”

   “” Kwanini uulize wakati ni tumbo langu…?””

   “” Aahaa,, Bandit mkubwa, huenda ndio kazi iliyokupa ubusy.””

MInii akamgeukia kwanza jina hili itakuwa ni mara ya pili kulisikia kinywani mwa huyu mtu, aliwaka hasira.

   “” Umeniitaje… Alee…!!?”

Alexander ikabidi amsogelee nayeye kwani pia alimuita kifupi teenaa alizidi hata hiyo X kuimalizia ilimpa mzigo kwake mbona ni kama kazidi kumkosea?.

“” Nahisi unanitafuta Minii Mimi sio Alex Tena sahii waniita vibaya kama watu wa kule Kanda ya ziwa Mimi naitwa Alee Leo…!?”

Minnie akabaki kucheka tu, kweli alimuweza kicheko chake kiliambatana na kupaliwa, Alexander alimtizama tu Kisha alisema kimoyo moyo ” ulifaa kuzima kabisa” akafanya kusogea kunako Mlango akifungua na kutoka nje. Minnie muda huo alitafuta maji na kunywa angalau kikohozi kikakata lakini neno bandit halikuisha katika ufahamu wake.

   “” Yote sawa tu atajua mwenyewe.””

Muda huo Alexander aliingia akiwa kaambatana na mpishi akilalamika.

  “” Utovu Gani wa nizamu mnaouendeleza hapa,, Chai ndio tungeshindia siku nzima..!!? Kama mmechoka kazi Bora muache sio kutushindisha njaa, Ayaa niitie tolu kwanza( alimaanisha kiongozi wa wale wapishi)

   “” Sawa Bosi, Naomba unisamehe Leo watu walikuwa wengi, uaandaaji wa kugawa chakula ulikuwa mwingi.”

   “” Hebu toka hapa kwanza. “”

Dada yule alitoka lakini kwa MInii hakupenda kabisa kuona akifokewa, alitizama jengo la White House lilivyojaa watu wengi, kiasi kwamba angekuwa yeye aambiwe kugawa chakula bilashaka tumbo lake angelitimiza pekeyake na zaidi angegawa kwa Baba, Mama na White House na huyo mwingine angekuwa ni Alexander anaeishi nae chumba kimoja,, hao wengine ingekuwa ngumu kuwakumbuka.

   “” Wewe unawaza Nini kwani!!? Ukiwa white house hapa ni kula tu, Shida sisi zilipita mgongoni.”

MInii akamtizama ndipo akajua kumbe Alexander anadharau namna Ile, hakika alihisi kumkasirikia kwa muda huo hakutaka hata kukaa nae meza Moja, aliamua kujikunja kwenye sofa huku akichukua simu yake akichezea.”

“” Minnie, unajua katika nyumba hii Mimi sijawahi kukuamini kabisa make umekaa kama mpelelezi sijui Kwanini nashidwa kukuamini, Baba’ko akapendekeza Ghafla nikuoe, hivi unajua ujio wako hapa umekatisha ndoto ya mwanamke mmoja niliempenda sana kwa dhati! Nilipotoka hapa nilienda kuonana nae, analia tu hivi ulishawahi kuachwa na mtu umpendae akakaa mbali na wewe unajua maumivu yake?”

Maneno ya Alexander yalimfanya Minnie aamke kwani alifaa kuelezwa maneno Yale yanayohusu wadhifa wake si bora angeyajaji kichwani mwake si ingetosha na sio kumuelezea? Bilashaka ni alivuka mipaka yake akaamua kumuwakia.

   “” Ishia hapo, naona huniamini katika nyumba yako,, basi nitoe nje.. umekuwa ukiniita Bandit kwakunionaje, Kwa taarifa yako,, hii Ndoa Mimi sikutaka ila ongea na Baba’ko kwanini alimuomba Baba Mimi niolewe white house, bilashaka nyie ndio mnanipeleleza? Kwanza familia Gani hii utafikili upo jehanamu, hamna kutoka, muda wote ni Sheria Sheria,, wewe mwenyewe ni mtoto lakini hauna uhuru wowote unatoka kwa kujiibia wakati ni nyumbani kwenu ona ulivyorudi ukikibizwa hivi walinzi walikukimbiza eee…!!?”

   “” Minii basiiiiii…. Inatosha sasa,,, Acha kunipanda kichwani! Kumbuka Sheria kwasasa inatambua wewe ni mkewangu naweza fanya chochote na usinizuie.””

   “” Huwezi Alex, bila ridhaa yangu nasema huwezi.””

Alexander alihisi kuzima kwa huyu mwanamke mwendawazimu kwake Mwenye ulimi mrefu kama Joka la pangoni, na Bado kinywa chake kilichachuka kama katiwa pilipili na mbaya zaidi hakuwa muelewa kutaja jina lake kila siku angerudia kuita Alex tena sahii anaishia Alee, alihisi kumuwasha kofi lakini mkono wake ulitetemeka nakujikuta akipiga ngumi ukutani, mpaka Minnie akashituka na kuinama make ilitua karibu yake tu.

Alikuja kuinua kichwa tayari Alexander alikuwa akitoka nje, Minii ilibidi auwahi Mlango na kuufunga huku akijutia na kushika mdomo wake jinsi ulivyokosa kituo, na vipi kama angetiwa Kofi angeweza kweli kupambana na mwanaume, Mbona alikosa kufikilia mapema kitu kama hicho ni hatari kwake? Ilibidi asogee mezani na kuanza kula chakula kwani njaa tayari ilimshika kwa ule mshituko.

Alikula chakula kingi kwa hasira Kisha alishika simu yake na kumtafuta Baba’ke alimtumia ujumbe.

   “” Nahisi kama nitashidwa hii kazi uliyonipatia.”

Message ilimfikia Mzee Mzobe alifanya kuisoma tu Kisha akatabasamu, alijua Binti yake Kuna kitu kakutana nacho lakini aliishia kuzungumza huku akiweka simu mezani.

“” Lazima akili yako ichangamshwe kwanza Ili ubongo wako uwe tayari kupambana sio kila siku akili yako imelala lala, lazima iamshwe na wewe amka ukapambane.”

Huku kwa Minnie alisubili majibu lakini haikuwa vile alivyotegemea, ilibidi akae atulie huku akikumbuka maneno ya Baba’ke mara nyingi alipenda kumwambia asiwe mnyonge zaidi apambane, na kingine alimsihi mazungumzo ya yeye na Baba’ke yalifaa yawe ya kifamilia na sio ya mission tenaa. Hapo hapo ndio anakumbuka tayari kakosea na vipi Baba’ke akijibu halafu message ionwe na Alexander, ilibidi achukue simu haraka na kuandika ujumbe tenaa.

   “” Samahani Baba niliteleza,,, usijibu chochote nilichokutumia, Mimi naendelea kupambana huku na nipo sawa.”

Ujumbe ukamfikia Mzee Mzobe huu ulimfanya atabasamu kabisa akiamini Binti yake anazidi kuimalika, matukio madogo madogo ndio yalimpatia nguvu ya kupambana.

Muda huo Mlango ukafunguliwa Minii akawahi kufungua huku akiwa na wasiwasi huenda ni Alexander kamrudia, Ile anafungua Mlango anashaa anakutana na mtoto wa kama miaka Saba au nane hivi alikuwa wa Kike. Mtoto yule aliingia ndani mara tu baada ya Mlango kufunguliwa. Minii akawa hamuelewi ikabidi amfuate nyuma nyuma akimkagua kipi anafanya.

Mtoto alizidi kukagua ndani baadae aliingia bafuni huku akiita.

   “” Ba’mdogoo..!! Upo wapi?” Minii ndio akajua kumbe alimtafuta Alexander ikabidi amjibu.

   “” Ba’mdogoo katoka.”

Mtoto ilibidi amsogelee karibu Kisha alimshika mkono akimtizama Minii .

  “” Ma’mdogo… Baba aliniahididi zawadi, nilijia zawadi yangu.””

  “” Ooh! Princess…. Zawadi yako hii hapa…!!””

Alikuwa ni Alexander kasimama mlangoni akiwa na kibox akifanya kutandaza mikono yake kumpokea mtoto.

Minii akageuka kumtizama kwani muda huo alionesha kuwa na furaha ni kama hivi punde hawakuzozana ndani. Alibaki kuwatizama tu Kisha akaendelea na ubusy wake.

Alexander alifanya kumnyanyua princess wake Kisha alimuita.

   “” Ooh miriii….!!””

Minii akawa amegeuka kuwatizama muda huo walikuwa wakilishana ice cream 🍨🍦 akafikilia ni kama aliitwa yeye muda huo ikabidi ajikaushe tu.

   “” Mirii,,, Si umeshiba Sasa…!!?

Alexander akarudia kuzungumza huku akimpiga jicho Minii ambae hakusita kujibu. “” Hayakuhusu”” Miriii akawa kamtizama Baba’ke mdogo Kisha akamtizama tena Minii wakajikuta wakimcheka kwa nguvu.

Minii alijisikia vibaya niaje aliminya Pease alilokuwa akilila kwa kucha zake utazani panya ndio aligusa pale kwa kulidonoa Kisha akalitupa.

“” Miniii,,,, unajua gharama iliyotumika kununua Hilo tunda? Au unatumia tu kwakuwa pesa si yako…!? Jifunze kukitunza kitu usicho kigharamia.”

Ghafla Kuna Sauti ilisikika nje ikiita,

   “” Mirickaaa…. Miriiii,,,… Mirickaaa!! Upo wapi jamani.”

Alexander alimtizama Mirii Kisha akamtizama Minii aliekuwa akimtizama kwa hasira ni kama alitaka kummeza, baadae aliamua kuachana nae akimtizama Miriii.

   “” Mama kakufuata, twende ukamuone.””

Nini Kitaendelea?  Vipi kuhusu Nick? Atapambana nae kulipa kisasi? Wewe Ungelipaje KISASI? Usikose SEHEMU YA SITA

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU

 

11 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version