Ilipoishia  “” Sawa, na usitoke kweli, White House imejaa Camera sehemu zote isipokuwa kwenye chumba chenu lakini vyumba vya watumishi vyote vimejaa Camera, hapo inatakiwa uwe makini kwanza make hatua ya kwanza ndio tumeianza ni wewe kuolewa na kijana wa white house, hatua nyingine nakutumia kwenye email hapo, utaipitia kama hutoelewa niulize nikueleweshe tafadhari.” 

Endeelea 

SEHEMU YA TANO

Minnie akafanya kuangalia Email kwa umakini zaidi maelekezo aliyokutana nayo ni kutafuta Flash pamoja na ushahidi wowote kutoka kwa White House kuonesha biashara haramu anazozifanya, Minii hakuelewa vizuri kwani alipaswa kufatilia biashara za white house na sio kuhusu kifo Cha Mama’ke ilibidi ampigie Baba’ke teenaa….

   “Lakini Babaa…. Maswala ya biashara haramu na kuhusu kisasi chetu, wapi na wapi?”

   “” Minnie,  sikiliza, Naomba ufate maelekezo yangu kwanza! Sio rahisi kukurupuka namna hiyo, fuatilia maongezi ya white house karibu ujue anashilikiana na nani, pia fatilia biashara zake kwasasa uzifahamu, kingine mfatilie Alexander pia huwa anahusishwa mambo mengi na white house.”

   “Sawa Baba! Kwakuwa nimeamua kulipa kisasi lazima nifate maelekezo yako Baba.”

   “” Sawa, jitahidi kufuta viashilia vyovyote vitakavyokufanya wakutie shaka.”

   “” Sawa.”

Minii baadae aliingia kwenye laptop akiweka documents zake vizuri baada ya kuhakikisha hakuna tatizo lolote hata Alexander akishika laptop ingekuwa ngumu kujua kahifadhi nini.

     °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°

Upande wa Nick alipata muda wa kufungua bahasha Ile akiwa amejipumzisha kwenye kivuli Cha mkaratusi.

   “” Hii bahasha,, Mama Naomi anayo.. itakuwa imegizwa toka Kwa nani?”

Nick alizidi kujiuliza huku akifungua Ile anafungua anashangaa anakutana na picha iliyomfanya ainuke na kukaa huku akiitizama kwa makini..

   “” Miniii…. Babaaa….!!!?”

Akazidi kushangaa make alimuona ni Minii akiwa ni mkubwa tena kabadilika kweli akiwa ni mrembo sana, Baba nae alikuwa ni kapendeza kweli kwa kutizama tu alionekana anae pesa nzuri hata mwili wake ulijengeka vizuri kwa lishe pamoja na mazoezi. Lakini haikuwa picha tu bali kulifatia ujumbe katika karatasi iliyokujwa vizuri alifanya kuikunjua Ile karatasi nakuanza kusoma.

  [ Nickson Mwanangu, Natumai ni mzima wa Afya njema, pia sisi ni wazima wa Afya kama unapotuona hapo juu kwenye picha, Nisamehe kwa kutoweka nyumbani bila taarifa ya kurejea kwangu, Siku hiyo nilimpata Miniii, kwa kifupi nipo nae na tunaishi vizuri tu, lengo la kukaa mbali na mji wetu ni kupata wasaa mzuri wa kujiandaa kulipiza kisasi, Naomba pia ujitunze huko uliko uhai pekee ni zawadi yetu kwetu,,,, kwa chini nimeweka namba yangu na ya Minnie, pindi upatapo ujumbe huu tutafute tafadhari. Tunakupenda sana ]

Nick akamaliza kusoma huku akihisi furaha isiyo na kifani, machozi ya furaha ma huzuni yaliambatana katika mboni zake kitu anachofikilia ni usalama mdogo wa maisha Yao sio rahisi kulipiza kisasi kwa mtu mwenye jeshi kubwa namna ile, alifanya kuwasitikia tu. Alifanya kusave namba zile, kiu aliyokuwa nayo haraka ni kumtafuta Miniii, alimpigia simu lakini iliishia kuita tu nakukata bila kupokolewa.

   “” Nini Sasa jamanii, Minnie pokea simu tafadhari ni Mimi Kaka’ko kipenzi Nick, please respond my phone.”

Nick alizidi kuongea huku akizidi kupiga tenaa, baadae alikumbuka hakusave namba ya Minnie tu hata ya Baba alisevu pia, alifanya kumpigia,. Akapokea.

Sauti nzito ikapenya kwenye masikio yake alikuwa ni Baba aliitikia “” Halloo..!!” Nick alibaki kutulia akiisikilizia sauti Ile ilipenya vizuri mpaka kwenye moyo wake na kuleta utulivu wa sekunde Tano hivi Kisha aliita. “” Baba…!!”

Mzee Mzobe akasikia sauti vizuri ya kijana wake, alitoa simu sikioni kwanza akifanya kuikagua namba Ile Kisha alirudisha sikioni akiendelea kuzungumza.

   “”” Nickson Mwanangu,, Nimekukumbuka sana, natumai umekuwa kijana mkubwa na unaweza kusimamia majukumu ya familia hata nisipokuwepo.”

   “” Baba,, Shikamoo.. !!! Nick nikama alikuwa kaduwaa alifanya kumpatia heshima Baba’ke kwanza.

   “” Nakusikia Nick,,, Halooo… Mbona huzungumzi tenaa…! Ee hallo..!!?”

Mtandao ulileta shida kidogo na kufanya mawasiliano yakate pande mbili.

   “” Hapana Baba, usiondoke tenaa nakupigia. Nick ni kama alichanganyikiwa alirudia kupiga tenaa lakini Network ikawa busy, alipata hasira na kuilusha simu yake lakini kwa bahati nzuri ilidakwa, Nick alikuwa katulia akisikiliza sauti ya Simu kutamiza chini lakini haikuwa vile ikabidi ageuke kutizama vizuri make aliipea mgongo.”

   “” Ni Nini unafanya lakini Nick…!?’ Alikuwa ni Eliud rafiki yake kafika na ndie aliidaka simu ile.

  “” Napaswa kufanya hivi, ni watu niliowasubili kwa muda mrefu, angalau tu nilipaswa kupata mazungumzo yao nijue walipo lakini haijawa vile..”

Eliud akawa hamuelewi vizuri, alitazama pembeni aliona Kuna picha ikabidi aichukue kwanza nakuitazama.

   “” Miniii ,, Baba… Si ndo hawa…!!?”

Nick ikabidi amuongezee na Ile barua aisome vizuri, baada ya kumaliza kuisoma ilibidi wakae kwanza kujadili.

   “” Wewe unafikili Minii na Baba walikutana vipi siku apotee na kule wanakoishi walifika vipi..!? Inamaana Minii alitekwa , Baba ndio akaenda kumsaidia?” au ilikuwaje kwanza upande wa MInii kukutana na Baba..!?”

Eliud alijaribu kuchakata ubongo huku akimtizama Nick.

   “” Haaa..!!! Naelewa basi? Yaani ndo nachanganyikiwa hapa! Ilitakiwa wapokee simu ndio wanieleze.”

Muda huo huo wakamuona Amri akija akiwa na team yake mara nyingi walizoea kutembea wanne lakini muda huo walikuwa watatu.

   “” Hifadhi vizuri hizo picha kwanza, halafu napaswa kumuuliza vizuri Amri na wenzake Ile siku walisema wamemuona Minii msituni alikuwa kuwinda, Sasa ikawaje? Make ndio hiyo hiyo siku alipotea, au walimteka.. !?”’

Nick aliongea huku akihifadhi vizuri Ile bahasha kwenye mfuko wake wa suruali.

   “”‘ Ooh! Mjeda Nick, nahisi Kuna kazi ya kufanya unatakiwa kuongozana na Mimi..!? Amri aliongea bilashaka kwenye kundi la watu wanne yeye alikuwa muongeaji sana, au kwakuwa alitokea Kigoma..!!?”

Nick akabaki kumtizama Amri akatabasamu tu huku akimsogelea mmojwapo ya rafiki zake alifanya kumshika mkono begani.

   “” Eti Alex,  Ni sawaa….!!?””

Kijana huyu alitabasamu pia huku akitumia ishara ya kichwa kukubali, alionekana ni mkimya sana ila kwenye kazi alikuwa mwepesi kutumia akili yake sivyo kawaida, ukimya wake ulijazwa na maneno ya busara na akili yake aliitumia mara nyingi kufikilia kitu kwa undani kiasi kwamba akipewa mission afatilie lazima afanikishe.

Nick ilibidi aongozane nae Kuna kazi walipatiwa na mkuu wao kuifatilia, Njiani ilibidi Nick afunguke huenda angepata majibu ya maswali yake.

   “” Ulisema siku Minii anapotea ulimuona polini akiwinda ndege..!!?”

  “” Ahaa,,,, Naona unataka kujua ..? Sio nilimuona Bali tulimuona nikiwa Mimi na Alex, Nashon na Elisha.”

  “” Ooh! Alikuwa akielekea wapi kwanii…!!?”

  “” Ni kule juu mlimani, hebu ngoja kwanza nikumbuke…!!?”

Nick akamgeukia akimpatia muda wa usikivu..

“”” Eeeh umekumbuka Nini…!!?”

“” Kule mlimani juu alikokuwa akielekea mara nyingi Kuna majambazi tumekuwa tukiwakamata wakiwa mlimani, wao huiba vitu na kuja kugawana,,, Sasa hapa nawaza kama alifika kule huenda majambazi wale walimuona na kumteka, nahisi akili yangu inaweza kuwa sahihi.””

Nick akashusha pumnzi kwanza ni kama Kuna ukweli ndani yake, alianza kupiga hatua akiwahi mbele.

   “” Sasa unawahi wapi teena…!!?”’

   “” Kwenye hio mission tuikamilishe mapema then twende msituni kwenye ule mlima huenda nikapata chochote kuhusu Miniii.”

Amri akabaki kumtizama akamfikilia Nick… inamaana alihitaji kupata mwili wa Miniii, au nguo au ni mifupa make ni kama miaka mitano apotee anaweza kuona Nini labda? Amri aliwaza tofauti kabisa pasina kufahamu Nick tayari ana taarifa za Minnie na Baba’ke ni wazima wa Afya bilashaka alitaka kujua huenda Minii alitekwa na majambazi ndio maana yupo salama, na kingine alitaka kujua huko wanakoishi huenda wapo chini ya himaya ya majambazi wakiwatumikia, kuwakomboa ndio kitu kikubwa kilitawala fahamu zake.

°°°°°°°°°°°°°°°

Huku kwa Minnie muda huo alikuwa kapitiwa usingizi aliamka na kushika simu yake huenda Alexander alimtafuta make ni muda sana tangu aachwe kwenye kile chumba hajarejea, lakini kwenye simu yake alikuta ni namba iliyosomeka kwa 075670227X aliitizama Ile namba kwa makini lakini hakuifahamu, bilashaka ni Nick ndie alimpigia tangu muda ule wapotezane alibadilisha line tayari, aliamua kuipigia lakini kabla hajapiga Mlango ulibishwa ikabidi ailishe kupiga.

Alienda kufungua Mlango anashangaa kumuona Alexander uso wake unatiririka jasho.

“” Wewe pisha bhana mlangoni, halafu funga mlango na akikugongea mtu mlamgo! Mwambie ndo naamka, ngoja nioge kwanza.””

“” Akhaaa!! Sijui ndo nini huyu nae…!!? Eti kaamka sahii anaoga mbona simuelewi. Sijui kakimbizwa hukoo..!!?”

Nini Kitaendelea?  Vipi kuhusu Nick? Atapambana nae kulipa kisasi? Wewe Ungelipaje KISASI? Usikose SEHEMU YA SITA

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz   

KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU

 

 

13 Comments

  1. Peter Wilson on

    Uandishi wako unafikirisha sana kuunganisha matukio kuna baadhi ya wasomaji wako unawaacha, punguza kuchanganya matukio ata kidogo

Leave A Reply


Exit mobile version