Ilipoishia ” Minnie alitabasamu tu Kisha alienda kuegama kwenye moja ya nguzo iliokuwa ikiunganisha Kuta yao.

“” Haaa hata Sina niwazalo lakini Leo kwenye Darubini ya Baba, niliona Kambi ya jeshi ambayo utaenda kuchukua mafunzo pale, namna alivyokuwa akitizama Baba alikuwa na hasira nayo kweli nahisi Kuna kitu.”

Kipindi wanazungumza hayo Mzee Mzobe alikuwa akiyafatilia mazungumzo yao baada ya kusikia Kila kitu alitabasamu tu akiingia ndani.

Endelea 

SEHEMU YA PILI

Baadae waliachana kila mtu aliingia chumbani kwake kupumzika.

Asubuhi kulipopambazuka Mzee Mzobe ilibidi aanze kufatilia swala Zima la Nick kujiunga na jeshi, siku hiyo alishinda akitembea kwenye ofsi nyingi huku simu zake zisiishe ubize wa Kila muda. Nyumbani alibakia Minii siku hiyo aliingia kwenye chumba Cha Baba’ke kwani kuna kitu alikuwa akikitafuta, katika kutafuta alikutana na picha moja alifanya kuifuta kisha akaikumbatia kwa hisia, picha hii ilikuwa na taswira ya mwanamke mmoja mrembo alionekana kufanania sana na Minii, Minii baada ya kuitazama muda mrefu alifanya kuirudisha Kisha alizungumza.

   “” Napaswa kufanya kitu kwa ajili yako Mama, wote walioshiriki kukulaza chini lazima watalipa.”

Muda huo huo Nick alifika na yeye katika chumba hicho na alimkuta Dada yake kashikilia Ile picha alifanya kumuita kwanza “” Minii…!!” Minii ndio akashituka akiirejesha Ile picha kwa wasiwasi sana, Kaka’ke alimsogelea kisha akamshika mkono akimtoa kwenye chumba hicho.

   “” Unavyofikilia sivyo kabisa…!!?” Minii akafanya kujitoa kwenye mikono ya Kaka’ke kwanza huku akipandisha sauti.

“” Hapana, lazima watalipa Mamangu mimi alipaswa kuwa hai halafu wanatokea watu from nowhere wanamsababishia umauti, alikosea nini Mamangu, hapana kaka lazima walipe.”

Nick ikabidi akae atulie kando kwanza akimtizama Dada’ke alivyochafukwa alitamani kumjibu lakini akaamua kuondoka pale kimya kimya akielekea nje kidogo na nyumba Yao, Kuna rafiki yake aitwae Eliud alikuwa akimsubiri huku kavaa jezi za mazoezi, baada ya kumuona alimfuata.

   “” Oyaaa! Mbona umekata steam namna hiyo nimemsikia Minii anakupazia sauti kweli?”

   “” Aaa tuondoke bhana! Kitu tunachofikilia ni sisi kufanya mazoezi tu.” Eliud alibaki kutokumuelewa vizuri Nick, lakini akaamua kupotezea.

Huku kwa Minii siku hiyo haikwenda vizuri kwake aliamua kuchukua mshale akielekea porini kama ilivyo kawaida yake huenda angemalizia hasira zake kule.

Alifanya kuingia msituni Ile anaingia alisikia kelele za watu ni kama walikuwa wakizunguka msituni, Minii ilibidi atulie kwanza kwani alijua kuwa ni wanajeshi wapo kwenye matembezi yao ikabidi ajitokeze pembeni yao.

“” Ooh! Minii Mzobe, naona umekuja Mzobe Mzobe hapa! Vipi Baba’ko kakuruhusu?” Kijana mmoja aitwae Amri alimuuliza.

Minii hakutaka kuwajibu hata hivyo alikuwa ashawazoea sana kukutana na wanajeshi kwake aliwachukulia kawaida tu.

“” Hapa Mzee Mzobe kajizaa, mkorofi huyu kama Baba’ke tu, mwacheni itakuwa anaenda kuwinda ndege.

Kijana mmoja aliongea huku akifunga nyuzi za viatu vyake huku wenzake wakibaki kumtizama Minii kwa kumsindikizia macho.

Minii baada ya kufika tamati ya safari yake alikaa kwanza kuna kumbukumbu zilikuwa zikimtatiza lakini Ile amekaaa alisikia kama kuna watu walikuwa wakizungumza ikabidi azidi kusogea kwa ukaribu sana, aliwatizama kwa makini akajua ni tofauti na wanajeshi bila shaka itakuwa ni watu wa porini, wawindaji au majambazi, akazidi kutizama mazingira vizuri akaona ni kama walikuwa wakigawana mizigo iliyokuwa kwenye box.

   “” Akhaaa! Kumbe ni hawa manyang’anyi wa porini! Bila shaka wameiba vitu vya thamani au ni dhahabu…!!?”

Minii alizidi kujiuliza lakini hakuwa na majibu zaidi, ilibidi atulie pale kwa muda mpaka wakasambaa baada ya kuondoka tu! Ilibidi asogee katika mazingira Yale! Ile anafika aliona Kuna vipakti vya unga unga vimemwagika Minii ikabidi achukue Ile pakti akifanya kuikagua kwanza kwa bahati mbaya ule unga unga alivyoushika ukawa umemmwagikia kwani Ile pakti ilikuwa imechanika huenda na wao waliona bora kuiacha.

Ule unga ulipelekea Minii kuanza kukohoa mfululizo, taratibu alianza kuhisi kichwa kinakua kizito aliuhisi uzingizi mzito unaanza kumuelemea, akili aliyokuwa nayo pale ilimtuma ajiegeshe kwa muda kidogo kwani hata kutembea miguu inakuwa mizito.

     ++++++++

Huku nyumbani masaa yalizidi kusogea pasina kumuona Minii, Mzee Mzobe alishidwa ustahimilivu ikabidi amfuate Nick.

   “Muda ule natoka niliwaacha ndani mkiwa na Minii, Sasa atakuwa wapi?”

   “” Aaa Baba…. Mimi nilitoka nilimuacha ndani! Sijui alikoenda.”

Mzee Mzobe ikabidi aingie chumbani kwake alitoka na gobole, Nick akawa anamshangaa ikabidi amfuate.

   “” Baba lakini Nini hiyoo? ” unaenda kumfanya nini Miniii, usimuue tafadhari.”” Nick akazidi kujitahidi kumsihi Baba’ke asifanye hivyo lakini haikusaidia zaidi ya kumfungia geti akimuonya asitoke.

“” Sasa ni Nini Baba ataenda kufanya,, maskini mdogo wangu …

Nick akazidi kuongea akizunguka ndani ya fensi akiangalia kama anaweza kuruka Ili akamzuie Baba’ke asifanye kitu kibaya kwa Minii”

 

BAADA YA MIAKA KADHAA KUPITA.

Ni miaka mitatu ilipita tangu tukio la Baba kuondoka nyumbani baada ya kusubili ujio wa Minii kutokurejea nyumbani aliamua kutoka na gobole au mtutu wa Bunduki japo hatukujua uelekeo wake ilikuwa ni kwenda kumtafuta Miniii au laah!

Huku kwa Nick siku zilivyozidi kusogea katika miaka hiyo kuna Baba aliachiwa maelekezo na Mzee Mzobe alichukua jukumu la kumuendeleza Nick kutimiza ndoto yake alioipambania kwa muda mrefu, tayari alikuwa ni Mwanajeshi aliekamilika kwa mafunzo yote.

Upande Mwingine alionekana Minii akiwa kwenye jumba kubwa lenye takribani ya Ekari tatu za mraba, lilikuwa ni jumba kubwa la mfanyabiashara mashuhuri sana, mfanyabiashara huyu alijenga nyumba yake ikiwa ni kisiwani kabisa akilipatia jumba hili Utambulisho kama ” White House” Jumba hili lilijaa watu wa kila aina watu wake wengi walikuwa wakihudumiwa na watumishi mbalimbali, kwani watu waliokuwa wanafamilia kazi Yao ilikuwa ni kula na kunywa.

Ndani ya jumba hili halikuisha sherehe mbalimbali, Kila siku watu wake walijawa furaha sana wakienjoy kwa burudani nzuri ya mziki mlaini ulisikika masikioni huku vinywaji mbalimbali vilisheheni kwenye meza pindi mziki huu unaposikika.

Huku kwa Minii muda huo alimaliza kufanya mazoezi yake alifanya kuingia bafuni na kufungulia maji laini kabisa yenye uvuguvugu akifanya kuosha mwili wake kwasabuni yenye marashi kabisa huku povu lake likikolea katika mwili wake, baada ya kumaliza kuweka mwili wake safi aliingia kwenye kabati akitafuta nguo ya kuvaa, lakini ndio anakumbuka kuna nguo maalumu iliandaliwa kwaajili yake alifanya kuitazama Kisha akasogea na kuishika nguo hio ilikuwa ni spesho kabisa kwa mtu anaeenda kufunga Ndoa.

Wakati Bado yupo pale Kuna mtu alifika mlangoni kumgongea Minii akawa amemruhusu aingie.

   “” Madam unasubiliwa nje  tayari sherehe imeanza watu wote wanakuangaza wewe.”

   “” Sawa nakuja! “

Minii hakuwa muongeaji sana zaidi ya kutekeleza tu. Alimaliza kujiandaa huku akijitizama kwenye kioo kwa muonekano wa nguo Ile alijikuta akitabasamu tu huku akipiga hatua kufungua Mlango, Ile anafungua tu tayari Kuna Ladies watatu walifika kumpokea huku wakimshika mkono wakielekea katika sehemu ya tukio.

Kuna Mlango mwingine ulifunguliwa, ulionekana ni mkono wa mfunguaji ulikuwa umeng’aa kwa saa nzuri ya gharama huku ngozi ya mkono huu ulikuwa nadhifu sana, vinywelee vyake viliweza kulaliania ni kama umeona sufu, haikuishia hapo tu mkono huu ulituelekeza Hadi kwenye taswira ya mtu huyu ndipo tunamuona alikuwa ni kijana maridhawa alivalia suit yake ya Dark blue, huku mguuni akitupia kiatu cheusi kwa kumtizama tu utajua huenda katika sherehe Ile aliyokuwa akusubiliwa Minii hata yeye alisubiliwa vilevile kama mtu maarumu, Ile anatoka tu Kuna gentleman nne walitokeza wakimpokea kama Mwana wa Mfalme wakimuelekeza uelekeo atakapofaa kuwepo.

Huku kwa Minii muda huo anazidi kupiga hatua kwa pembeni kidogo aliona Kuna garii inaingia alivyotazama vizuri aliona sura iliyofanana na Nick alifanya kutabasamu huku akimpatia ishara ya salamu kupitia macho yake na kudhibitisha tabasamu lake ni kweli ni mzima, lakini alizungumza.

   “Kama upo hapa! Naamini nipo salama.” 

Nini Kitaendelea? Atapelekwa Jeshi? Usikose SEHEMU YA TATU 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote 

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

11 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version