UTANGULIZI

Katika maisha mara nyingi ubaya uliowahi kutendeka au kutokea katika familia au jamii mbalimbali umekuwa ukizunguka na kuishi katika vizazi mbalimbali huenda ni Ile utasikia wazazi wako, ndugu, jamaa, rafiki au watu fulani walikufanyia hivi au walitufanyia hivi lazima watalipa kwa mabaya waliyotenda,, kauli hii humpelekea mtu kuapiza kwa viapo mbalimbali huenda ni kwa miungu anayoiamini au ni kwa Mungu unayemtumikia wewe  na kusahau hatima ya maisha ya mtu ipo mikononi mwa MUNGU. Leo tutaenda kuangalia simulizi yetu itakayo tukumbusha vitu vingi sana kuhusu Mkasa huu.

SEHEMU YA KWANZA 

Ni pembezoni kabisa karibia na Kuta za wanajeshi nchini Tanzania, kulikuwa kuna nyumba zilijegwa na wanakijiji  pembezoni na miliki hiyo nia ni kuanzisha makazi ya wanakijiji hao huku milima na miti mbalimbali ikizungunguka eneo hilo Ili kuyafanya mazingira hayo yawe nadhifu, haikuishia misitu tu bali hata mito pamoja na mabonde ziliambatana kwa pamoja kutiriirisha maji katika mazingira yale.

Wanakijiji wa Kanda hii mara nyingi walijihusisha na kilimo, uvuvi pamoja na biashara ndogo ndogo zilizotokana na nguvu ya kilimo na mara nyingi biashara hizi walikuwa wakiwauzia wanajeshi waliotoka kambini, ikiwemo na watumishi wa serikali kwenye kada tofauti tofauti kama walimu, wauguzi na baadhi ya sekta nyingine nao walijenga katika mji huo huku baadhi ya nyumba nyingi zilikuwa ni za wanajeshi wengi wao walianzisha makazi yao huku wakileta familia zao katika mji huo  wakiepuka uhatarishi wa mahusiano ya mbali katika Ndoa zao huenda ungeleta magomvi katika miji.

Katika Kijiji hiki Kuna familia moja ilikuwa maarufu sana ambayo ni ya Mzee Mzobe, familia hii ilionekana kujitenga sana na wanakijiji kwa kutoshirikiana katika shughuli mbalimbali na hii yote ni kwasababu Mzee huyu alikuwa ni mkali sana na hapo nyuma aliwahi kuwa mwanajeshi, kuna sababu kadhaa zilipelekea kuachishwa kazi na kuwa mtu wa kawaida sana,  Familia ya Mzee Mzobe ilikuwa ni familia ya watu watatu yaani, Mzee Mzobe alikuwa Baba wa watoto wawili ambao ni wakike na wakiume,; wakike aliitwa MINNIER japo huyu ndiye mdogo na wengi wao walipendelea kumuita (Minii) na wakiume huyu   aliitwa NICKSON kwa kifupi humuita ( Nick) Elimu ya watoto hawa ilikuwa ni kidato cha nne baada ya hapo hawakuendelea na masomo zaidi ya kujikita kwenye shughuli za kawaida wakishirikiana na Mzee Mzobe ( Baba Yao) Ili maisha yaende mbele.

Katika watoto hawa Nick alipenda sana kuwa mwanajeshi lakini Baba’ke muda mwingi amekuwa akimzuia na kumpeleka sokoni kuuza nafaka, huku kwa Minnie mara nyingi yeye hupenda kwenda msituni kuwinda wanyawa huku akitumia silaha ya mishale Kawa kiwindio japo ni kwa kujificha ficha sana Baba’ke asijue.

Siku moja Majira ya usiku Mzee Mzobe alionekana kuwa  nje akipunga upepo huku mkononi alishikilia darubini akiangaza mazingira ya Kambi ya jeshi, Kila atazamapo Kambi hii alionekana ni mtu mwenye hasira sana, Baadae Minnie alifika na kukaa kando yake, Mzee Mzobe ikabidi amrushie Ile darubini mkononi akimwambia.

“” Ukitazama hapo unaona Nini?”

Minii ikabidi achukue darubini akifanya kutizama usawa wa eneo alilokuwa akitazama Baba’ke, baada ya kutizama alifanya kuweka darubini kwenye kiti chake akimgeukia Baba’ke akizungumza

“” Naona ni Kambi ya jeshi ikiwa na wanajeshi wake.”

“” Afadhari kumbe unaona vizuri, Umbali uliopo hapa kufika kule ni kama kilomita tano hivi unafika.” Ila Kuna wakati tutaenda kule.”

Minii akabaki kumtizama Baba’ke kwa Yale maneno aliyoyaongea akiyasindikizia na Mvinyo akinyanyua Glass yake kwa bashasha akishusha fundo Moja kwanza kwa kusikilizia Radha yake malizawa kabisa. Akisubili swali kwa Minii.

“” Kwani Baba unamaanisha Nini?”

“” Nick atakuwa wapi? Au kanitoroka teenaa?””

Baba nae akamuuliza swali.

Muda huo Nick ndio akafika akiwa kalowa mwili wake chepele huku tisheti yake aliweka pembeni. Walimtizama kwa pamoja huku Minii akipiga hatua kumsogelea karibu akifanya kugusa mwili wake kwa ncha ya kidole.

“” Unanatana kweli, kaoge kwanza.”

Nick alifuata maelekezo ya Mdogo wake huku akiondoka lakini Baba alimsimamisha kwa maneno.

“” Vipi bado una ndoto ya kwenda jeshini?”

Nick akashituka kwanza asiamini ni kweli aliulizwa yeye au maneno Yale yalielekezwa sehemu nyingine? Ikabidi ageuke.

“” Ooh! Unamaanisha ndoto yako haijafifia, kwa kusimama tu nimegundua kitu, basi nitashughulikia.”

“” Aa a..a,,, kweli Baba…!!?’

Mzee Mzobe ikabidi amfuate Kisha alimgongagonga begani akikitumia kichwa chake kama ishara ya kuzungumza, ni kweli kakubali.

Minii alihisi furaha ya ajabu alimuwahi Kaka’ke akamkumbatia huku akiruka ruka, anaona ndoto ya Kaka’ke siku zote ilikuwa ni kwenda jeshi. Baadae ndio akajishitukia baada ya kuhisi joto Kali la Kaka’ke akafanya kubinya pua, akisogea pembeni, Nick akabaki kumtizama tu Kisha akacheka akajua kamnukisha jasho lake.

“” Sio vizuri hivyo, Nguo zangu zote zimenuka ,,,,, we we wewe tu, Acha Nikafue tu.”

Baba akabaki kuwatizama wanae Kisha alibaki kucheka tu, ni kweli walipendana sana, Baada ya Nick kuondoka Minnie akabaki na Baba’ke akimtizama anamfikilia huyu Binti yake yeye alikuwa na Ndoto Gani katika maisha yake?

“” Ayaa, Na wewe Binti yangu unataka kufanya Nini labda hapo mbeleni, unajua sielewagi unapendelea kazi Gani? Au utabaki kunipikia tu?””

Minnie ndio akakumbuka muda mwingi yeye hupendelea kwenda polini kuwinda ndege na wanyama wadogo wadogo na ameifanya kama Siri japo huwa anamshilikisha Kaka’ke mara tu baada ya kurudi alimletea kitoweo kisirisiri nae akamuahidi kumtunzia Siri, kwa Nick yeye alikuwa akienda karibu na Kambi za jeshi wanapofanyia mazoezi wanakaa sehemu wakitazamia mazoezi na mwisho huja kujaribishia mazoezini  akiwa na Rafiki zake wa mtaani. Kwahiyo Mzee Mzobe alifichwa Siri hii na hakuwahi kuhisi kitu chochote kwa watoto wake kwani walikuwa na uhuni wanamna hiyo? bilashaka angesikia angewaadabisha kweli.

Mzee Mzobe alibaki kumtizama Binti yake ambae haoneshi kutoa majibu kwa uharaka aliamua kuondoka pale akiwa ametamka maneno kadhaa.

“” Utafaa kuwa mpishi wa hapa siku zote naona hauna kipaji.”

Minnie alibaki peke yake pale mpaka Kaka’ke akaja kumfuata angalau ajue ni kipi yeye atafanya kama yeye ataenda jeshini Inamaana atabakia nyumbani?

“” Minii, kwanini na wewe usitake kuwa mwanajeshi?””

Ni sauti yakaka’ke ilimshitua baada ya kuona akining’inia kwenye mti.

“” Wewe mparachichi wa Baba huo utavunja, shauri yako.”

Nick akafanya kujirusha kwa kutua.

“” Nimeanza kupiga hatua Sasa, muda si mrefu nakuwa mwanajeshi.”

“” Ahaaa, ndo wafikiri wanitamanisha…!!? Mimi sijui nafikiria Nini tu, Ila nawaza Kila mtu apite njia yake siku Moja tukutane kwenye pambano haijalishi tutapita njia gani mbaya ila hakikisha tunaonana.”

Nick ikabidi amsogelee Kisha akamkoa kichwani akimtizama kwa makini akizungumza.

“” Sumu ulioinywa naona imeanza kufanya kazi yake, lakini safari yetu itakuwaje ndefu kama wewe utabakia hapa hapa nyumbani?’

Minnie alitabasamu tu Kisha alienda kuegama kwenye moja ya nguzo iliokuwa ikiunganisha Kuta yao.

“” Haaa hata Sina niwazalo lakini Leo kwenye Darubini ya Baba, niliona Kambi ya jeshi ambayo utaenda kuchukua mafunzo pale, namna alivyokuwa akitizama Baba alikuwa na hasira nayo kweli nahisi Kuna kitu.”

Kipindi wanazungumza hayo Mzee Mzobe alikuwa akiyafatilia mazungumzo yao baada ya kusikia Kila kitu alitabasamu tu akiingia ndani.  Nini Kitaendelea? Atapelekwa Jeshi? Usikose SEHEMU YA PILI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Stori Nyingine Kwa Kumtumia Chochote 

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

22 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version