Wengi wamekua wakiamini kuwa ni kama imekuwa kama dharau kwa mzawa kocha Juma Mgunda kila timu inapopoteana (mwendelezo mbovu) na makocha wa kigeni kutimuliwa au kuondoka katika timu ya Simba huwa inamkumbuka Juma Mgunda na kumpa timu tena.

Nani asiyejua uwezo wa Juma Mgunda katika ligi hii?Hakuna ambaye hata kidogo anaweza kuwa na hofu juu ya uwezo wa wake na wengi wa wapenzi wa soka Tanzania wanaamini kuwa ni muda rasmi wa Simba kumuamini na siyo wakufanya kibarua cha saidia fundi ila anastahili kupewa timu kama kocha mkuu, na kitu kikubwa ni yeye kama kocha kuendelea kudumaza uwezo wake kwa kuendelea kung’ang’ania Simba SC ingawa kwa wakati mwingine unaweza kusema pia ni maokoto.

Ndiyo, Mgunda siyo kocha wa kwenda kufundisha wanawake au kwenda kufundisha vikundi vya vijana tena vijana wenyewe wanatengenezwa kisiasa tu lakini ukija kwenye uhalisia ni uongo mtupu.

Mgunda atapewa heshima yake endapo ataondoka simba sc na kwenda kufundisha timu nyingine za ligi kuu kama ambavyo aliifanya klabu ya Coastal mpaka kufika fainali ya kombe la FA, Namungo nk, maana anaweza kuwa kocha mkuu kwenye timu yoyote ukitoa Simba na Yanga ambazo zinaamini katika makocha wa kigeni zaidi.

Maoni yangu: Binafsi ninaheshimu sana uwezo wa kocha huyu ila kitendo cha kupewa timu kila makocha wanapoondoka siliungi mkono na kumuona Mgunda hana msimamo bali anafurahi sana kuwa saidia fundi.

SOMA ZAIDI: Fredy Ni Mchezaji Mzuri Akitumiwa Vizuri Ataisaidia SIMBA

9 Comments

  1. Mgunda ni kocha mkubwa na ana uwezo wa kufundisha timu yoyote apa tanzania tatizo timu zetu haziamini kwenye makocha wazawa na wakiwaleta wageni wanafanya vibaya Simba wamwamini mgunda ni kocha mzuri

  2. Ghettominds on

    Juma Mgunda ni kocha mzuri ila kwa timu kama ya Simba ni timu ambayo inahitaji watu wa mpira watakao kupa matokeo ya mda mfupi(project ya mda mfupi). Mgunda kupewa kuiongoza Simba ni pale tuu kama Simba watakubali kuwa na project ya mda mrefu ila kwa project ya mda mfupi sioni kama Mgunda anafaa, hana exposure yakutosha ya Mashindano makubwa ambayo Simba anashiriki ndio maana unaona kumuaminiwa inakuwa ngumu.

  3. Khalfani Khalifa Timotheo on

    Mgunda ni kocha mzuri shida kubwa kwenye kikosi kizima cha simba maana kwa kikosi hiki hata umlete pep guardiola wa man city bado hatutaona matunda kikubwa wafanye usajili mzuri

  4. KWA SIMBA HII DOZI PEKEE NI MAFUTA YA MWAMPOSA TU MAAN INAKEL. KIKUBW MXIMU UJAO WAXIFANY UXAJIL KWA KUPANIC WATULIE MAAN WAXHAJUA PANAP VUJA WAMLUDIXHE (MOSSES PHIRI) NA WAXIWE WABAHILI KUMWAGA MAOKOTO KAMA WANATAK KUFIK MBALI WAXIXAJILI WACHEZAJI LUNDO KAMA MBEGU ZA MABOGA by
    William mwangende 05

  5. Pingback: Simba SC Na Roho Ngumu Kwa Mtibwa Sugar Ligi Kuu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version