Kuna wakati usipokuwa mwerevu kwenye maisha yako ukaamini ulipo hakuna atakaekufikia basi kuna siku utakutana na matukio ambayo yatakushangaza sana na utabaki umepigwa na butwaa kwani  yatakushangaza kweli kama AFCON ya mwaka 2023 inavyoendelea kushangaza ulimwengu.

Kwenye dunia ya sasa kila kitu kinahitaji akili kubwa sana  hata kama ulishapiga hatua 10 mbele dhidi ya washindani wako na usishangae siku mshindani wako akiwa hatua moja nyuma yako kama tuu hautojali kuhusu kukua na kubadilika haswa kuwekeza kwenye utafiti na ubora.

Ukiishi kwa mazoea kuna siku utajikuta nyuma geuka upo nyuma na aliyekuwa nyuma yako yupo mbele  hii ndio hali inayotokea sasa na kuzikumba timu au mataifa ambayo yalikuwa nembo ya soka katika bara la Afrika, mabingwa na magwiji haswaa kwenye ramani ya kabumbu barani afrika, walilala usingi mzito wakasahau kuwa wakati wao wanalala mataifa mengine yaliamka na kuandaa mipango kazi yao vyema na sasa wamewasogelea mno au hata baadhi kuwapita

Kipigo  cha Ivory Coast kimegongelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la mataifa makubwa katika Afcon ni sawa kila timu inafungaa ila wapenda soka wengi wasingetarajia kipigo kile cha goli 4 kwa mwenyeji kwenye ardhi ya mababu zake  anaruhusu nyavu zake kutikiswa mara 4 tena mbaya zaidi bila majibu pale Uingereza mtangazaji nguli hupenda kusema “four goal nill”

Miaka imezidi kwenda tumeona Misri,Ivory cost,Cameroon,Ghana na mataifa  mengine makubwa yanavyohangaika kusaka alama kwenye michuano, mataifa ambayo yamekuja na mipango kazi yao mizuri  yamekuja juu yanawashangaza mno.Rais wa Shirikisho la soka la Cameroon na mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Taifa  Samuel Etoo alitoa maneno makali dhidi ya wachezaji wa taifa lake lakini hii inaweza kuleta maana kwangu ni hapana kuna usingizi hawa wakubwa wamelala kuamshwa inatakiwa wakutane na vipigo kama hivi washtuke kuwa hawako kwenye eneo la faraja  tena warudi kwenye tamaduni zao, waweke mikakati thabiti ya kupata watu bora wa kuliwakilisha taifa.

Hii inanitia furaha sana kuona sasa ubora hautafutwi kwa kundi fulani soka linachezwa, na watu wanaona hadharani. watu werevu wanaonesha walivyojenga timu zao washiriki wanaonekana na wale tia maji tia maji nao wanaonekana anguko hili ni muhimu na hatupaswi kulifikiria vingine kwasababu tunapaswa kuamka kutoka kwenye mazoea, kombe la dunia lijalo afrika itaongezewa timu bila anguko hili watu hawatafanya homework zao vyema bila anguko hili wangendelea kubaki kuamini kuwa wao ni wababe wa soka barani Afrika.

Kwa matokeo wanayoyapata kipindi hiki itawatoa magetoni watahitaji kurudi kwenye ufalme wao hapo tutaona jasho na damu likitoka na hii itakuwa tunu ya Afrika kuelekea kombe la dunia lijalo ni aibu kuongezewa timu alafu timu 1 pekee ndio itoboe kwelekea 16 bora au robo fainali, huku tukikumbuka timu zao ulaya zinabebwa na hawa mastar wetu waliotoka viunga vya Yaounde, St Pedro, Johannesburg, Cairo, na. miji mingine mingi Afrika.

Ni vipaji halisi vinaenda kulisha ardhi za nchi zao na kunogesha soka lao wakati huo huo bado wanatuzidi kwenye timu za taifa, anguko hili ni muhimu kwa afya ya soka la afrika watu warudi kwenye uwekezaji, waongeze umakini na nguvu ili tuone wale wababe wetu wakirudi kwenye zama zao na kuiwakilisha vyema africa. usipotoka kwenye comfort zone huwezi kupiga hatua.

SOMA ZAIDI: Cape Verde Na Funzo Kubwa Kwa Mataifa Madogo Kisoka

 

Leave A Reply


Exit mobile version