Siyo kero linapotajwa jina la mchezaji Clatous Chota Chama kwa wana michezo, lazima ulitaje pindi michuano ya kimaitafa hususani Ligi ya mabingwa inapokaribia, kilichofanywa na mchezaji huyu ni kama muhuri wa moto kwenye mioyo ya wana michezo wengi Tanzania haswa mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba.

Ukweli usiopingika, Mwamba wa Lusaka alifanya makubwa na bado anaendelea kufanya makubwa katika viunga vya Msimbazi haswa katika wakati ambao unaiona Simba SC ilipohitaji matokeo ya ushindi tu, aliziamua mechi ngumu kwenye miguu yake, rejea mchezo na Nkana FC ya Zambia pale Simba liipotinga hatua ya makundi ya michuano hiyo lakini pia dhidi ya As Vita Club na kwenda robo fainali.

Linapozunguzwa jina lake fahamu kuwa uvumilivu unahitajika na anapaswa mchezaji mwingine kutoka mbele na kuipa heshima jezi ya klabu yake. Kiburi cha Chama kipo hapo ndio maana viongozi wakimzingua huwa anakaa kimya huku akijua deni lake litalipwa na mashabiki wa Simba.

Wamepita wachezaji wengi sana na wenye vipaji katika ligi yetu lakini kuna namna ambavyo Chama ametufanya tuamine mpira ni akili na mpira unapita katika njia zake na anatuonesha kuwa wapo viungo wachache sana wenye ubora kama wake duniani ambao wakishika mpira unakua makini sana kuona atafanya jambo gani ambalo litakua la maajabu.

Tuendelee kuwataja wachezaji wetu lakini jina la Clatous Chama litaendelea kuwa lenye heshima kwenye mpira wetu, nitamuheshimu zaidi yule aliyemleta mchezaji huyu nchini na kutufanya tuone kuwa inawezekana kama tukiwekeza kwa wachezaji bora kama yeye.

SOMA ZAIDI: Awesu Tushakujua Wewe Ni “Mchawi” Wa Soka

 

4 Comments

  1. Pingback: Mashabiki Yanga Timizeni Wajibu Wenu Mko Nyumbani - Kijiweni

  2. Pingback: Mashabiki Yanga Msimfurahie PACOME Tekelezeni Wajibu - Kijiweni

  3. Pingback: Nani Atafuzu Robo Fainali Na Asec Mimosas Kundi La Simba? - Kijiweni

  4. Pingback: Mwacheni Aucho Acheze Mpira Mnachokionesha Ni Chuki - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version