Kibu Denis Prosper ndio ajenda iliyopo mezani kwa sasa na Tanzania nzima ipo mezani kujadili mada hii! Kwanza sipo hapa kuzungumza kuhusu Takwimu za Mchezaji wala kuchagua upande wowote kuhusu hili bali nasimama hapa kwenye uhalisia

Sidhani kila mmoja kama anajiuliza maswali haya ninayojiuliza Mimi!  Moja, Je ni kweli Thamani inayotajwa inafaa kusimama kwa Mchezaji husika? Je, hiyo pesa ambayo anahitaji ni sahihi Simba kuitoa kwa sasa? Tatu, Simba hawawezi kupata mchezaji mzuri kwa pesa hiyo? Nne, Kwanini Simba matukio ya hivi yananirudia sana? Simba wanahitaji kutoka wapi na kwenda wapi?

Baada ya kumaliza kujibu maswali hayo nadhani umeanza kupata picha taratibu, binafsi sina upande wowote ila ukweli ni kwamba nyakati kama hizi Menejimenti nyingi za wachezaji ndio sehemu zao na wanajua namna ya kucheza nazo ukikaa vibaya utashindwa kwenda njia sahihi kwa wakati huo kutokana na msukumo uliopo nje

Kinachofanywa ni mchezaji kupandishwa Thamani kwa Mchezaji ambapo mara nyingi Timu Pinzani, Waandishi wa habari na Vyombo vya habari na vingine hutumiwa kwa kiasi kikubwa sana kusukuma Thamani ya kitu husika kwa wakati huo hivyo usipokuwa makini utaacha njia yako na utatembea kwenye njia yao bila kujua

Labda nitoe vitu vichache tu ambavyo vinafanya Thamani ya mchezaji kuwa kubwa ambapo vichache ni Umri wa mchezaji husika, kiwango chake kwa wakati huo na Thamani ya mkataba wake kwa sasa! Chukua hivyo vitu vichache kisha vitumie kwenye mada iliyopo mezani kuhusu Kibu Denis ndani ya Simba SC halafu chukua hapo juu vile vitu ambavyo nisema vinatumiwa kupandisha Thamani ya mchezaji

Last! Kama unahitaji kupiga hatua kubwa kutoka ulipo basi kuna muda ni lazima kukubali kufanya maamuzi magumu ambayo yataendana na mipango yako kwa wakati husika, THAMANI DHIDI YA MABADILIKO 🇹🇿

Let’s Go!!.

SOMA ZAIDI: Simba SC Na Roho Ngumu Kwa Mtibwa Sugar Ligi Kuu

19 Comments

  1. Madhara ya kuruhusu watu wa nje ya kazi kukushauri, iko hivi Kibu Denis ni mchezaji wa kawaida sana ila anajazwa kiburi na wachambuzi na mashabiki ndo maana anajiona anastahili malipo zaidi ya hapo alipo lakini uhalisia wakubaliane abakie Simba ili afanye Improvements lakin kuhama Tim sio best option
    Milles^

  2. Nafikiri wanasimba hawanabudi kumuacha Kib D akatafute changamoto zingine maana hiyo ni kazi yake Zaid lazima angalie kuliko na manufaa Zaid maana anaandaa kesho yake but awe mwangalifu Kwa uchaguzi atakao ufanya

  3. Naongea ukweli mchungu Kibu ni mchezaji mzuri hatukatai ila anatakiwa ajue kama kamaliza mkataba wake ndani ya Simba njia bora kwake na kwa Simba ni aongeze tu mkataba ila kuhusu swala la kuachana na Simba na kutegemea apate Team bora kuliko Simba ndani ya nchi na nje ya Nchi hilo ni swala zito sana lina fikirisha sana sana atapata Team zenye uwezo wa kawaida tu sio zile Big Profile…✍️

  4. Peter Ignas on

    Kama anaenda aende tu, wakajazane yanga, mana tumechoka kila tukiamka matukio Simba hayaishi,

    Na hapo bado mana utasikia chama nae kaliamsha huko mara kidogo utaskia inonga nae, hujakaa vizuri utasikia chemalone mara ngoma

    Kwa style hii tutauana kwa stress

  5. Ifike mahali watu wajue mpira ni kazi,
    Mfano; Ukiambiwa huku tutakupa 15 million/month, na ulipo unalipwa 8 na mkataba unaisha na unawaambia wakupandishie hawataki, Je utabaki hapo? Kwa upande wangu mimi siwezi kubaki! Sasa ya nini maneno kumsema Kibu, ww baki na mapenz yako ya ushabiki, mchezaji yupo kazini na ni lazima aangalie kwenye maslahi yake binafsi kwanza kwasababu yeye tayar ni pro kwa Tz

  6. Tajiri ABAS on

    Aje kwa wananchi huku kumenogaaa,huko msimbazi anapoteza uwezo wake na kipaji chake,

    Tajiri Abaaas- MWANZA.

  7. Calvin's HD on

    Kwa thamani iliyopo mezani ni thamani tofauti na thamani ya mchezaji mwenyewe, Maana yake nini mchezaji thamani yake kwanza huanza pale anapokua na mchango positively Kwa timu. Kibu ana mchango ila Siwa thamani hii, Kwa nafasi yake alitakiwa kuwa na mchango zaidi ya tunaouona Kwa Sasa hivyo wake Maza Moja wafanye Negotiation

  8. Kwa kibu bado mapema Sana kufanya maamzi ya kuihama Simba. kwa Sasa atulie huku akiimarisha ubora wake kwan Kila mchezaj mzaw anahitaj kua Kama SAMATA hivo inahjitaj kuvumilia ili kuyafikia malengo. Isitoshe kibu anahitaj kuimarisha uwezo wake ili akitoka simba aende kilabu kubwa Zaid ambayo itampa mafanikio aliyo kuwa anahitaj. Huwez kutoka Simba ukaenda YANGA Wala AZAM, unakua unajirudisha nyuma mwenyew. KIBU TULIA MAFANIKIO YAKO YAPO HAPO ULIP ILA UKTOKA KABLA NDO TUMEKUSAHAU HIVO.✍️✍️🤝🤝

  9. Pingback: Pamba Jiji FC Ni Mkombozi Wa Soka Na Maisha Mwanza? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version