Wachezaji huwa wanakuwa na sifa zao na wanatofautiana sana kwa mchezaji mmoja na mwingine na hapa ndipo namkumbuka mchezaji wa klabu ya Simba anayeitwa Saleh Karabaka moja kati ya wachezaji wenye vipaji vikubwa sana ambao bado hawajapata nafasi ya kuaminiwa na kocha Benchikha bado.

Moja ya sifa kubwa ya Karabaka ni zile za kuwa hatari sana katika mikimbio haswa akiwa na mpira au kwenda kujiweka sehemu sahihi ya kupasiwa mpira huwa anajua sana sehemu ambayo anaweza kupata nafasi ya kucheza kiwanjani na huwa anakabiliana vyema na mpinzani.

Kama kuna dhahabu ambayo Simba wanayo ndani basi ni huyu kijana, akiwa third man runs huwa anafanya pressing kwa ustadi na kuweka mpira wavuni kutokana na utulivu wake akiwa katika eneo la mbele.

Nafikiri Abdelhak Benchikha amuangalie kwa jicho la tatu, akigawana dakika na wenzake waliopo kikosini kwa sasa itakua vyema sana kwake lakini pia na ukuaji wa soka la Tanzania.

Karabaka atamlipa sana Benchikha na Simba kwa kujituma sana kwake na kufanya “Third man runs” yani pale wenzake wawili wanapopasiana halafu yeye anafanya runs bila mpira kwenda kwenye space iliyowazi iwe goli au assist huwa anafanya hivyo

Huyu kijana ni wazi kuwa kipaji kizuri sana anacho, anahitaji kupewa nafasi ili ajiamini zaidi lakini uwepo wa Clatous Chama nyuma yake ambaye ni Bima itamfanya kufanya mikimbio akiwa huru na kufanya jukumu la kuweka mpira wavuni, na hilo huwa analipatia sana.

 

SOMA ZAIDI: Barua Kwa Wachezaji Wa Simba Kuelekea Mchezo Na Jwaneng

1 Comment

  1. Pingback: Tunamkosea Heshima GSM Tuuzungumze Ukweli Tu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version