Kikosi cha Simba SC kimeweka kambi yake Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Ahly ambao ni mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika na niseme tu hii itaongeza kitu kikosini na itapunguza bughza za hapa na pale. Ukikitazama Kikosi unaona ile ari za wachezaji ni kubwa sana.

Nitapongeza sana wazo la kuipeleka timu huko Visiwani, kushinda siyo kucheza hata kutuliza akili pia inaongeza chachu ya ushindi. Naiona Simba SC ikienda kufanya vizuri katika mchezo wake ule na Al Ahly.

Hakuna hofu na tusiruhusu uoga wa aina yoyote ile kuelekea mechi hii, naamini viongozi wa Simba na wanachama wake wameshajua mwiba wa kumchoma mpinzani wake huyu, kwangu hua sina shaka na mnyama katika michezo ya namna hii.

Silaha moja wapo ni kuona mashabiki wa Simba SC kama ilivyo kawaida yao kufurika pale kwa Mkapa, hilo kwao siyo la kuwaelekeza hua wanajua nini chakufanya ingawa mechi za hivi karibuni imekuwa ni tofauti kidogo.

Siioni ile Uwanja kujaa full na kumfanya mpinzani aweweseke sijui imeletwa na nini lakini mchezo huo ujao linaenda kufanyiwa kazi na Viongozi wenyewe. Hakika Simba SC ni timu ya mfano.

Nadhani ni wakati sasa wa kumuacha Benchikha aendelee kupambana na wachezaji lakini na mbinu za kuhakikisha wanamfunga AL AHLY katika mechi zote 2 na kufuzu hatua ya nusu fainali lakini sasa wanaohitajika kwa nguvu zaidi ni mashabiki ambao siku zote huwa ni moja ya wale ambao wanawapa nguvu wachezaji katika kupambana uwanjani.

SOMA ZAIDI: Hii Ndio Mbavu Ya Kushoto Ya Azam Fc Yenye Balaa Zaidi

Leave A Reply


Exit mobile version