Wakati wengi wakiwa na mawazo na maswali mengi kuhusu mchezo kati ya Yanga dhidi ya CR Belouizdad ambao utaamua hatma kubwa sana kwa klabu ya Wananchi kutinga hatua ya robo fainali.

Hii ni kama ile kwenye maandiko ya kitabu cha Biblia pale Yohana na wenzake walipokuwa wameshajikatia tamaa kuhusu kazi yao ya uvuvi na kujipatia Samaki. Hakuna kitu kibaya kama tumaini likiondoka maisha mwako. Yesu anamwambia Yohana beba NYAVU zako kazishushe mpaka KILINDINI yaani katikati mwa bahari kwani wao walishazoea kuvua Samaki mwanzo mwanzo mwa bahari.

Ukirejea mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad wapo baadhi ya mashabiki mioyo yao ni kama Yohana ambaye alishajikatia tamaa, lakini alichokisema Ali Kamwe kuhusu nguvu ya mashabiki katika uwanja wa Mkapa ni ukweli MTUPU. Yawapasa mashabiki kuujaza uwanja kwa wingi kisha kuishangilia timu muda wote wa mchezo kwani hii hii itawapa nguvu kwa kiasi kikubwa wachezaji na kupata ushindi.

Kwenye mpira hakuna neno haiwezekani, hutakiwi kuondoka na huo msemo utakuja kushangaa. Yesu alipomwambia Yohana maneno yale alijua kuwa roho ya Kibinadamu inapambana na mwili ile ya haiwezekani, adui namba moja kwenye maisha ni hiyo roho lakini Bwana alitaka kuonekana mbele yao kisha wakashusha NYAVU zao na kilitokea ni Samaki ambao hawakuwa na idadi ndivyo ilivyo sasa kwa Yanga wakati huu.

Siku ya Jumamosi ni historia kwa wachezaji, viongozi, mashabiki na kila mpenda michezo kwa YANGA SC kwenda kuifunga timu ya CR Belouizdad kisha kusubiri matokeo ya mwisho ambapo itatafutwa sare tu. Hii kwangu naiona inawezekana na timu kwenda zake robo fainali. Uwanja wa Benjamin Mkapa ni sehemu ya wageni kuangua vilio siyo sehemu yao ya kucheka pale.

SOMA ZAIDI : Mwacheni Aucho Acheze Mpira Mnachokionesha Ni Chuki

1 Comment

  1. Pingback: Kwa Hili Ayoub Kaitia Matatani Simba Kimataifa? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version