Wakiwa nafasi ya 12 na alama zao 16 katika msimamo wa ligi kuu Tanznaia bara hii leo wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo JKT Tanzania wanawakaribisha wekundu wa msimbazi klabu ya Simba ambao wako nafasi ya 2 na alama 33 katika mchezo utakopigwa kuanzia majira ya saa 10 alasiri.

Huu ni mchezo mwingine muhimu kwa Simba na JKT, Simba wanaingia kwenye mchezo huu wa kiporo wakihitaji alama 3 ili kuweka matumaini karibu zaidi ya kugombania ubingwa na kumbuka kuwa ushindi wa leo Simba watafikisha alama 36 watabakiza alama 4 dhidi ya mpinzani wake Yanga, so far quality ya kuondoka na ushindi kwenye mchezo wa leo wanayo kutokana na mwendelezo usioridhisha wa klabu ya JKT.

Lakini wanaenda kucheza na JKT ambao nao hawapo kwenye nafasi nzuri wanahitaji alama ili kujinasua kwenye nafasi ya 12 na alama 16, faida ambayo wapo nayo leo ni watakuwa nyumbani uwanja ambao utakuwa mgeni kwa Simba huku ukiwa afadhali kwa JKT kwani ndio huutumia kwa maandalizi ya mechi zao.

Licha ya faida hiyo bado JKT wataingia timu ya pili dhidi ya Simba na ili kupata matokeo chanya wanatakiwa kuwapa heshima yao Simba ambao wana wachezaji wenye ubora mkubwa zaidi yao.

Simba wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Geita Gold uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba huku wakiwa na malengo ya kuhakikisha wanashinda kila mchezo ulio mbele yao kwakuwa wanahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi msimu huu.

Huu utakua mchezo wa kwanza wa ligi katti ya JKT Tanzania vs Simba kuchezwa Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo kwahiyo matokeo yoyote yatayo tokea itakuwa ni historia kwa timu zote mbili lakini kumbuka kuwa Onana atakua nje katika mchezo wa hii leo.

SOMA ZAIDI: Huwezi Kumchukia Kayoko Kama Una Upenda Mpira

Leave A Reply


Exit mobile version