Kuna njia nyingi za ubashiri ambazo wawekezaji wa mikeka wamekua wakizitumia ili kuhakikisha kuwa wanashinda mikeka yao ya kila siku wanayoweka kwa kuweka Option ambazo ni watu wachache sana huweka na hii leo tutaangazia ubashiri katika Kupatikana kwa Kadi mchezoni (Betting in Bookings).

Ubashiri huu unahusisha kuchagua kadi kupatikana kipindi cha kwanza pekee au kuchagua zipatikane kipindi cha pili au zipatikane za mchezo wote na hapa tunamaanisha Total Booking in First Half, Total Bookings in Second Half na Total Booking in the match.

Katika njia hii kumbuka kuwa una uhuru wa kuchagua ziwe kadi nyingi au kadi chache katika mchezo au kubashiri timu gani ipate kadi nyingi au timu ipi ipate kadi chache katika mchezo husika.

Tuanze Kwa Kutazama Idadi Ya Card Kipindi cha Kwanza

Wapo ambao huamua kutumia njia ya kupatikana kadi kipindi cha kwanza pekee ambapo unaweza kuamua kuchagua kwa kuweka Total Bookings Over au Total Bookings Under. Mfano unaweza kuamua katika mchezo husika kuwe na Card zaidi ya 3 kwa kipindi cha kwanza yaani Total Bookings 1st Half Over 2.5. Ukiamua kuchagua kuwa kipindi cha kwanza kusipatikane zaidi ya card 3 unaweza kuweka 1st Half Total Cards Under 2.5.

Namna Ya Kubashiri kupatikana kwa kadi kipindi cha pili

Katika kipindi cha 2 mara nyingi watu hubashiri kama wanavyobashiri kipindi cha kwanza lakini utofauti wake mkubwa ni kuwa kumbuka kusema 2nd Half Total Bookings maana kuna wanaochanganya 1st Half na 2nd Half hivyo kuwa makini katika kuusuka mkeka wako. Mfano unaweza kuamua katika mchezo husika kuwe na Card zaidi ya 3 kwa kipindi cha pili yaani Total Bookings 2nd Half Over 2.5. Ukiamua kuchagua kuwa kipindi cha pili kusipatikane zaidi ya card 3 unaweza kuweka 2nd Half Total Cards Under 2.5.

Kubashiri kadi za jumla katika mchezo husika

Nadhani hii ndio njia nzuri zaidi katika kuweka kadi japokua haina uhakika wa moja kwa moja kwani zipo baadhi ya mechi ambazo hutoka kadi chache sana ambazo huwezi kutegemea na zipo ambazo zinaweza kutokea kadi nyingi na ukawa hujapanga kutokea kwa kadi hizo.

Katika hatua hii ni vyema kufahamu kuwa hapa kadi za jumla maana yake unachanganya za kipindi cha kwanza na zile kadi ambazo zitapatikana kipindi cha pili ndo ziwe idadi yake. Mfano ukabashiri Total Bookings Over 4.5 maana yake kuwe na kadi zaidi ya 4 katika mchezo mzima au Total Bookings Under 4.5 maana yake kuwe na kadi chini ya 4 katika mchezo wote.

Kubashiri kadi za timu pekee

Wapo ambao huamua kubashiri kuhusu kadi za timu husika pekee na mbinu ni ile lakini katika hili kinachobadilika ni kuwa unabashiri kwa timu moja pekee kuwa wapate kadi zaidi au kadi chache pekee.

 

Kama ni mwekezaji unayetamani kushiriki katika njia hii ya ubashiri zipo ligi ambazo huwa kunakua na kadi nyingi zaidi katika mchezo mmoja haswa ligi za nchi zinazopatikana bara la America na baadhi ya mechi za ligi kuu ya Uingereza na zile za Ujerumani. Ni muhimu kuzingatia machaguo yako na kuhakikisha kuwa kiasi unachoweka ni rahisi kukipata wakati mwingine utakapokipoteza.

SOMA ZAIDI: Ligi Bora Za Mpira Wa Miguu Unapobetia Kona

 

 

4 Comments

  1. Pingback: Huu Hapa Mkeka Wa Leo Jumatano - Kijiweni

  2. Pingback: Nini Maana Ya Halftime/Fulltime Katika Betting? - Kijiweni

  3. Pingback: Mkeka Wa Leo Jumanne Timu 10 Odds 87 - Kijiweni

  4. Over 4.5 ni zaidi ya 4 na sio zaidi ya 5 kama mlivochambua hapi juu ila zaidi ya 5 ni 5.5 ndo maana ukiweka option ya over 4.5 kwa cards zikatokea 5 basi ni valid (win) ila cards zikitokea 4 itakua ivalid (loss)

Leave A Reply


Exit mobile version