Fantasy Premier League (FPL) ni mchezo wa mtandaoni ambao huwa ni bure kabisa kujiunga na kuutumia ambapo unapata nafasi ya kusajili na kutengeneza timu yako kwa kuchagua wachezaji 15 kutoka ligi kuu ya Uingereza ambapo unapewa budget ya kiasi cha Milioni 12.

Ni moja kati ya mchezo maarufu duniani unaohusisha mpira wa miguu ukiwa na watu zaidi ya Milioni 8 wanaoocheza mchezo huu ambapo watu wanashindana na marafiki zao au hata watu wengine ambao unakua huwafahamu ili kushinda alama na baadae kujishindia zawadi mbalimbali.

Katika kikosi ambacho unakiandaa kumbuka kuwa unasajili magolikipa wawili , mabeki watano , viungo watano Pamoja na washambuliaji watatu ambapo wachezaji watatu unaweza kuwasajili kutoka katika timu moja inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Wakati ukiwa unaandaa kikosi chako cha Fantasy Premier League kuna mambo haya ambayo unatakiwa kuyazingatia:

  1. Bajeti; Kumbuka unakua na bajeti ya £100m kwa ajili ya kuandaa kikosi cha wachezaji 15 pekee wa kikosi chako ambapo unatakiwa kuwa makini na gharama za mchezaji wakati unamnunua ili iendane na bei ya bajeti yako
  2. Uchaguzi wa kikosi: Katika kikosi ambacho unakiandaa kumbuka kuwa unasajili magolikipa wawili, mabeki watano, viungo watano Pamoja na washambuliaji watatu. Uchaguzi wa kikosi unatakiwa kuwa na uwiano sawa wa mfumo wako uwanjani.
  3. Klabu za Ligi Kuu:Wachezaji watatu unaweza kuwasajili kutoka katika timu moja inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza. Ili kuwa na uhuru wa kuchagua wachezaji kutoka timu mbalimbali za ligi kuu.
  4. Uchaguzi wa mchezaji: hakikisha unachagua wachezaji wanaoendana ili kuweza kuhakikisha kuwa unapata pointi nyingi zaidi ambapo itabidi uangalie uwezo wake uwanjani na jinsi ratoiba ya ligi ilivyo.
  5. Magolikipa: Kuwa na magolikipa zaidi ya wawili inakuhakikishia kuwa ni rahisi kubadilisha endapo atapata kadi au kuumia lakini hapa itabidi uchague golikipa ambaye ana balaa katika kutoa mipira ya hatari lakini pia ambaye una uhakika ana balaa katika kusave penati endapo ikitokea.
  6. Mabeki: Chagua mabeki ambao wako vizuri katika kukaba na kushambulia haswa wale mabeki wa kulia na kushoto ambao wanajitihada kubwa sana katika kuchangia magoli katika timu.
  7. Viungo: Ili uhakikishe kuwa unapata pointi nyingi hakikisha kuwa unachagua viungo ambao wanahusika sana katika upatikanaji wa mabao katika timu lakini pia ambao wana ubunifu wakiwa pia na uwezo wa kufunga pia itakua poa zaidi. Usisahau wale ambao wanauwezo wa kupiga na kufunga mipira ya kutenga.
  8. Mafowadi: Chagua wale ambao wao kupachika mabao ni jambo la kawaida kwao wenye uchu wa kufunga watakusaidia sana.

Kumbuka kuwa katika FPL una uwezo wa kununua na kuuza mchezaji katika kikosi chako katika msimu mzima ambapo ni kila baada ya mechi za wikiendi ambapo watakuwekea idadi ya wachezaji wa kununua na kuuza.

SOMA ZAIDI: Hii Ndio Michezo 8 Hatari Zaidi Duniani

5 Comments

  1. Jamani me naitwa Robert unatokea morogoro naomba mnielekeze jinsi ya ujinga na fantasy league me pale mwishoni wanakata sijui Wana taka nini pale

Leave A Reply


Exit mobile version