Kuelekea michuano ya mataifa barani Afrika (AFCON) itakayofanyika nchini Ivory Coast, yapo matukio kadhaa ambayo yalishika vichwa vya habari na kuwafanya watu wengi kutaka kuyafuatilia ili kufahamu zaidi kuhusu matukio haya na moja kati ya tukio liloshangaza wengi ni kuhusu jezi za timu ya Taifa ya Cameroon ambazo walivaa katika michuano ya mwaka 2002 na 2004.

Wakati wa michuano ya AFCON kwa mwaka 2002 Cameroon walishinda michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 2002 kwa kuwafunga Senegal kupitia mikwaju ya penalti kwenye fainali. Licha ya kuchukua ubingwa lakini kinachokumbukwa sana na wanamichezo barani Afrika ni jezi za Cameroon (Simba Wasioshindwa) ambazo zilikuwa hazina mikono. Baada ya kuchukua ubingwa wa AFCON pia walifuzu kombe la dunia lilofanyika nchini Japan mwaka 2002  wakiwa na kikosi cha wachezaji kama Samuel Etoo, Marc Vivien Foe pamoja na Rigobrt Song walivyotaka kutumia jezi hizi walizuiwa na FIFA kuzivaa kwenye kombe la dunia.

Baada ya kushangaza umma na jezi za namna hiyo za kukata, Cameroon wakaendelea tena na vituko vyao ambapo mwaka 2004 wakati wa michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Tunisia walikuwa na jipya tena ambapo walivalia jezi moja iliyoshikana – fulana na kaptura.

Kufuatia jezi hizi mpya ambazo walikuja nazo Cameroon Fifa hawakufurahia, na ikizingatiwa kwamba walikiuka ahadi ya awali ya kuzitumia kucheza mechi za makundi pekee, Fifa waliwapiga faini kwa kucheza mechi ya robo fainali ambayo walishindwa na Nigeria.

Michuano ya AFCON inatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Ivory Coast kuanzia tarehe 13/01/2024 mpaka tarehe 11/02/2024 nchini Ivory Coast huku viwanja takribani 6 vikitumika katika mechi mbalimbali.

Endelea kufuatilia zaidi kuhusu taarifa zinazohusu AFCON kwa kugusa hapa.

 

1 Comment

  1. Pingback: Mastreka Hatari Wa Kuchungwa AFCON 2023 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version