Anaandika mwana mitandao maarufu Tanzania anayefahamika kama Ujugu Hapa

Nataka leo tuongee soka kiufundi, story za porojo zikae pembeni.

Unapotaka kuona uwezo wa mchezaji, Kabla ya takwimu za uwanjani ( Goals & assists), na kabla ya kumpa mchezaji muda kuna vitu lazima unaviangalia kwa mchezaji yeyote kwenye namba anayocheza

Ahoua anacheza namba 10. Hili ni eneo ambalo tunategemea mchezaji aweze kuwa na ubora mkubwa wa kuunganisha midfield line na forward line. Yeye anakua shimoni pale kufanya MIPANGO MIKAKATI. Mchezaji anaecheza hilo eneo bila kupepesa macho lazima awe na AKILI KUBWA.

Tukimchukulia, Jean Charles Ahoua kama Case study yetu, na namba anayocheza (Namba 10 – Attacking midfielder) tutampima kwa sifa zifuatazo;

> Uwezo wa kupiga pasi, na kuchagua pasi sahihi ( Passing ability)

> Uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za mabao, na kufunga

> Uwezo wa kukokota mipira, na kucheza anapokua chini ya presha kubwa.

> Vision — Uwezo wa kuyasoma mazingira uwanjani, kuelewa matukio yanayotegemewa kutokea kabla hayajatokea, na kufanya maamuzi sahihi

> Maamuzi sahihi (Decision making)

Nimeangalia mechi 4 alizocheza Ahoua; Mechi dhidi ya – Simba vs APR, Simba vs Yanga, Simba vs Coastal Union, Simba vs Tabora United.

Katika mechi hizo zote, sijaona ‘Upekee’ wa Ahoua — Namaanisha sijaona uwezo binafsi kutoka kwake, either kwenye kupiga pasi hatari, kufunga, au kukokota mipira.

Kwenye hizo mechi nne, hakuna hata mechi moja ambayo alitengeneza nafasi za mabao hata mbili na kusema kweli hii namba 10 imefanya kazi yake. Lakn kumbuka mechi zote alizocheza ameaminiwa kuanza.

Kwenye hizo mechi nne, huoni ni kwa namna gani Ahoua anakusisimua kwa pasi murua za kukuinua kwenye kiti ww kama shabiki na kusema huyu mchezaji ni fundi haswaa.

Kwenye hizo mechi nne nmemuona Ahoua ambae anakaa sana na mipira bila sababu

Nimemuona Ahoua ambae uwezo wake wa kupiga pasi na kuchagua pasi ya kupiga ni mdogo mno. Namba 10 anasifika kwa kupiga forward pasi, zile pasi ndani ya mashimo ( In pocket spaces), pasi za kuvunja mstari wa mabeki, na midfield line.

Namba 10 hutakiwi kupiga pasi za kawaida kawaida. Lazima uwe namba 10 hatari wa kuogopwa. Angalia mifano kama ya wachezaji kama Mesut Ozil au Odegaard.

Nimemuona Ahoua asie na uwezo binafsi. Kuna muda mechi inachafuka, sehemu za kupiga pasi hazionekani. Hapa ndipo namba 10 unaamua kujikana nafsi, na kuibeba timu mgongoni, unachukua boli unakusanya kijiji chako, unatengeneza nafasi kwa wengine wafunge mabao.

Nmemuona Ahoua ambae anapiga mashuti hovyo hovyo na yasiyo na target.

Haya yote ambayo nmeongea, hayahitaji mchezaji kupewa muda. Ni sifa ambazo namba 10 anakua nazo kabla ya kupewa muda, kabla ya kuzoea ligi, kabla ya kuangalia amefunga bao ngp kwa msimu.

Ni rahisi kwa namba 10 kufunga bao za kutosha, kutoa pasi za mabao kama nafasi yake anayocheza anafanya maamuzi mengi kwa usahihi. Ahoua nadiriki kusema ananiangusha, ananifikirisha, na kunihuzunisha sana. Ananifanya nifikirie labda Simba ingepambana kumbakisha Chama

Anatufanya tunawaza, ilikuaje Ahoua alikua MVP?

Pima MVP wote waliokuja Bongo miaka ya karibuni, angalia mabalaa yao uwanjani, then muangalie na yeye Ahoua. Jibu baki nalo

Naomba ieleweke, siandiki ili kumsagia kunguni, au kumponda. Lakini wote soka tunaliangalia kideoni. Je nyie kama mashabiki mmeona kipi cha ajabu mpaka sasa kutoka kwake?

Ila sio kesi, turudi kwenye ule msemo wetu pendwa: APEWE MUDA, AZOEE LIGI.

Asalaam Aleykum

SOMA PIA: Ni Wakati Wa Vilabu Kula Matunda Ya Timu Za Vijana

15 Comments

  1. Hauwezi uka mtathmin mchezaji kwa mechi chache kiasi icho anapewa mda aonekane azizi k ni mfano mzuri aliwaka mda gani si baada ya kina mayele kuondoka kabisa

  2. Kinacho tokea ni kwamba watu wanatka ahoua acheze kama alivyokua chama ni kitu ambcho hakiwezekan nd kwanza simba tunajenga team kila mtu ana unique yke huyu jamaa anajua boli ni swala la muda tu jana kaanz na assist 1 goli la che fondoh na muda zaidi nd utaongea

  3. artificial traveller on

    kabla atuja mpa chezaj muda tunapaswaa kumjuaa…. jean Charles Ahoua n mchezaji mtulv Sanaa anajuaa n wakat gan anapaswaa kueka pas au wakat inahtajka yy mwenyew ndo afanyee maamuziii ya kushutiii langoo mambo kama haya yanafanya tuceeme anahtaj muda kuoneshaa alchonachoo

  4. Shida inakuja mnataka ahoua acheze kama chama hicho kitu hakipo ana kila sifa ya namba 10 ila tuh angalia na kikosi hizo pasi hatari anampigia nani? Ilihali striker mukwala unakuta yupo pembeni kabisa hizo pasi anapga wapi kabla hujamuhukumu ahoua basi anza na mukwala kwanza🙏

  5. Ayah nenda kamnyang’anye Tuzo ya MVP ss …. We c unajua zaidi kuliko shirikisho la soka la Ivory coast 😅😅

    #Wachambuzi wa hali ya hewa bana 😅😅😅😅😅

  6. Unayo sema ni kweli ila bado mapema kumuhukumu kuna mechi 29 za ligi kuu za kutuonyecha uwezo wake pamoja na kombe la shirikisho zote sikiicha bila kuonyesha alicho nacho hapo ndio tunajua tumepigwa na panga linamuhusu

  7. Tumepigwa hapa, maana kuna passi hata mimi ningetoa kwa stracker lakini anachofanya ni mshangao, kuzoea nini bwana, kutoa pasi kwa mfungaji inahitaji kuzoea!!! nilishasema kwa Fredy hakuna kitu watu wakasema apewe muda, muda akapewa bado hakuna kitu. Debora mbona amejitafuta tiyari na yupo kwenye mstari

Leave A Reply


Exit mobile version