Siku zote sio vibaya kurudia njia iliyokupa mafanikio . Tena kama njia mpya uliyoichagua imeshindwa kukupa mafanikio . Lakini swali kubwa ni je utayapata mafanikio uliyoyapata mara ya kwanza endapo utaamua kuirudia njia hiyo tena hakuna uwakika wa asilimia 100 kama utapata mafanikio ya zamani na mpira umeonesha hilo na simba wamekuwa mfano halisi wa maelezo ya hapo juu.

Kwenye mpira kuna neno linaitwa project yani mradi ni neno dogo lililobeba maana kubwa na vipengele vingi ndani yake ili timu kufanikiwa lazima iwe na mradi ambao unaelezea maono ya timu mradi unaweza kutumia mda mrefu au mfupi kutekeleza na mradi unaweza ukafanikiwa au usifanikiwe

Kila mradi una mahitaji yake mfano (wachezaji , kocha , benchi la ufundi , manager wa timu , mkurugenzi mtendaji na vitu vingine vingi ) na kama kuna mradi wa simba uliwahi kuwa na mafanikio basi ni ule mradi wa 2017 hadi 2021 baada ya hapo hakujawahi kuwa na mradi uliyowahi kuleta mafanikio kwa simba tena .

Hivo kuna wakati uongozi wa simba uliokuwepo tokea wakati ule hadi sasa wanaamini kuwa kuna baadhi ya vipengele vilikuwepo katika mradi ule kama wakivirudia vinaweza kuwapa mafanikio kitu ambacho ni kama ubashiri tu yani bahati na sibu hakuna uwakika wa jambo hilo

Walikaribu kuwa rudisha baadhi ya wachezaji waliowahi kuwepo katika mradi uliopita ikiwep Clotaus Chama, Luis Miquissone pia hawa wote walirudi lakini hawakuweza kuyapata mafanikio kama waliyoyapata miaka ya nyuma.

Kwasasa ni ndoto za kumrudisha Mkurugenzi Mtendaji Barbara Gonzalez je wakimrudisha wataweza kupata mafanikio kama waliyoyapata chini yake inabidi tujiulize wanataka kurudisha mradi uliopita au au kuboresha mradi mpya kwa kutumia baadhi ya vitu vilivokuwepo kwenye mkataba uliopita hilo ndio swali kubwa kwa sasa kwa mashabiki wa simba

Lazima watambue yakuwa Barbra alifanya kazi na uongozi wa wakati ule uliopita wa simba na je watarudisha uongozi wote ikiwemo kocha na benchi la ufundi maana hii ndio njia pekee ya kuiga mradi kwa asilimia 100 na kuwa na uwakika lasivo je barbra atahitaji kusema anamuhitaji nani na nani katika uongozi ili simba ivuke na ipate mafanikio kama niivo kuna watu watalazimika kuachia nafasi zao kwajili ya mafanikio ya klabu

Mradi ni kitu kikubwa sana na hakihitaji wiki au msimu mmoja kutekeleza inaweza kutumia hata misimu miwili kisha msimu wa 3 mradi ukaanza kuzaa matunda sidhani kama mashabiki wa simba wako tayari kwa uvumilivu huo wakuwa loosers misimu miwili ijayo lakini inabidi wakumbuke kuwa wakati wanabeba kombe mara nne mfululizo

Yanga walikuwa wanajenga kitu kilichotumia muda kukamilika hadi kuwapa matunda na engineer hersi ndio uhimili wa mradi huu wa sasa wa yanga nisiwafiche ni kama tu marehemu Hans poppe alivikuwa nguzo ya simba katika miradi yao yofauti tofauti

Nina amini katika utendaji kazi wa barbara gonzalez kama atapewa mda na nafasi yakufanya maamuzi kwajili ya mradi mpya wa Simba.

SOMA ZAIDI: Uso Wa Saido Ntibazonkiza Unazungumza Mengi 

4 Comments

  1. Arusha Property Agency on

    Ujio wa Mo Dewji utaleta mabadiliko at least kwa Simba kuelekea misimu inayofuta… Msimu huu unaoanza kazi itakuwa ngumu kidogo lkn Misimu inayofuata Simba itakuwa tishio Barani Afrika

Leave A Reply


Exit mobile version